Elimu ya kuwakabili nyoka na n'ge itolewe mashuleni

Bella Ciao

JF-Expert Member
May 28, 2019
1,804
4,444
Habari wakuu?

Watu wengi hapa kwetu Tanzania wakiona nyoka kitu cha kwanza wanawaza ni kumuua. Bila kujua nyoka wana faida nyingi sana katika eco-system na pia wanaweza kutumika katika tafiti mbalimbali za kisayansi.

Ikumbukwe siyo nyoka wote wana madhara kwa binadamu bali wana faida kwetu kuweza ku-control wadudu, panya, vichakoro n.k

Elimu ya kukabiliana na nyoka hasa wenye sumu ingetolewa mashuleni ili kupunguzwa mauaji ya nyoka.

Au ingewapa uwezo maaskari wa kulinda maliasili (rangers) endapo mtu ameona nyoka katika eneo lake apige simu kwa national park au game reserve iliyopo karibu ili waje kuwakabili wenyewe!

Screenshot_20200301-141532.jpeg
Screenshot_20200301-141728.jpeg
Screenshot_20200301-142004.jpeg
 
Mkuu tafiti za kisayansi Africa? 😂

Inamaana Hao scientists tangia waanze hizo tafiti za kuhusu nyoka mpaka leo hawajamaliza? Mbona wanazijua species za aina zote wale ambao ni very poisonous na mpaka ambao hawana madhala kwamba maisha ya binadamu?

Kwa Africa ukimuona nyoka anachostahili ni kifo tu. Sema watoe elimu ya jinsi gani ya kuwatambua na kuepuka madhala yasababishwayo na nyoka hao ili wakati wa kumwinda asikuzidi maarifa.
 
Mkuu tafiti za kisayansi Africa?

Mkuu utafiti unaishaga? We utajuaje kama sumu ya nyoka ni dawa ya corona?..

Utafiti haushi kila siku zinagundilika sub-species mkuu
 
Kwangu mimi bora nikutane na simba ntajua chakufanya lakini sio joka
 
Mkuu utafiti unaishaga? We utajuaje kama sumu ya nyoka ni dawa ya corona?..

Utafiti haushi kila siku zinagundilika sub-species mkuu
Nakubaliana nawe Mkuu kuwa tafiti haziishi ila kwa Africa especially kwetu hapa hatuna mazingira hayo ya kupenda tafiti. We mwenyewe ni shuhuda wa sera za nchi yetu zimeegemea wapi, mama wajawazito tu mpaka leo bado wanajifungulia njiani, madawa ya malaria tu tunashindwa kusupply mpaka vijijini, Ije kuwa tafiti za vitu ambavyo havina impact kubwa kwa maisha ya mtanzania mkuu?
Let's talk through experiences
 
Sawa mkuu nimekuelewa
 
Back
Top Bottom