Elimu na nadharia ya muziki

Diamond na Ali Kiba mnayajua haya? Ama kwa hakika muziki ni kipawa kutoka kwa Mungu
Muziki mwingi ni kipaji cha kuzaliwa nacho, lakini kipaji hicho kikichanganywa na utaalamu basi matokeo yanakuwa ni mazuri zaidi. Kuna waimbaji kadhaa ambao vipaji vyao ni vya juu sana na viko kweye taaluma kabisa na wala hawahitaji mtaalamu mwingine, lakini kama huna utaalamu huo, ni vizuri kutafuta mtaalamu kukuthibitishia tungo zako ili uingie kwenye ushindani kikamilifu. Waimbaji wengi wa kimarekani wana watu maalumu wa kuwatungia nyimbo kitaalamu, kwa mfano mtunzi wa nyimbo nyingi za Michael Jackson alikuwa ni Quincy Jones, na vile vile maproducer wengi ni wataalamu wa muziki kwa hiyo hata ukitunga wimbo wako kutokana na kipaji chako kinavyokutuma, wao wataunyoosha na kuuweka katika misingi ya kitaalamu kabla ya kuutoa.
 
Hiyo ni kweli kabisa mkuu...!!!

Chords and Chord Progression

Kumbuka kuwa huko nyuma tulieleza kuwa katika sauti zote 12 za kwenye Octave moja ni sauti saba tu zinazoshabihiana, ambazo mwanzoni tulizionyesha kwa namba za kirumi I-II-III-IV-V-VI-VII, tukimalizia na sauti ya nane VIII ambayo ni sauti ya kwanza kwenye kwenye Octave inayofuata. Zile sauti 12 za octave hujulikana pia kama chromatic scale, wakati sauti hizo saba zinazoshabihiana hujulikana kama diatonic scale. Sauti hizi za diatonic scale kuanzia ya chini hadi ya juu ndizo zina majina kama ifuatavyo kwenye jedwali hili:

SautiJinaMatumizi
ITonicSauti za kupumzikia; hutumika mwanzo na mwisho wa phrase moja
IISupertonic
IIIMeadiantSauti za kuhama kutoka na kuingia kwenye tonic
IVSubdominat
VDominantSauti za Kuchangamsha, yaani zenye msukumo sana
VISubmediant
VIILeading
VIIINext tonicSauti ya kupitia kuingia na kutoka kwenye octave inayofuata.

Jedwali hili tutalirudia tena huko mbele, lakini kwa leo nataka tuzichambue tena sauti hizo kwa kuchanganya sauti tatu tatu zijulikanao kwa pmaoja kama diatonic triad, kwa mfano wakati wa kupiga piano. Kuna chords za kutumia sauti nne nne pia lakini hizo sitazijadili ili kupunguza urefu wa post.

Chords hutumiwa sana kwenye miziki ya piano kwa kila mkono kubonyeza vibonyezo vitatu au vinne kwa kwa mpigo, na kwenye miziki ya magitaa ambapo mpigaji anapiga nyuzi tatu au nne kwa mpigo.
1565341925187.png

Wapigaji wa magitaa maeneo yetu haya ya Africa ya mashariki na ya kati hasa wapiga magitaa ya solo wa Kongo hawatumii sana hizi chords, wao hupiga ile Diatonic scale moja kwa moja, ndiyo maana utaona mikono yao inakwenda kwa haraka sana katika kubonyeza na kukwapua nyuzi za gitaa kwenye mkono wa gitaa, na vile vile wanachambua uzi mmoja mmoja. Watu wanaopiga gitaa kwa kutumia chord huwa hawatembezi mikono mikono yao haraka haraka kwenye mkono wa gitaa, na hupiga nyuzi tatu au nne kwa mpigo. Angalie utofautishe mifano hii miwili ya upigaji magitaa ya solo

Wapiga gitaa wengi wanaotumia chords hupiga kwa kutumia chord za sauti nne nne ambazo nimesema kuwa hatutazijadili kwenye mfululizo huu.

Major and Minor Chords

Katika sauti hizo saba michangayiko ya sauti tatu tatu zinazoshabihiana inaitwa triads na huundwa kwa kuruka sauti moja baina yao, kwa mfano C+E+G, na zinajulikana kama diatonic triad chords. Sauti au noti ya chini kabisa katika mchanganyiko huo huitwa ROOT, halafu noti ya pili huitwa THIRD MAJOR (ni ya tatu kutoka kwenye ROOT) na ile sauti ya tatu huitwa PERFECT FIFTTH (ni ya tano kutoka kwenye ROOT).
1565342282257.png

Kuna aina mbili za michanganyiko hiyo: major chord na minor chord. Maneno major chord na minor chord hapa yasichangwane na major diatonic scale na minor diatonic scale ambazo tumekwishajadili. Major diatonic chords na minor diatonic chords zinapatina kwenye diatonic scale zote yaani kwenye major diatonic scales na kwenye minor diatonic minor scales. Kwa hiyo unaweza kuwa major chord kwenye scale ya C-major na vile vile kwenye scale ya A-minor ingawa chords hizo hazitahusisha noti zinazofanana. Inawezekana kuwa na mchanganyiko wa sauti nne ujulikanao kama seventh ambao huongeza noti moja ijulikanayo pia kama the seventh juu ya perfect fifth; hatuzazingumzia hizo diatonic seventh chords.

Sauti tatu za Major Cord zinatengana kwa urefu wa 2K-3N halafu sauti tatu za Minor chord zinatengana kwa urefu wa 3N-2K. Kwenye mtengano huu 2K inaonyesha kuwa zimeachana kwa hatua kamili mbili, na 3N inaonyesha kuwa zimetengana kwa nusu hatua tatu kwenye chromatic scale.

Nitaongelea diatonic chords za C-major diatonic scale na A-minor diatonic scale tu nikitegemea kuwa maelezo haya yataweza kutumika kwa diatonic scale nyingine zote tulizoongea huko nyuma

Kumbuka tena kuwa sauti za C-major ni C-D-E-F-G-A-B-C, kwa hiyo chord zake zitokanazo na kuruka sauti moja moja zitakuwa ni

CEG, DFA, EGB, FAC,GBD, ACE, BDF, CEG

1565343532142.png

Sasa kwa vile note za chromatic scale zinatengana kwa nusu hatua na ni hizi hapa

C C#-D-D#-E-F-F#-G-G#- A-A#-B

Utaona kuwa kutoka C hadi E kuna nusu hatua nne, sawa na hatua kamili 2, halafu kutoka E hadi G kuna nusu hatua tatu, kwa hiyo Chord CEG ni major chord. Kwenye chord DFA tunaona kuwa kutoka sauti D hadi F kuna nusu hatua tatu, halafu kutoka F hadi A kuna nusu hatua nne sawa na hatua kamili mbili, kwa hiyo DFA ni minor chord. Tukiendelea na chord EGB tunakuta nusu hatua tatu kati ya E na G, na vile vile nusu hatua nne kati ya G na B, kwa hiyo hiyo nayo ni minor chord. Chord FAC ina nusu hatua nne kati ya F na A, na vile vile nusu hatua tatu kati ya A na C, kwa hiyo EGB ni major chord.

Kwa utaratibu huo huo tunaweza kumalizia kwa kuonyesha kuwa GBD ni Major chord na ACE ni minor chord. Mambo ni tofauti kidogo kwenye chord na BDF kwa sababu kuna nusu hatua 3 kati ya B na D, na vile vile nusu hatua 3 kati ya D na F, kwa hiyo chord hii siyo major wala siyo minor bali inajulikana kama diminished chord. Wanamuziki wengi huwa hawaitumii chord hii kwenye tungo zao kwa vile haijichanganyi vizuri na hizo chord nyingine.

Chord hizi hutambulishwa kwa root notes zake C, Dm, Em, F,G, Am, Bo na C; katika notation hii C ina maana ya major chord CEG, na Dm ina maana ya minor chord DFA. Itaonekana kuwa kwenye major scales zote, major cords ni zile za kwanza, nne na tano; kwa hiyo chord za kwenye major scale zimepewa namba za kirumi

I-ii,ii,IV,V,vi,viio

1565343564188.png

Yaani zile namba zilizoandikwa kwa herufi kubwa ni major chords, na zile za herufi ndogo ni minor chords na ile inayoishia na o ni diminished chord.

Ukitumia utaratibu huo huo pia kwenye natural minor scales, utagundua uwa major chords ziko kwenye nafasi ya 3, 6 na 7, wakati minor chords ziko kwenye nafasi za 1,4, na 5, na ile diminished chord iko kwenye nafasi ya 2. Kwa kutumia mfano wa scale ya A-minor, Diatonic chords zake ni

ACE, BDF, CEG, DFA, EGB, FAC,GBD, ACE,

Kama ionekanavyo kwenye picha hii
1565343656047.png

Chords hizi zinafanana kabisa na chords za kwenye C-major key kwa vile A-Naural minor na C-major zinatumia sauti zile zile ila katika mipangilio tofauti. Tatizo liko kwenye chord EGB, kwani iwapo utakuwa kwenye A-natural minor amabayo sauti zake ni A-B-C-D-E-F-G-A basi chord hiyo inakuwa ni minor chord, hata hivyo ukiwa kwenye A-harmonic minor ambayo sauti zake ni A-B-C-D-E-F-G#-A yaani noti ya G imepandishwa juu kwa nusu hatua basi chord hiyo ya EGB itakuwa ni major chord. Vile vile ukiwa kwenye A-medolic minor ambayo sauti zake ni A-B-C-D-E-F#-G#-A, chord hiyo ya EGB itakuwa na maana tofauti. Kwa hiyo uwe makini iwapo unatumia scale ya natural minor au harmonic minor au au melodic minor.

Chord za minor scale zimepewa namba za kirumi pia kama

i,iio,III,iv,v*,VI,VII

na pia zinatumia majina ya root notes zake na kuonyesha kama ni minor kama ilivyo kwenye cleff hii

1565344836394.png

Ni vizuri kuelewa kuwa matumizi ya meneno Major chord na minor chord hayana maana ya kufifisha umuhimu wa minor chord na kukuzu ule wa majopr chord, ni kama ambavyo tuliona kwenye major scale na minor scale kuwa zote zina umuhimu sawa lakini Major scale ina sauti za "furaha", walaki minor key ina "sauti" za huzuni kwani katika muziki kuna miziki inayotungwa kwa ajili ya huzuni na nyingine kwa ajili ya furaha. Ni vivyo hivyo pia kwenye michanganyiko ya chords; major cord ni mchanganyiko wa sauti za furaha, wakati minor chord ni mchanganyiko wa sauti za huzuni, yaani sauti zisizo na msisimko sana. Kwenye wimbo wowote ule, aina zote za chord yaani major cords na minor chords hutumika kwenye sehemu mbalimbali za wimbo. Iwapo lengo ni kumfanya msikilizajajisikie "kuchangamka" kwenye sehemu fulani ya wimbo, basi sehemu hiyo inaandikwa kwa kutumia major chords; vile vile iwapo lengo ni kumfanya msikilizaji ajisikie "kuhuzunika" basi sehemu hiyo ya wimbo inaandikwa kwa minor chords.

