Elimu na nadharia ya muziki

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
15,297
18,896
Post zangu kwenye thread hii zitakuwa ni ndefu kidogo kwa kina kuliko nilvyozowea kuandika. Mara kwa mara zitakuwa zinaambatana na video za Youtube kusupport maneno yangu. Zisome ukizingatia hali hiyo.

Muziki ni mtiririko wa sauti zilizopangwa kwa urefu wa muda tofauti tofauti ili kutuma ujumbe fulani wa kisaikolojia na kifiziolojia kwenye mwili wa msikilizaji. Inaaminika kuwa mawasiliano ya kwanza ambayo binadamu huzaliwa nayo ni muziki. Watoto wanapozaliwa hujua miziki miwili tu: kulia na kucheka






Ingawa vicheko vya watoto vina ujumbe mmoja tu kuwa nimefurahi, vilio vyao huwa vinatuma jumbe mbalimbali, akina mama wazazi wao huzeielewa jumbe hizo haraka sana. Kuna jumbe za kusema nimechoka, kuna jumbe za kusema sikutaki, na kadhalika, kama inavyoelezwa hapa



Nimeanzisha thread hii ili kujadiliana utaalamu wa muziki kwa kutumia Kiswahili rahisi. Binafsi nitaitumia kwanza kuelezea nadharia ya muziki kadri ninavyoielewa ambayo nina imani kuwa kuna wanaoifahamu vizuri zaidi na wasioifahamu kabisa. Ninataka kulenga wale wasioifahamu, hasa vijana chini ya miaka 30.

Baada ya kupitia nadhania hiyo, nitaiunganisha na tungo mbalimbali zilziowahi kutokea na kuzichambua kelezea kwa nini tungo fulani za muziki hupendwa na wasikilizaji kwa muda mrefu sana na nyingine huingia sokoni na kutoweka kama vile hazikuwahi kuwepo.

Karibuni
 
MUSICAL NOTES -1 (OCTAVES)

Kama nilivyofungua thread hapo juu, muziki ni mpangilio wa sauti zenye kudumu muda tofauti tofauti kuweza kutuma ujumbe fulani kwa msikilizaji. Sauti tofauti kwenye muziki hutofautiana makali (pitch) ambapo kila ukali wa sauti unaitwa noti (note). Kuna noti kumi na mbili za asili zinazoweza kutumika kwenye muziki ambazo kila keyboard au chombo chochote cha muziki kinaweza kutoa kama ilivyoonyeshwa kwenye picha ya keyboard hapa chini. Sauti hizi kumi na mbili kwa pamoja zinaitwa Octave moja ambapo iwapo sauti zote zikitumika basi hujulikana kama Chromatic Octave. Ukali wa sauti hupanda kutoka sauti za chini hadi sauti za juu, kwa hiyo chombo kimoja kinaweza kumudu Octave zaidi ya moja kwa mfano piano moja inaweza kuwa na Octave nyingi kama ionekenavyo kwenye picha hii hapa chini.

1149533


Kuna vyombo vyenye Octave moja tu kwa mfano flute yenye mashimo sita na vingine ambavyo havikamilishi Octave yoyote kama vile ngoma ambayo ina note moja tu.
1149534


Kwa vile kila ngoma ina noti moja tu, basi ili kuweza kuwa na note nyingi za ngoma, inabidi kutumia ngoma kadhaa zanye ububwa tofauti katika kundi linaloitwa drum set.
1149535



Octaves zimegawawanyika katika aina sita za saba kama ifutavayo hapa:

(1) Sauti za kwanza ni juu na nyororo sana ambazo mara nyingi ni za wasichana wadogo; hizi huitwa Soprano. Sauti hizi hutumika sana kwenye uimbaji wa miziki ya Opera kama hapa



(2) Sauti zinazofuata huitwa Mezzo-soprano, hizi pia ni za wanawake sana ingawa wanaume pia huweza kuziimba lakini huwa hawaendi mbali sana. Mfano wa uimbaji wa Mezzo-soprano ni huu wa sarah Brightman



na huu wa Mbilia Bel ingawa uliimbwa na Nana Akumu Bolengo



(3) Sauti za tatu ni Contralto au Alto. Sauti hizi pamoja na zile za nne na za tano hapa chini ndizo zinazoimbwa na waimbaji wengi sana. Wanawake wengi sana wanaoimba sauti za zao asili bila kuzibana kama vile Madonna, Rihanna, na Ray C huimba sauti hizi.





Kuna wanaume pia wanaoimba sauti hizo, lakini huwa wanachanganya na countertenor kama nitakavyoeleza hapa chini.

(4) Sauti za nne ni Countertenor. Waimbaji wengi sana wa kiume duniani huimba sauti hizi za countertenor, wakiwa ama wanaruka kidogo kuingia kwenye alto, au kutelemka kidogo kuingia kwenye tenor. Waimbaji wengi wa namna hii (siyo wote) hutumia nguvu sana kuimba kwa sababu wengi wao huwa hawaimbi katika sauti zao za mapumziko. Hawa ndio waimbaji unaweza kusema kuwa sauti zao za maongezi hazifanani kabisa na wanavyoimba. Waimbaji kama Mbaraka Mwishehe (alikuwa akichanganya kidogo kigogo Countertenor na tenor), Diamond (anachanganya sana Countertenor na tenor), Alikiba (anachanganya sana Countertenor na Alto), na Usher Raymond






(5) Sauti za tano ni Tenor. Hizi ni sauti asili za wanaume; waimbaji wengi wa kiume Nigeria wanaimba sauit hizi, kwa mfano Davido na P-Square kabla hawajagawanyika. Wengi wa waimbaji hawa huwa hawana mashaka kabisa na sauti zao, kwa hiyo huwa hawafanyi modification yoyote kwenye sauti hizo.




(6) Sauti za sita ni Baritone. Hizi ni sauti nzito za wanaume zinazoimbwa na wanaume wengi ambao hawana mashaka kabisa na sauti zao; kwa mfano Elvis Presley na Jose Chameleone.




