Elimu kuhusu Kifafa cha Mimba: Fahamu Chanzo, Dalili, Tiba na Tahadhari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Elimu kuhusu Kifafa cha Mimba: Fahamu Chanzo, Dalili, Tiba na Tahadhari

Discussion in 'JF Doctor' started by Mbu, Aug 17, 2008.

 1. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #1
  Aug 17, 2008
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  Una experience yoyote ya mgonjwa aliyeshawahi patwa na huo ugonjwa?

  Nishasikia hadithi za kusikitisha na kukatisha tamaa jinsi wakunga wetu Bongo walivyo wazembe kuwasaidia kina mama wanaoshikwa na kifafa cha mimba.

  - Kifafa cha mimba ni nini?

  - Nini inasababisha kifafa cha mimba?

  - Dalili zake na ushauri wa haraka iwapo mama mjamzito atakumbana na hali hiyo?

  2.

  Michango kutoka kwa WanaJF

   
 2. Triplets

  Triplets JF-Expert Member

  #2
  Aug 18, 2008
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 1,103
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Mbu, nimepata hii article from internet...I will be back. I have experienced hii kitu...

  Kifafa cha mimba (eclampsia)
  Overview
  Eclampsia, a life-threatening complication of pregnancy, results when a pregnant woman previously diagnosed with preeclampsia (high blood pressure and protein in the urine) develops seizures or coma. In some cases, seizures or coma may be the first recognizable sign that a pregnant woman has preeclampsia.


  There has never been any evidence suggesting an orderly progression of disease beginning with mild preeclampsia progressing to severe preeclampsia and then on to eclampsia. The disease process can begin mild and stay mild, or can be initially diagnosed as eclampsia without prior warning.

  Preeclampsia usually occurs in a woman's first pregnancy but may occur for the first time in a subsequent pregnancy.


  Causes
  No one knows what exactly causes preeclampsia or eclampsia.

  Since we don't know what causes preeclampsia or eclampsia, we don't have any effective tests to predict when preeclampsia or eclampsia will occur, or treatments to prevent preeclampsia or eclampsia from occurring (or recurring).

  Preeclampsia usually occurs with first pregnancies. However, preeclampsia may be seen with twins (or multiple pregnancies), in women older than 35 years, in women with high blood pressure before pregnancy, in women with diabetes, and in women with other medical problems (such as connective tissue disease and kidney disease).

  Preeclampsia may run in families, although the reason for this is unknown.

  Preeclampsia is also associated with problems with the placenta, such as too much placenta, too little placenta, or how the placenta attaches to the wall of the uterus. Preeclampsia is also associated with hydatidiform mole pregnancies, in which no normal placenta and no normal baby are present.

  There is nothing that any woman can do to prevent preeclampsia or eclampsia from occurring.

  Symptoms (Dalili)
  The hallmark of eclampsia is seizures. Similar to preeclampsia, other changes and symptoms may be present and vary according to the organ system or systems that are affected. These changes can affect the mother only, baby only, or more commonly affect both mother and baby. Some of these symptoms give the woman warning signs, but most do not.

  The most common symptom and hallmark of preeclampsia is high blood pressure. This may be the first or only symptom. Blood pressure may be only minimally elevated initially or can be dangerously high; symptoms may or may not be present. A common belief is that the risk of eclampsia rises as blood pressure increases above 160/110 mm Hg.

  The kidneys are unable to efficiently filter the blood (as they normally do). This may cause an increase in protein to be present in the urine. The first sign of excess protein is commonly seen on a urine sample obtained in your provider's office. Rarely does a woman note any changes or symptoms associated with excess protein in the urine. In extreme cases affecting the kidneys, the amount of urine produced decreases greatly.

  Nervous system changes can include blurred vision, seeing spots, severe headaches, convulsions, and even occasionally blindness. Any of these symptoms require immediate medical attention.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. Visenti

  Visenti JF-Expert Member

  #3
  Aug 18, 2008
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 1,031
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 133
  ECLAMPSIA (kifafa cha mimba) ni matokeo ya mwisho au complication ya PRE-ECLAMPSIA (EPH gestosis), si kila mjamzito mwenye PRE-ECLAMPSIA anaishia na ECLAMPSIA, hallmark ya PRE-ECLAMPSIA ni dalili tatu, ambazo ni HIGH BLOOD PRESSURE (hYPERTENSION), EDEMA (kuvimba miguu au mwili mzima) na PROTENURIA (mkojo unakuwa na protein nyingi).

