Elimu ya alama lugha ya alama itolewe katika kila ofisi ya Umma

elicklucas1

New Member
Jul 15, 2024
1
0
Kero moja wapo inayo wakumba watu wenye ulemavu wa kutosikia yani viziwi katika ofisi za Umma au atawatu binafsi ni ubaguzi wa kutoelewana.

Unakuta kiziwi anahitaji huduma ila wahudumu wanashindwa kuelewana nao na kutokana na wingi wa watu wanamua kuwatelekeza na kuwambiaa wasubiri huku wengine hupewa huduma kitu ambacho sio haki kwao.

PIa kero nyingine ni kuona viongozi wa watu wenye ulemavu wa kutosikia wakitumia pesa ambazo ni malumu kwa kuwainua Viziwi kiuchumi kwa sababu viziwi wanashindwa kutetea haki zao kwa sababu ya hali ya usikivu.

Pia hudharaulika kwa sababu ya elimu duni ninaomba mamlaka husika na serikali iangalie hili na itoe elimu ya lugha ya alama katika kila ofisi ya umma ikiwemo hospitali, police mahakamani ili kujenga mazingira rafiki ya kupata huduma bora za kijami kwa usawa wa kijinsia.

Imekuwa kero kubwa sana kuona viziwi wanabaki nyuma sana katika Jamii na Serikal inatoa pesa nyingi ila atujui zinako kwenda naomba Serikal ifatilie kero hii na kuitatua imekuwa kikwazo sana.

Soma pia: Serikali iongeze zaidi wataalamu wa elimu maalum ya lugha za ishara na alama
 
Back
Top Bottom