Elimu kuhusu Kifafa cha Mimba: Fahamu Chanzo, Dalili, Tiba na Tahadhari

Habarini wapendwa,

Nina maswali kuhusu huu ugonjwa uwapatao wanawake wajawazito, kifafa cha mimba:

1. Ni nini chanzo cha ugonjwa huu?
2. Zipi dalili za huu ugonjwa?
3. Je, inawezekana kuwa nao na bado ukaendelea kulea mimba na kujifungua bila tatizo lolote?

I just lost my baby today, I was so dejected nilipoambiwa my wife had "kifafa cha mimba" and there's no way to keep the baby-to-be, just a month to go azaliwe. Imeniuma coz sikujua kuhusu huu ugonjwa.
 
Oooh no, pole sana mkuu. Wacha tusubiri wataalamu watueleze. Kifafa cha mimba ni kibaya sana. Either upoteze mama au mtoto au wote wawili.
 
Thanx Preta. Nilipoambiwa hii kitu sikuamini, na doctor akasema tu tuna terminate ujauzito leo, I was like whaaaat?
 
Last edited by a moderator:
Nasubiri wataalamu waweke source za science hapa, nami niweke source za ulimwengu wa vitu visivyoonekana. Kimsingi mwombe sana Mungu anapokua kwenye hali hiyo kuna mawili mama au mtoto akutoke. Mwombe sana Mungu aepushe hilo.
 
Me kuna rafiki yangu alipatwa nacho ila alifanyiwa operation akiwa na miezi nane. So mtoto aliwekwa kwenye incubator for 3week akaruhusiwa kumchukua ila kwa saiv mama yuko shwari na mtoto. Pole sana kaka.
 
Kwanza pole sana mkuu.

Kifafa cha mimba kitaalamu hujulikana kama ECLAMPSIA. Ni kati ya magonjwa ambayo yanaongoza katika kusababisha vifo vya wamama wajawazito katika 3rd world countries, Tanzania included.

Chanzo cha ECLAMPSIA:

Kiukweli, hakuna kitu kimoja ambacho kinafahamika kuwa ndio kisababishi cha ugonjwa huo, yaani chanzo bado hakijafahamika, lakini kuna risk factors (visababishi) nyingi nyingi ambazo ziko associated na eclampsia.

Pia ziko theory nyingi sana zinazojaribu kuelezea ni kitu gani hasa kinatokea wakati wa eclampsia(watu wengine huuita eclampsia kama 'a disease of theories' kwa sababu hii). Baadhi ya risk factors za eclampsia ni kama zifuatazo:

1. Kama ni mimba ya kwanza kwa mama.
2. Kama kuna historia ya eclampsia kwa mama yako/ndugu yako.
3. Kama una chini ya miaka 20 au zaidi ya miaka 40 wakati wa ujauzito.
4. Kama ulikuwa na tatizo la high blood pressure kabla ya ujauzito.
5. Kama uzito wako ni mkubwa kulingana na urefu wako(overweight/obesity).
6. Kama una historia ya eclampsia mimba iliyopita.
7. Mimba ya mapacha.
8. Kama baba wa ujauzito huo ni a new partner kwa mama.

Dalili za tatizo hili: Naomba kwanza nikueleze kuhusu PRE-ECLAMPSIA ninapokuelezea kuhusu dalili za eclampsia: kwa sababu eclampsia kwa kawaida huanza kama pre eclampsia, na ikiwa very severe ndo inakuwa eclampsia(think of this like a spectrum, where by at the low end you have pre eclampsia, and at the high end you have eclampsia).

Pre eclampsia ni pale ambapo mama mjamzito anakuwa na blood pressure ambayo ni kubwa kuliko kawaida!!(MARA NYINGI CUT OFF POINT NI 150/90). Hii huendana na dalili zingine kama maumivu makali ya kichwa,kuvimba miguu,maumivu ya chembe moyo(epigastric pain),kushindwa kuona vizuri(blurred vision),mapigo ya mtoto kushuka,mtoto kutokukua vizuri tumboni(intra uterine growth restriction)...

Pressure ikiendelea kupanda zaidi huweza kupata kondo la mtoto kuachia kabla ya muda(abruptio placenta), mtoto kufia tumboni, figo kufeli, seli chembe-sahani za mama kupungua (hizi ndio husaidia damu kuganda pale unapopata jeraha) na kusababisha mama kutoka damu sana na hata kufariki.

Sasa, kama pressure ikiendelea kupanda bila intervention yoyote, mama pia hupata Seizures/convulsions(degedege/kifafa), na pia kuchanganyikiwa(confusion), na hata kupoteza fahamu(loss of consciousness).

Kwa hiyo basi dalili za eclampsia ni zile zote za pre eclampsia kujumlisha kifafa/degedege.

Pre eclampsia na eclampsia hutokea mara nyingi kuanzia wiki ya 24, na pia baada ya kujifungua. Mara chache pia inaweza kutokea kabla ya wiki 24.

