Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,527
- 19,383
- Thread starter
- #81
Hiyo inatokana na maumbile ya miili kati ya wanaume na wanawake. Binadamu wote wanatoa sauti zao kwa kutoka kwenye vocal tract, yaani koromeo. ambayo kwa watoto wadogo ni fupi sana ndiyo maana wanakuwa na sauti za juu zaidi. Kwa watu wazima, wanaume wana vocal tract zenye urefu wa kama cm 17 wakati za wanawaek zina urefu wa kama cm 14 tu. Karibu na mwishoni mwa vocal tract, kuna misuri ijulikanayo kama vocal chords; misuli hii inapocheza cheza (vibrate) ndiyo hutoa sauti. Sauti inayiskika kutoka kinywani mwa mwimbaji inategema sana na urefu wa vocal tracts zake, ulaini wa wa vocal chords zake, na vile vile kipenyo cha vocal chords zake. Sasa wanawake maumbile yao yana vocal chords laini, zenye kipenyo kidogo na vile vile vocal tracts zao ni fupi. Hivyo kiasili sauti zao zinakuwa na pitch ya juu zaidi kuliko wanaume.Mkuu Ahsante kwa somo zuri..
Mimi nina shida moja. I'm a man na hua naimba kanisani lakini sauti yangu naona inafaa kuimba Alto..ila imebidi niimbe bass. Je hivi kwanini Soprano na alto waimbe wanawake tu.? Mimi napenda alto zaidi
Maelezo hayo unaweza kuyatafrisi kivitendo kwa kuangalia muundo wa aina mbali,mbali za saxophones. Bass saxophone inatumia reed (vocal chords) ngumu, na saut inasafiri umbali (vocal tract) mrefu kutoka kwenye reed hadi kwenye kinywa cha saxophone hiyo ukilinganisha na Soprano saxophone.