  PREECLAMPIA inagundulika kirahisi kwa kutumia elimu kidogo hata katika zahanati, kama mama anahudhuria kiliniki akiwa mjamzito (>90% ya akina mama wajawazito wanahudhuria kiliniki Tanzania), mama mwenye hali hiyo huwa lazima apelekwe kwa mganga/dakitari kwa ufuatiliaji zaidi na anashauriwa kuhudhuria kiliniki mara nyingi kuliko wajawazito wengine, na hupewa dawa za kupunguza pressure (HYPERTENSION).

  Daktari hutakiwa kufanya grading ya hiyo hali (EPH gestosisi scoring/grading),ambapo kuna makundi matatu ya ukali wa EPH (Mild EPH, Moderate na Severe) mwenye Severe EPH htakiwa kulazwa/hupewa rufaa kwenda ktk hospitali yenye watalaamu na facilities za kutosha kwa uangalizi wa karibu, anaweza asiruhusiwe kurudi nyumbani mpaka MWISHO WA MIMBA.

  KUTIBU ECLAMPSIA NI SHUGULI PEVU, ni EMERGENCY na inahititaji skilled hands, Kama mama ata-develop ECLAMPSIA (Kifafa cha Mimba) juhudi zinafanyika kumwokoa mama na si vinginevyo, ambapo ni kutibu kifafa na ku-terminate mimba kwa haraka sana bila kujali umri wa mimba hiyo, kama mtoto ata-survive ni bahati yake, lakini wanakuwa na complications nyingi na wachache wana-survive, sometimes with life long sequelae.

  Mimba inaweza kuwa-terminated kwa njia ya operation (caeserian section) au kama hali inaruhusu ni ku-speed up process ya kuzaa kwa madawa yanayoongeza uchungu (oxytocic drugs)

  ECLAMPSIA inaogopwa sana na ukienda kila wodi ya maternity utakuta ukutani kumebadikwa kanuni/GUIDELINES za ku-deal na ECLAMPSIA.

  Mimba ikishakuwa terminated huwa ndiyo mwisho wa KIFAFA CHA MIMBA na dalili zote zinapotea, lakini hali hii inaweza kurudia kwa mimba inayofuata.

  Hakuna ujanja au Tekinologia ya kujua kuwa mama akipata ujauzito utaweza kupata PRE- ECLAMPIA na ECLAPSIA

  Kuhudhuria kiliniki (antenatal clinc) ni muhimu sana ili kuweza kufanya screening ya matatizo kama haya, na ikigundulika mapema inasaidia kupunguza madhara mengi ya hali hiyo.
   
 4. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #4
  Aug 19, 2008
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ee Mungu mwepushe mke wangu na tatizo hili, aje ajifungue vizuri watoto wetu. thank you.
   
 5. P

  Positive Thinker Senior Member

  #5
  Aug 19, 2008
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 110
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Triplets Thank very much for this post it is real nice Mama watoto the next 10 days Inshallah anaweza kujifungua na muomba mungu asipate hayo matatizo.
   
 6. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #6
  Aug 19, 2008
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...mw'mungu atawavusha salama.

  ...Mgogoro unakuja pale 17% ya vifo vya kina mama Tanzania vinatokana na kifafa cha mimba.

  ...Katika sababu mojawapo inayosababisha vifo vya kina mama kutokana na kifafa cha mimba ni Uzembe, dharau, na ujuzi mdogo wa wauguzi :(:(:( !!!

  Really sad, inabidi siku ya siku kumshikisha muuguzi/wauguzi 'kitu kidogo', la sivyo unaweza mpoteza mama na mwana hivi hivi unaangalia

  ...hali inatisha kwa kweli.
   
 7. m

  muvimba Member

  #7
  Aug 20, 2008
  Joined: Apr 20, 2008
  Messages: 76
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 15
  Ni kweli mwa maoni yako mchongoma lakini si wauguzi woote kuwa ni wazembe mara nyingi unakuta mama yupo mabali na health facilities as the results anakuja katika advanced stage ambapo inakuwa shida sana mtu kumsaidia, mbali na hiyo look on our health facilities, disp nyingi hazina dawa za kutosha kuweka ku manage mama amabaye anakuwa na hali kama hii ya kifafa cham mimba hata hiyo wanayoita Lytic coctatai drugs kwa ajili ya ku control fits and spasm inakuwa hakuna hivyo lazima ana end with death.

