Bonheur Travels Tanzania
JF-Expert Member
- Dec 29, 2020
- 252
- 499
Ndugu WanaJF,
Tunafahamu si kila mmoja ni mzoefu wa kufanya safari kwa usafiri wa ndege. Sababu ni nyingi, ila kwa uchache ni hofu, kipato au sababu tu ya kusafiri kwa ndege haijatokea bado.
Pia, usafiri huu licha ya kuwa ni wa haraka na uhakika, una changamoto zake lukuki ambazo zinapelekea wasafiri wengi kupoteza pesa na kuharibu ratiba zao kwa sababu mbalimbali.
Bonheur Travels Tanzania kupitia uzi huu maalum, tumeona ni vyema tutoe elimu kwa umma kuhusu safari za ndege kwa ujumla kwa njia ya kujibu maswali yenu moja kwa moja. Ni matumaini yetu uzi huu utakuwa rejea muhimu kwa kila anayetaka kutumia usafiri wa Anga kwa matembezi, shughuli za kibiashara na mengineyo.
Tunakaribisha maswali yote kuanzia mchakato wa kupata hati ya kusafiria, maombi ya visa, ukatishaji tiketi na nyaraka zote zinazohitajika ili kuweza kusafiri. Aidha, maswali kuhusu vitu ambavyo msafiri anatakiwa kuvifanya na vile vya kuepuka kuvifanya, zoezi la ukaguzi Uwanja wa Ndege, Muda wa Kuwasili, Kuunganisha Ndege, Usafiri baada ya Kutua na mambo mengine.
Si mbaya kupitia uzi huu pia, wale wenye uzoefu wakasaidia kuongezea mambo mengine muhimu yanayohitajika. Lengo ni kuondoa hofu na kutoa elimu kwa wasafiri wapya sambamba na kubadilishana uzoefu kwa wale wanaosafiri mara kwa mara.
Karibuni kwa Maswali turahisishe maisha!