Elimu ya bure kwa wale 'Washamba' tu na wenye 'Chuki' na Goli 'halali' kabisa la Simba SC dhidi ya Azam FC huko Songea katika ( ASFC ) leo

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,544
108,865
Nianze Kwanza kwa Kumshukuru Mchambuzi 'mahiri' wa Mpira kutoka Clouds FM Kipindi chao cha Michezo cha Sports Extra Farahani (Farhan) Kihamu kwa Ufafanuzi wake ulioenda Shule (Kidato)

Na nikiri kuwa 100% ya kile nitakachokiandika hapa nimekitoa Kwake Mchambuzi huyu Farahani Kihamu na siyo Kwangu GENTAMYCINE ila nami pia naileta hii Elimu wengine pia (hasa Mashabiki Washamba na Mbumbumbu ) wa Yanga SC nanyi muipate na mbadilike.

TUKIO LA LEO SIYO JIPYA NA LIMESHATOKEA
Kilichofanywa leo na Mchezaji Mwerevu na Wakili wa Kujitegemea Bernard Morrison akiwa na Simba SC ikicheza na Azam FC siyo kipya duniani bali kilishatokea pia katika Mechi za Tottenham Hotspurs dhidi ya Aston Villa na Liverpool FC dhidi ya Barcelona ambapo Wachezaji Harry Keane na Trent Alexander Anorld walizifungia Timu zao husika.

KWANINI KISHERIA GOLI LA LUIS MIQUSSOINE NI HALALI KABISA?
Katika moja ya Kanuni (Sheria) ya Faulo kama iliyotokea kuna Kipengele kinaitwa 'Quick Play' ambacho kinampa uhalali Mchezaji aliye karibu na Mpira eneo lililotengwa na Mwamuzi Kuuanzisha haraka hata bila ya ruhusa ya Mwamuzi.

Kwa Tanzania ni Kitu kipya ila kwa Wachezaji Werevu (Geniuses) kama Bernard Morrison ambaye pia ameshacheza Ligi Bora, Kubwa na iliyoendelea sana ya PSL huko nchini Afrika Kusini alikuwa anaijua na ndiyo leo kaitumia na Kuisaidia Simba SC yake Kuibuka na Ushindi muhimu na wa halali.

WALICHOKOSEA WACHEZAJI WA AZAM FC KWA MWAMUZI NI HIKI
Mara baada tu ya Faulo ( Rafu ) ile kutokea walichopaswa kwa uharaka ule Kukifanya Wachezaji wa Azam FC ni Kwanza Mmoja wao Kumzonga Mpigaji wa Faulo ( hasa kwa mbele) ili asipige huku Wachezaji wengine wakiendelea Kujipanga na siyo Kushangaa na Kubung'aa hovyo kama Wachezaji wa Azam FC kisha Goli halali (la Miquissone) likifungwa wanaanza Kulialia huku wakitafuta Huruma kutoka kwa 'Washamba' Wenzao Mashabiki wa Yanga SC.

KWANINI MWAMUZI (REFEREE) YUKO SALAMA KIMAAMUZI HASTAHILI LAWAMA?
Ni kwamba hata Yeye ( Mwamuzi ) anaijua vyema tu hii Sheria ya 'Quick Play' na ndiyo maana alipoona Simba SC wameshapata Goli huku Yeye akiwa bado anazozana na Wachezaji wa Azam FC wakati akitaka Kuwapanga waweke Ukuta huku akijua kuwa Kanuni Kuu ya FIFA ni acha Mpira uchezwe hakukona sababu ya Kunikataa Goli ukizingatia limeanzia kwa 'Genius' Morisson na aliyefunga pia nae ni 'Genius' Mwenzake Simba SC Fundi Luis Jose Miquissone.

Msipoelewa hapa hamtoelewa tena...!!
 
we jamaa mbona Kuna wakati huwa unaanzisha mada nzuri,ila kitakacho kuvurugia hiyo mijineno yako,usiwadharau wenzio kiasi hicho,wewe Mimi nakufatilia Sana thread zako,na huwa nazipenda na Mimi ni mwana yanga haswa,ila unapo insult,au kuonyesha dharau iliyo pitiliza sio,wewe GENTAMYCINE,Hilo lizingatie,nilikuwepo songea game nimeliona ndio narudi zangu nakoelekea,pande za kifanya-njombe, night kwa night,huku songea Kona zipo asee
 
Kitu ambacho mpira wa Tanzania hautakaa uendelee ni pale Simba anapofanya makosa hakuna mshabiki wa Simba atakubali kwamba lile ni kosa atatumia nguvu kubwa ikiwemo matusi ili kutetea uongo, na hii pia ipo kwa mashabiki wa Yanga wakifanya kosa mashabik watatumia nguvu kubwa kuwatetea huu ndo mpira wa Tanzania ulivyo
 
Tatizo mmezoea soka la ndondo.Maguvu mengi,mbio hadi unauacha mpira nyuma akili kisoda.Sheria za soka hamjui.
Mnapoambiwa Simba ni chuo kikuu cha soka muwe mnaelewa.
Kitu ambacho mpira wa Tanzania hautakaa uendelee ni pale Simba anapofanya makosa hakuna mshabiki wa Simba atakubali kwamba lile ni kosa atatumia nguvu kubwa ikiwemo matusi ili kutetea uongo, na hii pia ipo kwa mashabiki wa Yanga wakifanya kosa mashabik watatumia nguvu kubwa kuwatetea huu ndo mpira wa Tanzania ulivyo
 
Ni uhuni tu. Mpira wa Faulo ya Morrison ulitoka nje ya uwanja hivyo kwa namna yoyote ile ni lazima mwamuzi ahusike kuuanzisha. Msifananishe hii ya leo na scenarios nyingine.