Kwa bahati mbaya sana, matibabu ya ECLAMPSIA ni termination of the pregnancy!! bila kujali wiki za ujauzito!!
Lakini, kama mama akiwa na dalili za pre eclampsia(kabla hajapata seizures/degedege ambapo na jina la ugonjwa litabadilika pia).

Kulingana na dalili za mama na wiki za ujauzito, madaktari wanaweza kujaribu kushusha presha yake kwa dawa na kumfanyia a close monitoring na kuangalia kama wanaweza ku push huo ujauzito ili awezee kudeliver, na hapa care kubwa ni kumantain blood pressure ili isiwe juu na kusababisha ECLAMPSIA.

I hope I have tried to explain vizuri, huu ni ugonjwa ambao ni complex na una mambo mengi, nimejaribu kutumia lugha ya kawaida; na samahanini sana kwa kuchanganya lugha, kama kuna kitu hakijaeleweka mnaweza kuuliza for more explanations. Eli79
 
Je dr nini kifanyike kuzuia au kujinga endapo mwanamke akiwa mjamzito
 
DAWA YA MARADHI YA MARADHI YA KIFAFA:

Kila Tiba kati ya zifuatazo ni yenye kujitegemea.Chagua iliyo rahisi kwako.Isipokufaa ndipo uchague nyengine

TIBA 1:
Chukua udi swalib (udi sulb) kijiko kimoja cha chai (5ml),chukua na kijiko kimoja cha chakula (10ml) cha mbegu za habbat Sawda.

Twanga pamoja halafu changanya na Asali safi ya nyuki kijiko kimoja (10ml).
Tumia mchanganyiko huu kutwa mara tatu (1×3) kwa muda wa miezi mitatu hata mwaka mmoja (miezi 3-miezi12).

TIBA 2:
Kunywa maji yaliyochemshwa na Harmal.Kisha baada ya kunywa ujipake kifuani Mafuta ya Habat Sawda na unywe kijiko kimoja (10ml) cha mafuta hayo.


Treating epilepsy through herbal

Pomegranate+leaves+can+help+curing+epilepsy+as+per+indian+traditional+medicines+ayurveda.JPG


Epilepsy* is an ailment that can be cured but the patient and his/her family members need to take certain precautions. As far as natural and herbal ways of treatment are concerned, here are a few remedies:

1. Give onion juice (around 3 ounce) daily mixed with small quantity of water in the morning. It has to be given regularly for at least 40 days.

2. If the patient is given slight 'heeng' (Asafoetida) along with lemon to chew, it will be helpful to the epileptic. The patient shouldn't immediately gobble it up, rather let it in the mouth and chew slowly.

3. Bake garlic (light broiling) for a while in oil and administer it to the person suffering from epilepsy on a regular basis.

4. Take 60 gms 'henna' (mehndi) juice along with 250 gm milk. It cures the condition as per ayurveda.

4. A wonderful remedy in Indian ayurvedic medicinal system is to boil pomegranate leaves (100 grammes) in 500 gramme water. When just a quarter water remains, filter it and add 60 gramme 'ghee' and an equal amount of sugar. Give it to patient twice in day, in the morning and in the evening. Mostly it works.

Tumia Dawa kisha uje unipe Feedback.By MziziMkavu.

MziziMkavu hapo unazungumzia tiba ya kifaa cha mimba (eclampsia) au kifafa (epilepsy)?
 
Je dr nini kifanyike kuzuia au kujinga endapo mwanamke akiwa mjamzito
Kitu cha muhimu katika huu ugonjwa ni kwa wale wamama ambao wana risk factors(kama nilivyozitaja mwanzoni) kufanyiwa a close follow up kwa kuhudhuria clinic mara kwa mara, na kupima presha kila anapohudhuria clinic hiyo, na aanzishiwe dawa pale ambapo presha inaonekana kupanda. Kwa hiyo kama kaka Eli79 inabidi ujauzito ujao shemeji awe anahudhuria clinic angalau kila mwezi, kwa sababu tayari yupo kwenye high risk.
 
Last edited by a moderator:
Pole sana mkuu! Familia yangu iliwahi kupata tatizo kama hilo. Tulipoteza mtoto mwaka 85, alizaliwa akiwa hai wiki 34, akafariki muda mfupi baadaye. Tulifanikiwa kupata mtoto mwingine kwa njia ya upasuaji, lakini ilibidi kipindi chote cha ujauzito kuwa chini ya usimamizi wa madaktari. Mungu Akupe faraja na amani, lakini kama walivyoshauri wengine usikate tamaa na Mungu Atakusaidia!
 
Dr VR na mjazito mwenye pressure ya chini nae yuko kwenye hiyo risk.
 
Pole sana kwa kupoteza mtoto.

Nina rafiki yangu aliambiwa ana kifafa cha mimba mimba ikiwa na miezi 7 (kama nakumbuka). Nchi za wenzetu wanagundua kwa kuwapima wanawake wakati wa clinic hata kabla dalili hazijaonekana kwa macho. Walichofanya ni walimzalisha kabla ya muda na mtoto akabaki hospital mpaka akakomaa.

