Elimu si kitu. Wenye pesa wengi ni std seven au hakuna darasa kabisa

Jabman

JF-Expert Member
Jul 27, 2016
1,005
1,337
Nimefanya tafiti kidogo maeneo ya Mbeya, Iringa na Bariadi kuhusu elimu. Watu wengi 68℅ walisema kuwa elimu si muhimu sana kwao kwa sababu wengi wa waliosoma maisha yao ni duni ukilinganisha na vilaza.

Walitoa mifano ya matajiri 10 bora katika Wilaya zote nilizotafiti kuwa wote hawana shule isipokuwa Wilaya ya Bariadi nilikuta mmoja tu kwenye 10bora(Vijisenti).

Wewe unasemaje kuhusu hili?
 
Leteni hoja sasa, idadavuliwe unalete mada halafu inaiacha pending nyie veeeepe
 
Mkuu Wasomi wako bize kufanya wewe uendelee kutumia smartphone and tablet yako kulogin apa, Hao hao wasomi wamekutungia sheria makini kuhakikisha weew na mali zako uko salama, hao hao wasomi Husimamia pesa zako ww tajiri kuhakikisha Hazitumiki ovyo, hao ndio planers wakubwa wa project zako iwe tajiri, Tukisema wote tuusake utajiri na tuachane na shule hakuna ataekuwa tajiri Mzuri, Tutalingana tu , Maarifa kwanza

Sio kila binadamu yuko focused kuwa tajiri sana wapo wanaofata interest mfano kuna matajiri wakubwa tu hutamani kuwa maraisi, Kuna watu huhatarisha maisha kuelekea anga za mbali kufanya uchunguzi Hawa wote hawako focus deeply kujirimbikia pesa
 
Ni kwamba hakuna uhusiano was uwezo wa kumiliki pesa na elimu ya mtu. Elimu ya mtu humsaidia kumudu mazingira tu si kumiliki pesa
 
Mtu mwenye Elimu yake uwezi kumfananisha na Kilaza, Mtu mwenye elimu yupo na nafasi kubwa sana ya kufanikiwa kimaisha hapa Duniani kuliko kilaza, Mtu mwenye elimu atatumia elimu yake bila kutoa jasho jingi na kufanikiwa , mtu mwenye elimu anaweza kuwa na elfu 10 akai manage vizuri kuliko kilaza,kifupi hata mafanikio ya hao wasio na elimu utakuta kamuweka mtu mwenye elimu hili kufanya kazi zake zifanikiwe.Elimu ndio ufunguo wa Maisha. Usidanganyike ndugu. Wewe angalia au chunguza katika maisha ni yupi kati ya mwenye Elimu na mwenye pesa bila bila elimu ufirisika ki maisha haraka. Utapata jibu. Aahaa wee usicheze na Elimu ndugu.
 
Mnaongelea utajiri gani wa manyoka au wenye roots zinazoeleweka by the way matajiri wenye utajiri endelevu hapa tz hata abroad wana elimu Mengi,Manji,METL,Mafuruki,Dangote,Lowassa etc hata Bakhresa ana masomo sio fala yule dingi kama mnavodai,std 7 baadhi yao wana viutajiri vya manyoka mtu ana kaghorofa kamoja au anauza tumbao na vipampu viwili vya dizeli unamwita tajiri?! kafanye utafiti tena
 
Ila mkuu elimu nimuhimu sana, Mimi niaonavyo wenye elimu wengi maisha yao sio mabaya nawala sio masikini yaani kwaasilimia kubwa ukimkumta mwenye elimu ambaye hana kitu kabisa nimara chache nilazima mahitaji mahimu yafamilia anayatimiza, labda pawe kuna sababu nyingine ambayo itamfanya ashindwe kuhudumia familia yake kama ulevi, umalaya/uhuni namengineyo, ila sio kusema atakosa pesa yakuweza kuitunza familia, ila huyu ambaye hana elimu ukimkuta masikini ujue masikini kweli yaani hata shilingi elfu kumi kuishika mpaka afanye kazi ngumu nandio watanzania tuliowengi, me nachoona nibora tuwe watanzania wengi wenye hali zakawaida wenye uwezo wakumudu huduma muhimu kama elimu nzur, afya bora, makazi bora, kuliko kuwa namatajiri 20 katika jamii yenye watu milioni 1 wenye maisha duni yakupindukia
 