(7) Sauti za saba ni Bass. Hizi nazo ni sauti za kiume, lakini ni vigumu kumpata mwimbaji anayeimba bass tupu, waimbaji wengi wa bass huimba kati ya bass na baritone. Kwa mfano Jim Reeves na Nat King Cole wote walikuwa wanaimba kati ya bass na baritone
 
MUSICAL NOTES -1 (OCTAVES -Cont'd)

Kwa vile sikuweza kuweka media zaidi ya 15 kwenye post moja, post iliyopita itaendelea hapa chini.


Mwimbaji mwengine aliyekuwa akiruka kati ya bass na baritone ni huyu Nat King Cole hapa.




Kuna waimbaji kadhaa ambao wana kipaji cha kuimba Octave tatu na zaidi kwa kwa mfano Celine Dione na Luis Fonsi. Celine Dione aliiimba Soprano, Mezzo-Soprano na Alto kwa pamoja kwenye wimbo huu



wakati Luis Fonsi aliiimba Alto, Countertenor, Tenor na Baritone katika wimbo huu






Mifano niliyoweka hapa ni ile inayotumia sauti halisi za waimbaji zikiwa na mashairi kamili bila kuwa electronically modified. Imekuwa ni vigumu kupata mifano ya waimbaji wa siku hizi ambao ni maarufu kwa sababu mbalimbali. Kwa mfano waimbaji wa rap kama vile Kanye West, Jay Z, A.Y., au wale wanaoimba kama viongezo vya rap tu au wale ambao sauti zao zinakuwa za kielectronic Zaidi kama Vanessa Mdee.



Katika post ijayo nitaongelea namna ya kutumia Octave ya muziki kutokana na hizi sauti kumi na mbili kuunda kitu kinaitwa Musical Scale; yaani mchanganiyko wa sauti zinakubalianana katika wimbo mmoja kwenye kila Octave, na jinsi gani matumizi ya sauti zisizokubaliana katika Octave huweza kutoa Muziki ambao hauingii vizuri kwenye ubongo wa msikilizaji na ni rahisi kuchosha wasikilizaji wake haraka sana. Mifano ya miziki inayoshindwa kukidhi mahitaji ya mchanganyiko huo wa sauti zinazokubaliana kwenye Octave moja ni kama zile sauti za kwenye wimbo wa U-2 hapa chini ambao ulikuwa na biti nzuri lakini haukukubalika kabisa



Hapa Tanzania kuna nyimbo nyingi za namna hiyo, kwa mfano wimbo huu Diamond na wa Jay Dee ambazo zina tungo na mashairi mazuri, biti nzuri lakini zinachosha bongo za wasikilazji wake haraka sana. Zipo nyimbo nyingi Tanzania za aina hiyo ila nimechagua hizi mbili tu kwa vile waimbaji wake ni maarufu sana.



 
Najifunza
Karibu sana; kama unapenda kujua misingi ya tungo nzuli za muziki basi umefika nyumbani. Kutakutakuwa na post kila baada ya siku kama mbili hivi kwa vile nyingine zinahitaji kukusanya video za kutumia kama mifano- kama ulivyoona hapo juu.
 
MUSICAL NOTES-2 (SCALES)

Kama nilivyosema hapo juu Octave moja ina jumla ya sauti kumi na mbili za asili. Katika hiyo namba, ni sauti saba tu zinazoshabihiana na zinaweza kutumika katika wimbo mmoja; hivyo kuna sauti ambazo hazikubaliki. Watu wanaweza kushangaa kusikia kuwa mpangilio wa sauti hizi unafuata mahesabu za Abstract Algebra. Sauti hizi zipo katika algebraic structure inayoitwa Abelian Group lakini sitawapeleka huko.

Sauti zinazokubalika katika muziki ni zile tunazoweza kuimba

DO-RE-MI-FA-SO-LA-TI-(DO)

wakati hii DO nyekundu ya mwisho inajulikana kuwa sauti ya kufungia na huwa inatoka katika OCTAVE inayofuata, zile DO-RE-MI-FA-SO-LA-TI ndiyo sauti saba za OCTAVE moja. Kwa ujumla sauti zote zinakuwa ni nane; yaani saba kutoka OCTAVE husika na moja kutoka OCTAVE inayofuata; zote zimepewa namba za kirumi kama ifuatavyo:

I-II-III-IV-V-VI-VII-VIII

Sauti za DO-RE-MI-FA au I-II-III-IV zinaitwa lower tetrachord (tetrachord ya chini), wakati sauti za SO-LA-TI-DO au V-VI-VII-VIII zinaitwa upper tetrachord (tetrachord ya juu). Tetrachords hizi mbili kwa pamoja zinaunda kitu kinachoitwa mizani ya muziki (music scale). Kila mizani ina sauti zenye majukumu matatu; sauti za kupumzikia, sauti za kuchangamisha, na sauti za mpito baina ya kupumzika na kuchangamka.

Kabla ya kuelezea sauti hizi nane zinachaguliwa vipi kutokana na zile sauti 12 za asili kuunda mizani moja, ngoja kwanza tujaadili tabia na matumizi ya sauti hizo nane katika mizani moja kama ifuatavyo:
  1. Sauti I na Sauti II huitwa Tonic na Supertonic: Hizi sauti ni za kupumzikia kwenye wimbo kiasi kuwa shairi linatakiwa lianze na sauti hizi na vile vile kuishia na sauti hizi katika hali ya kupumzika.
  2. Sauti III na Sauti IV huitwa Mediant na Subdominant: Hizi ni sauti za kupitia kutoka au kuingia kwenye sauti za mapumziko.
  3. Sauti V, VI na sauti VII zinaitwa Dominant, Submediant, na Leading note. Hizi ndizo sauti za kuchangamsha shairi. Sehemu kubwa ya shairi inatakiwa iwe katika sauti hizi.
  4. Sauti VIII pia ni Tonic (next Octave). Sauti hii hutumika tu iwapo wimbo unatumia Octave mbili, ambapo ni lazima mwendo wa kutoka Octave moja kwenda nyingine upitie sauti hii.
Nyimbo ambazo huwa hazikidhi tabia hizi huwa ama hazichangamshi au zinachosha msikilazji. Na hata zile zinazochangamsha huwa hazikai katika kumbukumbu za msikilizji wake kwa muda mrefu. Kwa mfano, wimbo huu wa Diamond una matatizo mawili makubwa. Tatizo la kwanza ni kuwa unaimbwa katika Octave mbili, lakini transitition kutoka Octave moja hadi nyingine ni ya kasi sana. Yaani haupitii kwenye Tonic au subtonic ya Octave inayofuata. Tatizo la pili ni kuwa kwa vile unaimbwa katika OCTAVE mbili, umeanzia kwenye median na subdominant moja kwa moja bila kuwa na sauti za tonic/supertonic za kuanzia. Kwa hiyo wimbo wote umekosa sauti za tonic na supertonic, na hivyo ni rahisi sana kusahaulika na vile vile unaweza kuwachosha wasikilazaji wake haraka sana.