  Nimekuwa nikishuhudia zaidi ya akina mama 10 ndani ya miaka 8 ambao wamekuwa wakipata mauti kwa sababau tu Nurses hawana la kufanya,na hata hiyvo ndugu zanguni coverage ya trained health staff katika nchi hii is only 32% of the required staff, unafikiri ni lini hili gap litazibika, serikari inabidi ifanye jitihada za pamoja kuweza kuwa na health trained staff wa kutosha ili maternal mortality iweze kushuka.

  Mbali na hiyo kuna wenzangu wamechangia suala la rushwa, ni kweli kabisa rushwa ipo lakini pia unajua health staff wamekuwa wanadharaulika sana na policy makers, mtu kama Nurse anaomwa kama specimen lakini ni mtu muhimu sana katika secta ya afya, look Nurse anayefanya kazi USA au hapa jirani tu Emirate kipato chake kikoje lakini Nurse wa kibongo ni choka mbaya!!!!!!!! kwa hiyo hata kama ningekuwa ni mimi lakima ningevuta huo moto tu!!! how can I make like kwa mshahara wa 280,000 wakati nna watoto na nipo katika nyumba ya kupanga.

  Ok ndugu zanguni cha muhimu ni kumuwaisha mama hosp anapokuwa mjamzito na hivyo let us join all to advocate maternal mortality to the govermant so that extra funding can be re- allocated to the responsible ministry/firm.

  Ndimi,

  Muvimba
   
 8. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #8
  Aug 20, 2008
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...ufafanuzi mzuri sana ndugu Muvimba, lakini vile vile kwa dhana hiyo hiyo ya UMBALI na health facilities ingeingia vichwani mwa baadhi ya wauguzi na kuacha DHARAU yao ya "...ndio mkome, kwanini mmemchelewesha mjamzito!"

  ...Hivi kuna uwezekano wa ku control hizo spasm na fits kabla hazijatokea? ...au some nurses mistook it with labour pains?, ...it is scarry and cruel watching your spouse/mama mjamzito going thru this kwakweli!

  ...when nature is taking place, hizo labour pains ni kitendawili, hasa mama anapokuwa ana experirnce 1st pregnancy, false alarms kibao hata kama siku zinahesabika. Ndugu Muvimba, ubarikiwe sana kwa mchango wako.

  Shukran.
   
 9. Triplets

  Triplets JF-Expert Member

  #9
  Aug 26, 2008
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 1,103
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Positive thinker, nakutakia kila la kheri ktk kumkaribisha mwanao, shaka na wasiwasi ondoa kabisa…everything will be alright with God’s help

  Ilivyotokea kwangu mimi ni kwamba blood pressure ilianza kupanda gradually kwa kama wiki mbili, wakapima routine urine protein kwa nyakati mbili tofauti hakupata kitu, kwa vile nilikuwa naexpect twins waliniweka kwenye group la wenye uwezekano mkubwa kupata hili tatizo (high risk group)…wakacheki 24 hrs urine protein wakakuta iko juu,

  Hapo hapo nikalazwa na kuanza kutibiwa, wakati huo huo wakiniandaa kwa operation…any way …I was operated and at last we ended up with two health babies

  Utaona kwamba blood pressure ikiwa juu halafu urine protein kuwa negative kwenye routine check up haimaanishi kwamba huna pre eclampisia. Nafikiri kitu cha muhimu walichofanya ilikuwa ni ile kucheki 24 hrs urine protein, hii ni tofauti na ile test wanayofanya as routine tukienda clinic
   
 10. MtuSomeone

  MtuSomeone Member

  #10
  Oct 17, 2009
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  To JF Doctor!
  Mke wangu yupo wiki ya 32 na amekuwa diagnosed kuwa na kifafa cha mimba, amebeba mapacha!! Naomba ushauri na maoni ya kitaalamu kumsaidia yeye na watoto!!
  Asante
   
 11. Pangu Pakavu Tia Mchuzi

  Pangu Pakavu Tia Mchuzi Member

  #11
  Oct 18, 2009
  Joined: Jun 3, 2006
  Messages: 43
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Semesozi, kifafa cha mimba, au kwa lugha ya kitaalamu preeclampsia/eclampsia ni medical emergency. Nina imani kuwa mkeo sasa hivi atakuwa chini ya observation ya madaktari muda wote. Kama bado basi fanya hima uhakikishe kuwa anapata hiyo attention.

