Elimu ya hesabu katika jamii yetu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Elimu ya hesabu katika jamii yetu.

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Fundi Mchundo, Mar 15, 2008.

 1. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Hivi hii ni kwa wanafunzi peke yao? Kama walimu wenyewe wanakacha kufundisha hili somo GUMU, tunategemea nini kutoka kwa wanafunzi? Wahindi hivi wamefanikiwa vipi maana inaelekea kule wanatoa wataalamu wengi wa hisabati? Ikiwa jamii yenyewe, kuanzia wazazi na ndugu zake, inamueleza huyu mwanafunzi kuwa hili ni somo gumu ataacha kulikimbia? Pengine kuna haja ya kuangalia sera nzima ya elimu na namna mwanafunzi anavyopata elimu kuanzia chekechea. Kuna nchi nyingine walimu hufundisha masomo yote na anaenda na darasa analolifundisha kuanzia darasa la kwanza mpaka hapo wanapoingia ngazi nyingine ( sekondari n.k.). Hii inamuwezesha kuunganisha somo la hesabu na masomo mengine na kumfanya mwanafunzi kuliogopa kama somo maana anaona kuwepo kwake katika hayo masomo mengine anayoyamudu. Na mwalimu vilevile anaweza kujua udhaifu na nguvu za wanafunzi wake across the board! Inakuwa rahisi zaidi kujenga confidence ya mwanafunzi ambaye ni mzito katika hisabati kwa vile unajua ni mkali wa historia. Pengine hii itasaidia. Na kwa vile walimu watalazimika kufundisha masomo yote, hapatakuwa na hii kasumba ya kuspeshelaiz kuanzia mwanzo. Cha msingi ni kumfundisha mwanafunzi apende elimu, awe mdadisi na asiogope challenges. Mkazo wetu kwenye hii speshelaizesheni na kufundisha kwa rota kunachangia kwa kiasi kikubwa kwenye hali hii.


  Darasa la wanafunzi 40-45 bado ni kubwa mno kwa mwalimu kumudu. Idadi ya juu kabisa naamini kuwa ni 30 ingawa kwa wenzetu hata 25 inaonekana kuwa ni kubwa. Pamoja na kuangalia ukubwa wa madarasa ni muhimu vile vile kuangalia ujenzi na 'design' ya hizi shule. Shule zijengwe zikizingatia mazingira bora ya kufundishia. Madarasa yawe na mwanga wa kutosha ( natural light) hewa ya kutosha na salama ( sio kuweka magrili kila mahali kiasi kwamba pakitokea moto watoto wanakosa pa kukimbilia) na rangi za kuvutia. Pawe na uhusiano na mazingira ya nje, nchini kwetu matumizi ya courtyards yangesaidia na kadhalika na kadhalika. Vyote hivi haina maana ya kuongeza gharama bali ni kubadilisha mtizamo wetu na kuipa kweli heshima inayostahili sekta hii muhimu.

  Kwenye hili la mwisho, sina matumaini makubwa ukiangalia jinsi hata hotuba yenyewe ilivyokuwa deputised, kutoka kwa waziri, katibu mkuu, mkurugenzi hadi mkurugenzi msaidizi! wote wakubwa hawakuona umuhimu.
   
 2. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #2
  Mar 15, 2008
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  KWA KWELI SOMO HILI KATIKA JAMII YETU LIMETELEKEZWA. SI WALIMU,WAZAZI,WANAFUNZI NA JAMII KWA UJUMLA WAKE TUMELITUPA SOMO HILI....NI RAHISI LEO JAMII KUTETEA MUDA WANAOTUMIA VIJANA WETU KTK KUTUNGA MISTARI(bongoflava) BADALA YA KUHIMIZA MATUMIZI NA MAZOEZI ZAIDI YA SOMO HILI...
  walimu
  IMEKUWA NI JAMBO LA KAWAIDA KWA WALIMU KUWAKOMOA WALE WASIOJUA HESABU BADALA YA KUWASAIDIA NA KUWAJENGA WALIPENDE SOMO LENYEWE....VIPINDI VYA SOMO HILI VIKIKUTANA NA MWALIMU MKATISHA TAMAA VINAFANYA MWANAFUNZI AICHUKIE SHULE....
  [Uwanafunzi
  wanafunzi nao hufuata sana mob psychology ...kwani darasa linapochukia hesabu hukuta hakuna hata mmoja anayejibidisha....hasa wa kike ambao wamejitengea combinations zao HG...SOMETHING....!
  wazazi
  wazazi hawana muda wa kuwahimiza watoto wao badala yake matokeo mabaya yakija wanaogopa kuwaadhibu vijana wao ati watajinyonga na kubaki kuwaambia SHAURI YENU...!
  jamii
  jamii inapaswa ikiri kuwa imekosea na kurudi upya(REVIVAL) tuanze kujenga tabia ya ku-reward kuhusu hesabu, hata sisi watu wazima tuangalie ni wapi tuliaguka tukatubu(KAMA ULIACHA HESABU TOKA FORM TWO ANZA KUJIFUNZA TARATIBU KUANZIA HIZO ULIZOZIACHA NA KUENDELEA...NK)