Ni vigumu kuyatambua matatizo hayo bila kujua namna ya kuchagua sauti za kutumika katika wimbo, kwa vile hiyo siyo kazi ya haraka haraka kama maelezo ya hapo juu yanavyoweza kuwa yanaashiria kwani kiuhakika hakuna tafsiri kamili ya mwanzo na mwisho wa mzani mmoja; mzani inaweza kuanza na sauti yoyote ile kama tutakavyoona huko mbele. Iwapo mtunzi wa wimbo huo hapo juu alitaka wimbo uwe katika Octave moja, basi hakuchagua sauti zinazoshabihiana katika Octave hiyo. Katika post ijayo nitajadili namna ya kuchagua sauti za mzani.
 
Karibu sana; kama unapenda kujua misingi ya tungo nzuli za muziki basi umefika nyumbani. Kutakutakuwa na post kila baada ya siku kama mbili hivi kwa vile nyingine zinahitaji kukusanya video za kutumia kama mifano- kama ulivyoona hapo juu.
Ahsante
 
MUSICAL NOTES -3 (SCALES -Cont'd)

Ili kuweza kutambua sauti za kutumia kwenye mzani mmoja katika octave yoyote inabidi tuingie ndani kidogo kwenye nadharia ya muziki. Nadharia hiyo hutoa kanuni mbili kuu kama ifuatavyo:

Kanuni ya Kwanza: Sauti asili kwenye kwenye OCTAVE moja zinatofautiana kwa nusu hatua (Half Steps) au Semitones. Nusus hatua mbili zinaunda hatua kamili (full step) au Tone. Kwa hiyo Octave moja ina hatua tano na nusu kama inavyoonekana katika jedwali hili, iwapo utachukulia kuwa sauti ya kwanza ni hatua sifuli (Wengine hutafsiri kuwa sauti ya kwanza ni hatua ya kwanza pia, na hivyo kuwa na hatua sita na nusu).

Sauti123456789101112
Hatua00.511.522.533.544.555.5


Kanuni ya pili: Sauti zinazokubaliana katika OCTAVE moja zinapishana kwa kufuata mipangilio ya aina mbili. Mpangilio wa kwanza unaitwa major scale (mizani kuu), na mpangilio wa pili unaitwa minor scale (mizani ndogo).

Mpangilio wa major scale unakwenda kwa hatua za KKN-K-KKN, yaani K ni kuruka hatua kamili, na N ni kuruka nusu hatua. Kila KKN ni tetrachord moja, halafu -K- iliyopo kati ya tetrachord ya chini na tetrachord ya juu ni hatua kamili inayounganisha tetrachords hizo. Kwa hiyo iwapo sauti ya kwanza kwenye OCTAVE ni sauti asili namba 1, sauti asili zitakazoshabihiana katika octave hiyo kwenye major scale ni sauti za 1,3,5,6,8,10,12, (1). Wakati (1) ni sauti ya kwanza kwenye OCTAVE inayofuatia. Major scale ina sauti zote zilizozungumziwa hapo juu: kupumizikia, mpito na kuchangamsha.

Minor scales pia zina sauti hizo tatu: kupumizikia, mpito na kuchangamsha. Ila sauti za kuchangamsha kwenye minor scale siyo kali sana kama zile za kwenye major scale; ndiyo maana nyimbo nyingi za minor scale huwa ni za majonzi. Kuna aina tatu za minor scales: natural minor, harmonic minor, na melodic minor. Scale ambayo ni maarufu zaidi ni ile ya Natural minor scale. Harmonic na Melodic minor scales ni modification ndogo tu kwenye natural minor kwa kuuongesa msisistizo ama sauti ya saba au sauti ya sita na ya saba kwa pamoja. Ingawa nyingi zinatumika zaidi katika nyimbo za kwaya za makanisani, wanamuziki wa pop music huzitumia pia katika vipande vifupi vifupi vya nyimbo zao.

Mpangilio wa Natural Minor kutoka kwenye sauti ya kwanza ni KNK-KNK+K ambapo K ni kuruka hatua kamili (Tones), na N ni kuruka nusu hatua (Semitone) kama ilivyoelezwa hapo juu. Katika scale hii, KNK ni tetrachord moja wakati ile +K ya mwisho ni hatua nzima ya kuhamia kwenye Octave inayofuata. Kwa hiyo ukianza na sauti asili namba 1, sauti zake zitakuwa ni nyingine zitakuwa ni 1,3,4,6,8,9,11,(1). Scale hii haina leading note, kwa hiyo ni scale ambayo hutumika sana kwenye nyimbo ambazo zinatumia Octave moja tu na hutawalaiwa sana na sauti za median, subdominant, dominant; sauti za submendiant zinaingia kidogo sana kiasi kuwa wimbo unakuwa hauchangamshi kabisa. Mfano wake ni wimbo huu hapa; ingawa ni wimbo mzuri, msikilizaji wake anakuwa kama ana majonzi na huenda asiweze kunyanyuka kitinini kucheza.



