MO11
JF-Expert Member
- Mar 23, 2014
- 18,851
- 38,689
Habari za muda huu wanajukwaa.
Unajua kuna mambo yanakera ila ndivyo tunaishi tumezoea hata kama tunaonewa ila hatujui kama tunaonewa.
Shule ya msingi kila siku nilikua naambiwa niende na ufagio niende na kidumu cha maji nisipoenda nacho kazi ninayo hapa utasikia eti stadi za maisha ila kiukweli nafundishwa U GARDENER huu ni umasikini najengewa mazingira kwamba kazi hii hata nikifeli shule ndio naiweza maana shule sikufundishwa hata kushona nguo.
Hapo utaambiwa ulete mbolea shuleni ulete maua halafu unataka mtihani ukija ufaulu kwa maisha ya kawaida ukiwaangalia hawa wanafunzi shule wanaenda kuteseka ndio maana nasema unaonewa halafu hujui kama unaonewa kuna cha kubadilisha hapa.
Sekondari niliyoyashuhudia ukifanya kosa utachimbishwa visiki utachimbishwa mashimo wewe mpaka ujute kuna watu niliwashuhudia shule flani hivi maarufu hapa Dar wanafunzi wamebebeshwa lami huyu umemjenga kwamba yeye katika hii dunia anastahili kazi ngumu tu na shida maana shule ndio ulichofundishwa sio kitu kingine.
Usishangae mwalimu anayesifika sana shule ni yule anayejua kuchapa sio kivingine.
Masikini utaendelea kuwa masikini wewe na familia yako kuna wajinga wameamini elimu ni ufunguo wa maisha hii elimu inayotolewa shule za serikali aisee sio ufunguo wa maisha.
Elimu ya bongo ni UMASIKINI WA MAISHA YA WATANZANIA.