Elimu nzuri sana ya namna ya kunawa mikono, ila je watanzania wangapi wanamudu au kufikiwa na mfumo huo wa maji na sabuni haina hiyo?

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,348
6,471
Maelekezo ni mengi na mazuri kabisa, na yamekuwepo hata kabla ya Corona mpya kusumbua watu. Namna inayoonyeshwa kwenye video ni nzuri sana, ila je ni watanzania wangapi wanaweza kumudu mfumo huo wa maji?

Au ni wangapi wamefikiwa na mfumo huo wa maji? Je, watanzania wangapi wanamudu aina ya sabuni inayoshauriwa?

Maelekezo yaendane na kada au makundi ya watanzania. Sasa wa kijijini au wa Mburahati atafuataje utaratibu huo wa kunawa wakati huduma ya namna hiyo haipo?

 
Nilivyo fungua JF nikakuta hili tangazo hapa chini, kabla sijalisoma nikajua nimepigwa BAN
  • Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS
 
Kwa wenye kuvaa pete inakuwaje? Napendekeza kuivuta juu kidogo pete na kuirudisha sehemu yake na wakati wa kusuuza unafanya vivyo hivyo.
 
Back
Top Bottom