  TUKIAMUA TUNAWEZA....THIS IS TANZANIA....NIA TUNAYO...NGUVU TUNAZO...UWEZO TUNAO....!
  [/B][/B][/U][/B]
   
 3. Bin Maryam

  Bin Maryam JF-Expert Member

  #3
  Mar 15, 2008
  Joined: Oct 22, 2007
  Messages: 685
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  FM:

  Kwani kuna masomo gani ambayo watanzania wana-excel? Hisabati ni barometer. Kama kuna upungufu katika somo hilo basi kutakuwa na upungufu katika masomo mengine.

  Sababu ni nyingi. Lakini chanzo kikubwa ni utekelezaji mbaya wa mpango wa UPE. UPE ulitekelezwa kwa kuzingatia wingi na sio ubora. Vilevile mpango mzima ulihimiza kujua kusoma na kuandika na kuachia stadi zingine ambazo ni muhimu katika kupata maarifa.
   
 4. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #4
  Mar 15, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Bin Maryam,
  Ndiyo maana nimesema tuangalie mfumo MZIMA wa elimu. Tatizo ni kubwa kuliko hisabati. Naamini ni mtazamo wetu kama jamii kwenye suala hili la elimu. Ni kama vile kwenye mjadala wa nyumba. Badala ya kuangalia suala zima la makazi kwa WOTE tunashupaliana kuhusu nyumba zisizozidi 500 katika nchi ya watu milioni 35! iko kazi.
   
 5. Bin Maryam

  Bin Maryam JF-Expert Member

  #5
  Mar 15, 2008
  Joined: Oct 22, 2007
  Messages: 685
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  FM:

  Kwenye mjadala mmoja kuna jamaa (Mkandara) alisema Nyerere alianzisha vyuo vikuu lakini Mwinyi na Mkapa walishindwa. Na ukamjibu kuwa kuanzisha ni rahisi kuliko kuendeleza. Na ulikuwa sahihi kabisa.

  Kuna mambo tunayoweza kuyafanya. Kitu cha kwanza ni kuangalia ku-identify masomo muhimu. Masomo muhimu ni zana za mwanafunzi kujifunza masomo mengine. Masomo hayo ni Lugha na stadi za hisabati. Mtoto akichakuwa na ustadi katika masomo hayo, masomo mengine atajifunza kwa urahisi.

  Miaka ya nyuma kulikuwa na imani kuwa mwanafunzi atakayemaliza darasa awe na uwezo wa kurudi kijiji na kufanya kazi kwa kutumia elimu yake kuishi maisha bora na ya uzalishaji. Ukweli wa mambo tunauona ni kuwa wanaomaliza elimu ya msingi wana umri mdogo kuwapa majukumu ambayo watu wazima wanashindwa kuyafanya.

  Hivyo elimu ni lazima iendane na umri. Hata elimu ya jadi haikupeleka mtu jandoni kabla ya umri wake. Kwa mtaji huu elimu ya msingi ibaki kuwa elimu ya msingi na majukumu yake yawe kutoa stadi za kujifunza.

  Katika hoja zako unasema ni lazima tu-define vitu vinavyotufanya kuwa watanzania. Kuna nchi dunia zimeenda zaidi ya hapo kwa kuangalia nafasi yao katika dunia. Mfano mmoja ni Singapore, nchi hii ina idadi kubwa ya watu kwa eneo na nchi ndogo na walichohamua ni kushindana na kuinua uchumi wao kwa kutumia akili. Na kutokana kile walicho-define miaka ya 60, mitaala yao ya shule hiko very clear. Kwa mfano math na lugha ni vitu muhimu sana kwa shule za msingi kuliko masomo mengine. Kwa sababu wanaelewa kuwa ukishaelewa masomo hayo vizuri, masomo mengine hayatampa taabu mwanafunzi baadaye.

  Na sisi tulio-define kuwa nchi yetu ina mabonde mengi yenye rutuba na madini tupo pale, pale tulipo.
   
