Elimu kuhusu investment kwenye kampuni za tanzania yanayoanza kutoka makampuni makubwa ya nje | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Elimu kuhusu investment kwenye kampuni za tanzania yanayoanza kutoka makampuni makubwa ya nje

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by C.T.U, Sep 27, 2012.

 1. C.T.U

  C.T.U JF-Expert Member

  #1
  Sep 27, 2012
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 4,708
  Likes Received: 1,210
  Trophy Points: 280
  Wakuu habari zenu

  katika uwanja wa biashara sasa hivi kumekuwepo na wingi wa makampuni makubwa duniani katikan kila sekta, tukianza sekta ya Habari, Teknolojia, Media, Fedha, Afya na Madawa n.k
  na katika sekta hizo kumekuwa na makampuni mengi sana ambayo kwa namna moja au nyingine yamefanikiwa sana na hata kufikia kiwango cha kuteneneza 100 mill $ mpaka 1 bill $.

  Lakini ukianza kufuatilia kwa karibu kuwa hayo makampuni yamewezaje kufikia hapo walipo utagundua kuwa wale founders kama founders wao wenyewe sio walioifanya biashara zao siwe successful kulikuwa kuna wataalamu wamewaajiri, walikuwa na vifaa ambavyo ni advance (servers za facebook, yahoo e.t.c), swali la kujiuliza ni kuwa walipataje mtaji mkubwa kama huo??

  asilimia kubwa ya watanzania wanafikiri kuwa kuanzisha kampuni kubwa ni kitu ambacho ni ndoto na ni wazungu pekee ndio wanaweza na watu wenye pesa zao lakini wamesahau kuwa hata wazungu wanaowaona ni matajiri walikuwa ni watu wa kawaida tu ila hawakuogopa kwenye kufanya biashara .

  Tuje kwenye suala la mitaji

  kwa wenzetu wana makampuni ambayo wanalenga kuwekeza kwenye projects mbali mbali sio kama huku bongo mtu wenye idea ndio wanatafuta investors au mikopo bank wenzetu ma investors ndio wanatafuta watu wenye ideas

  makampuni kama Austin Ventures Austin Ventures ni watu ambao wanaonekana kabisa wao ni watu wanaotafuta watu wenye idea na kuinvest japokuwa hiyo ni kampuni inayotaka kuinvest USA tu bado hawjaanza kuinvest worldwide ila kuna wengine kama eVentures wao wana invest worldwide

  Wazo Langu

  wazo langu kwa kuwa nina imani na watanzania wenzangu kuwa ni watu wenye ideas ila wengi wao wanafichwa au kukatishwa tamaa au kuzungushwa na Ma BENKI ha ya hapa kwetu wanapoenda kuomba mikopo au kupewa riba za juu na kwa kipindi kifupi au watu wenye fedha zao ambao wamekuwa wakifuatwa na vijana wadogo kwa lengo la wao kuweka fedha zao kwenye biashara hizi
  na watu wenyewe watu wenye fedha zao (individual) ni kuwa either ni watu wasioingilika kirahisi yaani si rahisi kwa mtu huyo kukutana na kijana mdogo aliyemaliza chuo kikuu leo kukutana na mtu kama Rostam, Mengi, Bakhresa, au watu hao wenye fedha chafu maana ukisikia mradi fulani utasikia ni wa flani (mkubwa wa serikali) ambaye watu watadai kuwa kawekeza pesa chafu pale
  hivyo kumewafanya vijana hao kuanza biashara kwa kuunga unga , kwa mtaji midogo au kukimbialia kwenye soko la ajira kwa lengo la kuzicanga CAPITAL

  kwanini vijana wadogo wanaomaliza shule wasianze kwa kuandaa proposal , kutulia na kuanza kuandika business plan na KUTUMA PROPOSAL ZAO KWA MAKAMPUNI YA NJE ? yanayoplan ku invest worldwide....??

  kuna makampuni kibao ya INVESTMENTS wanataka kuinvest africa Tanzania ikiwa ni sehemu moja wapo.... Tanzania ni nchi ambayo inaendelea hivyo basi kuna opportunity nyingi sana ambazo vijana wa leo wanatakiwa waamke wazichangamkie

  kuna opportunity nyingi sana bado hazijakamatwa vizuri ila nikiangalia kwa makini naona kuna billion dollars ila watu hajaamka wanasubiri serikali iwafanyie kila kitu please guys lets wake up....

