Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,546
- 19,408
- Thread starter
- #21
MIZANI KUU ZA MUZIKI (Major Scales- cont'd)-TOLEO LA PILI
Katika toleo hili tutaangalia major scales zenye flats; zote pia huundwa kwa sauti zinazoruka hatua kwa mfumo KKN-K-KKN. Note za asili kwenye Octave zinakuwa ni C- D♭-D- E♭-E-F- G♭-G - A♭- A- B♭-B-C wakati zile sharp zimebadilishwa na flat zenye sauti sawa. Vile vile tunaanza na mizani ya kwanza ambayo ni C-major, halafu mizani inayofuata inatumia sauti ya nne ya sauti iliyopita ikiwa na flat kwenye mizani hiyo;
C-Major
Hii mizani ya C-major tumeiona katika toleo lililopita. Haina sharp wala flat yoyote ikiwa na sauti za C-D-E-F-G-A-B-(C ). Mizani inayofuatia ikiwa na flat itakuwa ni F-major kwa vile sauti ya nne katika C-Major ni F
Labda niongezee kwenye maelezo yangu ya awali kuwa wimbo wa It's All Coming Back To Me Now wa Céline Dion umo katika C-major, lakini unatumia sauti zinazojaza Octave mbili na nusu.
F-Major
Ukichukua sauti za asili zinazoanza na sauti ya F utakamilisha mizani kwa kutumia OCTAVE mbili zenye sauti F- G♭-G - A♭- A- B♭-B- C- D♭-D- E♭-E-F. Kwa hiyo ukichagua sauti za kufuata mtindo huo huo wa KKN-K-KKN utapata mzani wenye sauti za F – G – A – B♭ – C – D – E – F ambamo sauti B ni flat; hii inaonyeshwa kwa kuwekwa alama ya flat kwenye mstali wa kwanza kutoka juu kwenye note B. Scale yenye flat inayofuatia hii itakuwa ni B♭-major kwa vile sauti ya nne kwenye F-major ni B♭.
Nyimbo za Blank Space wa Taylor Swift na Locked Out of Heaven wa Bruno Mars zimeimbwa katika mizani hii ya F-Major. Labda niongezee pia kuwa wimbo wa Taifa wa Tanzania nao pia umeibwa katika F-major:
B♭-Major
Ukichukua sauti za asili zinazoanza na sauti ya B♭ utakamilisha mizani kwa kutumia OCTAVE mbili zenye sauti B♭-B- C- D♭-D- E♭-E- F- G♭-G - A♭- A- B♭. Kwa hiyo ukichagua sauti za kufuata mtindo huo huo wa KKN-K-KKN utapata mzani wenye sauti za B♭ – C – D – E♭ – F – G – A – B♭ ambamo sauti za B na E ni flat. Scale yenye flat inayofuatia hii itakuwa ni E♭-major kwa vile sauti ya nne kwenye B♭-major ni E♭.
Nyimbo za Irreplaceable wa Beyoncé na Rocket Man wa Elton John zimeimbwa katika mizani hii ya B♭-Major.
E♭-Major
Ukichukua sauti za asili zinazoanza na sauti ya E♭ utakamilisha mizani kwa kutumia OCTAVE mbili zenye sauti sauti E♭-E- F- G♭-G - A♭- A- B♭- B- C- D♭-D- E♭. Kwa hiyo ukichagua sauti za kufuata mtindo huo huo wa KKN-K-KKN utapata mzani wenye sauti za E♭ – F – G – A♭ – B♭ – C – D – E♭ ambamo sauti za A, B na E ni flat. Scale yenye flat inayofuatia hii itakuwa ni A♭-major kwa vile sauti ya nne kwenye E♭-major ni A♭.
Nyimbo za In My Head wa Jason Derulo na Valerie wa marahemu Amy Winehouse zimeimbwa katika mizani hii ya E♭-Major.
