Elimu ya Ester Bulaya ina shaka kama ya Mwigulu Nchemba

Dec 25, 2016
63
83
9fc63c3ba40bd1327acec4d6a01e23b3.jpg
 
Shaka yako ni nini hasa?

Maana hata tukirejea CV yake uliyoibandika kinafiki hapa inajieleza kwa ufasaha kabisa i.e;

Kidato cha nne > Kidato cha sita > Diploma yake ya mambo ya habari?

Nahisi wewe unadhani elimu isiyo na "shaka" kwa mujibu wako ni mpaka mtu uwe na shahada 1,2 ama 3 na hata nne kama "Mtukufu", lakini output tokana na elimu yake ni zero kubwa!!!

Au una shaka na jina lake kwamba ni la kuiba kama la huyo mwingine unayetaka kumlinganisha naye?
 
Asigwa, unako enda sio niya yako ni kuupunguzia makali uzi huu adimu, mbona hukusema, alivo ingilia jimbo la Mzee wa watu, na kumpokonya ubunge, je wakati huo hakuingilia maswala ya wanaume wakati yeye mwanamke?
 
Enyi vichaa wa Lumumba mliorogwa na aliyewaroga keshakufa acheni siasa za majitaka!
Huyu mzee wenu Wa -hasira a.k.a Tyson naona anawapotosha sana kwa hizo bk7. Bi Esther Bulaya kabla hajahamia CHADEMA alikuwa Mbunge wa kuteuliwa kwa tiketi ya CCM. Je, inakuwaje CV yake iwe imeshuka baada ya kuhamia CHADEMA?
Hii ni dalili ya mtu kufa maji, yaani hata unyasi ataungangania ili asizame! Wassira ameshakunywa maji tayari hivo kwa sasa anatapatapa lakini kwishne!!!
 
Sifa ya kuwa mbunge in kujua kusoma na kuandika. Hii CV hatuihitaji. Swali lingine tafadhali kama lipo kumhusu Bulaya. Kama halipo tuendelee na PhD ya Mkuu.

Hebu Lumumba watuletee CV ya Kibajaji(Johnstone Lusinde -Mtera) na Profesa Majimarefu-Korogwe Vijijini tuone nani msomi wakilinganishwa na Esther!!!!
 
sifa za ubunge ni
a)kujuj kusoma na kuandika kiswahili na kiingereza
b)kuwa na miaka 21 na zaidi
c)kuwa mwanachama wa chama cha siasa chenye usajiri wa kudumu
d)kuwa na akili timamu
e)kutokuwa na historia ya kuwa na kosa la jinai
nje ya hapo ni mbwembwe!
 
Shaka yako ni nini hasa?

Maana hata tukirejea CV yake uliyoibandika kinafiki hapa inajieleza kwa ufasaha kabisa i.e;

Kidato cha nne > Kidato cha sita > Diploma yake ya mambo ya habari?

Nahisi wewe unadhani elimu isiyo na "shaka" kwa mujibu wako ni mpaka mtu uwe na shahada 1,2 ama 3 na hata nne kama "Mtukufu", lakini output tokana na elimu yake ni zero kubwa!!!

Au una shaka na jina lake kwamba ni la kuiba kama la huyo mwingine unayetaka kumlinganisha naye?
Swali la msingi mkuu ni kuwa Je wanabunda walipata nini kutoka kwa mwanagombe!! aliyelimiliki jimbo kama mali yake!!
 
Baada ya kushindwa kesi na rufaa ya kwanza naona sasa mmekuja na 'rufaa ya pili'. Angalizo ni kuwa hizi 'mahakama za wananchi' zina wenyewe nyie hamziwezi!
 
Hebu Lumumba watuletee CV ya Kibajaji(Johnstone Lusinde -Mtera) na Profesa Majimarefu-Korogwe Vijijini tuone nani msomi wakilinganishwa na Esther!!!!
Na yule mwingine wa Iringa anayeitwa Jaha Pipo....Aliyeonekana akicheza ngoma hadharani baada ya kupitishwa sharia kuwa kiwango cha elimu anachotakiwa Mbunge kuwa nacho ni KUSOMA na KUANDIKA...
 
Back
Top Bottom