Elimu kwa Umma: Maswali na Majibu kuhusu Safari za Ndege na Changamoto zake

kwanini inatakiwa kuweka flight mode ukiwa kwenye ndege

Hili swali tulilitarajia, tulilisubiria.

Abiria wa Ndege huambiwa wazime vifaa vya kielektroniki vinavyotuma mawasiliano zikiwemo simu na tablets, au kuviweka katika hali ya ndege (Airplane Mode) ili kuepusha muingiliano wa mawasiliano ya ndege na kumchanganya rubani.

Hata hivyo, maendeleo ya teknolojia yamerahisisha siku hizi ndege nyingi zimeweka vifaa vya kuzuia muingiliano huo, hivyo abiria wanaruhusiwa kutumia vifaa vya mawasiliano wakiwa hewani bila shida.

Asante.
 
jinsi ya kupata visa

Kila nchi ina utaratibu wake wa namna ya kupata visa. Kwa bahati nzuri, siku hizi visa unaweza kupata mtandaoni kwa kujaza fomu na kuambatanisha nyaraka zote muhimu zinazohitaji kulingana na nchi husika.

Watu wengi si wajuzi wa kujaza fomu za maombi ya Visa, hivyo Bonheur Travels Tanzania tukiwa kama wazoefu na watoa huduma wa safari za ndege, tumejikita pia kuwasaidia kujaza fomu hizo na mchakato mzima hufanyika kwa ushirikiano kati ya mtu anayetaka kusafiri na wataalamu wetu.

Karibu sana kwa huduma.
 
Nashukuru huu uzi imenifungua mengi maswali yangu ni haya.

1 kwann ni lazima kwenye cocpit kuna marubani wawili?

2 kwann ukikata ticketi mapema gharama inakuwa ndogo?

3 unaruhusiwa kupakata mtoto kwenye ndege kama kwenye basi?
I mean ulipie siti 1 then uende na mtoto
 
Hili swali tulilitarajia, tulilisubiria.

Abiria wa Ndege huambiwa wazime vifaa vya kielektroniki vinavyotuma mawasiliano zikiwemo simu na tablets, au kuviweka katika hali ya ndege (Airplane Mode) ili kuepusha muingiliano wa mawasiliano ya ndege na kumchanganya rubani.

Hata hivyo, maendeleo ya teknolojia yamerahisisha siku hizi ndege nyingi zimeweka vifaa vya kuzuia muingiliano huo, hivyo abiria wanaruhusiwa kutumia vifaa vya mawasiliano wakiwa hewani bila shida.

Asante.
Mkuu samahani, sijaridhika na majibu yako/yenu.
Muingiliano wa mawasiliano kivp?
 
angani kuna network?
 
Kwasasa Sina swali, lakini naomba tu nikupongezeni kwamba ninyi ni kati ya watoa huduma wachache sana wenye uwezo wa kujibu maswali kwa ueledi na pasipo kukasirika hapa JF.

Hongereni sana na nina wapongeza kwa hilo.
 
Hili ni suala la kiufundi na kitaalamu.

Hata hivyo, zipo dondoo za usalama (safety tips) ambazo hutolewa kwa abiria mapema ili inapotokea hitilafu basi waweze kujihami wakati hatua nyingine za usalama zikichukuliwa.

Njia za haraka zinazofahamika inapotokea hitilafu angani (japo inategemea na level) ni pamoja na;

.- Ndege kutua kwa dharura katika eneo lolote elekezi

- Kutoa taarifa kwa vikosi vya uokozi ardhini ili kupokea abiria kutokea angani (evacuation)

- Abiria kutakiwa kuvaa jackets au miamvuli aina ya parachutes

- Mengineyo.

Asante.
Mala nyingi ndege hulipuka na kuua abiria pale tu inapopata hitilafu huko juu,.. sijawahi kusikia abiria wameruka Kwa parachuti au miamvuli unaweza kututoa hofu hapo?
 