Mpangilio wa harmonic minor kutoka kwenye sauti ya kwanza ni KNK-KNK+H ambapo K na N zina maana kama ilivyoelezwa hapo juu huku +H ikiwa na maana nusu hatua inyounganisha Octave inayofuata. Tetrachords za harmonic minor ni sawa kabisa na tetrachords za natural minor, yaani KNK. Kwa hiyo iwapo sauti ya kwanza ya harmonic minor ni 1, basi sauti za scale hiyo zitakuwa 1,3,4,6,8,9,11,(1). Kwa upande wake, tetrachords za melodic minor ni tofauiti sana na tetrachords nilizokiwsha taja hapo juu, yaani wakati scale zote hapo juu zina tetrachords zinazofanana, scale hii ya melodic haitumii tetrachords za aina moja. Tetrachord ya chini inapanda kwa step za NKK wakati tetrachoud ya juu inapanda kwa KKN, yaani tetrachord ya kwanza inapanda kwa kasi na ile ya pili inapanda polepole. Scale hii huanza kuwa kuruka step kamili kutoka sauti ya kwanza, halafu huunganisha tetrachord mbili kwa muundo wa K+NKK-KKN. Kwa hiyo ukianza na sauti asili ya kwanza, sauti za scale hii zitakuwa ni 1,3,4,6,8,9,10,(1) Sitatoa mifano ya hizi harmonic minor na melodic minor katika post hii ila nitazizungumzia tena huko mbele ya safari.

Maelezo hayo yanatosha kwa leo. Kwa wanaojua nadharia ya muziki watayaona ya kawaida sana ila kwa wale wanaotaka watoke kimuziki kwa kutumia sauti zao bila kuwa na shule yoyote, ni vizuri kuyajua haya wakati wakiwa wanatayarisha tungo zao.Katika post ijayo tutaanza kuangalia kwa undani zaidi jinsi ya kujenga mizani hizo za muziki.zaid.
 
MUSIC STAFF AND CLEFFS

Kabla ya kuendelea na maelezo kuhusu uchaguaji wa sauti za muziki, ngoja tuangalie mambo ya kinadharia kwanza. Sauti zitumikazo katika muziki hupangwa kwa kutumia mistali mitano inayojulikana kama STAFF, kama ionekanavyo hapa chini.

1151630


Kila msitali na kila nafasi kati ya mistali hiyo huwakilisha sauti moja. Kwa hiyo staff yote kuanzia chini ya msitali wa chini hadi juu ya msitali wa juu kuna sauti 11 zinazoonyeshwa kwa kutumia alama ya yai kama inavyoonekana kwenye picha hii hapa chini.
1151631

Ili kuongeza sauti zaidi ya hizo 11, kuna taratibu mbili za kutumia.

  • Utaratibu wa kwanza ni kuongeza au kupungua makali ya sauti kwa nusu hatua (half step) kwa kutumia sharp au flat kama ionekanavyo kwenye picha hii hapa chini. Ingawa sauti zote tatu ziko kwenye nafasi moja kwenye hiyo staff, sauti ya kulia (natural) ndiyo ile ya asili kenye nafasi hiyo, sauti ya katikati (flat) inapunguza ukali wa ile ya asili kwenye nafasi hiyo kwa nusu hatua, wakati sauti ya kushoto (sharp) inaongeza ukali wa sauti hiyo ya asili kwa nusu hatua.

1151632


  • Njia ya pili ni kutumia mistali ya leja (ledger lines) ambayo ni mistali midogo inayoongezwa juu au chini ya staff kama invyoonekana kwenye picha hii hapa chini. Kila msitali huongeza sauti mbili nje ya zile za kwenye staff, yaani sauti ya kwenye msitali wenyewe, na ile ya juu au chini ya msitali huo kulingana na msitali wenyewe ulipo kwenye staff. Kama ledger line hiyo iko chini ya staff, basi itaongeza moja sauti chini yake; vile vile iwapo ledger line iko jjuu ya staff, basi itaongeza sauti moja juu yake.
1151635






Aina za sauti zinazoweza kuwekwa kwenye staff hutambulisha kama CLEF. Kijumla kuna clefs za aina tatu kama inavyoonekana katika picha hii
1151636


Cliff ya juu inaitwa Treble Cleff: hii ni kwa ajili ya sauti za juu za Soprano, Contralto, na Counter tenor

Cliff ya kati inaitwa C- Cleff: Hii ni kwa ajili ya sauti za kati kama counter tenor, tenor, na baritone,

Cliff ya chini inaitwa Bass Cleff: hii ni kwa sauti za chini kama tenor, baritone, na bass

Kwa vile sauti zilizoko kwenye C-Cleff zinapatikana pia kwenye trebble cleff na kwenye bass cleff, ni kawaida nyimbo nyingi kuwa na cleff mbili tu: trebble cleff na bass cleff kama ionekanavyo kwenye wimbo huu wa hapa uliotoka mwaka 1985 kwa ajili kuchangisha hela za kusaidia Ethiopia iliyokuwa imekumbwa na ukame sana, watu wakawa wanakufa kwa njaa: Ulitungwa na Michael Jackson na Lionel Richie.

1151638






Katika post ijayo ndipo nitakapoanza kujadili sauti za kwenye kila cleff na namna ya kupangilia sauti zinazoshabihiana kwenye wimbo.

nkumbison, Madaga Gyole
 

Attachments

  • 1562883465963.png
    1562883465963.png
    1.7 KB · Views: 39
  • 1562883563042.png
    1562883563042.png
    1.7 KB · Views: 33
Tupo pamoja, nakufuatilia sana maana nimegundua kuna mengi nayafanya ktk muziki bila kujua
Kabla ya kuendelea na malezo kuhusu uchaguaji wa sauti za muziki, ndoja tuangalie mambo ya kinadharia kwanza. Sauti zitumikazo katika muziki hupangwa kwa kutumia mistali mitano inayojulikana kama STAFF kama ionekanavyo hapa chini.

