Elimu kwa Umma: Nafasi, Umuhimu, na Wajibu wa Vyama vya Upinzani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Elimu kwa Umma: Nafasi, Umuhimu, na Wajibu wa Vyama vya Upinzani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by dudus, Apr 19, 2011.

 1. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #1
  Apr 19, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,764
  Likes Received: 6,082
  Trophy Points: 280
  Nimesoma makala ya Mwanakijiji humu jamvini ikielezea kwa kifupi malengo ya vyama vya upinzani kama CHADEMA na yale ya chama tawala - CCM. Nampongeza sana.

  Ndugu zangu, sijui ni kwa makusudi au bahati mbaya kwamba tangu mfumo wa vyama vya vingi uingie nchini, wananchi hawajapewa elimu ya kutosha juu ya mfumo huo na suala hili limekuwa likipigiwa kelele na baadhi ya wadau lakini inaonekana wahusika wametia pamba masikioni.

  Hofu wanazotiwa wananchi ama na watawala, baadhi ya vyama vya upinzani, au mawakala wao naamini zinatokana na wananchi kutokuwa na elimu ya kutosha ya uraia hivyo kutambua wajibu na haki zao katika taifa. Na kwa hakika hili lisipofanyiwa kazi, hofu hizi zitaendelea kutawala kwa faida ya upande mmoja na hasara ya upande mwingine.

  Nadhani, ni muhimu kwa vyama vyote vya siasa vyenye mapenzi mema na taifa letu, asasi za kiraia (UDASA, n.k), pamoja na serikali kutoa elimu hii kwa wananchi. Kwa mfano kama lilivyofanyika kongomano la katiba UDSM, yangeweza pia kufanyika makongamano mengine sehemu mbali mbali nchini ili kuelimisha kuhusu mfumo wa vyama vingi na wajibu wa kikatiba. Makongamano haya yanaweza kujadili mada kama hizi:-

  (i) Maana ya vyama vingi
  (ii) Nafasi, wajibu, na haki za chama tawala.
  (iii) Nafasi, wajibu, na haki za vyama vya upinzani.
  (iv) Nafasi, wajibu, na haki za vyama/asasi za kiraia.
  (v) Nafasi, wajibu, na haki za taasisi za kidini.
  (vi) Wajibu na haki za raia.
  (vii) Wajibu wa serikali katika mfumo wa vyama vingi.
  (viii) Kujiandikisha na Upigaji Kura
  (ix) Umamluki wa Kisiasa: Vyama vya siasa, viongozi wa kisiasa, viongozi wa dini, n.k.
  (x) Namna ya kuwatambua na kuwachukulia mamluki wa kisiasa.
  (xi) Rushwa katika uchaguzi na nafasi na wajibu wa raia/mpiga kura.
  n.k. n.k.

  Pia mifano ya nchi kama Marekani, Japan, Uingereza, na hata Israel ambako kiongozi yeyote anaweza kuondolewa madarakani na hata kushitakiwa kama amefanya kosa lolote inaweza kutolewa.

  Nadhani kwa kutoa elimu hii hizi hofu za kijinga tunazokuwa nazo raia kwa kuwa tu kiongozi fulani kasema zitakwisha na hivyo wananchi kuchagua viongozi bila kuwepo kwa shinikizo lolote hata kama ni la kisaikolojia au la kiimani kutoka kwa viongozi wa dini.

  Nawasilisha.
   
 2. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #2
  Apr 19, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  elimu ya uraia si jukumu la serikali pekee...! pia kumbuka elimu ya uraia hutolewa mashuleni kuanzia shule za msingi,sekondari,vyuo, na elimu ya juu....!
  kila level ikijulikana kwa majina tofauti kama vile URAIA(SIASA), CIVICS, GENERAL STUDIES(G.S),DEVELOPMENT STUDY (D.S)
  Hivyo basi umakini na uzingatiaji wa masomo ni kitu cha msingi ili pia kuepuka itikadi ya kusoma ili kufaulu.....manake kusoma kwa lengo la kufaulu mara nyingi humfanya mwanafunzi pindi amalizapo mtihani asiwe na lolote kichwani kwake kwani alisoma ili afaulu
  my take:
  ELIMU HII HUTOLEWA MASHULENI, TUJIPANGE KWA WALE AMBAO HAWAKUBAHATIKA KUIPATA WAIPATE
   
 3. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #3
  Apr 19, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,764
  Likes Received: 6,082
  Trophy Points: 280
  Na wale ambao hawakubahatika kwenda shule? Au kama usemavyo, wale ambao walisoma kwa minajili tu ya kufaulu mitihani? Au wale wa umri wangu ambao tumejifunza siasa katika mfumo wa "chama kushika hatamu"? Sasa kwa taarifa yako hawa ndio wapiga kura muhimu na ndio wanopaswa hasa kufikiwa na elimu hii. Usishangae hata baadhi ya "viongozi" wa vyama vya siasa hawajui hata wajibu wao.
   
Loading...