Elimu ya awali Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Elimu ya awali Tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MZAWATA, Jun 29, 2011.

 1. M

  MZAWATA JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 555
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Taifa lolote lile duniani lenye mafanikio huwa linawekeza katika elimu ya awali (Early Childhood Education) kwan huo ndo msingi ambao unahitaji umakini wa hali juu katika maendeleo ya nchi yeyote ile. Nchi kama Italy, USA, England,Nigeria,Ghana, South Africa n.k hiz ni nchi ambazo zimejaribu kuonesha mfano katika kuwekeza elimu ya awali (watoto). Serikal yetu kwa kias kikubwa imejisahau sana katika eneo hili,imejikita zaid katika maeneo mengine, sina nia ya kuponda jitihada za serikali kuwekeza katika maeneo mengine la hasha! najaribu tu kuwakumbusha watanzania na serikali kwa ujumla juu ya umuhimu wa elimu ya awali kwa mustakabadhi wa baadaye wa taifa letu. Serikal iliondoa kozi ya Elimu ya awali katika vyuo vya ualimu labda kwa kukosa wataalamu (walimu) wa kufundisha kozi hizo, basi huu ni wakati muafaka wa kuzirudisha kozi hizo ukizingatia kwamba wapo wataalamu wa elimu ya awali wanaomaliza mwaka huu mwezi juni pale chuo kikuu cha Dodoma na pia mwaka ujao katika chuo Kikuu cha Dar es salaam. Njia pekee ya kujikomboa na matatizo ya kuwa na taifa lenye watu wabinafsi, wezi, mafisadi n.k ni kuanza kuwajenga watoto wetu tangu wakiwa wadogo kuchukia masuala haya, na tutaweza hili kama tutakuwa na wataalamu wa kuandaa watoto hawa kwa kushirikiana na jamii nzima ya watanzania. Naisihi sana serikal kuhakikisha inawekeza kwa watoto wetu ili kuwa na Taifa la baadae lenye mustakabadhi mzuri. Wizara ya elimu ina wajibu wa kuhakikisha suala hili linafanyiwa kazi kwa manufaa ya wanachi wa tanzania, taifa letu linaangamia kwa kuwa haya ndo matokeo ya tulichopanda, Waziri wa Elimu tunatarajia atakaposoma bajeti yake ya mwaka huu wa fedha 2011/2012 atasemea kuhusu mkakati wa serikali wa kuiniua Elimu ya awali. Asanteni sana Watanzania Wenzangu naomba kuwasilisha kwaajli yamjadala
   
Loading...