Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,529
- 19,384
- Thread starter
- #41
Muziki mwingi ni kipaji cha kuzaliwa nacho, lakini kipaji hicho kikichanganywa na utaalamu basi matokeo yanakuwa ni mazuri zaidi. Kuna waimbaji kadhaa ambao vipaji vyao ni vya juu sana na viko kweye taaluma kabisa na wala hawahitaji mtaalamu mwingine, lakini kama huna utaalamu huo, ni vizuri kutafuta mtaalamu kukuthibitishia tungo zako ili uingie kwenye ushindani kikamilifu. Waimbaji wengi wa kimarekani wana watu maalumu wa kuwatungia nyimbo kitaalamu, kwa mfano mtunzi wa nyimbo nyingi za Michael Jackson alikuwa ni Quincy Jones, na vile vile maproducer wengi ni wataalamu wa muziki kwa hiyo hata ukitunga wimbo wako kutokana na kipaji chako kinavyokutuma, wao wataunyoosha na kuuweka katika misingi ya kitaalamu kabla ya kuutoa.Diamond na Ali Kiba mnayajua haya? Ama kwa hakika muziki ni kipawa kutoka kwa Mungu