View attachment 1151630

Kila msitali na kila nafasi kati ya mistali hiyo huwakilisha sauti moja. Kwa hiyo staff yote kuanzia chini ya msitali wa chini hadi juu ya msitali wa juu kuna sauti 11 zinazoonyeshwa kwa kutumia alama ya yai kama invyoonekana kwenye picha hii hapa chini.
View attachment 1151631
Ili kuongeza sauti zaidi ya hizo 11, kuna taratibu mbili za hutumia.

  • Utaratibu wa kwanza ni kuongeza au kupungua makali ya sauti kwa nusu hatua (half step) kwa kutumia sharp au flat kama ionekanavyo kwenye picha hii hapa chini. Ingawa sauti zote tatu ziko kwenye nafasi moja kwenye hiyo staff, sauti ya kulia (natural) ndiyo ile ya asili kenye nafasi hiyo, sauti ya katikati (flat) inapunguza ukali wa ile ya asili kwenye nafasi hiyo kwa nusu hatua, wakati sauti ya kushoto (sharp) inaongeza ukali wa sauti hiyo ya asili kwa nusu hatua.

View attachment 1151632

  • Njia ya pili ni kutumia mistali ya leja (ledger lines) ambayo ni mistali midogo inayoongezwa juu au chini ya staff kama invyoonekana kwenye picha hii hapa chini. Kila msitali huongeza sauti mbili nje ya zile za kwenye staff, yaani sauti ya kwenye msitali wenyewe, na ile ya juu au chini ya msitali huo kulingana na msitali wenyewe ulipo kwenye staff. Kama ledger line hiyo iko chini ya staff, basi itaongeza moja sauti chini yake; vile vile iwapo ledger line iko jjuu ya staff, basi itaongeza sauti moja juu yake.
View attachment 1151635





Aina za sauti zinazoweza kuwekwa kwenye staff hutambulisha kama CLEF. Kijumla kuna clefs za aina tatu kama invyoonekana katika picha hii
View attachment 1151636

Cliff ya juu inaitwa Treble Cleff: hii ni kwa ajili ya sauti za juu za Soprano, Contralto, na Counter tenor

Cliff ya kati inaitwa C- Cleff: Hii ni kwa ajili ya sauti za kati kama counter tenor, tenor, na baritone,

Cliff ya chini inaitwa Bass Cleff: hii ni kwa sauti za chini kama tenor, baritone, na bass

Kwa vile sauti zilizoko kwenye C-Cleff zinapatikana pia kwenye trebble cleff and bass cleff, ni kawaida nyimbo nyingi kuwa na cleff mbili tu: trebble cleff na bass cleff kama ionekanavyo kwenye wimbo huu wa hapa uliotoka mwaka 1985 kwa ajili kuchangisha hela za kusaidia Ethiopia iliyokuwa imekumbwa na ukame sana, watu wakawa wanakufa kwa njaa: Ulitungwa na Michael Jackson na Lionel Richie.

View attachment 1151638





Katika post ijayo ndipo nitakapoanza kujadili sauti za kwenye kila cleff na namna ya kupangilia sauti zinazoshabihiana kwenye wimbo.

nkumbison, Madaga Gyole
 
Kama nilivyosema hapo juu Octave moja ina jumla ya sauti kumi na mbili za asili. Katika hiyo namba, ni sauti saba tu zinazoshabihiana na zinaweza kutumika katika wimbo mmoja; hivyo kuna sauti ambazo hazikubaliki. Watu wanaweza kushangaa kusikia kuwa mpangilio wa sauti hizi unafuata mahesabu za Abstract Algebra. Sauti hizi zipo katika algebraic structure inayoitwa Abelian Group lakini sitawapeleka huko.

Sauti zinazokubalika katika muziki ni zile tunazoweza kuimba

DO-RE-MI-FA-SO-LA-TI-(DO)

wakati hii DO nyekundu ya mwisho inajulikana kuwa sauti ya kufungia na huwa inatoka katika OCTAVE inayofuata, zile DO-RE-MI-FA-SO-LA-TI ndiyo sauti saba za OCTAVE moja. Kwa ujumla sauti zote zinakuwa ni nane; yaani saba kutoka OCTAVE husika na moja kutoka OCTAVE inayofuata; zote zimepewa namba za kirumi kama ifuatavyo:

I-II-III-IV-V-VI-VII-VIII

Sauti za DO-RE-MI-FA au I-II-III-IV zinaitwa lower tetrachord (tetrachord ya chini), wakati sauti za SO-LA-TI-DO au V-VI-VII-VIII zinaitwa upper tetrachord (tetrachord ya juu). Tetrachords hizi mbili kwa pamoja zinaunda kitu kinachoitwa mizani ya muziki (music scale). Kila mizani ina sauti zenye majukumu matatu; sauti za kupumzikia, sauti za kuchangamisha, na sauti za mpito baina ya kupumzika na kuchangamka.

Kabla ya kuelezea sauti hizi nane zinachaguliwa vipi kutokana na zile sauti 12 za asili kuunda mizani moja, ngoja kwanza tujaadili tabia na matumizi ya sauti hizo nane katika mizani moja kama ifuatavyo:
  1. Sauti I na Sauti II huitwa Tonic na Supertonic: Hizi sauti ni za kupumzikia kwenye wimbo kiasi kuwa shairi linatakiwa lianze na sauti hizi na vile vile kuishia na sauti hizi katika hali ya kupumzika.
  2. Sauti III na Sauti IV huitwa Mediant na Subdominant: Hizi ni sauti za kupitia kutoka au kuingia kwenye sauti za mapumziko.
  3. Sauti V, VI na sauti VII zinaitwa Dominant, Submediant, na Leading note. Hizi ndizo sauti za kuchangamsha shairi. Sehemu kubwa ya shairi inatakiwa iwe katika sauti hizi.
  4. Sauti VIII pia ni Tonic (next Octave). Sauti hii hutumika tu iwapo wimbo unatumia Octave mbili, ambapo ni lazima mwendo wa kutoka Octave moja kwenda nyingine upitie sauti hii.
Nyimbo ambazo huwa hazikidhi tabia hizi huwa ama hazichangamshi au zinachosha msikilazji. Na hata zile zinazochangamsha huwa hazikai katika kumbukumbu za msikilizji wake kwa muda mrefu. Kwa mfano, wimbo huu wa Diamond una matatizo mawili makubwa. Tatizo la kwanza ni kuwa unaimbwa katika Octave mbili, lakini transitition kutoka Octave moja hadi nyingine ni ya kasi sana. Yaani haupitii kwenye Tonic au subtonic ya Octave inayofuata. Tatizo la pili ni kuwa kwa vile unaimbwa katika OCTAVE mbili, umeanzia kwenye median na subdominant moja kwa moja bila kuwa na sauti za tonic/supertonic za kuanzia. Kwa hiyo wimbo wote umekosa sauti za tonic na supertonic, na hivyo ni rahisi sana kusahaulika na vile vile unaweza kuwachosha wasikilazaji wake haraka sana.