Wahaya hili tatizo hawanaga tofauti na baadhi ya makabila ambayo mama alikuwa ananitajia kama mifano ambao kwao hili tatizo ni kama sugu sababu (according to my mum) ni wahaya wanatumia mitishamba sana wakati wa ujauzito kama njia ya ku prevent hili tatizo na matatizo mengine.

Nakumbuka mama yangu alikuwa ananambia wewe acha kunywa hizi dawa uone kama hujapata kifafa cha uzazi.

Ni kibaya sana, unakuta mzazi anajing'ata wakati wa kujifungua, wengine wanakuwa vichaa kabisa na kuua watoto..nadhani kinaathiri ubongo pia.
 
Pole sana kwa kupoteza mtoto.

Nina rafiki yangu aliambiwa ana kifafa cha mimba mimba ikiwa na miezi 7 (kama nakumbuka)
Nchi za wenzetu wanagundua kwa kuwapima wanawake wakati wa clinic hata kabla dalili hazijaonekana kwa macho. Walichofanya ni walimzalisha kabla ya muda na mtoto akabaki hospital mpaka akakomaa.

Wahaya hili tatizo hawanaga tofauti na baadhi ya makabila ambayo mama alikuwa ananitajia kama mifano ambao kwao hili tatizo ni kama sugu sababu (according to my mum) ni wahaya wanatumia mitishamba sana wakati wa ujauzito kama njia ya ku prevent hili tatizo na matatizo mengine.

Nakumbuka mama yangu alikuwa ananambia wewe acha kunywa hizi dawa uone kama hujapata kifafa cha uzazi.

Ni kibaya sana, unakuta mzazi anajing'ata wakati wa kujifungua...wengine wanakuwa vichaa kabisa na kuua watoto..nadhani kinaathiri ubongo pia.

Shemeji hii kwa wahaya ni kweli. Mke wangu Mhaya. Mimba ya kwanza niliona wanatuma madawa mengi. Baada ya kupima mke ilionekana pressure hiko juu. alitumia hizi dawa tatizo hakuna.mama mkwe alisisitizw sana dawa.
 
Sijui kwann nimeingia huu uzi nimejikuta naogopa. Moto wa kwanza nilipata kifafa cha mimba nashukuru mungu nilipona mimi na mtoto. Kwa sasa nina mimba ipo miez ya mwishon ila tangu last week natumia dawa za kushusha presha maana ilikua juu sana, sina raha naogopa mnooo.
 
Kuongezea maelezo ya Dr hapo, ukisikia Pre eclampsia si chochote kigumu ila ni hali ya kupatwa na preha kwa mama mjamzito ambaye si mgonjwa wa presha kwa hali ya kawaida na inatokea mimba ikifika wiki 20 na kuendelea hali ambayo inaambatana na kuchuja kwa protini kwenye mkojo.(Kiwango maalum cha protini na presha pia kinatumika ku classify hili kama ni mild pre eclampsia au ni severe).

Pili, Eclampsia sasa(dalili zimeshatajwa na Dr hapo juu) huwa ina tabia ya kuwapata kina mama ambao wana/ wameingia kwenye "severe pre eclampsia" ambaye ni presha kali wakati wa ujauzito. Hii inamweka huyu mama katika hatari kubwa ya kuingia kwenye kifafa sasa au eclampsia yenyewe, shetani mkuu mwenyewe.

Kwa wale wenye presha kali na wanaonyesha dalili za hatari I.e. kizungu zungu, kichwa kuuma sana, maumivu juu ya kitovu hasa upande wa kulia, kushindwa kuona vizuri (features of impending eclampsia) wana kua managed kwa aggressive blood pressure control na pia dawa ya kumkinga na kifafa (MgSo 4 prophylaxis) ikifanikiwa kushuka anaangaliwa kwa karibu kujaribu ku delay tarehe ya kujifungua, depending on the mother's gestation age.

Akiingia kwenye eclampsia sasa anapewa dawa za kumtuliza na kuzalishwa baada ya hapo.

Unfortunately kuna kuaga na risk kubwa ya kumpoteza mtoto kutokana na kutozingatia matumizi ya dawa kwa wakina mama husika au hata hiyo presha yenyewe inaweza leta hiyo shida.

Kikubwa hapa ni kuhudhuria kliniki mapema na mara kwa mara na pia "kuzingatia matumizi ya dawa za presha" ni muhimu sana.

Mwezi mmoja tu kabla ya tarehe ya matarajio ya kujifungua ni tarehe salama pia ya kujifungua endapo atawahiwa kabla heart rate ya mtoto haijaanza kubadilika. Kwasababu kikubwa tunachohofia hapa ni maturity ya mapafu ya mtoto ambayo ni ya mwisho ku mature mtoto asije zaliwa na Respiratory Distress Syndrome. Huwa Tunatoa dawa ya kuharakisha hii process kwa kina mama wenye risk ya kujifungua kabla ya term.

CC Eli79
 
Back
Top Bottom