Elimu: Mgogoro wa Ardhi baina ya Makonda na GSM

Bashir Yakub

Member
May 27, 2013
84
1,561
ELIMU ARDHI MGOGORO WA MAKONDA NA GHALIB.

Bashir Yakub, WAKILI.
+255 714 047 241.

1. Ukinunua ardhi(nyumba,kiwanja,shamba)hakikisha unafannya transfer(kuhamisha umiliki kutoka aliyekuuzia kwenda jina lako Mnunuzi) mara moja kadri uwezavyo.

Wengi mkinunua kwasababu hakuna anayekulazimisha kufanya transfer kwa haraka basi mkishakabidhiwa hati na mikataba ya mauziano mnakaa nazo hata miaka 2 au 3 mkisema nikipata hela ndio nitafanya trasnsfer. Usifanye hivyo.

Mjue kuwa kama hujafanya transfer uwezekano wa aliyekuuzia kukuzunguka na kukuchezea ni mkubwa sana.

Mfano mmoja ni kuwa, aliyekuuzia anaweza kutoa taarifa ya kupotelewa na hati na hivyo kupatiwa taarifa ya Kupotea(lost report).

Kisha, akafanya Tangazo gazeti la kawaida na lile la Serikali(GOVERNMENT GAZETTE@GN).

Kisha, akafanya maombi ya kupatiwa hati mpya kupitia Form No. 3 Chini ya Kifungu cha 38 cha Sheria ya Usajili wa Ardhi, Sura ya 334.

Kisha, atapatiwa hati nyingine mpya. Kwahiyo kutakuwa na hati mbili katika ardhi moja, ile aliyokupa we mnunuzi na hii mpya ya kwake. Huu tayari ni mgogoro mkubwa kwako mnunuzi usiye na hatia(bonafide purchaser).

Akishakuwa na hati hayo mengine anaweza kuyakataa kirahisi, na pengine watu wa namna hii hata zile saini anazokuwa amekuwekea kwenye nyaraka nyingine zinakuwa sio zake.

Lakini mbaya zaidi ni kuwa, usipofanya transfer na wakati umeshanunua, shughuli zote zinazohusu ardhi hiyo, mfano kulipia kodi za ardhi, vibali vya ujenzi, tathmini, tozo na kila kitu kinaendelea kusoma jina la aliyekuuzia na kinafanyika kwa jina la aliyekuuzia.

Maana yake ni kwamba, ushahidi wote wa risiti na nyaraka nyinginezo unaendelea kumtambua aliyekuuzia kuwa mmiliki halali ambapo anaweza kutumia ushahidi huo dhidi yako

Ataonesha risiti zinamsoma yeye na atasema nilikuwa nilipia, atachukua hata kibali cha ujenzi bila we kujua na atakionesha kinamsoma yeye nk, nk.

Ndugu yangu wewe hapo kutoboa katika mazingira hayo unahitaji tu kudra za mwenyezi Mungu kama utabahatika kuzipata.

Lakini kama umefanya transfer mchezo huu ni mgumu sana na pengine usiowezekana, na hata ukiwezekana kwa nguvu ya rushwa ama mamlaka bado unaponyeka(curable) kwasababu system huonesha umiliki ulivyokuwa ukihama hadi mmiliki wa mwisho.

Ninachotaka kuwashauri mkafanye transfer haraka mnaponunua. Najua mnaogopa gharama hasa Capital Gain ambayo ni 10%. Lakini hii mbona inazungumzika na huwa inapungua.

Anyway mna uhuru wa kuchagua kati ya shari kamili ya kudhulumiwa ardhi yote au nusu shari ya hiyo 10%.

2. Mkinunua hakikisha mikataba yenu inashuhudiwa na mawakili. Nimeona ule wa Makonda na Gharib ulishuhudiwa na Wakili aitwaye Ibrahim Shineni. Huyu kwasasa ni nguzo muhim mno, yaan mno katika huu mgogoro.

Wakili kwa cheo chake ni afisa wa Viapo(Commissioner for Oaths), ni Mthibitishaji wa Umma(Notary Public), na pia ni afisa wa Mahakama.

Akiwa kwenye mkataba wako wa manunuzi ya ardhi ni mtu muhimu mno na shahidi wako muhimu anayeaminiwa sana na Mahakama.

Basi haya mawili yakufunzeni.
 
Wakili umeandika kwa kifupi sana, mkataba wa ardhi unahitaji menhi zaidi ya hayo, yaweke yote iwe somo kwa wana jumuia ya jf.
 
Makonda amekataliwa duniani na hata mbinguni.

Hii ndio karma sasa, na wasambaa wanasema ukitandika mvyedi na ugoshe mvyedi.

Kwenye nchi zilizo serious mtu kama Makonda anatandikwa risasi hadharani kwa ushetani aliofanyia watu.
 
makonda rudisha ardhi uliyopora enzi za mwendazake vitu vyote ulivyopora kwa kutumia mabavu pnd ulipokuwa na cheo rudisha haraka sana kabla aibu haijakukuta mana mtetezi wako hayuko tena hai.
 
Makonda amekataliwa duniani na hata mbinguni.

Hii ndio karma sasa, na wasambaa wanasema ukitandika mvyedi na ugoshe mvyedi.

Kwenye nchi zilizo serious mtu kama Makonda anatandikwa risasi hadharani kwa ushetani aliofanyia watu.

Amefanyaje ambacho wewe hujafanya. Watz kwa kujifanya wema
 
Makonda amekataliwa duniani na hata mbinguni.

Hii ndio karma sasa, na wasambaa wanasema ukitandika mvyedi na ugoshe mvyedi.

Kwenye nchi zilizo serious mtu kama Makonda anatandikwa risasi hadharani kwa ushetani aliofanyia watu.
Tatea eka mambeza!
 
Ndio maana habari za vijana huwa haziniwazishi. Ngoja niendelee kutumbua maisha nyumbani ntakutana nayo futi 6 chini
 
Alex Mgongolwa ameleta vielelezo, hadi nyumba ilijengwa na gsm, anazo hadi risiti za mkandarasi, sasa bashite alijengaje hiyo nyumba, ndio vinasubiriwa vielelezo avilete. at the end of the day, bashite ametishia kuwa gsm amuachie ardhi yake kabla hajaonyesha uozo wake, bahati mbaya akifanya hivyo tu gsm anatenda mahakamani kwasababu ni ngumu kuthibitisha tuhuma ambazo bashite atazitoa, atamfungulia kesi ya kudhalilishwa na kulipwa fidia kubwa, bashite hatakuwa na hela ya kulipa, mali zake zilizobaki zitataifishwa. ndicho ninachokiona kinakuja mbeleni.
 
GSM limempiga miti sana bashite na kumzawadia mavitu kibao, leo limemkinai linamgeuka….. pozi kwa pozi chukua notisi.
 
Dah, kwa vielelezi vile, tunasubiri bashite aje na maelezo alijenga hiyo nyumba au alijengewa na gsm, anamiliki vipi? nyumba ilijengwa 2017, bashite anasema alinunua 2013. ni kwamba alijengewa na gsm? lini umiliki wa kiwanja uliwahi kuhama? mbona conspiracy theory inataka kuja.
 
Back
Top Bottom