Chord Inversions

Hizo diatonic chords tulizojadili hapo juu zinajulikana kuwa ziko kwenye root positions zao, yaani sauti ya chini kabisa (bass) ni ya root note ya chord, ambayo ndiyo iko chini sana. Inversion ni kitendo cha kuhamisha noti moja au mbili kwa Octave nzima, mradi noti mojawapo ibaki kwenye nafasi yake. Kwa vile noti yoyote moja au mbili zinaweza kuhamishiwa chini au juu kwa OCTAVE moja basi katika noti tatu za triad moja kuna iversions nyingi kidogo. Hizo chord tulizoona hapo, juu ndio zinazoitwa root chords. Inversion maarufu zaidi ni First inversion na Second inversion kama ionekanavyo kwenye picha hii.
1565345572524.png

First inversion kuhamisha noti ya chini na kuipekea Octave moja juu ikiacha zile noti nyingine mbili mahala pake, na Second inversion huhamisha noti mbili za chini OCTAVE moja na kuacha noti ya tatu mahala pake. Kama chord ilikuwa kwa mfano CEG kama hiyo kwenye picha hiyo hapo juu, First inverstion yake inakuwa ni EGC* wakati C* ikiwa kweye Octave inayofuatia juu; kwa vile sauti yake ya chini sasa itakuwa ni E, basi hujulikana C/E, yaani chord ya C lakini ambayo bass note ni E. Second Inversion yake itakuwa ni GC*E* ambapo noti C* na E* ziko kwenye Octave inayofuatia juu, chord hii pia hujulikana C/G kwa maana kama nilivyoeleza hapo juu. Jambo la ajabu ni kuwa inversions hizi huwa hazibadilishi sana sauti ya mziki ila zinaongeza madoido ya muziki wenyewe na vile vile kufanya upigaji wake uwe rahisi hasa katika uimbaji na upigaji wa nyuzi za gitaa au vibonyezo vya piano.

Kwa mfano kwenye guitar badala ya kubonyeza nyunzi za C-chord kwenye root position ambazo ni ngumu kwa mpiga guitar kwa vile kidole kimoja kinatakiwa kiruke uzi mmoja na kubonyeza nyuzi mbili zinazofuata, mpigaji anaweza kupiga first inversion yake ya C/E akitumia kidole kimoja kubonyeza nyuzi zote na kile che pili kuruka nyuzi mbili na kubonyesa uzi mmoja wa tatu, au kwa kutumia second inversion ya C/G ambamo kidole cha kwanza kinabonyeza nyuzi zote, halafu kile cha pili kinaruka uzi mmoja na kubonyeza uzi mmoja tu wa pili.
1565345828284.png

Kuna jamaa waliotayaraisha poster linaloonyesha ubonyezaji wa nyuzi za guitar katika chord mbalimbali pamoja inversions zake; lipatikana Amazon. Linaoneka hivi
1565346074129.png

CHORD Progression

Huu ni mtililiko wa chords zinazotumiwa kwenye wimbo. Kwa leo sitaujadili sana mpaka nikishaanza kujadili mada ya mwafaka (harmony) kwenye wimbo. Kwa kawaida wimbo wowote hutumia chords mbili au zaidi ambazo zinaweza kuwa zijajirudia rudia kwa mfumo unaotabilika au usiotabilika. Tutukatane tena kwenye topic hii huko mbeleni.

Leo nitawaacha na wimbo huu maarufu sana wa Imagine ulioimbwa na John Lennon. Wimbo huo umo katika diatonic key ya C-major kwa kutumia triad chords hizi

C, Dm,Em F, G, Am,

Chord ya C kwenye mashairi inapigwa katika root position kama C ikifuatiwa na first inversion yake kama C/E; halafu pia chord ya Em kwenye kibwagizo inapigwa katika root position kama Em ikfuatiwa na first inversion yake kama Em/G. Wimbo wenyewe ni huu

[Mwanzo- Yyombo vitupu]
C - C/E - F
C - C/E - F

[Shairi la kwanza]
C - C/E - F
Imagine there's no Heaven

C - C/E - F
It's easy if you try

C - C/E - F
No hell below us
C - C/E - F
Above us only sky

[Kibwagizo Tangulizi]
F - Am - Dm - F

Imagine all the people
G - C - G - C
Living for today

[Shairi la pili]
C - C/E - F
Imagine there's no countries

C - C/E - F
It isn't hard to do

C - C/E - F
Nothing to kill or die for

C - C/E - F
And no religion too

[Kibwagizo Tangulizi]
F - Am - Dm - F
Imagine all the people
G - C - G - C
Living life in peace
[Kibwagizo]
F - G - C - Em - Em/G
You may say I'm a dreamer

F - G - C - Em - Em/G
But I'm not the only one

F - G - C - Em - Em/G
I hope someday you'll join us
F - G - C
And the world will be as one

[Shairi la tatu]
C - C/E - F
Imagine no possessions

C - C/E - F
I wonder if you can

C - C/E - F
No need for greed or hunger

C - C/E - F
A brotherhood of man

[Kibwagizo Tangulizi]
F - Am - Dm - F
Imagine all the people

G - C - G - C
Sharing all the world

[Kibwagizo]
F - G - C - Em - Em/G
You may say I'm a dreamer

F - G - C - Em - Em/G
But I'm not the only one

F - G - C - Em - Em/G
I hope someday you'll join us

F - G - C
And the world will be as one

Herman Cain alipokuwa CEO wa Godfather’s Pizza aliubadilisha akaimba Imagine there is no pizza kama ifuatavyo hivi

Lyrics za Cain ni hizi hapa chini; sikuzichambua muundo wake bali nime copy-n-paste

Imagine there’s no pizza
I couldn’t if I tried
Eating only tacos
Or Kentucky Fried
Imagine only burgers
It’s frightening and sad

You’re lucky you have pizza
To feed your kids for you
Only frosting or cookies
And no dishes you must do
I magine eating pizza
Each and every day

You may say it’s junk food
But to me it’s so much more
It gives my life its meaning
And it makes a lot of dough

Imagine mozzarella
Anchovies on the side
And maybe, pepperoni
Rounds out your pizza pie
Imagine getting pizza
Delivered to your door

You don’t have to give up now
On my skateboard I will go
I’ll be back in 30 minutes
I just bought Dominoes

All I am saying
Give pizza a chance
All I am saying
Give pizza a chance!
All I am saying
Give pizza a chance!
You got to, you got to, you got to
Give pizza a chance!

Wasomaji wangu wakuu nkumbison, Madaga, Gyole, Extra miles, MzaramoTz ; ingawa post hii ni ndefu, nadhani somo hili kuhusu mpangilio wa chords kwenye major scale na kwenye minor scale, maana ya major and minor chords, na chord inversion na matumizi yake katika kupiga muziki limeeleweka. Makala ijayo nitajadili miundo mbali mbali ya nyimbo na sehemu zake kabla ya kuanza utunzi wa melody.
 
Miundo ya Nyimbo- Sehemu ya 1

Wimbo siyo mpangilio wa wa sauti tu, lazima sauti hizo zipangwe katika muundo wa kuelewaka. Sehemu kuu za wimbo ni saba kama ifuatavyo:
1. Utangulizi (Intro)
2. Shairi (Verse)
3. Kibwagizo Tangulizi (Pre-chorus/Lift)
4. Kibwagizo (Chorus)
5. Kivuko (Bridge)
6. Pumziko (Break)
7. Tamatisho (Outro)
Pamoja na sehemu hizo saba, wimbo unaweza kpia kuwa na sauti za nyuma yaani background ambayo nia yake ni kikolezo tu lakini siyo lengo kuu la wimbo wenyewe. Siyo lazima kila wimbo uwe na sehemu zote hizo; kuwepo au kutokuwepo kwa sehemu fulani kwenye wimbo kunategemea na utashi wa mtungaji mwenyewe na namna alivyopanga kutuma ujumbe kwa msikilizaji wake. Matumizi ya sehemu hizi kuu ni kama ifuatavyo

Utangulizi
Hii ni sehemu ya muziki inayomkaribisha msikilizaji. Ukichukulia muziki kama hafla inayotegemea wageni wengi, basi Utangulizi ni kama yule mkaribishaji wa wageni anayewapokea na kuwaonyesha sehemu ya kuketi. Kama hakuna mpokeaji mzuri, baadhi ya wageni wanaweza kurudi bila kuingia ndani ya hafla yenyewe au kabla ya hafla kuanza. Wanamuziki wengi huipa sehemu hii umuhimu mkubwa sana ingawa ni sehemu ndogo sana ya wimbo. Ni muhimu kuifanya sehemu hii iwe tofauti na nyimbo nyingine kabisa ili kutoa impression kwa msikilizaji kuwa anasikiliza kitu kipya kabisa.

Tangulizi za nyimbo nyingi huwa ama ni vyombo vitupu, au ni sauti za waimbaji zinazokwenda pole pole kuliko beat ya wimbo wenyewe na huenda bila vyombo. Kwa mfano utangulizi wa wimbo huu wa Circle of Life uliotumika kwenye sinema ya Lion King ni ile sehemu ambayo mwimbaji anaimba bila vyombo ambayo ni hii hapa chini. Wimbo huu pia una sauti za backround zinazimbwa na wanakwaya kwa kurudia msitali huu

Ingonyama nengw' enamabala

Utangulizi huu hauonyeshi sauti hizi za background kwa vile zinajirudia tangu mwazo hadi mwisho wa wimbo; sehemu nilizowekea rangi haziko kwenye wimbo original wa movie ya Lion King lakini Lebo M kaziimba katika video hiyo niliyoweka hapo juu

Nantsi ingonyama bakithi baba
Sithi u ingonyama, ye ingonyama
Nantsi ingonyama bakithi baba ooo!
Hi yahalele aa
Siyo Nqoba
Awele dibo,
niwo na dhibo.
Sithi uu baba ingonyama,
Siyo Nqoba
Ingonyama, Ingonyama baba
Ingonyama nengw' enamabala
Nantsi ingonyama bakithi baba
Sithi u ingonyama, ye ingonyama
Nantsi ingonyama bakithi baba ooo!
Sithi u ingonyama, ye ingonyama

Tangulizi za nyimbo nyingi za WCB zina mambo yanayojirudiarudia, kama vile maneno “Wasafi” au “Hi Laizer.” Kufanya hivyo ni makosa kidogo kiutunzi kwani humrudisha msikilizaji aliyewahi kusikiliza nyimbo za zamani katika position ya kudhani kuwa anarudia nyimbo ambazo tayari anazifahamu kuliko kuwa katika position ya kutegemea kusikiliza kitu kipya.

Wimbo wa Michael Jackosn wa Billie Jean ambao ninatumia katika sehemu iliyobaki, Utangulizi wake ulikuwa ni vyombo vitupu.

