Elimu ya juu sio lazima kwa watanzania serikali yathibitisha

Ndugu yangu nashukuru kwa maoni yako haya.Lakini naomba ukumbuke kwamba sio watanzania wote wana uwezo kama wako,ambao sijui umeupata wapi mpaka unakua na kiburi kiasi hicho.Na hata kama wangekuwa nao, bado serikali ina wajibu wa kushiriki kawa njia moja au nyingine katika elimu ya watu wake.Hata nchi zinazojiita tajiri zinatoa mikopo ya elimu kwa vijana wake,sembuse Tanzania?Wewe unayetoa mawazo hayo potofu, inawezekana umesomeshwa na hela za kifisadi au na Mchonga.Kweli aliyeshiba hamjui mwenye njaa.Lakini la msingi zaidi ni kwamba na kuhurumia kwa vile umeshindwa kabisa kujua ajenda halisi ya tamko hilo.Si shangai lakini kwa vile watanzania walio wengi hatuko diagnostic.

Tikera sijui hukusoma sehemu hii hapa chini katika bandiko langu, au hujaelewa tu.

Kwa kifupi mimi nina advocate a centrist position, ambapo serikali inachukua wajibu kidogo na mwananchi anachukua wajibu kidogo.Hamna upande uanaobeba mzigo wote, kwani serikali yetu ina mambo mengi na wananchi wetu wengi masikini.

Hebu soma tena hapa

Elimu ya juu kwa nchi iliyo na challenges za kufanya resource allocation kama yetu bado ni privilege, itatolewa kwa wachache walioonyesha uwezo au wenye fedha, tuache kuifanya serikali kama baba tajiri ambaye atalipa kila bili yetu.

Na serikali nayo iache ubahili wa ajabu na mifumo ya ukiritimba wa kikoloni katika kusaidia wananchi wasiojiweza kupata elimu ya juu.

Ni katika kufuata misingi hii tu ndipo tunaweza kupata suluhishi la kati, lisiloegemea sana kwa upande wa serikali kubeba mzigo wa gharama zote za elimu, wala kwa mwananchi kubeba gharama zote.

Lazima kuwe na mlinganyo wenye uwiano unaowezesha taifa letu kujikwamua kiuchumi kwa kutumia elimu bila kuipa serikali wala mwananchi mzigo mkubwa isivyostahili.
 
Ndugu wanajamii serikali kupitia naibu waziri wa elimu imethibitisha elimu ya juu sio lazima kwa kila mtanzania kwa sababu serikali haina uwezo wa kusomesha watu wake.

Swali, hali kama ni kweli kwa aliyo sema naibu waziri, hapa si ndio mwanzo wa matabaka ya milele na milele, ambapo tutakuwa na kundi la watawala daima, ambapo mtoto wa masikini hatakuja kutawala nchi hii daima, ingawa nchi hii ni ya kwetu sosote?

Pili hivi ni kweli serikali haina uwezo wa kusomesha watu wake? ninavyojua kunamatumizi mengi yasiyo ya lazima kama warsha na makongamano ambayo hayana tija yoyote kwa nchi hii zaidi ya kuwa njia mbadala wa kipato kwa waheshimiwa.

Sasa kama serikali inaniya yakuendelea yenyewe na kuondoa umaskini kwa wanachi yake, je kweli hili litawezakana kama haitoi kipaumbele kwenye elimu ya juu kwa watu wake.

Sasa na vyuo vikuu vinavyo jengwa kama cha dodoma, wananani watakao kwenda kusoma, na hisi hapa serikali inajichanganya yenyewe, tukumbuke wanachi watanzania wengi hawana uwezo wa kifedha hata kwa mlo wa siku moja, kama serikali hitaki kuwasidia katika kusoma elimu ya juu, hivyo vyuo nivya nini?

Mkuu, hao wakubwa ukifuata kile wanachokisema watakupoteza tu. Ni wewe mwenyewe kuchagua kinachokufaa. Binafsi naongozwa na maxim hii: 'If the theory doesn't fit the practice, ignore the theory.' Elimu kwangu ni ufunguo wa faraja na 'as long as I am alive I'll make sure my children study to university level.'

Kwa hiyo, waseme elimu ya juu siyo lazima au la, kwangu mimi ni lazima. Unafikiri wao wataacha kuwasomesha watoto wao chuo kikuu kweli kwa vile hiyo elimu siyo lazima, si wanatudanganya wewe na mimi tu?
 
Back
Top Bottom