  Elimu ninayotaka kueleweshwa

  -je kuna sheria yeyote kuhusu uwekezaji hapa nchini??

  -kama mtu una proposal yako na umeongea na kampuni kubwa ya nje a uwekezaji iliyokubali kukupa pesa ya kufanya hiyo project je kuna gawio lolote ambalo serikali inabidi ipate??

  -je kuna security yeyote ambayo napata mimi mradi wangu usiporwe na serikali akapewa mtu mwingine ili waweze kugawana huyo third party na serikali fedha za mwekezaji huyo (rejea kesi ya sugu na ruge)

  Sekta ambazo zitavutia wawekezaji

  -Kilimo
  -Madini
  -Uzalishaji
  -Utalii
  -Usafirishaji wa Anga
  -Habari na Media
  -Filamu
  -Muziki


  Natanguliza shukrani...
   
 2. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #2
  Sep 27, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Nadhani tatizo inakuwa access kwa mtu wa kawaida kuwajua hao Angel Investors wa nje ngumu.Pia nadhani kutakuwa na ugumu kwa wao ku Invest pesa zao huku kwetu ukizingatia mambo kama political instability, unrealiable power, Poor infrastructure, kupata skilled individuals, bureaucracy n.kUkiangalia hapo utagundua Risk inakuwa kubwa sana huku kwetu ndio maana makampuni yanayo Invest Africa yanakuwa yanapata return kubwa na tunaishia kushangaa mrahaba serikali inapata 3% ni kutokana na hizi fear za wawekezaji.
   
 3. Gelange Vidunda

  Gelange Vidunda JF-Expert Member

  #3
  Sep 27, 2012
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 312
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wazo zuri lakini linazuilika kutekelezwa kwa sababu mbalimbali:
  1. Benki zote nchini hazitoi mkopo kwa biashara mpya (they don't lend to startup companies)
  2. Hao wanafunzi unaowasema wengi wanaweza kuwa na idea nzuri za biashara ila kwa namna moja au nyingine expirience/uelewa ni finyu - wanahitaji muongozo kama huo wa angel investors ambao kwa Tanzania haupo. Watu wengi hapa bongo wenye ideas lakini mtaji hawana simply ni kwamba hawakopesheki, either as in #1 au hawana kitu cha kuonyesha kama wanafanya/wamefanya biashara hizo.
   • Hata wale wanaoanza kwa tabu sana kwa nguvu zao wenyewe hawana uelewa wa kufikia mahala ambapo wataweza kukopesheka.
   • Uelewa mdogo, biashara zao hazijasajiliwa,
   • kuchanganya akaunti moja ya benki na kudeposit fedha za binafsi na za biashara humohumo
   • Lakini vilevile zile taasisi zilizowekwa kusaidia michakato mbalimbali kama hii ya biashara zinafanya kazi hafifu sana. Mfano TPSF ambao wao wamepewa jukumu la kusaidia kutoa mafunzo ya kibiashara are not very effective - personally I think they can do more.

  Angel investors in Tanzania actually exist but in a very disjointed way. Ukienda kule Ifakara na kwingineko katika bonde la mito Kilombero/Rufiji/Ruaha etc., kuna wafanyabiashara ambao wankopesha mbegu na pembejeo etc na unayekopa sharti ulipe in kind, yaani utalipa makubaliano kwa madebe ya mpunga. The drawback is yule investor ndiye anayefaidika sana manake yeye ana magodown ya mpunga na anamonitor bei za mpunga kwenye masoko yote, hususan DSM. Yule aliyekopa ends up being a subsistence farmer with just enough to feed his family and knows nothing else. Lakini kama angewezeshwa, afundishwe, aelewe kwamba katika mavuno yake ajifunze kuweka akiba kidogo benki za kule, ajisajili hata na wenzake wengine, na waende kukopa kwenye mabenki huko etc., nadhani wanaweza kufanikiwa in the long run.
   
Loading...