Machmadem
JF-Expert Member
- Jul 9, 2017
- 758
- 933
Leo tuzungumzie matumizi sahihi ya barakoa (face mask) maana Maradhi ya Corona (COVID19) yamekuja na mambo yake. Ingawa kwa wenzetu wa bara Asia hii desturi ya kuvaa barakoa ni ya kawaida kabisa katika maisha yao ya kila siku kwetu sisi huku haya ni “mashkolo mageni” kweli kweli. Sasa nataka nikuambie machache kuhusu matumizi sahihi ya barakoa kama inavyoshauriwa na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO).
Watu wanaotakiwa kuvaa barakoa ni wale walio karibu na wagonjwa wa Maradhi ya Corona (COVID19) [AMBAO KUTOKANA NA MAISHA YETU YA KUKUTANA NA MISONGAMANO KILA SIKU NI VYEMA TU KUIVAA MAANA NI NGUMU KUJUA WALIOTUZUNGUKA WAMEAMBUKIZWA AMA LAH)
Barakoa zinafanya kazi nzuri zaidi ya kumlinda mtu dhidi ya maradhi ya Corona kama zinatumiwa sambamba ya njia nyingine za kumlinda mtu dhidi ya kirusi cha Corona yaani kunawa mikono kwa maji safi yanayotiririka Na sabuni au vitakasa mikono.
Kama mtu ana kikohozi ya mafua NI LAZIMA AVAE BARAKOA ili awalinde wengine waliomzunguka.
Kabla hujavaa barakoa hakikisha mikono yako ni misafi
Ukivaa barakoa hakikisha imefunika kabisa pua na kinywa bila kuacha nafasi yoyote ya kupitisha hewa pembezoni (yaani kati ya barakoa na uso).
Epuka kabisa kugusa gusa barakoa baada ya kuivaa (kama unataka kuigusa hakikisha unanawa mikono kwanza)
Barakoa HAITAKIWI ILOWE hakikisha unaibadilisha kila baada ya saa 3-4 (IKILOWA na majimaji yatokayo kwenye mfumo wa hewa au/mate inaweza kuwa uwanja mzuri wa kutunza na kukuza viini vingine vya maradhi kama bakteria au fangasi vinavyoweza kukudhuru zaidi)
Ukitaka kuvua barakoa itoe kutokea nyuma (kwenye kamba zake) yaani usiguse mbele ya barakoa
Mwisho kabisa, matumizi ya barakoa ni muhimu sana kwa ulinzi wako na wale waliokuzunguka. Ingawa ni desturi mpya lakini kama nilivyosema tangu mlipuko huu wa COVID19 ulipoanza MAISHA YA MWANADAMU HAYATOKAA YAWE KAMA YALIVYOKUWA KABLA YA MLIPUKO, KILA SEHEMU YA MAISHA YETU ITABADILIKA TU! @tmh.healthcenter @cloudsfmtz
#CoronaNoma #COVID19 #CoronaInTanzania #tmhhealthcenter #afyatanzania #jilindeutulinde
note nimeshindwa ku upload picture
Sent using Jamii Forums mobile app