Bonheur Travels Tanzania ni Kampuni ya Wakala wa Safari (Travel Agency) yenye makao makuu yake nchini Tanzania.

Kwa maneno mengine, sisi ni wataalam wa tiketi za ndege na safari za maeneo ya kufikia (accommodation) na hata yale ya kitalii (destinations). Uwe unasafiri peke yako, na familia yako au kama timu, tunakusaidia kupata tiketi za ndege za bei rahisi na za kuaminika kwa safari za ndani na za kimataifa.

Mtu yeyote anaweza kutumia ushirikiano tulio nao na mashirika ya ndege ya ndani na ya kimataifa, kuandaa nasi safari kwa gharama nafuu na huwa tunahakikisha anawasili na kupata usafiri wa gari kutoka Uwanja wa Ndege hadi anakofikia.

Tunatoa huduma kwa watu binafsi, taasisi, mashirika na makundi mengine.
Ninapokata ticket kupitia nyinyi huwa kuna gharama natakiwa kuwalipa? au..
 
Nashukuru huu uzi imenifungua mengi maswali yangu ni haya.

1 kwann ni lazima kwenye cocpit kuna marubani wawili?

2 kwann ukikata ticketi mapema gharama inakuwa ndogo?

3 unaruhusiwa kupakata mtoto kwenye ndege kama kwenye basi?
I mean ulipie siti 1 then uende na mtoto

Karibu sana mkuu. Asante kwa maswali mazuri.

1. Ni muhimu. Sababu ya msingi ya kuwa na marubani wawili katika kila ndege ni usalama. Na hii ni kwa sababu endapo itatokea dharura kwa rubani mmoja, rubani mwingine ashike 'usukani' kusaidia. Kwa kuongezea, rubani mwenza hutoa maoni mbadala (second opinion) katika baadhi ya maamuzi, hivyo kupunguza makosa ya kirubani.

2. Ni kwa sababu za kibiashara. Ukikata tiketi mapema, ndege husika inakuwa tayari imepata uhakika wa mteja/abiria. Hesabu zinakaa sawa. Uamuzi wa kuweka punguzo la bei ni kutoa motisha ili kuvutia abiria wengi zaidi kwa safari ya tarehe husika, kuepusha ndege kusafiri na empty seats. Heri nusu shari!

3. Mashirika mengi ya ndege, kama sio yote, yanaruhusu watoto wadogo kupakatwa. Hata hivyo, kila shirika limeweka umri wa mtoto kulazimika kulipiwa siti yake.
 
Mkuu samahani, sijaridhika na majibu yako/yenu.
Muingiliano wa mawasiliano kivp?
Bila samahani mkuu, tungependa kufafanua swali lako lakini hapo tutalazimika kuelezea kwa lugha ya kitaalamu ambayo inaweza kuleta mkanganyiko zaidi.

Kwa lugha nyepesi, vifaa vya umeme vinavyobebeka zikiwemo simu za mkononi, hutoa ishara za redio (mwangwi, ukelele wa kieletroniki) ambazo maafisa wana wasiwasi zitaingiliana na mawasiliano ya ndege au udhibiti wa ndege na vifaa vingine vya elektroniki vya ndani ya ndege.

Marubani mara zote huwasiliana na watu wa "station" katika kuongoza ndege, kelele hizo za mionzi ya simu huenda zikapelekea kukosekana kwa masikilizano baina ya rubani na wataalamu hivyo kuleta usumbufu na hata ajali.

Hata hivyo, jambo hili bado linabishaniwa duniani kote.
 
angani kuna network?
angani kuna network?
Hapana, kuna umbali ukishavuka kwenda juu network connection inakata yenyewe kutokana na simu kutoweza kuunganika na minara ya mawasiliano ya kampuni husika.

Kinachoruhusiwa ni kutumia simu katika kupiga picha, kusoma vitabu, kusikiliza muziki, kucheza games na matumizi mengine yasiyohusisha network.
 
Back
Top Bottom