Ni vigumu kuyatambua matatizo hayo bila kujua namna ya kuchagua sauti za kutumika katika wimbo, kwa vile hiyo siyo kazi ya haraka haraka kama maelezo ya hapo juu yanavyoweza kuwa yanaashiria kwani kiuhakika hakuna tafsiri kamili ya mwanzo na mwisho wa OCTAVE moja; OCTAVE inaweza kuanza na sauti yoyote ile kama tutakavyoona huko mbele. Iwapo mtunzi wa wimbo huo hapo juu alitaka wimbo uwe katika Octave moja, basi hakuchagua sauti zinazoshabihiana katika Octave hiyo. Katika post ijayo nitajadili namna ya kuchagua sauti za mzani.


Kwenye post hii nilisahau kueleza kuwa kwenye nyimbo zinazojengwa kwa mashairi na vibwagizo, ni vizuri ama vibwagizo vyote viwe katika tonic na supertonic tu, au mashari yote yawe kwenye tonic na supertonic tu. Inaumiza ubongo wa msikilizaji iwapo mashairi yana sauti za kupumzika na kuchangamsha wakati vibwagizo pia vina sauti hizo za kupumzika na kuchangamsha..Ni vizuri kuamua iwapo uchangamshaji utakuwa kwenye mashairi yenyewe au kwenye vibwagizo vyake, lakini isiwe kote kote.

Tutaangalia zaidi kuhusu miundo za nyimbo na tabia zake huko mbele ya safari
 
MUSICAL NOTES 3 - STAFF NOTATION

Sauti asili saba zilizoko kwenye staff zimepewa majina ya herufi za alphabet A-B-C-D-E-F-G. Herufi hizi zilipangwa kwa kufuata sauti ndani ya kwenye bass cleff kama ionekanavyo hapa chini.
1152245



Kwa hiyo ukiziendeleza kwa mfumo huo huo kwenda chini na kwenda juu unapata sauti nyingi za kwenye kwenye clef zote mbili kama ionekanavyo kwenye picha hii hapa chini. Sauti C iliyoko kwenye ledger kati ya Bass cleff na Trebble cleff, ambayo nimezungusia rangi yekundu, inajulikana kama middle-C yaani C ya kati kati.
1152246



Sauti asili hizi A-B-C-D-E-F-G, peke yake yake hazitoshi kukamilisha sauti zote 12 za OCTAVE moja na pia hazishabihiani kuunda mzani mmoja wa sauti saba katika octave moja. Kwa hiyo kuna sauti za kati zinazoongezwa kama SHARP au FLAT zikiwa na tabia ya kuongeza au kupunguza ukali kwa nusu hatua kama tulivyoeleza huko nyuma. Octave moja ina SHARP/FLAT tano zilizopangiliwa kwa mfumo wa 1,2,1,2,1 yaani baada ya sauti moja unaweka sharp, halafu baada ya sauti mbili unaweka sharp na tena baada ya sauti moja unaweka sharp, na kuendelea. Process hii hukamilisha jumla ya sauti 12 zifuatazo

A-A#-B-C-C#-D-D#-E-F-F#-G-G#

Angalia kuwa A# (A-Sharp) iko kati ya sauti A na sauti B, yaani sauti A imeongezwa ukali kwa nusu hatua, lakini pia ukitelemsha sauti B kwa nusu hatua kuifanya iwe Bb (B-flat) unapata sauti hiyo hiyo, Kwa hiyo sauti hizo pia zinaweza kuandikwa

A-Bb-B-C-Db-D-Eb-E-F-Gb-G-Ab

Sasa hizo ndizo sauti asili 12 za OCTAVE moja; zimepishana kwa nusu hatua, yaani kutoka sauti B mpaka sauti C ni nusu hatua, wakati kutoka wakati kutoka sauti A mpaka A# pia ni nusu hatua. Kwa maana nyingine ni kuwa hakuna sharp wala flat kati ya sauti B na sauti C na vile vile kati ya sauti E na F. Kwa B-sharp ni sawa na C, na vile vile C-flat ni sawa na B. Ni vivyo hivyo pia baina ya sauti za E na F.

Ingawa vyombo vingi vinaweza kutoa sauti zote hizi, nitatumia piano kwa vile sauti zake zimejipanga katika msitali ulionyooka na ni rahisi kuzielewa. Gitaa lina sauti nyingi kuliko piano yenye key (vibonyezo 88), lakini sauti za gitaa zinategemea uzi wa gitaa lenyewe na mahali ambapo uzi huo umebonyezwa, jambo ambalo linakuwa ni gumu kwa mwanafunzi kufuatilia kwa haraka.
1152260


Sauti hizo 12 zimepangwa kwenye piano ambapo sauti A,B,C,D,E,F,G zinatumia vibonyezo vyeupe, wakati sauti A#, C#, D#, F#,G# au Bb, Db, Eb, Gb, Ab zinatumia vibonyezo vyeusi kama ionekanavyo katika picha hii (inabidi kuzumu picha hii ili kuweza kuziona vizuri).

1152369


Standard OCTAVE za muziki hazianzii sauti A, bali huanzia sauti C, kwa sababu ndiyo iko katikati ya Trebble cleff na Bass cleff. Piano yenye vibonyezo 88 ina Standard Octave kamili 7, na octave mbili sisizokamilika kama ionekanavyo kwenye picha hiyo hapo juu. Katika kutunga muziki mizani moja ya muziki inaweza kuwa ndani ya OCTAVE moja tu au ndani OCTAVE mbili kama tutakavyoona huko mbeleni.