Umeona wapi Mpira wa Direct free kick kuwa judged kwamba umetoka nje ya Uwanja? Kwahiyo ulipaswa kuamuliwa kuwa mpira wa kurushwa au Corner sio?
Kama hujui kitu bora nyamaza.
 
Write your reply...lile sio goli halali, hata refa hakuona mahali mpira ulipoanzia, alikuwa bize kuzozana na azam, tuache ushabiki refa amefanya makosa kukubali goli la kijinga vile
 
Nianze Kwanza kwa Kumshukuru Mchambuzi 'mahiri' wa Mpira kutoka Clouds FM Kipindi chao cha Michezo cha Sports Extra Farahani (Farhan) Kihamu kwa Ufafanuzi wake ulioenda Shule (Kidato)

Na nikiri kuwa 100% ya kile nitakachokiandika hapa nimekitoa Kwake Mchambuzi huyu Farahani Kihamu na siyo Kwangu GENTAMYCINE ila nami pia naileta hii Elimu wengine pia (hasa Mashabiki Washamba na Mbumbumbu ) wa Yanga SC nanyi muipate na mbadilike.

TUKIO LA LEO SIYO JIPYA NA LIMESHATOKEA
Kilichofanywa leo na Mchezaji Mwerevu na Wakili wa Kujitegemea Bernard Morrison akiwa na Simba SC ikicheza na Azam FC siyo kipya duniani bali kilishatokea pia katika Mechi za Tottenham Hotspurs dhidi ya Aston Villa na Liverpool FC dhidi ya Barcelona ambapo Wachezaji Harry Keane na Trent Alexander Anorld walizifungia Timu zao husika.

KWANINI KISHERIA GOLI LA LUIS MIQUSSOINE NI HALALI KABISA?
Katika moja ya Kanuni (Sheria) ya Faulo kama iliyotokea kuna Kipengele kinaitwa 'Quick Play' ambacho kinampa uhalali Mchezaji aliye karibu na Mpira eneo lililotengwa na Mwamuzi Kuuanzisha haraka hata bila ya ruhusa ya Mwamuzi.

Kwa Tanzania ni Kitu kipya ila kwa Wachezaji Werevu (Geniuses) kama Bernard Morrison ambaye pia ameshacheza Ligi Bora, Kubwa na iliyoendelea sana ya PSL huko nchini Afrika Kusini alikuwa anaijua na ndiyo leo kaitumia na Kuisaidia Simba SC yake Kuibuka na Ushindi muhimu na wa halali.

WALICHOKOSEA WACHEZAJI WA AZAM FC KWA MWAMUZI NI HIKI
Mara baada tu ya Faulo ( Rafu ) ile kutokea walichopaswa kwa uharaka ule Kukifanya Wachezaji wa Azam FC ni Kwanza Mmoja wao Kumzonga Mpigaji wa Faulo ( hasa kwa mbele) ili asipige huku Wachezaji wengine wakiendelea Kujipanga na siyo Kushangaa na Kubung'aa hovyo kama Wachezaji wa Azam FC kisha Goli halali (la Miquissone) likifungwa wanaanza Kulialia huku wakitafuta Huruma kutoka kwa 'Washamba' Wenzao Mashabiki wa Yanga SC.

KWANINI MWAMUZI (REFEREE) YUKO SALAMA KIMAAMUZI HASTAHILI LAWAMA?
Ni kwamba hata Yeye ( Mwamuzi ) anaijua vyema tu hii Sheria ya 'Quick Play' na ndiyo maana alipoona Simba SC wameshapata Goli huku Yeye akiwa bado anazozana na Wachezaji wa Azam FC wakati akitaka Kuwapanga waweke Ukuta huku akijua kuwa Kanuni Kuu ya FIFA ni acha Mpira uchezwe hakukona sababu ya Kunikataa Goli ukizingatia limeanzia kwa 'Genius' Morisson na aliyefunga pia nae ni 'Genius' Mwenzake Simba SC Fundi Luis Jose Miquissone.

Msipoelewa hapa hamtoelewa tena...!!
Sitegemei shabiki wa Simba atapinga ila kama ingekuwa ni kati ya Simba na Yanga basi UKUTA ungepangwa.
 
Kitu ambacho mpira wa Tanzania hautakaa uendelee ni pale Simba anapofanya makosa hakuna mshabiki wa Simba atakubali kwamba lile ni kosa atatumia nguvu kubwa ikiwemo matusi ili kutetea uongo, na hii pia ipo kwa mashabiki wa Yanga wakifanya kosa mashabik watatumia nguvu kubwa kuwatetea huu ndo mpira wa Tanzania ulivyo
Toka lini Yanga SC Fans wakawa Brainy?
 
Ndio maana yanga hatupendagi kufunga magoli ambapo baadae tutahitaji kuja na simulizi ndefu,piga bao kama la Yacouba Sogne hutokuja na mikeka ya maelezo hapa Jf,tarehe 23 mkija kutegemea "faulo janja janja" mtaacha uharo taifa
Hongereni kwa ushindi,japo wengi wenu hamjaufurahia,basi mnajikaza tu
 
Unateseka ukiwa wapi eti?
 
Back
Top Bottom