Chachata
JF-Expert Member
- Apr 29, 2011
- 201
- 134
Elimu inayotolewa katika nchi nyingi za Afrika ni Elimu iliyoachwa na wakoloni, Wakoloni hao walianzisha elimu katika makoloni yao kuweza kupata makarani wa kusaidia katika ofsi zao.Pamoja na elimu walianzisha pia dini na kupiga marufuku mambo mengi ya Waafika kama vile dawa za asili na ujuzi wowote waliokuwa nao waafrika, wafua vyuma walikatwa mikono na kuuawa ili kukomesha ujuzi wetu, inaogopesha sana
Harakati za kupinga ukoloni zilifanyanyika katika miaka ya 1960, harakati hizo zililenga kuwaondoa wakoni watu (wazungu). Wazee wetu walipinga ukoloni kwa nguvu zao zote lakini hawakupinga elimu ya kikoloni na mambo yao kwa nguvu zao zote. Hivyo wakoloni waliondoka wakaatuachia elimu yao ya kuandaa makarani, tukaanzisha shule na vyuo vya kuandaa makarani, watu wakosoma katika nyanja mbalimbali wakawa makarani wakubwa, hata waliomaliza vyuo vikuu madaktari na maprofesa wakafanya kazi za ukarani,hakuna ugunduzi, hakuna ubunifu, hakuna viwanda,hakuna jipya wote wakawa makarani.
Rai yangu ya leo ni kuwa asitokee mtu akawalaumu wasomi wetu maprofesa na madaktari eti hawagundui chochote, nao wamesoma makaratasi, wamejibu mitihani ya makaratasi, mengi waliyosoma kwenye karatasi hata hawajawahi kuyaona tusiwalaum.Ndiyo mana wapo akina prof Lipumba wanagombania ofisi Buguruni.
Katika hili tunatakiwa kujirudi, tuachane na elimu ya makaratasi na vyeti, tujifunze uharisia, tuiweke Elimu yetu katika uhalisia.Huo utakuwa mfumo sahihi
[HASHTAG]#Change[/HASHTAG] from abstract to real#