Mashairi
Kimsingi,wimbo wowote huwa unatakiwa kutuma ujumbe fulani kwa msikilizaji wake. Kuna watunzi wengi wa nyimbo za kiswahili huweka jumbe zao kwenye mashairi yenyewe lakini hilo ni kosa kiutunzi kwani ujumbe wa aina hiyo una tabia ya kupita kama upepo masikioni mwa msikilizaji. Ujumbe mkuu unatakiwa uwe kwenye vibwagizo ambavyo vinarudiwa mara kadhaa katika wimbo huo; kazi ya shairi ni kumtayarisha msikilizaji kupokea ujumbe unaofuata. Kuna mwanamuziki alisema kuwa vibwagizo ni wafalme wakati mashairi wasafishaji wa njia ya mfalme huyo.

Kuna wimbo mmoja wa zamani kidogo unaoitwa "Kimasomaso" ambao ulikuwa na mashiri mengi sana kwa kribu nusu saa. Watu wengi na huenda hata baadhi ya washiriki wa wimbo ule wanaweza kudhani kuwa ujumbe wa muziki ule ulikuwa kwenye mashairi yenyewe, lakini ukweli wenyewe ni kwamba ujumbe wa wimbo ule ulikuwa ni kuwaita ndugu za bibi harusi waje kusherehekea harusi hiyo hapo ukumbini, kwa hiyo mashairi yote yale matamu yalikuwa yanaeleza ni kwa nini ndugu hao wanatakiwa waje ukumbimi kusherekea, na baada kibwagizo kinawaita waje kusherehekea.

Lengo la wimbo wa Billie Jean ni kuwaambia wasikilizajii kuwa binti huyo Bille Jean siyo mpenzi wa mwimbaji na hata mtoto aliyezaliwa na binti huyo siyo wa huyo mwimbaji. Wimbo wenyewe una mashairi mawili tu. Shairi la kwanza linaeleza jinsi mwimbaji alivyokutana na kufahamiana na Bille Jean na wakacheza muziki pamoja ukumbini. Shairi la pili linaeleza jinsi uhusino wa mwimbaji huyo na Bille jean ulivyokuwa katika muda uliofuatia ili kusistiza kuwa hawakuwa katika uhusiano wa mapenzi kweli.

Kibwagizo-Tangulizi
Kama wimbo una vibwagizo vinavyotofautiona basi ni vizuri sana kuwe na kibwagizo-tangulizi kinachomtayarisa msikilizaji kupokea kibwagizo chenyewe baada ya shairi. Kibwagizo tangulizi kinakuwa kinafanana kwa kiasi kikubwa sana kwenye wimbo wote; hakibadiliki sana, labda mstali wa mwisho tu. Kuna nyimbo ambazo huanza na kibwagizo-tangulizi kabla ya shairi la kwanza na kurudiwa kila baada ya shairi hata kama hakuna kibwagizo ndani ya shairi hilo. Vibwagizo tangulizi vingi hutungwa kufanya msikilizaji atumainie kitu kikubwa ama kwa kuongeza au kupunguza sauti, au hata kwa kubadili kidogo rhythmn ya wimbo kuifanya iende kasi au pole pole kuliko shairi lenyewe. Hiki kinaweza kurudia maneno ya kwenye shairi lakini huwa hakiishi kwa kutumia sauti za kupumzika (Tonic) kwani lengo lake kuu ni kumpandisha midadi msikilizizaji apende kusikilza kibwagizo chenyewe au shairi linalofuata.

Kama wimbo una kibwagizo kiachofanana tu kwenye mashairi yote basi hakuna haja ya kuwa na Kibwagizo Tangulizi..
Kwenye wimbo huo wa Billie Jean kibwagizo tangulizi kilikuwa kinamwambia msikilizaji kuwa yeye mwimbaji alishaonywa mara nyingi kujiepusha na tabia za kuvunja mioyo ya wasichana. Akaendelea kuwa alishaoywa na watu mbalimbali pamoja na mama yake. Kwa hiyo ujumbe wake hauna maana ya kutaka kumvunja moyo binti yule bali kusema ukweli tu,

Kibwagizo
Kibwagizo kinaweza kuwa kirefu au kifupi sana lakini hicho ndicho kinachotakiwa kuwa na ujumbe mkuu wa wimbo. Ujumbe ulio kwenye kibwagizo unawekwa kwenye mistali inayojirudiarudia (refrain) ili kuusukuma kwa msikilzaji. Kwenye wimbo huo wa Michael Jackson ujumbe wake ni kuwa Billie Jean ni msichana waliyekutana tu na wala siyo mpenzi wake. Mtoto aliyezaliwa ni Billie Jeana siyo mtoto wa huyo mwimbaji kabisa. Ukuisikiliza tena utagundua kuwa ni kweli anatumia maneno machahe sana kutuma ujumbe wake lakini anarudiarudia mistali hiyo.

Kibwagizo kinatakiwa kiwe ndiyo kinaingia kwenye sehemu kubwa ya ubongo wa msikillizaji kabla ya kupumzika. Hii ndiyo sehemu inayotakiwa kuwa nzuri kuliko na yenye kulenga sana kuliko sehemu zote za wimbo kwa maneno na mapigo ya wimbo wenyewe; Kibwgaizo kitaishia na sauti za tobic kumpumzisha msikilizaji na kumpa nafasi ya kutafakali.

Kivuko
Kama sauti za mashairi na vibwagizo zinaoneka kurudianarudiana, zinaweza kusababisha msikilizaji kujisahahu. Kivuko (bridge) ni sehemu ndogo ya muziki ambayo hutofautiana sana na sehemu nyingine za wimbo kumshitua kidogo msikilizaji ajue kuwa wimbo bado unaendelea. Kivuko hutumia beat na sauti tofauti sana na zile zilizoko kwenye mashairi na kwenye vibwagizo. Nyimbo nyingi za muda mfupi mfupi wa dakika tatu huwa hazina vivuko.

Nimeongezea wimbo wa ziada wa Carly Rae Jepsen - Call Me Maybe baada ya kuwa nimeshaandika sehemu kubwa ya makala haya na kugungua kuwa hata wimbo huwa Michael Jackson haukuwa na Kivuko, Nahisi wimbo huu utasaidia kujua maana ya Kivuko (bridge) kwa vile lyrics zake nimeziongeza hapo chini. Wimbo wenyewe ni huu hapa

Pumziko

Pumziko ni sehemu ambamo mwimbaji haimbi ila hupuzika na kuacha vyombo vijaze nafasi hii. Nyimbo nyingi sana zina sehemu hii, na nyingi hui-abuse na kuacha sehemu kubwa sana ya break. Lengo kubwa la pumziko ni kutayarisha msikilizaji kupokea sehemu inayofuata ambayo inaweza kuwa ni tofauti sana na sehemu iliyotangulia, kwa mfano kuelekea mwisho wa wimbo. Kwenye wimbo huo wa Bille jean, Michael Jackson alitumia sehemu hii kumtayrisha msikilizaji kuelekea mwisho wa wimbo kwa kusistiza kuwa ingawa Billie jeana analazimisha, ukweli ni kuwe siyo mpenzi wake, na wala mtoto yule siyo wake.

Tamatisho

Tamatisho ni sehemu ya kumalizia wimbo. Inamtayarisha msikilazaji kuwa muziki ndiyo unaelekea ukingoni, na kumkumbusha tena ujumbe wa muziki uke. Mara nyinginie sehemu hii huwa ni vyombo vitupu bile kurudia ujumbe na sauti zake hupungua pole pole hadi mwisho wa wimbo, lakini wimbo huwa na impact kubwa sana iwapo utamaliza kwa kusisitiza ujumbe. Wimbo huo wa Billie Jean wa Michael Jackson umetamatishwa kwa kusistsiza kwa wasikilizaji kuwa Billie Jean siyo mpenzi wake tena na tena kabla hajelekea mwisho wa wimbo,

Lyrics za wimbo wote wa Billie Jean wa Michael Jackson ni huu hapa chini

[Shairi la Kwanza]
She was more like a beauty queen from a movie scene
I said, "Don't mind, but what do you mean, I am the one
Who will dance on the floor in the round?"
She said I am the one
Who will dance on the floor, in the round
She told me her name was Billie Jean
As she caused a scene
Then every head turned with eyes that dreamed of being the one

Who will dance on the floor in the round

[Kibwagizo-Tangulizi]
People always told me, "Be careful of what you do
Don't go around breaking young girls' hearts" (hee-eeh)
And mother always told me, "Be careful of who you love
And be careful of what you do (oh-oh)
'Cause the lie becomes the truth" (oh-oh)

[Kibwagizo]
Billie Jean is not my lover
She's just a girl who claims that I am the one (oh, baby)
But the kid is not my son, hoo!
She says I am the one (oh, baby)
But the kid is not my son (hee-hee-hee, no-no-no, hee-hee-hee)

Hoo!

[Shairi la Pili]

For forty days and for forty nights, the law was on her side
But who can stand when she's in demand?
Her schemes and plans
'Cause we danced on the floor in the round, hee!
So take my strong advice, just remember to always think twice
(Don't think twice) Do think twice! (ah-hoo!)
She told my baby we'd danced till three, then she looked at me
Then showed a photo of a baby crying, his eyes were like mine (oh, no)
'Cause we danced on the floor in the round, baby
(ooh, hee-hee-hee)

[Kibwagizo-Tangulizi]
People always told me, "Be careful of what you do
And don't go around breaking young girls' hearts"
(don't break no hearts!) (hee-hee)
She came and stood right by me
Then the smell of sweet perfume (ha-oh)
This happened much too soon (ha-oh, ha-ooh)

She called me to her room (ha-oh, hoo!)

[Kibwagizo]
Billie Jean is not my lover (hoo!)
She's just a girl who claims that I am the one
But the kid is not my son
No-no-no, no-no-no-no-no-no
Billie Jean is not my lover
She's just a girl who claims that I am the one (oh baby)
But the kid is not my son (oh, no, no)
She says I am the one (oh baby)

But the kid is not my son (no, hee-hee)

[Pumziko]
Ah, hee-hee-hee
Hee! Hoo!

She says I am the one, but the kid is not my son
No-no-no, hoo! (oh)
Billie Jean is not my lover
She's just a girl who claims that I am the one
But the kid is not my son
No-no-no, no-no-no-no
She says I am the one, but the kid is not my son (no-no-no)
She says I am the one (You know what you did)
She says he is my son (Breaking my heart babe)
She says I am the one

[Tamatisho]

Billie Jean is not my lover
Billie Jean is not my lover
Billie Jean is not my lover
Billie Jean is not my lover
Billie Jean is not my lover (Don't call me Billie Jean)

Billie Jean is not my...

Lyrics za wimbo wote wa Call Me Maybe wa Carly Rae Jepsen ni huu hapa chini

[Shairi la Kwanza]
I threw a wish in the well
Don't ask me, I'll never tell
I looked to you as it fell
And now you're in my way
I trade my soul for a wish
Pennies and dimes for a kiss
I wasn't looking for this

But now you're in my way

[Kibwagizo-Tangulizi]

Your stare was holding
Ripped jeans, skin was showin'
Hot night, wind was blowin'

Where you think you're going, baby?

