Elimu kwa Umma juu ya matumizi sahihi ya alama barabarani na uzingatiaji wa sheria

Katavi yetu

JF-Expert Member
Jul 30, 2018
837
1,000
Hongereni sana Wizara ya Mambo ya Ndani kupitia kitengo chenu cha usalama barabarani kwa kazi mnayofanya kupambana na waharifu wa barabara,pia hongereni wizara ya afya kwa kushirikiana na vyombo vyote vya ahabari nchini, mitandao ya kijamii n.k. katika kutoa elimu juu ya madhara ,namna ya kujikinga na virusi vya corona.

Hivyo basi wizara ya mambo ya ndani kupitia kitengo cha usalama barabarani inatakiwa iige mfano ije na elimu kwa umma na uhamasishaji kama uliofanywa kipindi hiki cha corona na wizara ya afya, vivyo hivyo hii wizara nayo inatakiwa ije na elimu kwa umma juu ya matumizi sahihi ya alama za barabarani na umuhimu wa kuzingatia sheria hasa maeneo yenye vivuko mfano; punda milia, matuta, msongamano wa wawatu n.k. Sina maana kwamba elimu hua haitolewi bali iongeze wigo kwa kushirikiana na vyombo vya habari,mitandao ya kijamii, blogs n.k

Ni wazi kwamba watanzania wengi bado hatuzingatii alama za barabarani hususani mikoani ambako traffic hawajasambazwa zile sehemu korofi na zenye vivuko,utakta mtu anaona kabisa pale kuna alama ya punda milia lakini bado atavuka bila hata kupunguza mwendo, au sehemu kuna speed limit ya 30KMH bado mtu anapita na speed ya 70kmh hasa hawa boda boda na mara nyingi maeneo ya mijini.

Hivyo basi kama elimu, kampeni na uhamasishaji ukifanyika kwa kiwango cha juu kwa kushirikiana na vyombo vya habari vyote nchini, na rais pia kama alivyo viomba vyombo vya habari vyote nchini katika kipindi cha Covid-19 kutumia japo dakika chache kuelezea madhara, njia za kujikinga n.k vivyo hivyo akafanya kwenye hii kampeni kuelezea matumizi ya alama za barabarani na kutii sheria bila shuruti basi tatizo la ajari zitokanazo na uzembe aidha wa madereva na watumiaji wengine wa barabara naimani litakua limepunguzwa. Na yule sasa atakae kiuka baada ya elimu hiyo kutolewa basi faini iwe juu yake.

Pia hiyo haitakiwi iishie hapo tuu bali wizara zote zinatakiwa ziige mfano na ziwezeshwe kufanya hivyo kutoa elimu mbali mbali yahusuyo wizara zao na yale yawapasayo Watanzania kuyafahamu, simaanishi kwamba elimu hazitolewi lahasha bali mkazo uongezwe zaidi na kasi iongezwe ili kuwaweka watanzania sawa.
 

Trinity

JF-Expert Member
Jul 20, 2017
580
1,000
Ningekua askar wa barabaran wanaovunja sheria za barabaran kwa makusudi wangeona cha moto, ningetoa mifano michache wengine wangestaarabika tu. Katavi yetu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom