SoC01 Elimu ni Msingi kwa Mtoto

Stories of Change - 2021 Competition

Jade_

Senior Member
Apr 19, 2015
122
214
Watoto wanaanza darasa la kwanza na wakifika darasa la nne tu mtihani wa taifa huu hapa. Huyu mtoto mdogo unamuekea akilini kwamba shuleni hajaja kujifunza bali amekuja kufaulu mtihani tu. Elimu ya msingi ndio palitakiwa pawe mahala ambapo mtoto anajifunza namna ya kujifunza. Palitakiwa pawe ambapo mtoto anahamasishwa kuwa mbunifu na awaze zaidi.

Watu wanasoma mpaka Harvard na Cambridge, wana shahada za kutosha. Wamejaa tele vyuoni wanasahihisha tu makaratasi, ni wachache sana wanaohangaika kuendeleza taaluma zao ili ziwe na faida chanya kwenye jamii. Hatuna wabunifu na wataalamu wanaoweza kusaidia kutatua shida mbalimbali zinazotukabili kwenye nchi. Wasomi wanatafuta namna ya kuwa mabosi ofisini, kuwa na manyumba na magari. Hayati JPM aliwalalamikia wasaidizi wake kwamba walishindwa kujiongeza mpaka awape amri. Shida hapa ni elimu yetu ya msingi.

Mtoto hawezi kuanza shule na moja kwa moja ukampa “notes”. Wanaanza kwanza na kuimba alfabeti kuchora na kucheza. Madarasa ya watoto yasiwe kama mapango yakutisha bali yawe na picha na michoro mbalimbali yapendeze. Unaweza kufikiri hivi vitu si vya muhimu au ni kitu kidogo sana, lakini lazima umvutie mtoto apende kusoma la sivyo hata atakapokuwa mtu mzima hatopenda kujifunza zaidi.

Tuchukulie mfano mtaala wa Uingereza katika hatua ya msingi. Watoto wanafanya mitihani mara chache sana wanapokuwa shule ya msingi. Je wanafanyiwaje tathmini? Shule itajuaje kama watoto wanajifunza? Tathmini hizi zipo za kusoma, kuandika na hesabu ambazo zinafanywa kwa ushirikiano mkubwa na wazazi nyumbani. Masomo mengine ya ziada kama historia, maarifa ya jamii nk wanafanyiwa majaribio kwa kuambiwa mwisho wa mwezi au muhula wawasilishe ripoti kuhusu mada fulani, au waigize au kuandika hadithi kuhusu mada wanazojifunza. Wanafundishwa namna ya kuandika ripoti, na kutoa nukuu pamoja na kuwasilisha vizuri. Embu niulize mtu kama huyu anapofika chuo utamlinganisha na mwanachuo aliyesoma kwa mtaala wa Tanzania?

Asilimia kubwa ya masomo yanakuwa kwa vitendo zaidi, na hawafundishiwi kama vile kuna mtihani wanaenda kufanya bali kwa nia ya kutaka kujua. Hii ni muhimu sana kwa mtoto mdogo. Unatakiwa umzoeshe mtoto apende kujifunza la sivyo akiwa mkubwa hatopenda tena kujifunza. Atakuwa anahusisha kujifunza na mitihani ambayo tayari ni maana hasi. Usimkaririshe mtoto kwamba kujifunza ni adhabu.

Si kila mtoto ana kipaji cha kusoma. Kuna michezo kama kuogelea, mpira wa miguu, long-jump, mpira wa pete, high-jump, kriketi, mpira wa kikapu nk. Najua kuna watakao sema vifaa, viwanja, pesa nk hamna, lakini sio lazima kuwe na viwanja na vifaa vyenye hadhi ya kimataifa ilimradi mtoto anoe uwezo wake na afurahie michezo hii.

Kuna na wale wasanii wanaopenda kuchora, kuimba na kucheza ala mbalimbali za muziki. Hivi vitu vilikuwepo kwenye mtaala wa Tanzania, ila waliondoa ili watoto wapate muda zaidi wa kukariri masomo ya darasani. Mwishowe walimaliza shule na serikali ikashindwa kuwapa ajira. Labda wangeendelea na michezo na sanaa leo wangeweza kupata ajira huko.

Nini kifanyike sasa? Tunatakiwa tufumue kabisa mfumo mzima wa elimu yetu ya msingi kama kweli tunataka kuwa na taifa la watu werevu na wanaoweza kushindana na kasi ya dunia. Tusilete mzaha na elimu ya msingi. Tuache kufanya watoto wadogo kama chambo cha kukaririshwa “notes”. Bora wakariri wakiwa sekondari kwenda juu. Walimu wanatakiwa wawe wabobezi kweli, wanaojua vizuri saikolojia ya ukuaji. Tunatakiwa kurudisha vipaumbele kwenye michezo na stadi za kazi. Tuwafundishe watoto wetu ujuzi ambao watakuwa nao mpaka watakapo ingia kaburini.