[Kibwagizo]

Hey, I just met you, and this is crazy
But here's my number, so call me maybe
It's hard to look right at you, baby
But here's my number, so call me maybe
Hey, I just met you, and this is crazy
But here's my number, so call me maybe
And all the other boys try to chase me

But here's my number, so call me maybe

[Shairi la Pili]

You took your time with the call
I took no time with the fall
You gave me nothing at all
But still you're in my way
I beg and borrow and steal
At first sight and it's real
I didn't know I would feel it

But it's in my way

[Kibwagizo-Tangulizi]

Your stare was holding
Ripped jeans, skin was showing
Hot night, wind was blowing

Where you think you're going, baby?

[Kibwagizo]

Hey, I just met you, and this is crazy
But here's my number, so call me maybe
It's hard to look right at you, baby
But here's my number, so call me maybe
Hey, I just met you, and this is crazy
But here's my number, so call me maybe
And all the other boys try to chase me

But here's my number, so call me maybe

[Kivuko]

Before you came into my life, I missed you so bad
I missed you so bad
I missed you so, so bad
Before you came into my life, I missed you so bad
And you should know that

So call me maybe

Baada ya tambulisho hizo za sehemu mbalimbali za wimbo, kwa vile post imeshakuwa ndefu sana itabuidi niishie hapa. Makala ijayo nidpo nitaingia ndani Zaidi kuhusu miundo mbalimbali za nyimbo.

Wasomaji wangu wakuu nkumbison, Madaga, Gyole, Extra miles, MzaramoTz ; ingawa post hii ni ndefu, nadhani somo hili kuhusu sehemu za wimbo limeeleweka. Makala ijayo nitaendelea kujadili miundo mbalimbali ya nyimbo kabla sijaanza kujadali namna ya kutunga melodies za nyimbo mbali mbalia.
 
Miundo ya Nyimbo- Sehemu ya 2

Baada ya kujadili na kuona sehemu mbalimbali za wimbo, sasa tutachambua miundo mbali mbali ya nyimbo. Kama tulivyoona huko nyuma, siyo lazima wimbo uwe na sehemu zote hizo tulizoeleza. Kwa mfano wimbo wa Billie Jean tuliotumia katika maelezo yaliyopita ulikuwa hauna Kivuko. Inawezakana kabisa wimbo ukawa hauna Kibwagizo au Kibwagizo-Tangulizi ingawa kila wimbo lazima uwe na Utangulizi na Tamatisho. Kuna nyimbo ambazo hazina hata mashairi, kwa mfano miziki yote ya instrumentals ina Utangulizi, Kivuko, na Tamatisho tu; haina hizo sehemu nyingine.

Ni muhimu kutahadharisha kuwa muundo huu ni kwa nyimbo ambazo zina influence ya miziki ya nchi za Magharibi tu. Ukifuatilia nyimbo za nchi za Asia na Mashariki ya kati hazifuati kabisa miundo nitakayojadili hapa, kwa mfano wimbo huu wa kihindi, ingawa unapigwa kwa midundo ya Western, maneno ya wimbo huo kama nilivyoweka hapa chini hayafuati kabisa miundo nitakayotaja hapo mbeleni kwenye makala haya

Muundo wa nyimbo hizo nyingi huanza na mashairi mawili au matatu, halafu ndipo vinakuja vibwagizo kadhaa

[Shairi 1]
Haaye tere baare mein toh sab se suna hai
Sabko pata hai ki tu apsara hai
Milti kahaan hai tu kab se khada hai
Aashiq tera haaye bechara

[Shairi 2]
Itna pata hai ki koi gufa hai
Lekin gufa saali khud laapata hai
Andar bhi ghuskar milti kahaan hai
Yaara phirun maara maara

[Vibwagizo]

Khel liye shot sabhi
Dekh liye spot sabhi
Hadd kahin bhi na lagi
Haanji haanji haanji lekin

Milegi milegi
Tujhe bhi milegi
Mujhe bhi milegi
Hoga chamatkaar

Milegi milegi
Sabhi ko milegi
Kabhi toh milegi
Sabar mere yaar

Aah!
ra ka ka ka…
yeah hey hey

La la la la la…
Geeli geeli hey hey!

Bola tha maine (bola tha maine)
Saari pehne (saari pehne)
Aayegi lene…
Dil tera, dil tera, dil tera, dil tera

Aaye akeli (haaye akeli)
Yaa laaye saheli (uff saheli)
Kisi bhi mili…
Milte ja milte ja milte ja milte ja

Mile le dream sajaage
Mile le cream laga ke
Zidd na kar o kaake
Naa ji naa ji naa ji naa ji, Kyunki!

Milegi milegi
Tujhe bhi milegi
Mujhe bhi milegi
Hoga chamatkaar
Milegi milegi
Sabhi ko milegi
Kabhi toh milegi
Sabar mere yaar

La la la
Geeli geeli geeli haah!
La la la
Geeli geeli hey hey

Miziki ya muundo huo ndiyo iliyokuwa maarufu sana kwenye eneo letu la Afrika ya Mashariki na ya kati miaka ile ya zamani, kwa mfano muziki huu wa Tabora Jazz

Utaufahamu kuwa unaanza na mashairi kadhaa halafu ndipo unabadilisha mdundo kuingia kwenye mdundo wa vibwagizo. Wimbo huo wa Tabora Jazz ulikuwa na midundo ya Vibagwizo-Tangulizi kwanza kabla ya kuingia kwenye midundo ya Vibwagizo vyenyewe na kuendelea hadi Tatamatisho.

Katika maelezo yafuatayo, nitazingatia mtindo wa Kimagharibi tu ambayo ndiyo maarufu sana siku hizi katika mabara ya Afrika, Ulaya, Amerika Kaskazini, Sehemu kadhaa za Amerika ya Kusini, Sehemu nyingi za Oceania, na vile vile kwenye visiwa vyote vya Carribean. Katika kufanya hivyo sitazunguzumia sehemu za Utangulizi, Pumziko na Tamatisho kwa vile inaeleweka kuwa sehemu hizi ni lazima ziwemo kwenye kila wimbo; nitakuwa nazungumzia zile sehemu za katikati tu.

Kimsingi kuna miundo mikuu mitano, lakini kila mwanamziki anaweza kufanya mabadiliko ya muundo kadri apendavyo. Kwa mfano kuna wanamuziki wengine huweka Kivuko mwanzoni sana wengine hukiweka mwishoni au katikati, vile vile kuna wanamuziki wanaounganisha mashairi mawili kabla ya Kibwagizo. Ili kuwa mtunzi mzuri na mbunifu, mwanamuziki anaruhusiwa kuunda muundo wake kadri apendanvyo mwenyewe mradi tu awe makini kuhakikisha kuwa kila sehemu ya wimbo wake inatekeleza majukumu yake sawasawa. Usitunge kutegemea wasikilizaji watasikia mashairi yote kwani ubongo wao unakuwa unatikiswa na mapigo ya muziki zaidi, ndiyo maana ujumbe unatakiwa uwe katika maeneo fulani ya wimbo na urudiwe rudiwe sana kusudi kuacha sehemu nyingine ziwe za kumfanya msikilizaji kucheza.

Muundo 1: Shairi-Shairi-Shairi…

Huu ndio muundo rahisi sana lakini pia huenda siyo maarufu sana kwani hauna mabadiliko sana ya kuuchangamsha ubongo wa msikilizaji. Kwenye muundo huu, ujumbe wa wimbo hubananishwa kwenye mashairi hayo kwa kuwa na mistali inayojirudiarudia kwenye kila shairi la wimbo wote, au kwa kurudia rudia mashairi kusudi ujumbe uweze kupita. Kwa vile mashairi yanarudiwa sana, mashiri hayo huweza huwekwa kwenye midundo inayobadilika badilika ili kupunguza mchoko kwa wasikilizaji wake. Kwenye maandiko ya kimuziki muundo huu huitwa pia AAA wakati alama ya A ikiwa na maana ya shairi. Muundo huu siyo maarufu sana siku hizi, nadhani baada ya elimu ya muziki kuenea sehemu mbalimbali za dunia; nyimbo zinaztumiea muundo huu ni zile zenye masairi mafupi sana, yake yale yenye mistali miwili au mitatu tu.

Baadhi ya nyimbo za zamani zilizokuwa katika mtindo huu hapa kwetu ni pamoja ni zile za Cuban Marimba ya Salim Abdallaha na Juma Kilaza kwa mfano wimbo huu wa ulioimbwa na Salum Abdallah mwanzozi mwa miaka ya sitini

Wimbo mwingine ni ule wa Wajomba Wamechacha wa Mbaraka Mwinshehe aliouimba miaka ya sabini hapa

Kwa Marekani, Bob Dylan naye katika wimbo wake wa “Tangled Up in Blue.” Alitumia muundo huu huu. Ukisikiliza nyimbo hizo utagundua kuwa mashairi yake yamo katika muundo wa kurudiarudia ujumbe wake, kwa mfano Salum Abdallah amerudia mashairi yote mara mbili, wakati Mbaraka amerudia sana maneno “ wapi mahari” kweye kila shairi .

Nitakosa fadhila kama sikuutaja wimbo wa Tanzania Yetu Ndiyo Nchi ya Furaha uliopigwana Atomic Jazz ambayo ilikuwa na makao yake kule Tanga miaka ya sitini na sabini.

Wimbo huu pia umo katika muundo huu huu wa AAA; ujumbe wake mkuu ni “Tanzania yetu ndiyo nchi ya furaha” na msitali huo umerudiwa mara nyingi sana

Muundo 2: Shairi-Shairi-Kiungo-Shairi

Muundo huu unafanana sana na huo muundo wa kwanza hapo juu wa Shairi-Shairi. Miundo yote miwili ina sifa zile zile ingawa muundo huu unajaribu kuongeza ukolezaji kwa kuweka Kiungo kimoja au viwili, lakini kimsingi miundo yote inafanana. Wimbo maarafu uliomibwa kwenye muundo huu ni ule wa Bill Joel

Huku kwetu Tabu Ley katika wimbo wake wa Mokolo Nokokufa aliuimba katika muundo huu huu ingawa kiungo chake kilikuwa kifupi sana na kinafanana na mashahri yenyewe, unaweza usikitambue haraka haraka

Kilwa Jazz nao waliupakuwa wimbo huo na kuutoa kwa Kiswahili kama Napenda Nipate Lau Nafasi hapa

Nyimbo hizi pia hubananisha ujumbe kwenye mashairi na kujitahidi kubadilishabadilisa midundo ya mashairi ili kuwafanya wasikilizaji wasichioke haraka

Muundo 3: Shairi-Kibwagizo-Shairi-Kibwagizo

Huu ni kati ya miundo iliyokuwa maarufu sana kwenye miziki ya pop za Kimarekani. Kuna mtu aliwahi kuandika kuwa nyimbo top 10 kwenye list ya Billboard ziko kwenye muundo huu ambao pia hujulikana kama ABAB ambapo A ni shairi, na B ni Kibwagizo. Chini ya muundo huu mtunzi anaweza kuanza na Kibwagizo kabla ya mashairi na hivyo kuwa Kibwagizo-Shairi-Kibwagizo-Shairi, yaani BABAB.