 6. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #6
  Mar 15, 2008
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  TUANZE KUWAJENGEA WATOTO WETU MSINGI WA HESABU.....KAMA JINSI ILIVYOKUWA ENZI ZETU KILA MZAZI HUSEMA YEYE WAKATI ANASOMA ALIKUWA AKISHIKA NAMBA MOJA DARASANI........! SIJUI NANI ALIKUWAGA WA MWISHO......HII ILTUPA COURAGE TUJITAHIDI DARASANI KAMA BABA/MAMA ALIVYOKUWA ANAONGOZA ENZI ZAKE....!
  JAMII JE TUKITUMIA NJIA HII (uongo mtakatifu) HATUWEZI KWA ASILIMIA FULANI KUSAIDIA KUINUA KIWANGO CHA HESABU....?
  ""mimi wakati nasoma nilikuwa sikosi hesabu....hata walimu waliniambia utakuwa na watoto wanaojua sana hesabu.....""
  ""kati ya masomo ninayoyapenda hesabu ni namba moja""
  ""enzi zangu wakati mwalimu anaandika swali la hesabu ubaoni mimi tayari nilikuwa nimepata jibu"

  MANENO KAMA HAYA NA MENGINEYO YANAWEZA KUCHANGIA KWA KIASI KIKUBWA KUJENGA MSINGI MZURI WA KUIPENDA HESABU KWA WATOTO WETU....!
  SHUKRANI KWA mwl.wangu wa hesabu kwa ushawishi WAKE kwa wanafunzi kuipenda hesabu (mwl.JACKSON KATONGE)
   
 7. Kubwajinga

  Kubwajinga JF-Expert Member

  #7
  Mar 16, 2008
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,190
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  FM,
  Nakubaliana na wewe kabisa juu ya umuhimu wa hisabati. Hisabati ndio msingi wa elimu. Hata hivyo, tunaweza kuilaumu UPE, lakini UPE ni sehemu ndogo sana ya tatizo na ilipita wakati wake kipindi kirefu kilichopita. Shida kubwa kwa taifa letu ni la resources kutotumika kwa ajili ya hapo baadaye, bali hutumika kama zima moto, leo leo mawazo ya kesho ni kama hayapo.

  Kama tunataka kuboresha elimu yetu, inabidi tu-focus kama miaka 10 na zaidi ijayo na kuanza kuandaa misingi bora hivi sasa. Kikubwa cha kuanza kuandaliwa ni waalimu bora maana ndio rahisi kuliko infrastructure, lakini tumewachuna wananchi kujenga substandard classes ambayo hayana waalimu. WBank hivi sasa wamemwaga pesa kibao kurekebisha mfumo wa elimu ya msingi na sekondari lakini nina uhakika matokeo yake yanaweza yasiwe mazuri kwa vile hakuna msisitizo kwenye hili kwa serikali hii ya JK. Hili sio suala kubwa la ajenda yake hivi sasa.

  Kama idadi ya waalimu bora haitaongezeka, hisabati na elimu kwa ujumla itakuwa ni ndoto kwa TZ maana hisabati zinahitaji waalimu wazuri na sio wababaishaji. Waalimu wazuri wanaifanya hisabati kuwa enjoyable kwa wanafunzi.
   
 8. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #8
  Mar 16, 2008
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  KUSAIDIA SOMO LA HESABU INABIDI WALIMU WALIOPO NA TARAJALI WAPIKWE KWA MBINU MPYA NA ZA WENZETU WALIOFANIKIWA KTK SOMO HILI KUTOKA NCHI MBALIMBALI....!
  TUKITUMIA MTINDO WA GUEST SPEAKERSMASHULE YAJARIBU KUPATA WATAALAMU WA HESABU KUTOKA SEHEMU TOFAUTI......!
  HATA IKIWEZEKANA KTKT NCHI AMBAZO TUMESHIBANA NAZO.....KAMA JAPAN,URUSI,CUBA..NK!(sio mawazo ombaomba)AMBAPO MARA KWA MARA WAMEKUWA WAKITULETEA MA-EXPERT TOFAUTI KAMA INJINIA,MADAKTARI..NK SASA WATULETEE WALIMU WA HESABU......!
   
 9. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #9
  Mar 23, 2008
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Na Mafunzo Ya Kujiendeleza Kuhusu Somo Hili Yapewe Kipaumbele
   
 10. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #10
  Jun 17, 2008
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  maabara za hisabati ziongezwe....!
   
Loading...