Elimu, Uzalendo nini nguzo ya Taifa?

Mwifwa

JF-Expert Member
Apr 3, 2017
46,881
122,124
Kati ya awamu zote za serikali ya JMT zilizopita, Awamu ya Tano ni Serikali iliyojaa viongozi wenye viwango vikubwa vya Elimu kuanzia Maprofesa, Madokta na wengineo katika nynja zote za Uongozi.

Hii ni serikali ya viwanda ambacho ndio kipaumbele kikubwa awamu hii

Mbali na kuwa na Viongozi wengi wenye Taalumu za juu lakini hadi sasa bado hatujaona matunda yake japo kuanza kuyanusa au kuona dalili zake, Sijasikia au kuona kiwanda chochote au ubunifu wowote wenye sura ya kuzaa kiwanda

Je nini tatizo? Viongozi wetu wenye hizi Taaluma sio wabunifu?

Je hawana Uzalendo katika Taifa lao? Nini kifanyike kama Taifa ili kufikia Tanzania ya Viwanda.
 
Laana ya Mungu ikitua mahali hata lifanyike jambo gani hamtafanikiwa .
Wananchi wamekasirika sana na ukatili unaofanywa ndani ya nchi yao .
 
Laana ya Mungu ikitua mahali hata lifanyike jambo gani hamtafanikiwa .
Wananchi wamekasirika sana na ukatili unaofanywa ndani ya nchi yao .
Tusikakate tamaa tuendelee kupambana na kuelimisha juu ya haya mambo tutafanikiwa tu.

Sasa watu wameanza kutambua mbichi na mbivu mafanikio yapo mbioni kupatikana japo lazima tutoke jasho
 
Viwanda vinajengwa na sekta binafsi sio serikali. Halafu tatizo kubwa linaloturudisha nyuma kimaendeleo ni suala la wengi wetu kutojitambua na kushughulika na mambo yasiyokuwa na tija.
 
Maendeleo ya nchi huletwa na wananchi wa kawaida ambao huzalisha kivitendo, siyo viongozi ambao ni maneno zaidi. Siyo rahisi kupata ufanisi wa ujuzi na viwango vikubwa vya elimu kwa viongozi wa kisiasa.
Katika hali ya kawaida viongozi wa kisiasa hawatumii hata 0.5% ya taaluma zao. Uprofesa na PhD kwenye siasa ni mbwembwe tu. Ufanisi wao ni kwenye tafiti na kufundisha vyuoni kuzalisha wazalishaji.
Wataalam wabobezi wapewe kipato kikubwa kuliko wanasiasa wakitumika katika taaluma zao kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
 
Sawa mzalishajim mkubwa ni mwananchi lakini msingi wa uzalishaji anautengeneza kiongozi mfano Waziri wa Kilimo.

Sasa kama huyo kiongozi hana mbinu mbalimbali za kuimarisha na kushawishi uzalishaji tutrajie nini?

Hapo taaluma inatakiwa itumike ipasavyo.
 
Viwanda vinajengwa na sekta binafsi sio serikali. Halafu tatizo kubwa linaloturudisha nyuma kimaendeleo ni suala la wengi wetu kutojitambua na kushughulika na mambo yasiyokuwa na tija.
Je serikali ikiwa hovyo unadhani sekta binafsi zitaimarika?
 
Sawa mzalishajim mkubwa ni mwananchi lakini msingi wa uzalishaji anautengeneza kiongozi mfano Waziri wa Kilimo.

Sasa kama huyo kiongozi hana mbinu mbalimbali za kuimarisha na kushawishi uzalishaji tutrajie nini?

Hapo taaluma inatakiwa itumike ipasavyo.
Mkuu,
Hiyo ni dhana potofu tu iliyotukuzwa na mapokeo.
Kuwepo au kutokuwepo kwa waziri hakuathiri chochote kwenye uzalishaji. Kutibu mkuu anaweza kuripoti kwa waziri mkuu na mambo yakaenda kama kawaida.
Nafasi nyingi za kisiasa ni mfumo wa kupeana ulaji kisheria kwa jina la kuwatumikia wananchi, wakati hali halisi ni wananchi huwatumikia wanasiasa.
 
Laana ya Mungu ikitua mahali hata lifanyike jambo gani hamtafanikiwa .
Wananchi wamekasirika sana na ukatili unaofanywa ndani ya nchi yao .
.
Dua la kuku halimpati mwewe.

