Elimu kwa Umma: Maswali na Majibu kuhusu Safari za Ndege na Changamoto zake

Bonheur Travels Tanzania

JF-Expert Member
Dec 29, 2020
252
499
JNIA.jpg

Ndugu WanaJF,

Tunafahamu si kila mmoja ni mzoefu wa kufanya safari kwa usafiri wa ndege. Sababu ni nyingi, ila kwa uchache ni hofu, kipato au sababu tu ya kusafiri kwa ndege haijatokea bado.

Pia, usafiri huu licha ya kuwa ni wa haraka na uhakika, una changamoto zake lukuki ambazo zinapelekea wasafiri wengi kupoteza pesa na kuharibu ratiba zao kwa sababu mbalimbali.

Bonheur Travels Tanzania kupitia uzi huu maalum, tumeona ni vyema tutoe elimu kwa umma kuhusu safari za ndege kwa ujumla kwa njia ya kujibu maswali yenu moja kwa moja. Ni matumaini yetu uzi huu utakuwa rejea muhimu kwa kila anayetaka kutumia usafiri wa Anga kwa matembezi, shughuli za kibiashara na mengineyo.

Tunakaribisha maswali yote kuanzia mchakato wa kupata hati ya kusafiria, maombi ya visa, ukatishaji tiketi na nyaraka zote zinazohitajika ili kuweza kusafiri. Aidha, maswali kuhusu vitu ambavyo msafiri anatakiwa kuvifanya na vile vya kuepuka kuvifanya, zoezi la ukaguzi Uwanja wa Ndege, Muda wa Kuwasili, Kuunganisha Ndege, Usafiri baada ya Kutua na mambo mengine.

Si mbaya kupitia uzi huu pia, wale wenye uzoefu wakasaidia kuongezea mambo mengine muhimu yanayohitajika.
Lengo ni kuondoa hofu na kutoa elimu kwa wasafiri wapya sambamba na kubadilishana uzoefu kwa wale wanaosafiri mara kwa mara.

Karibuni kwa Maswali turahisishe maisha!
 
Kwann kwenye ndege hawagawi ugali au kande? Ikibd waruhusu watu tuingie navyakula vyetu Kama kwenye Basi?
Zipo sababu kadhaa zinazopelekea Uongozi wa Shirika la Ndege kuchagua aina maalumu za vyakula. Pia miongozo ya usalama na afya.

Hata hivyo, vyakula ambavyo huandaliwa mara nyingi ni vile vya haraka na visivyohitaji maandalizi ya muda mrefu, kwani hupikwa na kukaguliwa angalau saa 24 kabla "havijapackiwa" kwenye ndege.

Suala la chakula pia ni usalama. Itifaki za kiusalama (security protocols) haziruhusu abiria kupanda na vyakula kuhofia hatari mbalimbali zikiwemo sumu na ajali zitokanazo na vyakula vya moto kupitiliza n.k.

Kwa bahati nzuri, machaguo ya vyakula huongezeka kulingana na daraja la safari. Daraja la Biashara kuna machaguo mengi zaidi.

Asante.
 
Hahahahah Mwanangu Siti Ya Mbele Kabisa Na Umetoa Boko......
Ameuliza swali zuri. Watu wengi huhoji kwanini baadhi ya vyakula havipewi nafasi kwenye usafiri wa anga? Ni swali halali.

Ni matumaini yetu, mashirika ya ndege na mamlaka husika zitaangalia namna ya kuongeza orodha ya machaguo ya vyakula ili kuwe na machaguo ya kutosha kwa kila kundi la watu.

Kwa Shirika la Ndege #AirTanzania, vyakula vinavyoliwa kwa wingi na watanzania ni sehemu ya utamaduni. Wanaweza kuchukua na kulifanyia kazi hili la Makande na Ugali baada ya kujiridhisha kama lina uhitaji mkubwa.

Asante.
 
Mbona inchi nyingine tulizowazidi kiuchumi mfano Mozambique, usafili wa ndege ni wa kawaida sana, kwa nini Tanzania ndege ni garama kubwa?
Gharama za usafiri hutofautiana baina ya mashirika ya ndege kutokana na sababu nyingi zikiwemo ubora na viwango.

Pia, uwezo wa kufanya manunuzi (purchasing power) wa watumiaji huamua kuhusu gharama za huduma.

Aidha, kanuni za soko huria huchangia upangaji wa bei katika bidhaa au huduma husika.

Kwa suala la Tanzania na Mozambique, jibu huenda likawa moja kati ya hayo hapo juu.

Asante.
 
Ikitokea ndege imepata hitilafu juu huko huwa mna tumia njia gani kuokoa abiria?
Hili ni suala la kiufundi na kitaalamu.

Hata hivyo, zipo dondoo za usalama (safety tips) ambazo hutolewa kwa abiria mapema ili inapotokea hitilafu basi waweze kujihami wakati hatua nyingine za usalama zikichukuliwa.

Njia za haraka zinazofahamika inapotokea hitilafu angani (japo inategemea na level) ni pamoja na;

.- Ndege kutua kwa dharura katika eneo lolote elekezi

- Kutoa taarifa kwa vikosi vya uokozi ardhini ili kupokea abiria kutokea angani (evacuation)

- Abiria kutakiwa kuvaa jackets au miamvuli aina ya parachutes

- Mengineyo.

Asante.
 
Aina gani ya ndege ya ATCL inakwenda Chato?
Bila shaka ni ndege zote za ATCL zinazofanya safari za ndani.

Kwa mujibu wa Serikali, safari za Chato mkoani Geita zitaanza rasmi mnamo Januari 9 mwakani.

Taarifa kamili:

Tunaweza kukusaidia kupata tiketi kwa haraka na gharama nafuu endapo utahitaji.

Karibu sana.
 
Weka simu

Simu za ofisi ni +255 737 555522 na +255 757 212122

Unaweza kupiga kwa maswali, ufafanuzi au maoni. Namba hizo zinatumika pia kwa mahitaji ya huduma yoyote ya usafiri wa anga na matembezi ndani na nje ya nchi mbalimbali kwa shughuli za utalii, masomo, biashara na kadhalika.

Mazungumzo ni bure.

Karibu!
 
Unaelezea vipi usalama wa ndege hasa zile za masafa marefu kuvuka bahari.
Moja ya changamoto kubwa za usafiri wa anga ni kuvuka bahari (coasting out).

Ajali nyingi zimetokea hasa kwa ndege zenye uwezo mdogo zinapojaribu kufanya safari kwa kukatisha eneo la bahari kwa muda mrefu.

Ndio maana kwa ndege za kisasa (modern jets) zimekewewa engines zaidi ya moja hivyo hatari ya kupata ajali zinapovuka bahari imekuwa ndogo karibu na hakuna.

Maelezo mengine ni ya kiufundi na kitaalamu. Wajuzi wanaweza kuyaweka kwa lugha rahisi zaidi.

Asante.
 
Back
Top Bottom