Tatizo kuu la mfumo huu ambao nyimbo nyingi za kisasa zinaukwepa siku hizi kama ilivyo muundo wa kwanza na wa pili hapo juu ni hiyo ya kutokuwa na mabadiliko mengi ya sauti kumchangamsha msikilizaji. Miziki ya aina hii ni ile ambayo inatagemea maneno ya wimbo wenyewe kuliko sauti na mapigo yake kwa mfano nyimbo nyingi za taarabu na za rap ziko katika mfumo huu. Labda wimbo mmoja maarufu katika muundo huu ni pamoja na huu hapa

Muundo 4:Shairi-Kibwagizo-Shairi-Kibwagizo-Kiungo-Kibwagizo

Nyimbo za namna hii ndizo nyingi sana hasa kwenye maeneo yetu haya na zinakumbukika kirahisi sana iwapo sauti zake zitakuwa zimepangwa vizuri. Nyingi zinaanza na Kibwagizo kabla ya shairi la kwanza. Mifano niliyoweza kukusanya mara moja kutoka eneo letu hili ni Nerea wa Sauti Sol, Fimbo ya Mbali wa Saida Karoli, na Wanitafutia nini wa Ray C

Nerea wa Sauti Sol ni huu

Katika wimbo huo, Sauti Sol wameupa Kivuko viwili katika mpangilio wa
Kibwagizo-Shairi-Kibwagizo- Shairi- Kivuko-Kibwagizo-Mapumziko-Kivuko-Tamatisho

Ingawa wimbo huu unaonekana kama umeimbwa katika mizani ya C-Major, lakini Sauti Sol walifanya kazi ya ziada sana kuhakikihsa kuwa sauti za Dominant hawazipi umuhimu kabisa, wametembeza mashairi yao kati ya Tonic na Subdominant tu wimbo mzima, na hivyo kuufanya mziki uwe kama uko kwenye mizani ya minor ambayo ni ya kuhuzunisha lakini siyo hivyo. Sijui kama Sauti Sol wana mtaalamu wao wa muziki aliyewasaidia au ni kipaji tu kiliwapeleka huko lakini walifanikiwa sana.

Fimbo ya Mbali wa Saida Karoli ni huu

Saida Karoli kaupanga wimbo ifuatavyo
Kibwagizo-Shairi-Kibwagizo- Shairi- Kibwagizo- Shairi-Kibwagizo- Shairi - Kivuko-Tamatisho

Ingawa wimbo huu haukuwa sophisticated sana, sifa moja ya Saida katika wimbo huu ni kuwa aliuchangamsha zaidi kwa kuimba vibwagizo vyake katika Octave mbili mbili kuviongezea msisimko. Mwambaji wa kwanza alikuwa akianza kwenye Octave moja harafu Saida anarudia katika Octave ya juu yake; msikileze tena utaelewa ninalosema.

Wanifuatia nini wa Ray C ni huu hapa

Ray C naye kaupanga wimbo wake huo katika muundo huu
Kibwagizo-Shairi-Kibwagizo-Mapumziko-- Shairi- Kibwagizo- Kivuko-Kibwagizo- Kivuko-Mapumziko-Tamatisho

Wanamuziki wengi wa kimarekani huutumia sana mtindo huu pia.

Nitamkosea fadhila sana kama sitamkumbuka mkongwe Sipho Mabuse wa Afrika ya Kusini alipotumia muundo huo huo kusifia visiwa vyetu vya Zanzibar kwa wimbo huu

Maneno ya wimbo huo na muundo wake ni kama ionekanavyo hapa chini
[Utangulizi]
Zanzibar
Zanzibar
[Shairi 1]
Beautiful Island Eastern Side of (Of Africa)
South of ... out from a distance (Tanzania)
You can hear the marimba band
Play its sweet melodies (across the land)
Sweet sweet melodies
[Kibwagizo]
Zanzibar, ohh Zanzibar
Beautiful Island, (of Africa)
Zanzibar, ohh Zanzibar
Beautiful Island, (of Africa)
Zanzibar, ohh Zanzibar
Beautiful Island, (of Africa)
[Shairi 2]
Everbody is getting ready (come across the sea)
Now is the time to sing and dance (ujamaa)
Open your hearts to let your spirits free (ujamaa)
You can hear the marimba band
Playin sweet sweet melodies
[Mapumziko 1] -Instrumental
[Kibwagizo]
Zanzibar, ohh Zanzibar
Beautiful Island, (of Africa)
Zanzibar, ohh Zanzibar
Beautiful Island, (of Africa)
[Kiungo 1] -Instrumental
[Tamatisho]
Zanzibar
Ujamaa
Zanzibar
Ujamaa
Zanzibar
Ujamaa
Zanzibar
Ujamaa
Zanzibar
Ujamaa
Zanzibar
Ujamaa
Zanzibar
Ujamaa

Muundo 5: Shairi-KibwagizoTangulizi-Kibwagizo-Shairi-KibwagizoTanguliz)-Kibwagizo-Kiungo

Muundo wa 4 hapo juu na muundo huu hapa ndizo zinazoongoza dunia ya muziki wa kileo; .hata hivyo nyimbo nyingi za miaka ya karibuni zimekuwa zinafuata utaratibu huu sana zaidi ya ule wa Shairi-Kibwagizo-Shairi-Kibwagizo hapo juu. Kama msomaji atakumbuka tena wimbo ule wa Billie Jean wa Michael Jackson uko katika muundo huu huu. Wimbo maarufu sana Tanzania unaofuata mpangilio huu ni Kwangwaru wa Harmonize ambao kila msomaji hapa atakauwa anaufahamu.

Wimbo huu unaaza na Shairi, linalofuatiwa na KibwagizoTangulizi halafu Kibwagizo. Kwa vile waimbaji wakubwa ni wawili, mwimbiaji wa kwanza anaimba seti moja ya Shairi-KibwagizoTangulizi-Kibwagizo halafu mwimbaji wa pili naye anaimba vile vile kabla ya mwimbaji wa kwanza kumalizia tena kwa kuimba seti nyingine ya Shairi-KibwagizoTangulizi-Kibwagizo na wote kumaliziza na Kiungo. Tatizo la wimbo ule ni kama hauna ujumbe rasmi, kwani ile sehemu kuu ya Kibwagizo inayourudiwarudiwa ni neno Kwangwaru tu ambalo maana yake haijulikani labda kama lina maana fulani isiyokuwa ya Kiswahili. Ila kama ni jina la mtu basi ujumbe wa wimbo ni hafifu sana mpaka mtu aurudia mara kadhaa na aunganishe aunganishe sehemu mbalimbali za muziki wote ndipo ajue kuwa wimbo huo unambebeleza mpenzi. Najua kuwa kuna wanamuziki wengine siku hizi hawana time na ujumbe kwenye miziki yao bali wanaangalia kukubaliwk kwake tu ila lengo la wimbo wowote huwa ni kutuma ujumbe fulani.

Muundo huu huweza kubadilishwa kidogo kwa kuanza na KibwagizoTangulizi kikifuatiwa na kibwagizo kabla ya kuanza shairi lenyewe. Wimbo maarufu wa muundo huo ni ule wa Yemi Alade uitwao Johnny ambao ni mrefu sana ukiwa na mashairi matatu yanayoeleweka kabisa na nimeyaweka hapa kuonyesha sehemu hizo. Style ya Wimbo ni tofauti kidogo na nyingine kwa sababu umeanza na Kiungo kabla mashairi hayajaanza. Ujumbe wa wimbo uko wazi kabisa kuwa anamtafuta mwanamume wake Johnny, na utaona ujumbe ule ameurudia mara nyingi sana katika vibwagizo vyote. Mashairi yote yanazungumzia tabia za Johhny kwanza halafu kwenye kibwagizo bado anarudia kuwa bado anamtafuta Johnny wake tu; ni ujumbe ulio wazi kabisa.

[Utangulizi]
Ho ah
Ehn
Habokoto bokoto eh
Selebobo pon the beat (Selebobo on the beat)
Yemi Alade
It’s Effyzzie baby
[Kibwagizo-Tangulizi]
Johnny leave me follow Cynthia
And I don’t know what to do
And he talk say I no do am
Like the way Cynthia dey do
Johnny give Uche belle
He talk say he wan marry Nene
Nwokem ke di fe neme
Johnny mo, Johnny mo
[Kibwagizo]
I’m looking for my Johnny eh
Where is my Johnny
Johnny mo
Do you know Johnny…question
If I no see my Johnny
Fefe geme
[Kiungo]
I’m looking for my Johnny
I’m looking for my honey…(ya ya ya)
You telling me this, you telling me that
I say this is not for me
Johnny do me conny (Johnny)
Johnny do me conny (Jo-Johnny)
He’s doing me this
He’s doing me that
But I no go tell mummy (mummy)
[Shairi 1]
He go Canada
He go Tokyo
Yesterday he say he dey Morocco
He dance disco
He sing Awilo
Na lie
Na lie, na Pinocchio
This one na gobe…ayakata
Original gobe
See me see wahala eh
[Kibwagizo-Tangulizi]
Johnny leave me follow Cynthia
And I don’t know what to do
And he talk say I no do am
Like the way Cynthia dey do
Johnny give Uche belle
He talk say he wan marry Nene
Nwokem ke di fe neme
Johnny mo, Johnny mo
[Kibwagizo]
I’m looking for my Johnny….ah ayakata
Where is my Johnny
Johnny mo
Do you know Johnny…question
If I no see my Johnny
Fefe geme
Selebobo on the beat
[Shairi 2]
He get dollar
He get hummer
He dey drink palmi with Patience and Jonah
He dey Toronto
He dey Sokoto
Or the lie he dey lie
He dey sokoto…ha
This one na gobe eyeh…ayakata
Original gobe
See me see wahala eh
[Kibwagizo-Tangulizi]
Johnny leave me follow Cynthia
And I don’t know what to do
And he talk say I no do am
Like the way Cynthia dey do
Johnny give Uche belle
He talk say he wan marry Nene
Nwokem ke di fe neme
Johnny mo, Johnny mo
[Kibwagizo]
I’m looking for my Johnny eh..eh eh eh
Where is my Johnny
Johnny mo
Do you know Johnny…question
If I no see my Johnny…ah
Fefe geme
[Shairi 3]
He go Canada
He go Tokyo
Yesterday he say he dey Morocco
He dance disco
He sing Awilo
Na lie, na lie na Pinocchio
This one na gobe…ah ayakata
Original gobe
See me see wahala eh
[Kibwagizo-Tangulizi]
Johnny leave me follow Cynthia
And I don’t know what to do
And he talk say I no do am
Like the way Cynthia dey do
Johnny give Uche belle
He talk say he wan marry Nene
Nwokem ke di fe neme
Johnny mo, Johnny mo
[Kibwagizo]
I’m looking for my Johnny
Where is my Johnny
Johnny mo
Do you know Johnny…question
If I no see my Johnny
Fefe geme ..eh
[Tamatisho]
Selebobo on the beat
Yemi Alade eh

Wasomaji wangu wakuu nkumbison, Madaga, Gyole, Extra miles, MzaramoTz , Frega Bao,MRI; ingawa post hii ni ndefu, nadhani mjadala huu hili kuhusu miundo mbalimbali ya nyimbo umeeleweka. Makala ijayo nitanza kujadili utungaji wa Mkong'osio wa wimbo, yaani Melody kabla sijaanza kujadali namna ya kuunganisha sauti mbalimbali katika wimbo mmoja yaani mwafaka au harmony.
 
