Elimu kwa Umma: Maswali na Majibu kuhusu Safari za Ndege na Changamoto zake

Bonheur travel Tanzania ni nini?
Bonheur Travels Tanzania ni Kampuni ya Wakala wa Safari (Travel Agency) yenye makao makuu yake nchini Tanzania.

Kwa maneno mengine, sisi ni wataalam wa tiketi za ndege na safari za maeneo ya kufikia (accommodation) na hata yale ya kitalii (destinations). Uwe unasafiri peke yako, na familia yako au kama timu, tunakusaidia kupata tiketi za ndege za bei rahisi na za kuaminika kwa safari za ndani na za kimataifa.

Mtu yeyote anaweza kutumia ushirikiano tulio nao na mashirika ya ndege ya ndani na ya kimataifa, kuandaa nasi safari kwa gharama nafuu na huwa tunahakikisha anawasili na kupata usafiri wa gari kutoka Uwanja wa Ndege hadi anakofikia.

Tunatoa huduma kwa watu binafsi, taasisi, mashirika na makundi mengine.
 
Mnaweza kuendelea kuuliza maswali na kuomba ufafanuzi wa masuala yote yahusuyo safari za ndege.

PM iko wazi pia kwa watakaotaka kuuliza maswali yao pembeni.

Karibuni.
Wananikera kufika eapot mapema, ndege inaondoka saa tisa wananambia nifike saa nane, pili kwa uwanja wa zamani kwa hapa kwetu wanakagua mara mbili (temino 2) ila kule mbeya nilikaguliwa mara moja tu
 
Ameuliza swali zuri. Watu wengi huhoji kwanini baadhi ya vyakula havipewi nafasi kwenye usafiri wa anga? Ni swali halali.

Ni matumaini yetu, mashirika ya ndege na mamlaka husika zitaangalia namna ya kuongeza orodha ya machaguo ya vyakula ili kuwe na machaguo ya kutosha kwa kila kundi la watu.

Kwa Shirika la Ndege #AirTanzania, vyakula vinavyoliwa kwa wingi na watanzania ni sehemu ya utamaduni. Wanaweza kuchukua na kulifanyia kazi hili la Makande na Ugali baada ya kujiridhisha kama lina uhitaji mkubwa.

Asante.
Huwez kuweka kila chakula wewe. Unaweza kujamba ukaharibu safar nzima. Kuna mekanizim flan inatumika nafikir hata ukijamba vile vyakula vyao havinuki.
 
Vitu gani vinahitajika ili MTU aweze kupanda ndege kwa safari za ndani ya nchi
Vitu gani vinahitajika ili MTU aweze kupanda ndege kwa safari za nje ya nchi

Maswali mazuri na ya msingi sana.

Kwa safari za ndani ya nchi, nyaraka muhimu zinazohitajika ni:

1. Kitambulisho chako kinachotambulika (NIDA/Leseni)
2. Hati ya Kusafiria (Passport)
3. Tiketi ya Safari yako.

Kwa safari za nje:

1. Passport
2. Visa (fuatilia utaratibu wa nchi husika)
3. Cheti cha hali ya afya yako
4. Kitambulisho

Mambo ya ziada kwa safari zote:

1. Fanye maandalizi ya kutosha na uzingatie sana muda wa kuwasili uwanja wa ndege (masaa 2 hadi 3 kabla ni vizuri zaidi).

2. Toa nakala ya nyaraka zote ili kujihami na dharura yoyote itakayojitokeza.

3. Beba pesa taslimu (cash) kiasi, usiiamini sana mifumo ya elektroniki.

4. Jiunge na mifumo ya mawasiliano, malipo ya kimataifa (wezesha kadi za benki).

5. Usimuamini mtu yeyote kirahisi uwapo safarini.

Asante.
 
Kwa nini wakati wa ukaguzi kabla ya kuboard huwa wanakataza vitu vya vimiminika kama vile maji, dawa ya mswaki, perfume, lotion mtu asiingie navyo kwenye mizigo anayo board NATO ndani ya ndege? Kwani vitaleta shida gani?
Bonheur Travels Tanzania

Swali zuri.

Vimiminika vinazuiwa kwa sababu za kiusalama. Sababu ya msingi hasa ni kwamba teknolojia ya vifaa vya ukaguzi katika viwanja vingi vya ndege bado haina uwezo wa ku-scan na kujua kama vimiminika ni tishio/hatari au la! Lengo la kuvizuia ni kulinda usalama wa ndege na wasafiri wengine.

Hata hivyo, dawa ambazo zinazofahamika na baadhi ya vitu huruhusiwa baada ya mkaguzi kujiridhisha.

Asante.
 
