Elimu ni Msingi wa Maendeleo Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Elimu ni Msingi wa Maendeleo Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kamundu, Dec 26, 2008.

 1. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #1
  Dec 26, 2008
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Watanzania wenzangu wanamikakati wote hapa tunakubaliana na ukweli kwamba Tanzania kuendelea kwa muda mrefu inahitaji elimu. Kuwapiga vita mafisadi ni swala muhimu sana kwa nchi lakini tukikaa chini na kufikiria je ni kitu gani tufanye ili nchi yetu iendelee na iwe na ushindani ni elimu. Hivyo mimi ningependekeza tuanze kumulika ufisadi wa elimu na tujiulize kama elimu ya msingi au ya kidado cha nne inatosha kwa madogo wetu. Shule mpya za sekondari zina hadhi ya chini kuliko shule za mkoloni! kama Kibara, Tambaza, Ilboru, Umbwe, Weruweru, n.k.Vilevile tutoe mawazo mfano mimi nafikiri bado serikali ingetakiwa kukuza shule ambazo zipo badaya ya kujenga shule mpya zenye hadhi ya chini mfano badala ya Ilboru kuchukuwa wanafunzi 800 basi ongeza mabweni na wanafunzi kwani wanafunzi wanahitaji vitu vya msingi kama Library na viwanja vya mpira. Vilevile sisi wote na watoto wa Kikwete wamesoma kwasababu ya imani kuwa elimu ni muhimu hivyo basi JF tuwe mstari wa mbele kuhimiza elimu ya juu. Vilevile tubadilishe mfumo kwa mwanafunzi kusoma miaka zaidi ya kumi na kumaliza shule bila kujua kutumia coputer au hata kusoma hatutafika. Mimi nabahati ya kuja USA na kusoma na kupata elimu nzuri lakini nasikitika na kuwaonea huruma Watanzania ambao hawajapata bahati kama mimi na elimu inafungua mambo sana.
   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  Dec 27, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kamundu,
  Swala zuri sana lakini inakuwa vigumu sana kwa viongozi wetu kuona umuhimu wa elimu ikiwa elimu yenyewe ni biashara kwanza. Hakuna standard iliyowekwa kwa shule kuwa passed na board yetu na nafikiri hatuna hata chombo cha kutazama vitu muhimu ambavyo shule zetu zinatakiwa kuwa navyo katika elimu..
  Nachofahamu mimi shule zote zinajitahidi sana ktk kiingereza kwa sababu ndio somo linalotakiwa ktk market ya kazi nchini na kwa bahati mbaya limekuwa shida kubwa kwa watoto wetu waliozaliwa ktk mazingira ya kiswahili kukutana na lugha mpya ktk masomo yao yote wakati lugha yenyewe haipandi..
  Labda kama itawezekana kuwepo na sheria ya shule zote kuwa na vifaa vifani kuweza kupata kibali cha kufundisha na serikali yenyewe ktk shule zake iweke malengo ambayo pamoja na kuwa serikali ni lazima wayafikie laa sivyo shule haiwezi kupata kibali...
  Tatizo la Umaskini na uhaba wa kitu unatufunga mikono kiasi kwamba tunashindwa hata kukemea mapungufu..sasa matokeo yake tunajkuwana shule nyingi ambazo hazina vifaa wala walimu wenye ujuzi wa kutosha..Huku Ulaya mwalimu bila degree huwezi kufundisha high school na shule kama haina library, maabara na hata usafi tu inaweza kufungiwa..
  Lakini njoo Bongo, Zahanati zinafunguliwa kama vile duka la mshihiri kona ya Kariakoo, Hotel zinafunguliwa maadam una mtaji basi ili mradi kila kitu kinachotakiwa ni fedha sio ujuzi na vifaa ambavyo vinakubalika kuendesha shughuli hiyo... Ni sawa na kurusha ndege na abiria ambayo una hakika haiwezi kupitishwa na IATA, rubani ambaye hakupitiwa uwezo wake zaidi ya kuwa na liseni..
  Tunakwenda kwa nguvu ya Mungu tu ndugu yangu.
   