Acha nikae sehemu nitulie nimeze vitu!Ahsante sana umejuaje Kama nilikuwa natafuta darasa!
 
Miundo ya Nyimbo- Sehemu ya 1

Wimbo siyo mpangilio wa wa sauti tu, lazima sauti hizo zipangwe katika muundo wa kuelewaka. Sehemu kuu za wimbo ni saba kama ifuatavyo:
1. Utangulizi (Intro)
2. Shairi (Verse)
3. Kibwagizo Tangulizi (Pre-chorus/Lift)
4. Kibwagizo (Chorus)
5. Kivuko (Bridge)
6. Pumziko (Break)
7. Tamatisho (Outro)
Pamoja na sehemu hizo saba, wimbo unaweza kpia kuwa na sauti za nyuma yaani background ambayo nia yake ni kikolezo tu lakini siyo lengo kuu la wimbo wenyewe. Siyo lazima kila wimbo uwe na sehemu zote hizo; kuwepo au kutokuwepo kwa sehemu fulani kwenye wimbo kunategemea na utashi wa mtungaji mwenyewe na namna alivyopanga kutuma ujumbe kwa msikilizaji wake. Matumizi ya sehemu hizi kuu ni kama ifuatavyo

Utangulizi
Hii ni sehemu ya muziki inayomkaribisha msikilizaji. Ukichukulia muziki kama hafla inayotegemea wageni wengi, basi Utangulizi ni kama yule mkaribishaji wa wageni anayewapokea na kuwaonyesha sehemu ya kuketi. Kama hakuna mpokeaji mzuri, baadhi ya wageni wanaweza kurudi bila kuingia ndani ya hafla yenyewe au kabla ya hafla kuanza. Wanamuziki wengi huipa sehemu hii umuhimu mkubwa sana ingawa ni sehemu ndogo sana ya wimbo. Ni muhimu kuifanya sehemu hii iwe tofauti na nyimbo nyingine kabisa ili kutoa impression kwa msikilizaji kuwa anasikiliza kitu kipya kabisa.

Tangulizi za nyimbo nyingi huwa ama ni vyombo vitupu, au ni sauti za waimbaji zinazokwenda pole pole kuliko beat ya wimbo wenyewe na huenda bila vyombo. Kwa mfano utangulizi wa wimbo huu wa Circle of Life uliotumika kwenye sinema ya Lion King ni ile sehemu ambayo mwimbaji anaimba bila vyombo ambayo ni hii hapa chini. Wimbo huu pia una sauti za backround zinazimbwa na wanakwaya kwa kurudia msitali huu

Ingonyama nengw' enamabala

Utangulizi huu hauonyeshi sauti hizi za background kwa vile zinajirudia tangu mwazo hadi mwisho wa wimbo; sehemu nilizowekea rangi haziko kwenye wimbo original wa movie ya Lion King lakini Lebo M kaziimba katika video hiyo niliyoweka hapo juu

Nantsi ingonyama bakithi baba
Sithi u ingonyama, ye ingonyama
Nantsi ingonyama bakithi baba ooo!
Hi yahalele aa
Siyo Nqoba
Awele dibo,
niwo na dhibo.
Sithi uu baba ingonyama,
Siyo Nqoba
Ingonyama, Ingonyama baba
Ingonyama nengw' enamabala
Nantsi ingonyama bakithi baba
Sithi u ingonyama, ye ingonyama
Nantsi ingonyama bakithi baba ooo!
Sithi u ingonyama, ye ingonyama

Tangulizi za nyimbo nyingi za WCB zina mambo yanayojirudiarudia, kama vile maneno “Wasafi” au “Hi Laizer.” Kufanya hivyo ni makosa kidogo kiutunzi kwani humrudisha msikilizaji aliyewahi kusikiliza nyimbo za zamani katika position ya kudhani kuwa anarudia nyimbo ambazo tayari anazifahamu kuliko kuwa katika position ya kutegemea kusikiliza kitu kipya.

Wimbo wa Michael Jackosn wa Billie Jean ambao ninatumia katika sehemu iliyobaki, Utangulizi wake ulikuwa ni vyombo vitupu.

Mashairi
Kimsingi,wimbo wowote huwa unatakiwa kutuma ujumbe fulani kwa msikilizaji wake. Kuna watunzi wengi wa nyimbo za kiswahili huweka jumbe zao kwenye mashairi yenyewe lakini hilo ni kosa kiutunzi kwani ujumbe wa aina hiyo una tabia ya kupita kama upepo masikioni mwa msikilizaji. Ujumbe mkuu unatakiwa uwe kwenye vibwagizo ambavyo vinarudiwa mara kadhaa katika wimbo huo; kazi ya shairi ni kumtayarisha msikilizaji kupokea ujumbe unaofuata. Kuna mwanamuziki alisema kuwa vibwagizo ni wafalme wakati mashairi wasafishaji wa njia ya mfalme huyo.

Kuna wimbo mmoja wa zamani kidogo unaoitwa "Kimasomaso" ambao ulikuwa na mashiri mengi sana kwa kribu nusu saa. Watu wengi na huenda hata baadhi ya washiriki wa wimbo ule wanaweza kudhani kuwa ujumbe wa muziki ule ulikuwa kwenye mashairi yenyewe, lakini ukweli wenyewe ni kwamba ujumbe wa wimbo ule ulikuwa ni kuwaita ndugu za bibi harusi waje kusherehekea harusi hiyo hapo ukumbini, kwa hiyo mashairi yote yale matamu yalikuwa yanaeleza ni kwa nini ndugu hao wanatakiwa waje ukumbimi kusherekea, na baada kibwagizo kinawaita waje kusherehekea.

Lengo la wimbo wa Billie Jean ni kuwaambia wasikilizajii kuwa binti huyo Bille Jean siyo mpenzi wa mwimbaji na hata mtoto aliyezaliwa na binti huyo siyo wa huyo mwimbaji. Wimbo wenyewe una mashairi mawili tu. Shairi la kwanza linaeleza jinsi mwimbaji alivyokutana na kufahamiana na Bille Jean na wakacheza muziki pamoja ukumbini. Shairi la pili linaeleza jinsi uhusino wa mwimbaji huyo na Bille jean ulivyokuwa katika muda uliofuatia ili kusistiza kuwa hawakuwa katika uhusiano wa mapenzi kweli.

Kibwagizo-Tangulizi
Kama wimbo una vibwagizo vinavyotofautiona basi ni vizuri sana kuwe na kibwagizo-tangulizi kinachomtayarisa msikilizaji kupokea kibwagizo chenyewe baada ya shairi. Kibwagizo tangulizi kinakuwa kinafanana kwa kiasi kikubwa sana kwenye wimbo wote; hakibadiliki sana, labda mstali wa mwisho tu. Kuna nyimbo ambazo huanza na kibwagizo-tangulizi kabla ya shairi la kwanza na kurudiwa kila baada ya shairi hata kama hakuna kibwagizo ndani ya shairi hilo. Vibwagizo tangulizi vingi hutungwa kufanya msikilizaji atumainie kitu kikubwa ama kwa kuongeza au kupunguza sauti, au hata kwa kubadili kidogo rhythmn ya wimbo kuifanya iende kasi au pole pole kuliko shairi lenyewe. Hiki kinaweza kurudia maneno ya kwenye shairi lakini huwa hakiishi kwa kutumia sauti za kupumzika (Tonic) kwani lengo lake kuu ni kumpandisha midadi msikilizizaji apende kusikilza kibwagizo chenyewe au shairi linalofuata.

Kama wimbo una kibwagizo kiachofanana tu kwenye mashairi yote basi hakuna haja ya kuwa na Kibwagizo Tangulizi..
Kwenye wimbo huo wa Billie Jean kibwagizo tangulizi kilikuwa kinamwambia msikilizaji kuwa yeye mwimbaji alishaonywa mara nyingi kujiepusha na tabia za kuvunja mioyo ya wasichana. Akaendelea kuwa alishaoywa na watu mbalimbali pamoja na mama yake. Kwa hiyo ujumbe wake hauna maana ya kutaka kumvunja moyo binti yule bali kusema ukweli tu,

Kibwagizo
Kibwagizo kinaweza kuwa kirefu au kifupi sana lakini hicho ndicho kinachotakiwa kuwa na ujumbe mkuu wa wimbo. Ujumbe ulio kwenye kibwagizo unawekwa kwenye mistali inayojirudiarudia (refrain) ili kuusukuma kwa msikilzaji. Kwenye wimbo huo wa Michael Jackson ujumbe wake ni kuwa Billie Jean ni msichana waliyekutana tu na wala siyo mpenzi wake. Mtoto aliyezaliwa ni Billie Jeana siyo mtoto wa huyo mwimbaji kabisa. Ukuisikiliza tena utagundua kuwa ni kweli anatumia maneno machahe sana kutuma ujumbe wake lakini anarudiarudia mistali hiyo.

Kibwagizo kinatakiwa kiwe ndiyo kinaingia kwenye sehemu kubwa ya ubongo wa msikillizaji kabla ya kupumzika. Hii ndiyo sehemu inayotakiwa kuwa nzuri kuliko na yenye kulenga sana kuliko sehemu zote za wimbo kwa maneno na mapigo ya wimbo wenyewe; Kibwgaizo kitaishia na sauti za tobic kumpumzisha msikilizaji na kumpa nafasi ya kutafakali.

Kivuko
Kama sauti za mashairi na vibwagizo zinaoneka kurudianarudiana, zinaweza kusababisha msikilizaji kujisahahu. Kivuko (bridge) ni sehemu ndogo ya muziki ambayo hutofautiana sana na sehemu nyingine za wimbo kumshitua kidogo msikilizaji ajue kuwa wimbo bado unaendelea. Kivuko hutumia beat na sauti tofauti sana na zile zilizoko kwenye mashairi na kwenye vibwagizo. Nyimbo nyingi za muda mfupi mfupi wa dakika tatu huwa hazina vivuko.