If you want to be rich,don't go to school!Robert Kiyosaki.
Wasomi ni watumwa wa matajiri kama Bahresa,Dangote,nk
 
Elimu ni zaidi ya kutafuta pesa mataifa makubwa yameendelea na kuwa na matajiri wakubwa kwa kuwa kuna planners wazuri mfano hakuna tajiri au maamuma aliegundua kuwa mtwara kuna gesi na ina cubic feet ngapi ila ni wabobezi na watafiti waliofanya kazi hiyo na baadae matajiri au wenye mitaji ndio watawekeza na kuongezea utajiri wao, mfano mwingine ni kule Shinyanga ambako Dr. Williamson mtaalam wa Geology ndie alifanya utafiti wa kina juu ya madini yaliopo Mwadui, matajiri wengi wakubwa duniani wanajihusisha na mafuta, madini kama chuma au watengeneza machine mbali×2 wanatumia wasomi wabobez ktk uzalishaji wao, hata Bakhresa anatumia vijana wasomi kufanya utafiti kujua mahitaji ya customers hivyo matajir wakubwa wanaujua umuhim wa wasomi, hata Regnard Mengi pamoja na kuwa yeye ni msomi ila haachi kutumia bussness plan za wasomi wengine hivyo ikitokea elimu au wasomi wakafutika ktk hii dunia basi matajir watapungua ndo maana nchi zenye wasomi wengi kama Russia, USA, England ndizo zenye matajiri wa kutisha duniani na nchi zisizo na wasomi ndizo zenye mafukara wengi mfano mwingine hapa africa matajir wengi wanapatikana Nigeria, South africa, Misri, n.k na utagundua hizi ndo nchi zenye wasomi wengi, na kama kuna tajiri ambae hahusishi wasomi basi anafedha zakubadirishia mboga au ataishia kuwa tajir ktk kijji chake. Hitimisho; utajir na elimu ni Pete na chanda na penye utajir pana elimu na penye elimu pana utajir na kinyume chake
 
mada yake ni nzuri ila ni ya kwenye kahawa,usiijadili kisomi hutampa jibu analolitaka.ndugu vijisenti kwa bariadi sio tajiri kwani mali zake bariadi ni kidogo sana anajulikana kwa ubunge.matajiri wa bariadi pesa wameipata migodini na huko ni ya kubahatisha wengi wanarudi mikono mitupu hatakupoteza maisha.mataiiri wa bariadi niwale wenye ndondocha,
kusoma ni jambo la uhakika sio la kubahatisha malengo yanatimizwa,nafikiwa tofauti na kilimo,ufugaji au biashara .changamoto kwenye usomaji zinachanganuliwa kiraisi na msomi anasonga mbele tofauti na kilimo,biashara hizi kwanza uwe na ;capital ya kutosha ,eneo lenye mzunguko wa pesa,bado changamoto kubwa la wizi,vibaka,wapiga fatuma na kubwa lao ushirikina wa kufikia:machuma ulete,kuibiwa nyota ,kunyanganywa wateja kichawi.kuwekewa mikono ya fisi.nk
 
hata wewe kama unautaka utajiri nenda bariadi ila masharti najua yatakushinda kuna wale watoto wa fisi aliyezaa na msukule wa kike hiyo ni mali ilete ni kupeleke utajirike faster
 
nani kasema kuwa ukiwa Na elimu unakuwa hauna hela?? Billgates mbna kasoma Na ana elimu kubwa tu Na ni tajiri?? Mack zuckernburg naye mbna kasoma ana elimu kubwa tu Na ni tajiri? We cjui ka umefanya tafiti itakuwa umesikiliza story za vijiweni
 
Back
Top Bottom