Nikiwa mwanza na nataka kwenda arusha ni lazima niwe na visa? Kwanini ukisafiri kwa ndege wanadai kitambulisho chochote
Kwa safari za ndani ya nchi hutakiwi kuwa na Visa. Kitambulisho ni kwa sababu za kiusalama tu. Unatakiwa utambulike wewe ni nani na unaenda wapi kufanya nini.

NB: Matishio ya uvunjifu wa amani na mauaji ndio chanzo cha kuanzishwa kwa mifumo ya utambuzi.
 
Wananikera kufika eapot mapema, ndege inaondoka saa tisa wananambia nifike saa nane, pili kwa uwanja wa zamani kwa hapa kwetu wanakagua mara mbili (temino 2) ila kule mbeya nilikaguliwa mara moja tu

Ni muhimu kufika mapema uwanja wa ndege ili uweze kupata muda wa kuhakikisha kila kitu kipo sawa kabla hujaanza safari.

Hata hivyo, kusubiri ni jambo linalowakwaza wasafiri wengi, ndio maana uwekezaji mkubwa hufanyika katika viwanja vya ndege mbalimbali kwa kuweka vivutio na ubunifu mwingi ili kuburudisha wasafiri na kuwaondolea upweke, kero ya kusubiri.

Mfano, uwanja wa ndege wa Singapore kuna migahawa, kumbi za sinema, intaneti ya bure, mabwawa ya kuogelea, vyumba vya mazoezi, bustani za vipepeo na vitu vingine vingi ili kila msafiri anayefika mapema afurahi na kutokereka.

Asante.
 
Kwa nini wakati wa ukaguzi kabla ya kuboard huwa wanakataza vitu vya vimiminika kama vile maji, dawa ya mswaki, perfume, lotion mtu asiingie navyo kwenye mizigo anayo board NATO ndani ya ndege? Kwani vitaleta shida gani?
Bonheur Travels Tanzania
Dr, hii ilianza baada ya tukio la September 11, kuna vijana aligundulika wanasafiri na mabomu ya vimiminika na nia yao ilikua kulipua ndege inayotoka au inayokwenda Marekani ikiwa na idadi ya Wamarekani kadhaa.

FBI walipata hiyo tip na kuanza kukagua mizigo yote ya hand luggage inayoingia na kutoka na habari zilienea katika msako ulianza katika airport zote duniani.

Wale vijana walikamatwa, na kweli katika mizigo yao ya safari walikua na visu vibiriti na chemikali zinazolipuka. Walitaka kufanya tukio kama la September 11.
 
Maswali yangu hayo hapo chini sijui kama umeyaona


1.He,ninaruhusiwa kuingia na kondom ndani ya ndege ya abiria
2.Je, naruhusiwa kuoga nikiwa ndani ya ndege ya abiria

Tumeyaona na tunayajibu.

1. Ndiyo, unaruhusiwa kuingia na condom ndani ya ndege ya abiria. Condoms sio vinywaji wala vilipuzi na hazijatajwa kwenye orodha ya vitu visivyoruhusiwa kupanda navyo kwenye ndege.

2. Mashirika mengi ya ndege hayaruhusu abiria kuoga wakiwa ndani ya ndege. Mashirika ya Ndege yanayoruhusu abiria kuoga ndani ya ndege zao ni: Emirates na Etihad (ambayo huchukuliwa ndio mashirika bora daraja la kwanza).

Sio kuoga tu, hata huduma za massage na usafi mwingine wa mwili (SPA) hufanyika kwa madaraja ya biashara na kuendelea.

Kimsingi, ndege za Emirates na Etihad hutoa huduma bora na za kipekee kwa wateja wake.
 
Halafu hivi marubani huwa hawajisaidii haja ama huwa wanavaa pampas

Jibu ni Ndiyo. Marubani hutumia vyoo na hujisaidia kama watu wengine.

Utaratibu unaotumika ni huu;

Wakati mmoja wa marubani anahitaji kutumia maliwato, mhudumu wa ndege huingia ndani ya chumba (cockpit) halafu rubani huyo hutoka kwenda maliwatoni, kisha mlango hufungwa akihakikisha kuwa kuna watu wawili wamebaki.

Asante.
 
Dr, hii ilianza baada ya tukio la September 11, kuna vijana aligundulika wanasafiri na mabomu ya vimiminika na nia yao ilikua kulipua ndege inayotoka au inayokwenda Marekani ikiwa na idadi ya Wamarekani kadhaa.
FBI walipata hiyo tip na kuanza kukagua mizigo yote ya hand luggage inayoingia na kutoka na habari zilienea katika msako ulianza katika airport zote duniani.

Wale vijana walikamatwa, na kweli katika mizigo yao ya safari walikua na visu vibiriti na chemikali zinazolipuka. Walitaka kufanya tukio kama la September 11.
Duuhhh.....!!! Interesting aisee, I never knew about this!
Shukrani sana.
 
Back
Top Bottom