Nimeongezea wimbo wa ziada wa Carly Rae Jepsen - Call Me Maybe baada ya kuwa nimeshaandika sehemu kubwa ya makala haya na kugungua kuwa hata wimbo huwa Michael Jackson haukuwa na Kivuko, Nahisi wimbo huu utasaidia kujua maana ya Kivuko (bridge) kwa vile lyrics zake nimeziongeza hapo chini. Wimbo wenyewe ni huu hapa

Pumziko

Pumziko ni sehemu ambamo mwimbaji haimbi ila hupuzika na kuacha vyombo vijaze nafasi hii. Nyimbo nyingi sana zina sehemu hii, na nyingi hui-abuse na kuacha sehemu kubwa sana ya break. Lengo kubwa la pumziko ni kutayarisha msikilizaji kupokea sehemu inayofuata ambayo inaweza kuwa ni tofauti sana na sehemu iliyotangulia, kwa mfano kuelekea mwisho wa wimbo. Kwenye wimbo huo wa Bille jean, Michael Jackson alitumia sehemu hii kumtayrisha msikilizaji kuelekea mwisho wa wimbo kwa kusistiza kuwa ingawa Billie jeana analazimisha, ukweli ni kuwe siyo mpenzi wake, na wala mtoto yule siyo wake.

Tamatisho

Tamatisho ni sehemu ya kumalizia wimbo. Inamtayarisha msikilazaji kuwa muziki ndiyo unaelekea ukingoni, na kumkumbusha tena ujumbe wa muziki uke. Mara nyinginie sehemu hii huwa ni vyombo vitupu bile kurudia ujumbe na sauti zake hupungua pole pole hadi mwisho wa wimbo, lakini wimbo huwa na impact kubwa sana iwapo utamaliza kwa kusisitiza ujumbe. Wimbo huo wa Billie Jean wa Michael Jackson umetamatishwa kwa kusistsiza kwa wasikilizaji kuwa Billie Jean siyo mpenzi wake tena na tena kabla hajelekea mwisho wa wimbo,

Lyrics za wimbo wote wa Billie Jean wa Michael Jackson ni huu hapa chini

[Shairi la Kwanza]
She was more like a beauty queen from a movie scene
I said, "Don't mind, but what do you mean, I am the one
Who will dance on the floor in the round?"
She said I am the one
Who will dance on the floor, in the round
She told me her name was Billie Jean
As she caused a scene
Then every head turned with eyes that dreamed of being the one

Who will dance on the floor in the round

[Kibwagizo-Tangulizi]
People always told me, "Be careful of what you do
Don't go around breaking young girls' hearts" (hee-eeh)
And mother always told me, "Be careful of who you love
And be careful of what you do (oh-oh)
'Cause the lie becomes the truth" (oh-oh)

[Kibwagizo]
Billie Jean is not my lover
She's just a girl who claims that I am the one (oh, baby)
But the kid is not my son, hoo!
She says I am the one (oh, baby)
But the kid is not my son (hee-hee-hee, no-no-no, hee-hee-hee)

Hoo!

[Shairi la Pili]

For forty days and for forty nights, the law was on her side
But who can stand when she's in demand?
Her schemes and plans
'Cause we danced on the floor in the round, hee!
So take my strong advice, just remember to always think twice
(Don't think twice) Do think twice! (ah-hoo!)
She told my baby we'd danced till three, then she looked at me
Then showed a photo of a baby crying, his eyes were like mine (oh, no)
'Cause we danced on the floor in the round, baby
(ooh, hee-hee-hee)

[Kibwagizo-Tangulizi]
People always told me, "Be careful of what you do
And don't go around breaking young girls' hearts"
(don't break no hearts!) (hee-hee)
She came and stood right by me
Then the smell of sweet perfume (ha-oh)
This happened much too soon (ha-oh, ha-ooh)

She called me to her room (ha-oh, hoo!)

[Kibwagizo]
Billie Jean is not my lover (hoo!)
She's just a girl who claims that I am the one
But the kid is not my son
No-no-no, no-no-no-no-no-no
Billie Jean is not my lover
She's just a girl who claims that I am the one (oh baby)
But the kid is not my son (oh, no, no)
She says I am the one (oh baby)

But the kid is not my son (no, hee-hee)

[Pumziko]
Ah, hee-hee-hee
Hee! Hoo!

She says I am the one, but the kid is not my son
No-no-no, hoo! (oh)
Billie Jean is not my lover
She's just a girl who claims that I am the one
But the kid is not my son
No-no-no, no-no-no-no
She says I am the one, but the kid is not my son (no-no-no)
She says I am the one (You know what you did)
She says he is my son (Breaking my heart babe)
She says I am the one

[Tamatisho]

Billie Jean is not my lover
Billie Jean is not my lover
Billie Jean is not my lover
Billie Jean is not my lover
Billie Jean is not my lover (Don't call me Billie Jean)

Billie Jean is not my...

Lyrics za wimbo wote wa Call Me Maybe wa Carly Rae Jepsen ni huu hapa chini

[Shairi la Kwanza]
I threw a wish in the well
Don't ask me, I'll never tell
I looked to you as it fell
And now you're in my way
I trade my soul for a wish
Pennies and dimes for a kiss
I wasn't looking for this

But now you're in my way

[Kibwagizo-Tangulizi]

Your stare was holding
Ripped jeans, skin was showin'
Hot night, wind was blowin'

Where you think you're going, baby?

[Kibwagizo]

Hey, I just met you, and this is crazy
But here's my number, so call me maybe
It's hard to look right at you, baby
But here's my number, so call me maybe
Hey, I just met you, and this is crazy
But here's my number, so call me maybe
And all the other boys try to chase me

But here's my number, so call me maybe

[Shairi la Pili]

You took your time with the call
I took no time with the fall
You gave me nothing at all
But still you're in my way
I beg and borrow and steal
At first sight and it's real
I didn't know I would feel it

But it's in my way

[Kibwagizo-Tangulizi]

Your stare was holding
Ripped jeans, skin was showing
Hot night, wind was blowing

Where you think you're going, baby?

[Kibwagizo]

Hey, I just met you, and this is crazy
But here's my number, so call me maybe
It's hard to look right at you, baby
But here's my number, so call me maybe
Hey, I just met you, and this is crazy
But here's my number, so call me maybe
And all the other boys try to chase me

But here's my number, so call me maybe

[Kivuko]

Before you came into my life, I missed you so bad
I missed you so bad
I missed you so, so bad
Before you came into my life, I missed you so bad
And you should know that

I missed you so, so bad

[Pumziko]
It's hard to look right at you, baby
But here's my number, so call me maybe

[Kibwagizo]

Hey, I just met you, and this is crazy
But here's my number, so call me maybe
And all the other boys try to chase me

But here's my number, so call me maybe

[Tamatisho]

Before you came into my life, I missed you so bad
I missed you so bad
I missed you so, so bad
Before you came into my life, I missed you so bad
And you should know that
I missed you so, so bad

So call me maybe

Baada ya tambulisho hizo za sehemu mbalimbali za wimbo, kwa vile post imeshakuwa ndefu sana itabuidi niishie hapa. Makala ijayo nidpo nitaingia ndani Zaidi kuhusu miundo mbalimbali za nyimbo.

Wasomaji wangu wakuu nkumbison, Madaga, Gyole, Extra miles, MzaramoTz ; ingawa post hii ni ndefu, nadhani somo hili kuhusu sehemu za wimbo limeeleweka. Makala ijayo nitaendelea kujadili miundo mbalimbali ya nyimbo kabla sijaanza kujadali namna ya kutunga melodies za nyimbo mbali mbalia.
Pamoja mkuu
 
Nimemaliza makala kuhusu miundoa ya nyimbo, kanzia keshaonitaanza kuelezea taratibu za utunzi melody za muziki unaopenya sana ubongoni mwa msikilazji. Kuna nyimbo ambazo hata zikiwa na mdundo mzuri na video nzuri huwa zina melodies ambazo zinamchosha sana masikizaji na kusahaulika haraka sana, kwa hiyo katika makala zijazo tutazungumzia mambo hayo.
 
Sana tuu Teacher! Tupo Pamoja
 
Nimeelewa sana
 
Nimemaliza makala kuhusu miundoa ya nyimbo, kanzia keshaonitaanza kuelezea taratibu za utunzi melody za muziki unaopenya sana ubongoni mwa msikilazji. Kuna nyimbo ambazo hata zikiwa na mdundo mzuri na video nzuri huwa zina melodies ambazo zinamchosha sana masikizaji na kusahaulika haraka sana, kwa hiyo katika makala zijazo tutazungumzia mambo hayo.
Tunasubiri mkuu, kwa kweli unanisaidia sana
 
Tunasubiri mkuu, kwa kweli unanisaidia sana
Still waitin
Ile article niliyokuwa nimeashatayarisha ilipotea baada ya computer kuzimika; huo uzembe wangu kutosevu. Huwa ninaandika makala hizi katika MSWord, halafu nipo nazihamishia hapa. Safari hii nilifanya makosa ya kuipoteza kabla sijaisevu, na unfortunately hata autosave copy haionekani. Nitaanza tena upya.

Updates:

Samahani nimeweza kupata kipande fulani cha faili lile, ngoja nitakiweka hapa muda mfupi ujao nisije kipoteza tena. Nitaondoa sehemu ambazo bado nilikuwa naandika kusudi niwe na usalama zaidi kenye ile sehemu iliyokwisha kamilika.
 
Hii shule nene sana, sidhani kama kuna chuo cha sanaa hapa nchini kina mwalimu anayeyajua haya.
 
Melody ya Muziki- Melodic Contour and Melodic Motion

Mkong’osio au melody ndiyo sehemu kubwa ya muziki ambayo hukumbukwa sana na wasikilizaji kwani ndiyo inayoingia sana ubongoni mwa msikilazaji; ni muungano wa sauti inayobadilika badilika kwa vipindi mbalimbali kadri muda unavyokwenda. Melody nzuri ni zile zinazofananana na mazungumzo yanayohusisha maswali na majibu; yaani zina vipindi vyenye msukumo au maswali (tension) sana na vipindi vyenye kuondoa msukumo huo au majibu ya maswali (tension release).

Post hii isome kwa makini sana kwa sababu ndiyo inajenga msingi wa kutunga nyimbo zinazoweza kuingia sana kwenye ubongo wa msikilizaji na hivyo zikawa za kukumbukwa kwa muda mrefu sana. Nadhani sehemu hii ndiyo ambayo wanamuziki wetu wengi sana hawajui, kwani nimechambua nyimbo zao nyingi na kuona kama zinatungwa kwa uvumbuzi (intuition) tu na mara nyingi haziangalii ukweli huu. Jikumbushe tena maana ya phrase na measure kwenye wimbo kama tulivyozijadili huko nyuma.

