Jade_
Senior Member
- Apr 19, 2015
- 122
- 214
Watoto wanaanza darasa la kwanza na wakifika darasa la nne tu mtihani wa taifa huu hapa. Huyu mtoto mdogo unamuekea akilini kwamba shuleni hajaja kujifunza bali amekuja kufaulu mtihani tu. Elimu ya msingi ndio palitakiwa pawe mahala ambapo mtoto anajifunza namna ya kujifunza. Palitakiwa pawe ambapo mtoto anahamasishwa kuwa mbunifu na awaze zaidi.
Watu wanasoma mpaka Harvard na Cambridge, wana shahada za kutosha. Wamejaa tele vyuoni wanasahihisha tu makaratasi, ni wachache sana wanaohangaika kuendeleza taaluma zao ili ziwe na faida chanya kwenye jamii. Hatuna wabunifu na wataalamu wanaoweza kusaidia kutatua shida mbalimbali zinazotukabili kwenye nchi. Wasomi wanatafuta namna ya kuwa mabosi ofisini, kuwa na manyumba na magari. Hayati JPM aliwalalamikia wasaidizi wake kwamba walishindwa kujiongeza mpaka awape amri. Shida hapa ni elimu yetu ya msingi.
Mtoto hawezi kuanza shule na moja kwa moja ukampa “notes”. Wanaanza kwanza na kuimba alfabeti kuchora na kucheza. Madarasa ya watoto yasiwe kama mapango yakutisha bali yawe na picha na michoro mbalimbali yapendeze. Unaweza kufikiri hivi vitu si vya muhimu au ni kitu kidogo sana, lakini lazima umvutie mtoto apende kusoma la sivyo hata atakapokuwa mtu mzima hatopenda kujifunza zaidi.
Tuchukulie mfano mtaala wa Uingereza katika hatua ya msingi. Watoto wanafanya mitihani mara chache sana wanapokuwa shule ya msingi. Je wanafanyiwaje tathmini? Shule itajuaje kama watoto wanajifunza? Tathmini hizi zipo za kusoma, kuandika na hesabu ambazo zinafanywa kwa ushirikiano mkubwa na wazazi nyumbani. Masomo mengine ya ziada kama historia, maarifa ya jamii nk wanafanyiwa majaribio kwa kuambiwa mwisho wa mwezi au muhula wawasilishe ripoti kuhusu mada fulani, au waigize au kuandika hadithi kuhusu mada wanazojifunza. Wanafundishwa namna ya kuandika ripoti, na kutoa nukuu pamoja na kuwasilisha vizuri. Embu niulize mtu kama huyu anapofika chuo utamlinganisha na mwanachuo aliyesoma kwa mtaala wa Tanzania?
Asilimia kubwa ya masomo yanakuwa kwa vitendo zaidi, na hawafundishiwi kama vile kuna mtihani wanaenda kufanya bali kwa nia ya kutaka kujua. Hii ni muhimu sana kwa mtoto mdogo. Unatakiwa umzoeshe mtoto apende kujifunza la sivyo akiwa mkubwa hatopenda tena kujifunza. Atakuwa anahusisha kujifunza na mitihani ambayo tayari ni maana hasi. Usimkaririshe mtoto kwamba kujifunza ni adhabu.
Si kila mtoto ana kipaji cha kusoma. Kuna michezo kama kuogelea, mpira wa miguu, long-jump, mpira wa pete, high-jump, kriketi, mpira wa kikapu nk. Najua kuna watakao sema vifaa, viwanja, pesa nk hamna, lakini sio lazima kuwe na viwanja na vifaa vyenye hadhi ya kimataifa ilimradi mtoto anoe uwezo wake na afurahie michezo hii.
Kuna na wale wasanii wanaopenda kuchora, kuimba na kucheza ala mbalimbali za muziki. Hivi vitu vilikuwepo kwenye mtaala wa Tanzania, ila waliondoa ili watoto wapate muda zaidi wa kukariri masomo ya darasani. Mwishowe walimaliza shule na serikali ikashindwa kuwapa ajira. Labda wangeendelea na michezo na sanaa leo wangeweza kupata ajira huko.
Nini kifanyike sasa? Tunatakiwa tufumue kabisa mfumo mzima wa elimu yetu ya msingi kama kweli tunataka kuwa na taifa la watu werevu na wanaoweza kushindana na kasi ya dunia. Tusilete mzaha na elimu ya msingi. Tuache kufanya watoto wadogo kama chambo cha kukaririshwa “notes”. Bora wakariri wakiwa sekondari kwenda juu. Walimu wanatakiwa wawe wabobezi kweli, wanaojua vizuri saikolojia ya ukuaji. Tunatakiwa kurudisha vipaumbele kwenye michezo na stadi za kazi. Tuwafundishe watoto wetu ujuzi ambao watakuwa nao mpaka watakapo ingia kaburini.
Wazazi walimu na walezi kwa ujumla tuache kukaripia watoto kila wakiuliza maswali au kuongea tusiwafokee na kuambia “nyamaza!”. Tuache watoto waongee kadiri ya uwezo wao na wakikosea tuwaonye vizuri. Shule za serikali ziwe na usafiri watoto wasiteseke kwenda na kurudi. Tuwekeze vilivyo kwenye elimu ya msingi. Tutengeneze kizazi cha watoto wenye ujasiri na uwezo wa kujieleza pamoja na kutaka kujua na kufanya zaidi.