Elimu Tanzania inakwama wapi?

MZEE WA MSALALA

New Member
Jul 25, 2021
2
0
ELIMU TANZANIA SHIDA NINI?

kwa mjibu wa Jamii Forums, Mwaka 2017 wavulana 36,434 waliacha shule, na wasichana 29,708 waliacha shule Katika Mwaka huo na kufanya jumla 66142.

Miaka mitatu baadaye yaani 2020 wavulana 96,683 waliacha shule ikiwa ni mara 2.65 ya 2017 na waschana 71,151 Mwaka 2020 waliacha shule ikiwa ni mara 2.4 ya Mwaka 2017 na kufanya jumla ya 167, 834 kwa Mwaka 2020 ikiwa ni mara 2.53 ya 2017.

Kwa kuhitimisha tunaweza kusema kila baada ya Miaka mitatu(3) ongezeko la wanafunzi 10,100 juu ya ongezeko la awali huacha shule.

Sababu ni zipi hasa?

1. Usitegemee mtoto ataipenda elimu kama anatembea umbali wa zaidi ya kilometa 1 kusaka elimu. Kuna shule ukiwa unaenda Ngara Inaitwa Kumunazi kaangalie watoto wa pale wanatoka umbali kiasi gani. Kuna shule pia Inaitwa Kasharazi nenda kaangalie.

2. Usitegemee mtoto ataipenda shule kama anakaa kwenye miundombinu mibovu ya madarasa, vyoo na Mazingira kiujumla. Kuna shule darasa la Kwanza Hadi darasa la Saba Zina wanafunzi zaidi ya Mia nane(800) na Zina matundu ya vyoo chini ya Sita kwa wote wasichana na wavulana. Unategemea mtoto aipende shule ?

3. Usitegemee mwalimu unampeleka shule vijijini na huduma yake ya makazi(nyumba za waalimu) iko vibaya Kisha afundishe kwa Moto wote mwanafunzi afaulu, matokeo yake Ni shule kufeli. Na hapa usitegemee mzazi kumpeleka mwanafunzi shuleni Kisha asubiri miaka Saba iishe mwanae afeli, Ni wachache Sana.

4. Watoto zaidi ya 100 wanakaa kwenye darasa Moja lenye uwezo wakubeba watoto 40-45 Kisha aipende shule

5. Mwalimu maslahi yake madogo amepanga (no housing) , Mishahara kiduchu matokeo yake ni kulimisha wanafunzi, kubebesha maji wanafunzi kwakisingizio cha “tunamfundisha majukumu”. Endeleeni kumfundisha hayo majukumu akishayajua aache shule aende machimboni au vibaruani ili akafanye hayo majukumu kwa pesa kuliko Bure.

6. Ni mwenyeji wa Jimbo la msalala na kwa kiasi kikubwa nimesoma na hata kukulia huko. Msalala imezungukwa na Uchimbaji wa madini kwa kiasi kikubwa na kilimo. Angalia machimboni, utakuta watoto kwa wingi; je mamlaka husika haziwaoni kama ni watoto na wanatakiwa wawe shule? Msalala watoto wengi wameacha shule kwa sababu ya machimbo.

7. Kama Viongozi wetu wanatuambia tujiajiri na mfumo wetu wa elimu haufundishi kujiajiri zaidi tu wale waliopita VETA, mzazi na mtoto washawishike vipi kupelekana shule?

8. Wazee wanafia kwenye nyadhifa huku vijana wanakaa mitaani. Sasa mzazi anashawishikaje kumpeleka mwanaye shule au kumuacha aendelee?

9. Kuna ng'ombe kumi na elimu Bila ajira Kisha mzazi ashawishike kumuacha binti yake mwenye miaka 16+ aendelee kusoma na hata pia ndio matokeo ya Ndoa za utotoni.

10. Katika nafasi za kisiasa za kuendesha Mihimili kama bunge,k uongoza majimbo, kata wameaminiwa watu wasio na elimu Kisha bado tunamtaka mzazi au mwanafunzi aipende elimu?

11. Je, ni kwasababu elimu tumeidharau Kama Viongozi wetu tuliowachagiua kama wabunge(hifadhi jina) wamefikia hatua ya kuzalilisha elimu na kusema hakuna umuhimu Tena wa wasomi Kama (jina hifadhi) nakutaka serikali iwaamini wao. Je, mtoto anayesikia haya ataona haja ya yeye kuwa msomi Kama taaluma Inaonekana sio msaada?

12. Najaribu kufikiri, je ni wasomi wanadhalilisha taaluma zao na kuwafanya watoto wasione umuhimu wa taaluma hizo?

Naipongeza serikali kwa hatua inazoendelea kuchukua kuboresha mfumo huu wa elimu

1. Kupandisha madaraja Kama ilivyotangazwa siku za Hivi karibuni kutatia hamasa hata wazazi kuanza kuweka imani Katika elimu

2. Kutangaza ajira Mpya mfano zile 6,000 kutaleta Tija pia Kama kichocheo

3. Kuendelea na ujenzi wa miundombinu ya elimu kama madarasa, vyoo, nyumba za waalimu n.k. Kila la kheri
4. Mishahara kuongezewa kutaleta hamasa kwa waalimu

MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI AFRIKA
 
Back
Top Bottom