Wazazi walimu na walezi kwa ujumla tuache kukaripia watoto kila wakiuliza maswali au kuongea tusiwafokee na kuambia “nyamaza!”. Tuache watoto waongee kadiri ya uwezo wao na wakikosea tuwaonye vizuri. Shule za serikali ziwe na usafiri watoto wasiteseke kwenda na kurudi. Tuwekeze vilivyo kwenye elimu ya msingi. Tutengeneze kizazi cha watoto wenye ujasiri na uwezo wa kujieleza pamoja na kutaka kujua na kufanya zaidi.
 
Tunaiita elimu ya msingi ila cha ajabu hatujui tunajenga msingi gani......
 
Hichi ni kitu cha ukweli kabisa. Watu wengi hawaelewi jinsi elimu ya mtoto anapokuwa mdogo (2-10) inavyomuathiri mpaka anapokuwa mkubwa. Ukikosea mtoto akiwa mdogo umekosea maisha yake yote.
Ndio mkuu unakuwa umeua kabisa ubunifu na udadisi wa huyu mtoto.
Hata aende wapi hautarudi tena.
 
Ni kweli tupu, mimi binafsi nimesoma kwa vita sana kiasi kwamba tangu nimemaliza mitihani sitaki kusoma kitabu chochote…. nilishachoka na navichukia vitabu.
 
Hahaaa bora umetoa uzoefu wako.
Watu wanakua na chuki ya vitabu kwasababu vinawakumbushia machungu ya utotonii.
Hii ni aina mojawapo ya "trauma".
 
Elimu si kwamba ni ya msingi tu bali ndio msingi wenyewe wa maisha.
 
Nakubaliana na wewe katika hili swala la mageuzi katika Elimu yetu.Naomba tuanze upya kabisa ili tuboreshe vizazi vyetu.
 
Watoto wanaanza darasa la kwanza na wakifika darasa la nne tu mtihani wa taifa huu hapa. Huyu mtoto mdogo unamuekea akilini kwamba shuleni hajaja kujifunza bali amekuja kufaulu mtihani tu. Elimu ya msingi ndio palitakiwa pawe mahala ambapo mtoto anajifunza namna na ya kujifunza. Palitakiwa pawe ambapo mtoto anahamasishwa kuwa mbunifu na awaze zaidi.

Watu wanasoma mpaka Harvard na Cambridge, wana shahada za kutosha. Wamejaa tele vyuoni wanasahihisha tu makaratasi, ni wachache sana wanaohangaika kuendeleza taaluma zao ili ziwe na faida chanya kwenye jamii. Hatuna wabunifu na wataalamu wanaoweza kusaidia kutatua shida mbalimbali zinazotukabili kwenye nchi. Wasomi wanatafuta namna ya kuwa mabosi ofisini, kuwa na manyumba na magari. Hayati JPM aliwalalamikia wasaidizi wake kwamba walishindwa kujiongeza mpaka awape amri. Shida hapa ni elimu yetu ya msingi.

Mtoto hawezi kuanza shule na moja kwa moja ukampa “notes”. Wanaanza kwanza na kuimba alfabeti kuchora na kucheza. Madarasa ya watoto yasiwe kama mapango yakutisha bali yawe na picha na michoro mbalimbali yapendeze. Unaweza kufikiri hivi vitu si vya muhimu au ni kitu kidogo sana, lakini lazima umvutie mtoto apende kusoma la sivyo hata atakapokuwa mtu mzima hatopenda kujifunza zaidi.

Tuchukulie mfano mtaala wa Uingereza katika hatua ya msingi. Watoto wanafanya mitihani mara chache sana wanapokuwa shule ya msingi. Je wanafanyiwaje tathmini? Shule itajuaje kama watoto wanajifunza? Tathmini hizi zipo za kusoma, kuandika na hesabu ambazo zinafanywa kwa ushirikiano mkubwa na wazazi nyumbani. Masomo mengine ya ziada kama historia, maarifa ya jamii nk wanafanyiwa majaribio kwa kuambiwa mwisho wa mwezi au muhula wawasilishe ripoti kuhusu mada fulani, au waigize au kuandika hadithi kuhusu mada wanazojifunza. Wanafundishwa namna ya kuandika ripoti, na kutoa nukuu pamoja na kuwasilisha vizuri. Embu niulize mtu kama huyu anapofika chuo utamlinganisha na mwanachuo aliyesoma kwa mtaala wa Tanzania?

