Elimu ya juu sio lazima kwa watanzania serikali yathibitisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Elimu ya juu sio lazima kwa watanzania serikali yathibitisha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gosheni, Feb 6, 2009.

 1. Gosheni

  Gosheni Senior Member

  #1
  Feb 6, 2009
  Joined: Oct 28, 2008
  Messages: 189
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 60
  Ndugu wanajamii serikali kupitia naibu waziri wa elimu imethibitisha elimu ya juu sio lazima kwa kila mtanzania kwa sababu serikali haina uwezo wa kusomesha watu wake.

  Swali, hali kama ni kweli kwa aliyo sema naibu waziri, hapa si ndio mwanzo wa matabaka ya milele na milele, ambapo tutakuwa na kundi la watawala daima, ambapo mtoto wa masikini hatakuja kutawala nchi hii daima, ingawa nchi hii ni ya kwetu sosote?

  Pili hivi ni kweli serikali haina uwezo wa kusomesha watu wake? ninavyojua kunamatumizi mengi yasiyo ya lazima kama warsha na makongamano ambayo hayana tija yoyote kwa nchi hii zaidi ya kuwa njia mbadala wa kipato kwa waheshimiwa.

  Sasa kama serikali inaniya yakuendelea yenyewe na kuondoa umaskini kwa wanachi yake, je kweli hili litawezakana kama haitoi kipaumbele kwenye elimu ya juu kwa watu wake.

  Sasa na vyuo vikuu vinavyo jengwa kama cha dodoma, wananani watakao kwenda kusoma, na hisi hapa serikali inajichanganya yenyewe, tukumbuke wanachi watanzania wengi hawana uwezo wa kifedha hata kwa mlo wa siku moja, kama serikali hitaki kuwasidia katika kusoma elimu ya juu, hivyo vyuo nivya nini?
   
 2. Elusive

  Elusive JF-Expert Member

  #2
  Feb 6, 2009
  Joined: Nov 26, 2008
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
   
 3. Gosheni

  Gosheni Senior Member

  #3
  Feb 6, 2009
  Joined: Oct 28, 2008
  Messages: 189
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 60
   
 4. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #4
  Feb 6, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Bwana gosheni unayoyaongea YANA MSINGI.
  Si kweli kwamba serikali haina hela YA KUSOMESHA.au kuwekeza kwenye elimu ili kizazi kinachofuuata KIJITEGEMEZE KITAALUMA na wataalamu katika fani mbali mbali ambazo hadi leo hii serikali inaazima wataalamu kutoka nchi zilizoendelea.

  Tungefikiria kuwekeza kwenye taaluma na fani mbali mbali,basi safari za kwenda india kutafuta wataalamu wa upasiaji wa moyo labda zingepungua sana.Na huenda watu wangesafiri kutoka mataifa mbali mbali kwa ajili ya huduma za kitaalamu ZINAZOFANANA NA MFANO HUSIKA HAPO JUU.

  Ninachokiangalia katika fikra na mawazo yangu ni kwamba serikali inashindwa ku-ALLOCATE FUND ya kutosha katika sekta ya elimu,ili walau wafikie mahala watu wasilalamike.

  Au pengine ni MFUMO UNAOTUMIKA HAUKIDHI MATAKWA ya walio wengi.

  AU TUSEME WAZIRI MTOA KAULI HII AMEONGEA KISIASA ZAIDI

  ukweli sielewi elewi jamani

  THERE IS NO FREEDOM TO THE ENEMIES OF REEDOM
   
 5. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #5
  Feb 6, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Naomba kwanza mnitajie nchi zilizoendelea na ambapo elimu ya juu wananchi wote wanasomeshwa bure na serikali. Msinitajie China kwa sababu ni nchi INAYOendelea siyo iliyoendelea. Alafu tuchukue mifano yote tuifanyie discussion na tu-compare with the world's largest economy - USA.
  Mi nadhani elimu ya juu SIYO haki na siyo lazima. Ni muhimu zaidi kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya hasa vulnerable like women and children. Na iwe huduma kweli si kama sasa hivi ya danganya toto. Kama tukiamua ku-invest seriously in health and basic education, only then and only then can we talk about elimu ya juu. Otherwise it is a waste of our resources kupeleka watoto wetu kupata elimu ya juu ambayo haina maana na haina standard katika vyuo vyetu.
   
 6. U

  Ufunuo wa Yohana JF-Expert Member

  #6
  Feb 6, 2009
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 317
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 35
  Ala kumbe! ndiyo maana mimi niliamua kuishia la saba tu na ninaishi vizuri kuliko hata yule wa PHD
   
 7. Gosheni

  Gosheni Senior Member

  #7
  Feb 6, 2009
  Joined: Oct 28, 2008
  Messages: 189
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 60
  Norway, Sweden hizi ni mfano wa nchi ambazo zimendelea, na elimu ya juu ni bure, ni nao ushahidi, kuna marafiki zangu ambao ni watanzania wansoma huko na wanasema elimu huko ni bure
   
 8. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #8
  Feb 6, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Kaitoa jana bungeni...nilimsikia kupitia BBC swahili
   
 9. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #9
  Feb 6, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  U meant developed au sio bwana? nyingi tu uscandinavia ni bure......au labda una maana developing ambapo tanzania nayo haimo....tanzania ni nchi iliyosimama sio inayoendelea.....
   
 10. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #10
  Feb 7, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Mimi nadhani elimu ya msingi na ndiyo haki ya kila mtoto. Ilikuwa hivi hata enzi zile. Elimu ya juu kwa kiasi kikubwa ni kwa faida ya mtu mmoja mmoja na familia/koo zao. Engineers, madaktari, n.k. wangapi wamesomeshwa bure elimu ya juu na kuishia kutafuta Green pastures nje? Ni busara zaidi uwekezaji uelekwezwe zaidi kwenye mabarabara na maji badala ya elimu ya juu.
   
 11. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #11
  Feb 7, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Wakulu huyo wazili wala hakukosea kwani alifuata muongozo sijui kama ni wa katiba ya Sisi. M au Tanzania. Ila ukweli ni kwamba kwa tanzania elimu ya lazima ni mpaka darasa la saba. Hii ipo documented japo sinakumbukumbu ni katika document zipi fuatilieni tupeane updates. Kwahiyo waziri hakukosea. Kimsingi kunamambo mengi sana yanahitaji marekebisho. Kazi kwelikweli.
   
 12. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #12
  Feb 7, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,199
  Trophy Points: 280
  Tuachane na mawazo ya kisoshalisti ya kwamba serikali itatulipia kila kitu. Elimu ya juu si lazima kwa kila mwananchi, na hamna nchi duniani ambayo inafanya elimu ya juu kuwa lazima (elimu ya juu kwa maana ya post secondary higher learning)

  Kufanya elimu ya juu kuwa lazima utakuwa ni udikteta kama ule wa Pol Pot wa kuwaua wasomi wote. Kuna watu wengine wanaamini katika kusoma kutoka katika maisha, sasa utalazimisha hawa waingie vyuoni?

  Aliyeleta maada ama hajaweza kusema alichotaka kukisema au kalewa usoshalisti. Nakubali serikali yetu haiwezi kuacha mzigo wa kusomesha watu uwe kwa wananchi kwa asilimia 100 (hata mabepari wa magharibi wanatoa misaada. Marekani serikali inatoa mikopo na zawadi, Ujerumani elimu ya juu ni bure, lakini si lazima, tuelewe tofauti hata hapo)

  Elimu ya juu kwa nchi iliyo na challenges za kufanya resource allocation kama yetu bado ni privilege, itatolewa kwa wachache walioonyesha uwezo au wenye fedha, tuache kuifanya serikali kama baba tajiri ambaye atalipa kila bili yetu.

  Na serikali nayo iache ubahili wa ajabu na mifumo ya ukiritimba wa kikoloni katika kusaidia wananchi wasiojiweza kupata elimu ya juu.

  Ni katika kufuata misingi hii tu ndipo tunaweza kupata suluhishi la kati, lisiloegemea sana kwa upande wa serikali kubeba mzigo wa gharama zote za elimu, wala kwa mwananchi kubeba gharama zote.

  Lazima kuwe na mlinganyo wenye uwiano unaowezesha taifa letu kujikwamua kiuchumi kwa kutumia elimu bila kuipa serikali wala mwananchi mzigo mkubwa isivyostahili.
   