 3. J

  Jujuman JF-Expert Member

  #3
  Dec 27, 2008
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 248
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watz wote twamkumbuka kiongozi aliesema "Elimu ni msingi wa maisha" usemi huo utabakia kuwa hapo nao si kwa Watz pekee kote Duniani. ndio mana tunastajabia maendeleo ya wenzetu ktk sekta hiyo.na wao hawakufika hapo kwa mwaka mmoja au kumi na moja they took time, na sisi muda mwingi tumepoeza ndani ya 47 years ya uhuru. kwani kauli ile "Elimu ni msingi wa maisha" si ya jana, hivyo tahadhari na yakini tulikua navyo, tulichokosa ni MIPANGO na hili la mipango takriban ni ktk Sekta zote, na tatizo ni wale tunao waamini watutumikie kugeuka mbwa mwitu na kuanza kuweka mbele Matumbo yao na jamaa zao WAKAFISIDI kiasi cha kuingia upofu wasione tena, aliepewa maswala ya Elimu asijue ameyatupa wapi, aliepewa Afya,Fedha,Maliasili nk Wote hao wakarukia biashara ya kujitaarisha kustaafu kwa kupora Maliza Taifa tena mchana kweupeeeeeeeeee! je hiyo ELIMU itapatikana??
  Ule msemo RUSWA NI ADUI WA HAKI SITATOA WALA SITAPOKEA urudishwe ktk matangazo na mabilboards usaidie kuzindua japo wachache.
   
 4. mwakatojofu

  mwakatojofu JF-Expert Member

  #4
  Dec 29, 2008
  Joined: Dec 17, 2008
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  elimu ndio kitu cha kwanza kabisa kwa umuhimu kwa maendeleo ya jamii yoyote. ni mashuleni/vyuoni ndimo tunamojifunza uhasibu, udakitari, uhandisi, kilimo kwa njia za kisasa na nk. hebu fikiria jamii isiyoelimika!

  hata hivyo tunahitaji sio tu msukumo bali pia kuweka nguvu zetu huko. tunahitaji kuwekeza pesa kwa ajili ya kununulia vifaa vya shuleni/vyuoni, vitabu, mabati kwa ajili ya ujenzi wa hayo mashule/vyuo na nk. pesa pia inahitajika kufundushia wafundishaji. wakiwa butu kazi haitoenda.
  hizo hela za kuweka huko ndo hizo zinazochukuliwa kwa njia mbalimbali - misamaha ya kodi, ununuaji radar, ndege, etc. najua hizo hela zingeweza kutochukuliwa na bado zisingewekwa kwenye elimu.

  ili twende sawa inabidi hata hivyo kiswahili tukiache. kiwe kinafundishwa kama somo la lugha. tangia vidudu, msingi, sekondar mpaka vyuoni tuwe tunatumia kiingereza. sababu ziko nyingi kama vile;
  1. sisi tuko kama mil 38 hivi. ni sehemu ndogo sana ya wakaz wa dunia hii. tukiwa na lugha yetu peke yetu itakuwa ngumu kuchanganyana na wengine
  2. tumeshaona inakuwa vigumu vijana wa wanaojifunzia kiswahili huku chini kucope na kiingereza katk ngaz ya sekondar na chuo
  3. gharama kubwa ya kuitafsiri vitabu kuingia ktk kiswahili
  4. wakenya, waganda na weusi wenzetu karibu wote wako bize na lugha za waliokuwa wakoloni wao. sisi tukisema tujitumbukize kutumia kiswahili tangia vidudu mpaka chuo kikuu tutaumia. wakenya, waganda, wamalawi, na nk tukae tukijua hawatokaa watuunge mkono.

  shule za kata si mbaya. tunaweza kuchukulia kama mwanzo. sio lazima tuanze tukiwa perfect. idea ile ni nzuri. baadae tutakuwa na vyuo vya ufundi vya kata au tarafa. then shule za sekondar za vijij.
  nasema si mbaya kwa sababu tayar tunania ya kuwa na shule hizo. tayar tunazo na tumeshaona mapungufu yake. cha kufuata ni kuyakabili. wanaopngilia mambo yetu na fedha zetu tukiona wanayadharau mapungufu ya hizo shule ni kuwapigia makelele mpaka kieleweke
   
Loading...