Asilimia kubwa ya masomo yanakuwa kwa vitendo zaidi, na hawafundishiwi kama vile kuna mtihani wanaenda kufanya bali kwa nia ya kutaka kujua. Hii ni muhimu sana kwa mtoto mdogo. Unatakiwa umzoeshe mtoto apende kujifunza la sivyo akiwa mkubwa hatopenda tena kujifunza. Atakuwa anahusisha kujifunza na mitihani ambayo tayari ni maana hasi. Usimkaririshe mtoto kwamba kujifunza ni adhabu.

Si kila mtoto ana kipaji cha kusoma. Kuna michezo kama kuogelea, mpira wa miguu, long-jump, mpira wa pete, high-jump, kriketi, mpira wa kikapu nk. Najua kuna watakao sema vifaa, viwanja, pesa nk hamna, lakini sio lazima kuwe na viwanja na vifaa vyenye hadhi ya kimataifa ilimradi mtoto anoe uwezo wake na afurahie michezo hii.

Kuna na wale wasanii wanaopenda kuchora, kuimba na kucheza ala mbalimbali za muziki. Hivi vitu vilikuwepo kwenye mtaala wa Tanzania, ila waliondoa ili watoto wapate muda zaidi wa kukariri masomo ya darasani. Mwishowe walimaliza shule na serikali ikashindwa kuwapa ajira. Labda wangeendelea na michezo na sanaa leo wangeweza kupata ajira huko.

Nini kifanyike sasa? Tunatakiwa tufumue kabisa mfumo mzima wa elimu yetu ya msingi kama kweli tunataka kuwa na taifa la watu werevu na wanaoweza kushindana na kasi ya dunia. Tusilete mzaha na elimu ya msingi. Tuache kufanya watoto wadogo kama chambo cha kukaririshwa “notes”. Bora wakariri wakiwa sekondari kwenda juu. Walimu wanatakiwa wawe wabobezi kweli, wanaojua vizuri saikolojia ya ukuaji. Tunatakiwa kurudisha vipaumbele kwenye michezo na stadi za kazi. Tuwafundishe watoto wetu ujuzi ambao watakuwa nao mpaka watakapo ingia kaburini.

Wazazi walimu na walezi kwa ujumla tuache kukaripia watoto kila wakiuliza maswali au kuongea tusiwafokee na kuambia “nyamaza!”. Tuache watoto waongee kadiri ya uwezo wao na wakikosea tuwaonye vizuri. Shule za serikali ziwe na usafiri watoto wasiteseke kwenda na kurudi. Tuwekeze vilivyo kwenye elimu ya msingi. Tutengeneze kizazi cha watoto wenye ujasiri na uwezo wa kujieleza pamoja na kutaka kujua na kufanya zaidi.
Kinachonichanganya zaidi in kuona watoto wa shule za awali wakipewa monthly test huku wazazi tukitamba na 'A' za kwenye makaratasi kwamba mwanangu yuko vizuri.
 
Kuna dada mmoja Mghana, yeye passion yake ilikua ni kushona tangu akiwa binti wa miaka 16. Mama yake aliendesha guest house ya familia, hivyo ali buni shuka na pazia za guest, yule dada akianza kumsaidia mama yake. Kutoka pale alianza kushona magauni akawa fundi mzuri.

Baba yake akimwambia yeye hakuzaa fundi charahani. Asome awe na career. Yule dada alisoma architecture na akawa architect mzuri sana.

Baada ya kuhitimu aliamua kufungua duka la mitindo.
 
Bora hakuacha kipaji chake na aliweza kupractice utotoni.
Huku Tz watoto wadogo kabisa wanapewa masomo mengi utafikiri wapo sekondari, muda wa kupractice vipaji au hobbies hawana kabisa. Muda wakua wabunifu kufikiria mambo ya ziada nje ya masomo ya kawaida hawana.
Anatumia elimu yake ya ubunifu kubuni mitindo ya nguo. Nyumba yake na duka lake ame buni ramani mwenyewe. Yaani mpaka unaona raha matumizi yake ya akili
 
Kweli wamevurugwa haswa upande wa elimu
Mtoto unamkuta mvivu hata kukimbia hawezi
Tangu asubuhi ni kukaririshwa tu
Mafundisho ya hovyo
Kwa kweli sio shule tulizosoma sisi bali ni tofauti kabisa
Bila mzazi kujiongeza unakuwa na mtoto asiekuwa na raha kabisa
 
Kabisa. Pona ya mtoto ni mzazi kuwa na busara hata kidogo kwasababu mfumo wa elimu unawaharibu watoto.

Mtoto lazima awe active
Apewe mazoezi ya kutosha na pia afundishwe mengine nje ya masomo

Sisi mpaka vipepeo tulikuwa tunaenda kukamata
Unachora na hata PE ilikuwa ya uhakika
Na masomo tumeyamudu pia
Sasa mtoto wa darasa la pili madaftari utafikiri yuko la 7
 
Back
Top Bottom