 13. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #13
  Feb 7, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,199
  Trophy Points: 280
  Tofautisha bure na lazima, hata huko Norske, Sverige na Deutschland usijidanganye kwamba elimu inatolewa "bure". Inawezekana kukawa hamna "tuition fee" lakini wananchi wao wanalipa kwa namna nyingine, kama vile kwa kukatwa kodi kubwa.

  Sisi unemployment / underemployment iko rampant, kwa hiyo hata uzalishaji hatuna, kodi hatulipi, halafu na elimu ya bure tunataka hapo hapo.

  Serikali ikituambia ukweli kwamba elimu ya juu si lazima, na serikali haina uwezo wa kutusomesha wote, tunaona kama tumetukanwa.

  Mimi kawaida niko mbali kabisa na kuitetea serikali, lakini wananchi tunapobweteka katika fikra za katikati ya karne iliyopita inakera na ni lazima niseme.
   
 14. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #14
  Feb 7, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Hapana, Tanzania ni nchi inayorudi nyuma,
   
 15. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #15
  Feb 7, 2009
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  kweli bwana kila wakati bungeni utasikia' Ndiyoooooooooooooooo!!!' kwaaa kwaaaa kwaaa paa paa paaa!!!
   
 16. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #16
  Feb 7, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Nani alikueleza kwamba Tanzania ni nchi yetu sote?. Wenye nchi na walanchi wanajulikana. Kuhusu elimu ya juu ama ya chini hayo ni matatizo ya akina pangu pakavu tia mchuzi, wenye nchi familia zao ni lazima zipate elimu ya juu toka nje ya Tanzania.
  Unachoongea kinasikitisha lakini huo ndio ukweli wenyewe. Enzi za zamani watu walipata nafasi ya kwenda shule bure, kutibiwa bure. Mimi nikiwa moja wapo nilipata bahati hiyo. Daftari likiisha unakwenda kwa mwalimu wa somo unamwonesha na unapatiwa jipya. Unakwenda Hospital yoyote na unatibiwa bure. Wakati ule nchi ilikuwa haichimbi madini na wala haikuwa na utitiri wa viwanda kama leo. Viwanda vilikuwa vinahesabika lakini iliweza kutoa huduma muhimu kwa jamii bure. Kwa dhati ninampongeza hayati Mwl Julius K Nyerere kwa hilo.
  Leo hii nchi inachimba madini, ina viwanda vingi sana, ina wasomi wengi sana katika kila fani lakini kibaya zaidi inashindwa kutoa huduma kama hizo kwa jamii.

  Watanzania ni lazima tujiulize kulikoni?, hata kama ni mabadiliko ya hali ya maisha mbona pengo la matajiri na masikini linazidi kukua kila kukicha?.
  Kwa mtazamo wangu ni kwamba nchi imepoteza dira (mwelekeo) na hakuna anayejali. Tutawaeleza nini wajukuu zetu hapo baadaye watakapokuja kujikuta wakitumikishwa ndani ya nchi yao?. Tuliutafuta uhuru kwa shida sana ili tujitawale lakini cha ajabu tumewaita tena wale tuliowaondoa ili waje kututawala tena. Ninaogopa sana ninapofikiria suala hili. Kwaheri Tanzania
   
 17. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #17
  Feb 7, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mkuu Gosheni hii thread defeats logic ya reasoning.
  Tutofautishe kati ya umuhimu wa elimu ya juu an suala la uwezo wa serikali kusomesha wanafunzi wote wanaostahili kusoma.Hizi ni topics mbili tofauti kabisa na zenye dimensions ambazo kimsingi ni kubwa sana.
  Sitazamii serikali yenye "kichwa" kutoa tamko kama ulivyo liweka kwenye thread yako.Umuhimu wa elimu ya juu si tamko la mtu mdogo kama Naibu wa Waziri wa Elimu.Umuhimu wa elimu ya juu ni sera.Sera ambayo lazima iendane na matarajio ya maendeleo ya kijamii kiujumla.Mtu Mdigo wa wizara ya elimu hawezi kujuisha sera hiyo katika "interview" na redio.
  Suala la uwezo wa serikali ni kitu kingine.
  Watanzania lazima tukubali kuwa serikali iko kwenye mpito wa kujichangaya kwa sasa hivi.
  Watanzania wanatamani kuwa na matarajio ya wasomi wengi tu, hivyo vyuo vikuu vingi sana vimeanzishwa katika muda huu wa miaka 15 iliyopita.
  Katika muda huu miundo mbinu ya kutoa elimu hii ni ileile, walimu(lecturers) ni wale wale, fungu katika bajeti halijaongezeka sana.
  Sasa tutegemee nini?
  Confusion hii ndio migomo na maandamano tunayoyaona kutoka vyuoni.
  Wengi hamuongelei quality ya elimu yenyewe ambayo imeshuka sana.Ushauri wangu kwako mkuu Gosheni,thread yako ni multidimensional.Igawe katika topics tofauti zilizomo na tuzijadili hapa.
   
