Elimu ya afya ya uzazi pekee ndio nguzo kuu katika utatuzi wa mambo haya!

Hamza Nsiha

JF-Expert Member
Jul 25, 2022
208
191
Ndugu, wanaJamiiForums nimatumaini yangu mu bukheri wa afya. Leo ningependa kuwashirikisha katika mjadala huu juu ya masuala mbalimbali ambayo yameshamiri kwa kiasi kikubwa kiasi kwamba hakuna tena mtu ambaye anajaribu kuweka jitihada katika kukemea masuala hayo.

a) Mpaka sasa, kuna ongezeko kubwa la watu wanaoshiriki ngono za jinsia moja (gay and lesbian)
b) Uraibu wa kuangalia filamu za ngono (ponographic contents)
c) Michezo ya kujichua. ( masturbation)
d) Shughuli hatarishi za kingono (prostitution)

Ukweli ni kuwa, mambo haya yameonekana kama mambo ya kawaida. Mfano mzuri ni kuhusu ripoti ya BBC iliyosema kuwa nchi nyingi zenye sheria ngumu dhidi ya vijana kutojihusha na ngono mpaka pale watakapoingia katika ndoa, ndizo zilizoonesha kuwa na idadi kubwa ya watu wenye uraibu wa kuifuatilia maudhui ya picha au video za ngono.

Mpaka sasa, hakuna tafiti za kisayansi zilizokamilika kuhusu madhara ya kujichua au kupiga punyeto, zaidi tu wataalamu wanasema punyeto haina madhara endapo haitoathiri shughuli za kila siku za mtu anaefanya jambo hilo.

Pia, makundi ya watu wa jinsia moja kila siku yanazidi kushamiri hadharani lakini bila kusahau kuna wengine wengi ambao hufanya mambo haya kwa siri kwani pindi mtu na mwenza wake wanapokuwa chumbani hakuna mtu ataefahamu vitu vitakavyofuata.

Je, unahisi watu wanaofanya hivi hawajui kama ni mambo yasiyokubalika katika jamii?
La hasha yote hayo wanafamu na hata wengine wanaamini kuwa ni dhambi kwa mujibu wa imani zao.

Hivyo, kwangu ninaona elimu juu ya afya ya uzazi ni mkombozi mkuuJe, kwako unahisi nini kingine kinaweza kusaidia katika mambo haya? wa yote haya.

Je, kwako unahisi nini kingine kinaweza kusaidia katika mambo haya?
 
a) Mpaka sasa, kuna ongezeko kubwa la watu wanaoshiriki ngono za jinsia moja (gay and lesbian)
b) Uraibu wa kuangalia filamu za ngono (ponographic contents)
c) Michezo ya kujichua. ( masturbation)
d) Shughuli hatarishi za kingono (prostitution)
Weewe uko kundi lipi hapo mkuu?
 
Just like ktk kipnd cha ukuaji mkuu, but slowly ukaisha......
Nitakuelezea kitaalamu uelewe kitu
Ipo hivi

Ukianza na B utahamia C ukichoka kua C utahamia D ila km wakati ulipokua B ulikosea njia za makuzi basi utajikuta umeangukia A, wewe umefikia wapi hadi sasa mkuu?
 
Mkuu, sio kila aliyepo kundi A ni kwa sababu ya makuzi........ nowadays kuna homonal imbalances, peer pressure na kasumba ya kufuata mkumbo malezi yanachukua asilimia kadhaa tu
 
Niache ili nijichue!?😂😂 Wale wauzaji wanatuokoa sana wanunuzi wao,msiwatoze aisee wasije wakapandisha bei.
Nalog off Z
[/QUOTE]
Ko mkuu, ww ni mwenyeji wa Uwanja wa Fisi, River side, Buguruni n.k😎
 
Back
Top Bottom