A♭-Major
Ukichukua sauti za asili zinazoanza na sauti ya A♭ utakamilisha mizani kwa kutumia OCTAVE mbili zenye sauti A♭- A- B♭- B- C- D♭-D- E♭-E- F- G♭-G-A♭. Kwa hiyo ukichagua sauti za kufuata mtindo huo huo wa KKN-K-KKN utapata mzani wenye sauti za : A♭ – B♭ – C – D♭ – E♭ – F – G – A♭ ambamo sauti za A, B,D, na E ni flat. Scale yenye flat inayofuatia hii itakuwa ni D♭-major kwa vile sauti ya tano kwenye scale hii A♭-major ni D♭.
Nyimbo za Happy wa Pharrell Williams na The Power of Love wa Céline Dion zimeimbwa katika mizani hii ya A♭-Major.
Mizani zinazofuata nimeziweka kwenye rangi tofauti pia kama kwenye toleo lililopita kwa vile tutaziangalia tena huko baadaye, kuona kuwa zinafanana na mizani nyingine; zinajulikana kama Enharmonic Major Scales
D♭-Major
Ukichukua sauti za asili zinazoanza na sauti ya D♭ utakamilisha mizani kwa kutumia OCTAVE mbili zenye sauti D♭-D- E♭-E- F- G♭-G-A♭- A- B♭- B- C- D♭. Kwa hiyo ukichagua sauti za kufuata mtindo huo huo wa KKN-K-KKN utapata mzani wenye sauti za D♭ – E♭ – F – G♭ – A♭ – B♭ – C – D♭ ambamo sauti za A, B, D, E, na G ni flat. Scale yenye flat inayofuatia hii itakuwa ni G♭-major kwa vile sauti ya tano kwenye D♭-major ni G♭.
Kwa vile scale hii ya D♭ ni sawa kabisa na scale ya ya C# kama tutakavyoona kwenye post inyofuata, basi nyimbo za Nyimbo za Sacrifice wa Elton John, na Umbrella wa Rihanna zilizoimbwa katika mizani ya C-Sharp zimo pia katika mizani hii ya D♭-Major.
G♭-Major
Ukichukua sauti za asili zinazoanza na sauti ya G♭ utakamilisha mizani kwa kutumia OCTAVE mbili zenye sauti G♭-G-A♭- A- B♭- B- C- D♭-D- E♭-E- F-G♭. Kwa hiyo ukichagua sauti za kufuata mtindo huo huo wa KKN-K-KKN utapata mzani wenye sauti za G♭ – A♭ – B♭ –(B) C♭ – D♭ – E♭ – F – G♭ ambamo sauti za A, B, C, D, E, na G ni flat. Angalia kuwa sauti ya nne (B) imegeuzwa kuwa C-flat kusudi kusiwe na B mbili zenye mkazo tofauti- C flat ni sawa na B. Scale yenye flat inayofuatia hii sasa itakuwa ni C♭ -major kwa vile sauti ya tano kwenye G♭ -major ni hiyo ya C♭.
Kwa vile scale hii ya G♭ ni sawa kabisa na scale ya ya F# kama tutakavyoona huko mbele pia, basi nyimbo za Nyimbo za Beat it wa Michael Jackson, Rude Boy wa Rihanna na Born this way wa Lady gaga zilizoimbwa katika mizani ya F-Sharp Major zimo pia kwenye mizani hii ya hii ya G♭-major.
C♭ -Major
Ukichukua sauti za asili zinazoanza na sauti ya C♭ utakamilisha mizani kwa kutumia OCTAVE mbili zenye sauti (B)C♭ C- D♭-D- E♭-E- F-G♭-G♭-G-A♭- A- B♭-(B)C♭ . Kwa hiyo ukichagua sauti za kufuata mtindo huo huo wa KKN-K-KKN utapata mzani wenye sauti za C♭ – D♭ – E♭ – F♭ – G♭ – A♭ – B♭ – C♭ ambamo sauti zote ni flat.
Scale hii haitumiwi sana na wanamuziki.Katika nyimbo maarufu zinazojulikan, sijawahi kusikia wimbo uliotolewa kuwa ni C♭ -Major, ila kunakuwa na nyimbo za B-major, kwa vile hizi ni scale zinazofanana kama nitakavyoeleza huko baadaye basi nyimbo zote za B-major pia ni za C♭ -Major.
Baada ya hapo, mizani ya F♭ haiwezekaniki kwa sababu kama tulivyoongea kutokuwezekana mizani ya G♯- huko nyuma.