 18. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #18
  Feb 7, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nashukuru kwamba sasa wamethibitisha wenyewe kawa sababu taarifa hizi tulikuwa nazo kupitia kwenye vyanzo vingine.Wameambiwa iwe hivyo na wakubwa.Mbona sisi tupo kwa ajili ya kuwatumikia wakubwa wa nchi za magharibi.Sasa kwa vile watawala wetu hawajui conspiracies zinazoendelea, wameingizwa mkenge katika kiwango kisichoweza kuelezeka.Na as long as hawa watawala uchwara wapo, mwisho wetu ni extinction.We are an endangered species!

   
 19. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #19
  Feb 7, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu nashukuru kwa maoni yako haya.Lakini naomba ukumbuke kwamba sio watanzania wote wana uwezo kama wako,ambao sijui umeupata wapi mpaka unakua na kiburi kiasi hicho.Na hata kama wangekuwa nao, bado serikali ina wajibu wa kushiriki kawa njia moja au nyingine katika elimu ya watu wake.Hata nchi zinazojiita tajiri zinatoa mikopo ya elimu kwa vijana wake,sembuse Tanzania?Wewe unayetoa mawazo hayo potofu, inawezekana umesomeshwa na hela za kifisadi au na Mchonga.Kweli aliyeshiba hamjui mwenye njaa.Lakini la msingi zaidi ni kwamba na kuhurumia kwa vile umeshindwa kabisa kujua ajenda halisi ya tamko hilo.Si shangai lakini kwa vile watanzania walio wengi hatuko diagnostic.

   
 20. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #20
  Feb 7, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Gosheni,

  Mbona alichosema huyo naibi waziri ni sahihi kabisa? Hakuna nchi hapa duniani ambayo ina uwezo na nia ya kusomesha watu wake wote mpaka elimu ya juu.

  Efficiency kwenye society yoyote inategemea diversity ya watu wake. Inatakiwa kuwe na wasomi wa vyuo vikuu kama madaktari, walimu, wanasheria, wachumi nk lakini pia mafundi mchundo, makuli, wabeba box nk. ambao hawahitaji elimu ya juu ili kuweza kufanya kazi zao kwa ufanisi.

  Inatakiwa tutumie pesa nyingi kuongeza uwezo wa VETA, secondary schools ili wananchi wetu wawe na at least basic education inayoweza kuwafanya wafanye kazi zao kwa ufanisi.

  Pia elimu nzuri ni ile inayomwandaa mwananchi kuwa tayari kupambana na mazingira yake, kwa mfano mkulima kuwa na uwezo wa kuongeza ufanisi kwenye kilimo nk.

  Nchi zilizoendelea wananchi waliosoma mpaka level ya vyuo vikuu hawazidi asilimia 50. Kwa mfano UK, Labaour walitaka at least asilimia 50 ya vijana waende vyuo vikuu, ahadi hiyo imeshindwa vibaya na matokeo yake zimeanzishwa baadhi ya courses ambazo hazina maana kabisa. Baadhi ya Wanafunzi wakimaliza wanakuwa useless na bila kuwa na ujuzi wa kuweza kuwasaidia kupambana na maisha. Je tunataka elimu za namna hiyo?

  Kwa Tanzania kama tutafikia 30% ya vijana wetu kufikia level ya university itakuwa hatua kubwa sana. Wanaobaki wanaweza wanaweza kugawanyika katika makundi mbalimbali kuanzia elimu ya kati mpaka wale ambao hawana formal education.
   
Loading...