Kumbuka tena kuwa katika sauti zote 12 za kwenye Octave moja ni sauti saba tu zinazoshabihiana, ambazo mwanzoni tulizionyesha kwa namna za kirumi I-II-III-IV-V-VI-VII, tukimalizia na sauti ya nane VIII ambayo ni sauti ya kwanza kwenye kwenye Octave inayofuata. Zile sauti 12 za octave hujulikana pia kama chromatic scale, wakati sauti hizo saba zinazoshabihiana hujulikana kama diatonic scale. Sauti hizi za diatonic scale kuanzia ya chini hadi ya juu ndizo zina majina kama ifuatavyo kwenye jedwali hili:

SautiJinaMatumizi
ITonicSauti za kupumzikia; hutumika mwanzo na mwisho wa phrase moja
IISupertonic
IIIMeadiantSauti za kuhama kutoka na kuingia kwenye tonic
IVSubdominant
VDominantSauti za Kuchangamsha, yaani zenye msukumo sana
VISubmediant
VIILeading tone
VIIINext tonicSauti ya kupitia kuingia na kutoka kwenye octave inayofuata.

Kwenye utunzi wa melody sauti hizi zimegawanywa katika mafungu mawilii; yaani stable tones na unstable tones. Sauti za Tonic, Mediant na Dominant ndiyo ndiyo stable tones, halafu zile Supertonic, Subdominant, Submediant, na Leading tones ni unstable tones. Tonic (I) ni stable zaidi ikifuatiwa na Dominant (V) na kuishia na Mediant (III) kwa stability. Sauti ya Leading note (VII) ndiyo ambayo ni unstable zaidi ikifuatiwa na Sebmediant (IV) halafu Supertonic(II) na kuishia na Subdominant (VI). Picha hii hapa chini inaonyesha mlingano wa stability katika sauti hizo.

1566046162182.png

Kwa waliofanya physics ya pendulum ukihusisha na potential energy, mnajua kuwa pendulum bob ikiwa inaning’ia freely chini ya kamba yake inakuwa stable kwa sababu potential energy ni ndogo sana; ukiiacha katika nafasi hiyo, itabaki imepumzika pale pale, ila ukiihamisha kutoka hiyo nafasi stable, basi itaanza kuswing kujaribu kurudi kwenye stable position yake. Ina maana unapoihamisha kutoka kwenye stable position yake basi unaiweka kwenye unstable position ambayo siyo comfort zone yake.
1566046307306.png

Sauti za diatonic scale pia zina tabia hiyo hiyo, hizo unstable tones zinakuwa zinamfanya msikilizaji atake zirudi kwenye kweye stable tones. Siku zote Leading tone itapenda kuingia kwenye Dominant, na Submediant nayo itapenda kuingia kwenye Dominant. Sauti za Subdominant nazo zitapenda kwenda kwenye Dominat kwa vile ni stable zaidi ya Mediant; hata hivyo zinaweza kwenda kwenye Mediant na kukubalika. Supertonic nazo zitapenda zaidi kwende kwenye tonic kwa vile hiyo ni stable zaidi ya median, lakini pia zinaweza kuingia kwenye mediant na kukubaliwa bila matatizo yoyote.

1566046390312.png

Kama tulivyosema huko nyuma wimbo mzuri huanza kwa sauti za Tonic au Supertonic lakini pia unaweza kuanza na Dominant kwa vile nayo ni stable tonic, lakini ni lazima kushia na sauti za Tonic kwa vile hiyo ndiyo sauti stable kuliko zote. Kutoka kwenye sauti stable na kelekea kwenye sauti unstable kunaweka msukumo mkubwa yaani tension ambayo humfanya msikilizaji atake iondolewe kurudi kwenye stable tena, ambayo ndiyo comfort zone ya ubongo; kipindi hicho cha sauti kuwa unstable kinajulikana kama Continuation, kwamba ukishaiingia kwenye unstable tone, basi msikilizaji anategemea uendelee ili urudi kwenye stable tone tena. Continutiation hutokea sehemu yotote katikati ya phrase, kabla phrase haijaisha lazima tension iondolewe kwa kiasi fulani. Wakati tension inaondolewa, inaweza kurudi kwenye stable kabisa yaani Tonic au kwenye less stable za Dominant au Mediant. Mapumuziko katika stability tone ya tonic inaitwa Finality, yaani hali inayomuashiria msikilizaji kuwa mambo yamekwisha. Mapumizko katika satuti za Dominant au Submediant yanajulikana kam Temporary repose, yaani mapumziko mafupi yanayompa msikilizaji nafasi ya kupumua akijua kuwa safari bado inaendelea.

Kwa kawaida melody nzuri hairudi kwende Tonic kabla shairi lote halijaisha, kwa hiyo wakati wa kumaliza phrase ndani ya shairi unaweza kuingia kwenye Mediant au Dominant, yaani temporary repose lakini usiashiririe finality. Kuondoa tension kabisa, yaani finality, hutokea mwisho kabisa wa shairi ambapo ndipo unarudi kwenye Tonic. Melody inatakiwa iwe inamjaza msikilizaji tension yaani upepo, na kuuondoa kidogo na kujaza tena na kuondoa kidogo hadi kufikia mwisho ndipo unaaondoa upepo wote na kufanya ubongo upumzike tena. Mambo haya ya kumjaza msikilizaji upepo na kuuonda hufanyika pia kwenye Vibwagizo Tangulizi, Vibwagizo na Vivuko; Utangulizi ni sauti unstable tu, Tamatisho ni saut stable tu. Mapumuziko pia yanachanganya sauti stable na unstable tu lakini hayana finality, yote yanaishia na temporary repose. Kwa vile Vibwagizo tangulizi vinamtayarisha msikilizaji kuskia kibwagizo, huwa haviishii na Tonic, vinaweza kuishia na Mediant au Dominant.

Melodic Motion na Melodic Contour

Mtungaji wa wimbo, iangalie melodi kama safari ya kupanda mlima wenye maumbile (contour) mbalimbali zenye vilima na mabonde yanayoruhusu mapumziko kidogo ndani na kisha mwishoni ni kushuka chini kabisa; safari hiyo hujulikana kama melodic contour. Upandaji, mapumziko na kushuka huo mlima hujulikana kama melodic motion. Kila utunzi una contour yake; safari inaweza kuanza kwa kuingia bondeni kabla ya kupanda tena, na vile vile inaweza kuanza kwa kurukia juu kabisa ya mlima na baadaye kuanza kutua. Contours zenye tension (contiuation) nyingi na mapumziko ya kati (temporary repose) mengi kabla ya kufikia mwisho (finality) hufanya ubongo wa msikilizaji kuwa busy sana na iwapo unapanda kwa spidi sana, yaani kama BPM yake ni kubwa sana basi unaweza kumchosha kuzikiliza haraka sana. Kukiwa na uwiano mzuri kati ya BPM na wingi wa vilima na mabonde kwenye controur hiyo, basi msikilzaji ataburudika sana na ataupenda sana wimbo huo.

Melodic contour nzuri ni ile yenye mlingano mzuri kati kupanda na kushuka na ina kilele (peak au sauti ya juu kabisa) kimoja tu, ambacho kinatakiwa kwenye sehemu ya pigo moja kubwa kwenye rhythm yako. Tofauti kati ya sauti ya chini kabisa sauti ya juu kabisa huitwa range. Melodic contours zenye range kubwa ndizo zenye tension sana na vile vile ndizo zinazosisimua sana kuliko zile zenye range ndogo. Mifano ya michache ya melodic Contours ni kama hizi zifiatayo; kila sehemu tambarare (plateau) ni sehemu ya kuondolea tension na kwenye slope ni sehemu yenye kujaza tension.
1566047226822.png
1566047243280.png

Mahairi ya wimbo wa Kwangaru wa Harmonize yanatumia melodic contour rahisi kama hii lakini yana peak moja kwa kila shairi, na range ya wimbo ni kubwa sana, ndiyo maana wimbo huo umekubalika sana, hauchoshi kirahisi.
1566047343289.png

Ingawa kibwagizo chake kina contour tofauti.

Kwenye mwendo huo wa melodic motion, kutoka point moja hadi nyingine, sauti zitakuwa zinabadilika kwa kutumia mojawapo ya style nne: (a) sauti zinazojirudia (repeats) kwa mfano kutoka sauti C hadi sauti C tena; (b) sauti zinazoruka kwa noti moja moja kwenda juu au chini (steps) kwa mfano kutoka sauti C mpaka sauti D kwenye C-major; (c) sauti zinazoruka noti mbili kwenda juu au chini (skips) kwa mfano kutoka sauti C mpaka sauti E kwenye C-major, na (d) sauti zinazoruka zaidi ya noti mbili kwenda juu au chini (leaps) kwa mfano kutoka sauti C mpaka sauti G kwenye C-major. Picha hii inaonyeshaa style hizo.

1566047447130.png

Ili kupata uwiano mzuri kati kati ya kupanda na kushuka kwenye contror yako, ukianza na steps kadhaa za kwenda upande mmoja, basi jaribu kuweka skips au leaps za kurudi upande ulikotoka kidogo kabla ya kurudi kwenye upande wa kwanza tena kama bado unaendelea, ila bila kuingia kwenye sauti stable tones. katika kufanya hivyo, punguza sana matumizi ya repeats kadri iwezekanavyo, na vile vile usiwe na steps nying sana usije ukashindwa kumsimumua msikilazaji wako.

Kati ya mapungufu makuu ya wimbo wa Diamond wa My Number one original ni kuwa una steps na repeats nyingi sana na vile vile hauna peak inayojulikana wazi wazi kwenye kila phrase, yaani range yake ilikuwa ndogo sana; hivyo ilikuwa ni rahisi kwa wimbo huo kuchosha msikilizaji wake haraka sana. Remix waliyofanya Davido ilirekebisha sana makosa hayo wakabadilisha steps nyingine kuwa skips na hivyo kuweza kuwa na peak kubwa kidogo kuliko mwanzo. Kupendwa wa My Number One remix hakutokani na davido tu bali vile vile ile balance ya tension na tension release iliyokuwapo kwenye wimbo huo tofauti na ule original ambao haukuwa na tension kabisa.

Katika Makala ijayo, nitaongelea dhana tatu kubwa kabla ya kuanza kutunga melodies zetu wenyewe na kuchambua melodies za waimbaji wengine; dhana hizo zitakuwa ni articulation, melodic motiffs na melodic phrases.

Tuendelea kutumia sauti za diatonic major na minor scales tu japokuwa kuna scales nyingine nyingi ambazo siyo diatonic (non diatonics scales), na ambazo siyo diatonic ambazo siyo major au major au minor (zinaitwa diatonic scale modes), lakini kama nilivyotambulisha huko nyuma, mambo hayo tatawaachia maveterani tu. Sisis tutatumia diatonic major na diatonic minor tu.

Wasomaji wangu wakuu nkumbison, Madaga, Gyole, Extra miles, MzaramoTz , Frega Bao,MRI; nadhani mjadala huu hili kuhusu melodic motion na melodic contours za nyimbo umeeleweka. Nimegundua kuwa kabla ya kuanza mjdala juu ya utungaji wa mkong'osio wa wimbo bado kuna mambo ya msingi kujadilia.katika mada ijayo tutajadili articulation, melodic motiffs na melodic phrases
 
Back
Top Bottom