ELIMU MUHIMU: Watanzania wengi bado wanahitaji elimu ya demokrasia kwani wamekata tamaa na maisha. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ELIMU MUHIMU: Watanzania wengi bado wanahitaji elimu ya demokrasia kwani wamekata tamaa na maisha.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jaji, Aug 28, 2012.

 1. Jaji

  Jaji Senior Member

  #1
  Aug 28, 2012
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jana nikiwa kwenye mkutano wa M4C kuna wakina mama wawili walikuwa pembeni yangu nikawasikia wakisema hawa wanatudanganya wakipata nawo watatutesa kama CCM wanavyotufanyia.

  Ikanibidi niingilie mada yao maongezi yakawa kama ifuatavyo. Jaji: kwanini mnasema hivyo mama zangu?

  Mama: hata CCM huwa wanatupa maneno ya kutufariji kama hivi. Jaji: unajua ccm wanafanya vyote hivyo kwa sababu ya kulewa madaraka? Mama: kivip? Jaji: kwa sababu wanajua hata wawafanyie nini hamuwezi kuwatoa.

  Mama: sasa tufanye nini mwanangu? Jaji: Ili maendeleo yaje lazima kuwe na ushindani wa vyama vya upinzani. kwani chadema wakiingia madarakani hawatataka kutoka hivyo watajitahidi kurekebisha makosa waliyofanya ccm ili wao wasitoke tena madarakani.

  Pia hao CCM wakirudi watafanya vizuri kwani watakuwa wameshaonja utamu na masahibu ya kuwa nje ya madaraka.

  Mama: kweli mwanangu Jaji: kwa mfano sokoni akiwa muuzaji ni mmoja anaweza kupanga bei kwa jinsi anavyoamua yeye mwenyewe ila wakiwa wengi basi ushindani hutokea na bidhaa huuzwa kwa bei nafuu.

  Mama: wakafurahi sana kidogo wakaanza kushangilia. wakaaanza kushangilia mmoja wao akamwambia mwenzake ila kweli tutakuwa mama ntilie hadi lini tunahitaji mabadiliko. nilifurahi sana kuwaona wameelewa. HIVYO BASI MAKAMANDA TUNATAKIWA KUWAELIMISHA WALE WASIOJIELEWA..
   
Loading...