Tena acha kabisa kumhusisha Mungu na masuala ya siasa zeny potevu. Hauna uzalendo hata kidogo, hutaki serikali ifanikiwe katika harakati zake za kuleta maendeleo.
Wananchi Tunaishi nao, na wote wameridhika na utendaji wa serikali ya awamu ya tano. kote nchini tunatembea na ripoti tunapewa, hakuna manung'uniko kam mnavyoeneza kwenye mitandao ya kijamii.

kwa Tabia kama zako na wengine ni wazi hamna nia ya dhati na nzuri kwa nchi ya tanzania. nia yenu serikali ishindwe kutekeleza sera zake! inakuwa kama ni wageni wa siasa, serikali ikishindwa kutekeleza sera maana yake nchi itayumba.
kwa kifupi nawaona nyie ni wasaliti tu, hamchelewi hata kutenda makosa ya uhaini.
 
Mwezangu mi kimtazamo wangu, ww una uchungu sana na chama flani sawa ni maamuzi yk ila si kila mwananchi anasapot upande wako ,hamna wananchi wanapenda maendeleo sanaa ila kwa mfumo huu tulionao bado kabisa ku improve, usilazmishe, ukipendacho kila mt akipende hamna, ss wananchi tunaangalia maendeleo vp yanakuwa kwel, akiwa hamna tutaongea tu, na si kwa mitandao ya kijamii tu ila popote pale .
 
mkuu, unamaanisha mini unaposema "sisi wanachi"? kumbuka hata mini ni mwananchi na niishipo nimezungukwa na wanachi. Wanachi ninaowajua mimi hawalaani serikali na chama kama inavyofanyika mitandaoni. Asilimia 80 ya wananchi wamefurahishwa na utendaji kazi wa serikali.

Sasa kama wewe una takwimu tofauti ziweke hapa, na useme hao wananchi ni wananchi wa nchi gani. Vyama vingine vimehamishia Propaganda zao mitandaoni. Tena bora ingekuwa propaganda, imekuwa ni kulialia tu na kusambaza chuki na uchochezi. Zaidi wanajibishana mipasho tu.
 
Ukihisi kuna mipasho hata ww unaingia ktk hiyo hiyo mipasho, utendaji wa kiongozi wako na muongozo wake kwetu cc ktk jamii ninayoishi pamoja na majiran ,(mtaa wa pili) haturidhishwi unajuwa si tulivunjiwa nyumba mm binafc nilizaliwa umo umo toka kipindi icho hadi leo tunaambiwa tumevamia pamj na majirani 123 ni uonevu kwa kweli nimepoteza mambo yangu mingi ya muhimu hata vyeti vyangu vingi vilipotea, hapa nilipo nipo jf ila nacoment jambo linalonigusa mm, na acha ivyo wazee walikwenda hadi mahakama na mahakama yenyewe ikasibitisha kuwa pale ni haki yenu ila serikali ilipuuza na ww ikiwa ni muangaliz wa habar mzur bac uliliona , na hata hivyo unayafumbia macho unajidai kila ulipokwenda unasema wanamsapot makuful unadhani nchi yt kwa kutumia akili ya mtu mmj kweli tutasong ,na dhulma hii ,bashite ni mnyonge kweli wa kubebwa kuliko ss kuja kuvunja nyumba zetu? ekesha anaambiwa PIGA KAZI BABA na wale walio fukuzwa makazini kwa kesi kama ya bashite , mheshmiwa MAGU kweli anasapotiwa na wt wengi kwel? au ww uvccm ,sijakuelewa mwezangu unajuwa ss tumedambaratika kifamilia kwa sabb ya mheshmiwa wako? nimegundua ww hujafanya takwimu wala hujawahi kufanya jmbo llt la uthibisho wa utendaji wa mheshmiwa wako ,rais wako ni wawanyonge ila muongo kamfanyia nn mnyonge zaidi ya kumkandamiza tu, TUTAISHI KAMA MASHETANI sikatai na ss ndio akatuvunjia nyumb ili tuish kwenye mibuyu shenz waahed, anatia uchungu, nyumbani hadi picha lake llikuwep kwa kumpenda mtetea wanyong kitaa kizima saiv amekua ukoma jina lake tu matapish, mi binafsi nalala kwa misaada ya wasamaria wema tu (BADO UNATAKA TAKWIMU?)
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom