Sikonge
JF-Expert Member
- Jan 19, 2008
- 11,550
- 6,062
Norway, Sweden hizi ni mfano wa nchi ambazo zimendelea, na elimu ya juu ni bure, ni nao ushahidi, kuna marafiki zangu ambao ni watanzania wansoma huko na wanasema elimu huko ni bure
Gosheni,
Hizi habari siku zote huwa mtu unapewa nusunusu au unaelewa na kukumbuka kile unachotaka kukumbuka. Wakati nikisoma , nilifika Sweden na kuelewa system, zao. Kwanza kwa kuanzia ni kuwa wao hawasomi bure ila wanakopeshwa ada na baadaye wanakuja kulipa. Wengi ili kupata shule kwani kwao ni shida na aghali, basi huwa wanakimbilia nchi za Estern Europe hasa masomo ya Uganga na huko wakimaliza, nchi zao zinaitambua hiyo degree kwani imetoka ndani ya European Union. Akianza kazi anaanza kukatwa. Hivyo ndugu yangu hamna cha bure.
Ila kwa Sweden ambako nilifika, jamaa wana system nzuri sana. Kwa mfano masomo ya ufundi (Engineering), haya husoma watu wachache sana na ikibidi hata wakali huletwa kutoka nje. Huko bwana inabidi kweli uwe mkali kwani ukilazimisha YATAKUSHINDA. Sasa hawa Wahandisi tuseme kama 100 wanakwenda kwenye viwanda vya akina Blaupunkt, Volvo, Ericksson, Saab, Scania, nk na hawa kazi yao inakuwa kufanya utafiti na ugunduzi wa vifaa au bidhaa mpya, na wakishafanya hivyo wanaingia kwenye kazi ya kuplan na kutengeneza/kuunda mkanda wa production. Wakishamaliza hapo ndipo wanaita Mafundi mchundo kama mimi na kuanza kuwaonyesha jinsi kila kitu kinavyofanya kazi kwa lugha ya kitaalamu. Wakimaliza hapo sasa wanachukuliwa akina form 4 au darasa la saba, wanafundishwa kazi kila mtu na ki-section chake. Jamaa wanapiga mzigo na anakuwa hajui hata anatengenza nini ila wale technicians na wahandisi. Hivyo ukiangalia ukweli ni kwamba huhitaji kuwa na Wasomi in Quantity ila quality.
Pia wenzetu wana vyuo vingi sana vidogovidogo kwa ajili ya kusomea masomo madogomadogo kama kwenye ukulima, mifugo, nk. Ni kama vyuo vya kilimo Tumbi, Ukiliguru, Ilonga etc. Ila huko wanafanya zaidi practical. Nafikiri kwa Tanzania tunahitaji hii system. Kama zile secondary za Lowassa zingelitakiwa kufanya hii kazi. Kwa mfano huku kwetu Sikonge tungeliletewa vyuo ambavyo vijana wanasomea kilimo cha kisasa, ufugaji wa kisasa na biashara kidogo ili watu wapate mwanga wa hizo shughuli zao na kuweka mahesabu ili kujua anapata hasara au lah.
Last edited: