Elimu ya kulea wagonjwa na wazee ifundishwe VETA uhitaji unaingezeka

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,272
Mara nyingi nimeona mabandiko humu jukwaani la ajira ya kumhudumia mgonjwa au mzee majumbani. Huku mtaani hitaji hili linaongezeka. Magojwa kama kiharusi huwapata watu wengi na kuna wanao athirika na kuhitaji msaada wa karibu katika kuendesha maisha yao ya kila siku.

Kutokana na uhaba wa ajira ni rahisi kumpata mtu anaeweza kutoa huduma, hasa unapotoa malazi na chakula juu ya mshahara. Watu hawa huwa wengi hawana uwelewa wa kazi. Huwa ni shida tu za maisha. Matokeo yake ni kuhatarisha maisha ya mgojwa.

Wataalamu wakiweka masomo haya VETA itakuwa ni rahisi kumpata mtu mwenye uewelewa hata wa elimu ya msingi ya kumpa sawa anaemhudumia.
 
Wabandika makucha na wanyoa viduku wataweza kweli..!? Mimi binafsi nina uzoefu na hicho ulichokiandika,asee uwe na moyo pia wa imani hivihivi siku mbili tuu una resign mwenyewe..!!
 
Back
Top Bottom