Sauti zilizo katika Octave 7 zote kuanzia na Contra Octave hadi Getsreep 4 Octave huonyeshwa kwa kuonezwa na namba ya inayoainisha kuwa ziko katika Octave gani,

C1-C#1-D1-D#1-E1-F1-F#1-G1-G#1,A1-A#1-B1-C2-C#2-D2-D#2-E2-F2-F#2-G2-G#2,A2-A#2-B2-C3-C#3-D3-D#3-E3-F3-F#3-G3-G#3,A3-A#3-B3-C4-C#4-D4-D#4-E4-F4-F#4-G4-G#4,A4-A#4-B4-C5-C#5-D5-D#5-E5-F5-F#5-G5-G#5,A5-A#5-B5-C6-C#6-D6-D#6-E6-F6-F#6-G6-G#6,A6-A#6-B6-C7-C#7-D7-D#7-E7-F7-F#7-G7-G#7,A7-A#7-B7-

C4
Nyekundu ndiyo middle-C

nkumbison, Madaga, Gyole, Extra miles
 
MIZANI KUU ZA MUZIKI -TOLEO LA KWANZA (MAJOR SCALES)

Baada ya kujua aina ya sauti (au note) zote zinazoweza kuingia masikioni mwetu, yaani kuanzia A1 mpaka G#7, sasa tunaanza na kueleza jinsi ya kuchagua sauti za kutumia kwenye mizani kuu, yaani sauti za furaha, baadaye ndipo tutaangalia namna ya kuchagua sauti za mizani ndogo, yaani sauti za huzuni. Huko mbeleni tukishaongelea urefu wa sauti na mwendokasi wake, nitaonyesha namna ya kutunga wimbo mzuri kwa kutumia FL Studio, DrDrum na Ableton Live na kuuchanganya na vyombo vya muziki electronically.

Kama tulivyoeleza kwenye hapo awali, mizani kuu huundwa kwa sauti zinazoruka hatua kwa mfumo KKN-K-KKN. Sauti ya chini kabisa inaitwa sauti ya msingi (root note), na ndiyo inatumika kama jina la mizani hiyo. Kila herufi kwenye Octave moja inatumika mara moja tu katika mzani, kwa hiyo huwezi kuwa na mzani wenye A na A# kwa mfano. Ila herufi ya kwanza ndiyo pia ya mwisho; yaani tonic ya kuingilia kwenye Octave inayofuata. Nadhani utakumbuka huko nyuma tulisema kuwa sauti nane za mzani ni ni DO-RE-MI-FA-SO-LA-TI-(DO), sasa herufi inayotumika kutambulisha D0 ya kwanza ndiyo pia hutumika kutambulisha (DO) ya mwisho.

Kuna jumla ya mizani kuu 16 kwenye OCTAVE moja, hata hivyo baadhi ya mizani hutumia sauti zinazofanana, kwa hiyo jumla ya mizani zenye sauti tofauti tofauti ni mizani 12 tu. Kuna formula moja ya kutambua sauti za mizani kuu kwa kutumia kitu kinaitwa circle of fifths na circle of fourths, lakini njia rahisi ni kuelekwa tu kuwa mizani moja inaweza kuwa katika OCTAVE mbili zenye sauti zifuatazo (kumbuka kuwa OCTAVE inaanzia sauti C).

C-C#-D-D#-E-F-F#-G-G#- A-A#-B- C-C#-D-D#-E-F-F#-G-G#- A-A#-B

na kila mizani kuu huitwa jina la sauti ya kwanza (root note) ikitumia sauti zilizochaguliwa mtindo wa kuruka hatua za KKN-K-KKN.

Mizani ya kwanza ni ni C-major, halafu mizani inayofuata inatumia ama sauti ya tano ya mizani iliyopita kukiwa na sharp kwenye mizani hiyo, au sauti ya nne ya sauti iliyopita ikiwa na flat kwenye mizani hiyo; kila utaratibu utatoa mizani nane nane.

Katika toleo hili, tutaanza na zile mizani nane zenye sharp kwanza halafu katika toleo litakalofuata ndiyo tutaangalia zile zenye flat. Maelezo haya yatatumia maneno yanayojirudiarudia lakini nadhani hiyo itasaidia kuifanya dhana yote kueleweka kwa kina zaidi. Safari hii sitaweka video moja kwa moja, ila nitaweka link na majina ya nyimbo tu ili kupunguza matumizi nafasi.

C-Major

Mizani ya kwanza ambayo ndiyo rahisi kwa wanamuziki wengi C-Major, yaani tonic note yake ni C; hii hutumia sauti za OCTAVE moja tu. Kwenye sauti za asili ziliko katika OCTAVE moja C-C#-D-D#-E-F-F#-G-G#- A-A#-B, ukianza na sauti C, halafu ukachagua zinazofuata kwa mtindo wa kuruka hatua za KKN-K-KKN utapata sauti za C-D-E-F-G-A-B-(C ). Hiyo ndiyo mizani kuu ya C-major, haina suati za sharp wala flat; ni rahaisi sana kupiga na kuimba katika mizani hii. Waimbaji wengi hutumia mizani hii. Mizani inayofuatia itakuwa ni G-major ikiwa na sharp kwa vile sauti ya tano katika C-Major ni G
1152516

Nyimbo za
Bad Romance wa Lady Gaga na When I Was Your Man wa Bruno Mars zimeimbwa katika mizani hii ya C-Major.


G-Major
Ukichukua sauti za asili zinazoanza na sauti ya G utakamilisha mizani kwa kutumia OCTAVE mbili zenye sauti G-G#- A-A#-B- C-C#-D-D#-E-F-F#-G. Kwa hiyo ukichagua sauti za kufuata mtindo huo huo wa KKN-K-KKN utapata mzani wenye sauti za G – A – B – C – D – E – F♯ – G ambamo sauti F ni sharp; hii inanyeshwa kwa kuwekwa alama ya sharp kwene mstali wa kwanza kuwa na not F kama ilivyoonyeshwa kwa alama nyekundu. Nyimbo za G-Major huwa zinachangamsha sana. Scale yenye sharp inayofuatia hii itakuwa ni D-major kwa vile sauti ya tano kwenye G-major ni D.