  Sidhani kama kuna ushauri wa maana utapata zaidi ya kuhakikisha kuwa mkeo anapata full time attention ya madaktari (Gynaecologist) hadi atapojifungua.

  Under normal circumstances, mwanamke mwenye preeclampsia anatakiwa awe chini ya uangalizi wa madaktari ambao watajitahidi ku-control BP yake na kuhakikisha (kwa njia za kitaalamu) kuwa hafikii kupata eclampsia.


  Pole kwa kuuguza na nawatakieni kila la kheri.
   
 12. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #12
  Apr 1, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,813
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Nani anafahamu ugonjwa huu na jinsi ya kujikinga nao. Ni vyema kujikinga kuliko kutibu. Karibuni
   
 13. Mama Mdogo

  Mama Mdogo JF-Expert Member

  #13
  Apr 1, 2010
  Joined: Nov 21, 2007
  Messages: 2,865
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  Kifafa cha mimba ni ugonjwa unaowapata wanawake wajawazito, hasa wenye mimba za kwanza. Kwa walio wengi, ugonjwa huu hutokana na kupanda kwa msukumo wa damu (High blood pressure). Ugonjwa huu utokeapo, mgonjwa hupatwa na degedege (convulsions).

  Sababu kamili za ugonjwa huu hazijukani. Hata hivyo kuna sababu mbalimbali ambazo zinaweza kusababisha uwezekano wa kupata ugonjwa huu zikiwemo:-

  (i) Mimba ya kwanza, hususan katika umri mdogo chini ya miaka 20 na umri mkubwa zaidi ya miaka 35.
  (ii) Wenye mimba ya mapacha hupata zaidi kuliko mimba ya mtoto mmoja.
  (iii) Ugonjwa wa shinikizo la damu au kisukari kabla ya kubeba mimba.
  (iv) Kuwa na ugonjwa wa figo kwa mama mjamzito.

  Hakuna chanjo wala tiba ya kuzuia ugonjwa huu, bali nguvu huelekezwa katika kuchukua hatua za kuepuka tatizo hili kwa kuwashauri wanawake wasibebe mimba katika umri mdogo au mkubwa sana.

  Aidha mama wajawazito wanatakiwa kuwahi kliniki ambako watafuatiliwa maendeleo yao ili kubaini dalili za mwanzo za kifafa cha mimba na kushauriwa kwenda hospitali kwa uangalizi zaidi.

  Kifafa cha mimba kikisha tokea nguvu huelekezwa katika kupunguza madhara yatokanayo na kifafa hicho. Kwa mfano kuzuia degedege isirudie rudie kwa kutoa dawa za kuzuia degedege. Kutoa dawa za kuteremsha msukumo wa damu, iwapo uko juu, na vile vile kumsaidia mama ajifungue mapema mara itakapoonekana mtoto amefikia umri wa kuzaliwa..
   
 14. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #14
  Apr 1, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Thanks mamdo kwa ushauri mzuri
   
 15. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #15
  Apr 1, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,813
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Asante MamaMdogo
   
 16. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #16
  Apr 1, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Asante MamaMdogo. Pia kwa kuongezea ni muhimu mama mjamzito kujitahidi kupunguza kiwango cha chumvi anayotumia, na hasa chumvi ya kuongezea mezani (raw salt)na pia kuongeza kiasi cha matunda anachokula. Kwa mimba ya kwanza, ni vizuri kufanya utaratibu wa kujifungulia hospitali kubwa just incase( badala ya zahanati). Ni muhimu kupata matibabu sahihi mara dalili za kifafa cha mimba zinapojitokeza.
   
 17. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #17
  Apr 1, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,813
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Walioko vijijini ndani wanapata sana shida kutokana na hili tatizo
   
 18. m

  mnyakyusa JF-Expert Member

  #18
  Apr 1, 2010
  Joined: Feb 24, 2010
  Messages: 248
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tunashukuru kwa ushauri
   
 19. Kobe

  Kobe JF-Expert Member

  #19
  Apr 1, 2010
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 1,756
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180

  kwenye blue matunda yanaongezea nini katika kukinga, na je vipi akiwa mjamzito kwa mara ya pili apunguze hicho kiasi cha matunda? naomba unifahamishe kiundani hapa madau.
   
 20. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #20
  Apr 1, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,813
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Matunda ya aina gani? inawezekana yote lakini kuna ambayo ni muhimu zaidi
   
Loading...