1152520


Nyimbo za
Unconditionally wa Katy Perry na Dangerous Woman wa Ariana Grande zimeimbwa katika mizani hii ya G-Major.

D-Major
Ukichukua sauti za asili zinazoanza na sauti ya D utakamilisha mizani kwa kutumia OCTAVE mbili zenye sauti D-D#-E-F-F#-G- G#- A-A#-B- C-C#-D. Kwa hiyo ukichagua sauti za kufuata mtindo huo huo wa KKN-K-KKN utapata mzani wenye sauti za D – E – F♯ – G – A – B – C♯ – D ambamo sauti za C na F ni sharp. Scale yenye sharp inayofuatia hii itakuwa ni A-major kwa vile sauti ya tano kwenye D-major ni A.
1152542

Nyimbo za
Summer Of '69 wa Bryan Adams na Beautiful Day wa U2 zimeimbwa katika mizani hii ya D-Major.

A-Major
Ukichukua sauti za asili zinazoanza na sauti ya A utakamilisha mizani kwa kutumia OCTAVE mbili zenye sauti A-A#-B- C-C#-D-D#-E-F-F#-G- G#-A. Kwa hiyo ukichagua sauti za kufuata mtindo huo huo wa KKN-K-KKN utapata mzani wenye sauti za A – B – C♯ – D – E – F♯ – G♯ – A ambamo sauti za C, F na G ni sharp. Scale yenye sharp inayofuatia hii itakuwa ni E-major kwa vile sauti ya tano kwenye A-major ni E.
1152539

Nyimbo za
Billie Jean wa Michael Jackson na Dancing Queen wa ABBA zimeimbwa katika mizani hii ya A-Major.

E-Major
Ukichukua sauti za asili zinazoanza na sauti ya E utakamilisha mizani kwa kutumia OCTAVE mbili zenye sauti E-F-F#-G- G#- A-A#-B- C-C#-D- D#-E. Kwa hiyo ukichagua sauti za kufuata mtindo huo huo wa KKN-K-KKN utapata mzani wenye sauti za E – F♯ – G♯ – A – B – C♯ – D♯ – E ambamo sauti za C, D, F, na G ni sharp. Scale yenye sharp inayofuatia hii itakuwa ni B-major kwa vile sauti ya tano kwenye E-major ni B.
1152534

Nyimbo za
Isn’t She Lovely wa Stevie Wonder na Slow Dancing In A Burning Room wa John Mayer zimeimbwa katika mizani hii ya E-Major.

Mizani zinazofuata nimeziweka kwenye rangi tofauti kwa vile tutaziangalia tena huko baadaye, kuona kuwa zinafanana na mizani nyingine; zinajulikana kama Enharmonic Major Scales.

B-Major
Ukichukua sauti za asili zinazoanza na sauti ya B utakamilisha mizani kwa kutumia OCTAVE mbili zenye sauti B- C-C#-D- D#-E-F-F#-G- G#- A-A#-B. Kwa hiyo ukichagua sauti za kufuata mtindo huo huo wa KKN-K-KKN utapata mzani wenye sauti za B – C♯ – D♯ – E – F♯ – G♯ – A♯ – B ambamo sauti za A, C, D, F, na G ni sharp. Scale yenye sharp inayofuatia hii itakuwa ni F♯-major kwa vile sauti ya tano kwenye B-major ni F♯.
1152514

Nyimbo za The Lazy Song wa Bruno Mars na Poker face wa Lady Gaga zimeimbwa katika mizani hii ya B-Major.

F♯-Major
Ukichukua sauti za asili zinazoanza na sauti ya F♯ utakamilisha mizani kwa kutumia OCTAVE mbili zenye sauti F#-G- G#- A-A#- B- C-C#-D- D#-E-F- F#. Kwa hiyo ukichagua sauti za kufuata mtindo huo huo wa KKN-K-KKN utapata mzani wenye sauti za F♯ – G♯ – A♯ – B – C♯ – D♯ – E♯ – F♯ ambamo sauti za A, C, D, E, F, na G ni sharp. Nyimbo za F♯-Major pia huwa zinachangamsha sana. Scale yenye sharp inayofuatia hii itakuwa ni C♯-major kwa vile sauti ya tano kwenye F♯-major ni C♯.
1152509


Nyimbo za
Beat it wa Michael Jackson, Rude Boy wa Rihanna na Born this way wa Lady gaga zimeimbwa katika mizani hii ya F-Sharp Major.

C♯-Major
Ukichukua sauti za asili zinazoanza na sauti ya C♯ utakamilisha mizani kwa kutumia OCTAVE mbili zenye sauti C#-D- D#-E-F- F#-G- G#- A-A#- B- C- C#. Kwa hiyo ukichagua sauti za kufuata mtindo huo huo wa KKN-K-KKN utapata mzani wenye sauti za C♯ – D♯ – E♯ – F♯ – G♯ – A♯ – B♯ – C♯ ambamo sauti zote ni sharp.
1152505


Nyimbo za
Sacrifice wa Elton John, na Umbrella wa Rihanna zimeimbwa katika mizani hii ya C-Sharp major.

Unaweza kushawishika kuwa ukichukua sauti ya tano ya C♯-Major utaweza kuunda G♯-major kwa kufuata mtindo huo huo, lakini hiyo haiwezekani kwa vile mfumo wa KKN-K-KKN kwenye sauti za G#- A-A#- B- C- C#-D- D#-E-F- F#-G-G#, unasababisha mizani ya G#- A#- C- C#- D#- F- G-G# ambayo haiwezekanaiki hasa kwa sababu sauti za C na G zinakuwa zinaingia kwa mikazo miwili tofauti, yaani natural na sharp.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom