Elimu Hizi za Wanasiasa Wetu Zinatusaidia nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Elimu Hizi za Wanasiasa Wetu Zinatusaidia nini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kichuguu, Nov 18, 2009.

 1. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #1
  Nov 18, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Mod, najua kabisa kuwa maudhui ya hii post yalishajadiliwa sana hapa, hata hivyo naomba uniruhusu nirudie tena kwani wahenga walisema si vibaya kujikumbusha mambo ya muhimu.

  Nilikuwa natafuta kopi ya sheria fulani pale kwenye tovuti ya Bunge nikakaribishwa na CV ya mbunge mmoja iliyonivutia sana ikanifanya niiangalie kwa makini. CV yenyewe nimeibandika hapa.

  [​IMG]

  Ukiangalia hiyo timeline ya hizo digrii nilizowekea alama na hayo madaraka aliyokuwa nayo serikalini, unashindwa kuelewa kama huyu mtu kweli alikuwa anafanya kazi au alikuwa shuleni. Na kama kweli mtu anaweza kusoma digii nyingi hivyo kwa muda mfupi linakuja swali jingine tena kuwa kwa nini hakuzipata digii hizo kabla hajapata madaraka?

  Kilichonifurahisha zaidi ni vile vyuo alikopatia digrii hizo. University of Phoenix imekuwa kwenye headlines kwa muda mrefu kuwa ni digrii mill, hivyo sitaiongelea. Ninapenda kuongelea hiyo University of Newcastle ambacho ni chuo cha heshima kubwa sana kitaaluma; kimoja kiko England na kingine kiko Australia. Ukiangalia digrii za mheshimiwa huyo utadhani kazipata kutoka mojawapo ya vyuo hivyo na unaweza kumheshimu sana hadi utakaposoma hii:

  Outrage in academic world at fake degrees sold online

  Mar 15 2008 by Liz Hands, The Journal


  FAKE degrees from the North-East’s top universities are on offer for less than £40 a time.


  Victoria Murphy holds a fake degree which was sold on the internet

  The bogus certificates, printed on parchment, carry replicas of university crests and embossed seals.

  They can be obtained at the touch of a button from an internet site which boasts that with its help, getting a certificate “is as easy as 1, 2, 3”.


  On offer are phoney qualifications in the name of Newcastle, Durham, Northumbria and Sunderland Universities.


  Academics at the region’s leading educational institutions and politicians are outraged at the scam.

  But Higher Education Minister Bill Rammell warned it was difficult to prosecute in cases like this.

  Durham City MP Roberta Blackman-Woods, of the Department for Innovation and Skills Select Committee, last night pledged to call for a Commons investigation.

  She went on: “If people are buying these degrees to pretend it is something they have, then that is surely fraudulent.

  “It is also unfair on the students who put a lot of time and effort into getting their qualification from a recognised institution.”


  A Newcastle University spokesman said: “The fact that this website is offering fake degrees is very worrying and we will be investigating it further.”

  A statement issued by Northumbria University said: “We absolutely oppose the selling of fake certificates, as it clearly undermines the hard work, talent and commitment of genuine students.”

  A warning was issued by Durham University. Their spokesman said: “Any attempt by someone to pass off a fake degree certificate as the genuine article could lead to serious repercussions for the person concerned.”

  And at Sunderland, they were anxious to emphasise the differences between their certificates and the fakes.

  They said: “We would expect all employers, as we do, to have a number of checks in place to ensure a potential employee’s credentials.”

  The website, The Certificate Factory, describes itself as “your online source for authentic fake degrees, fake diplomas, fake HNDs/HNCs, fake transcripts and more”.

  It boasts: “We can provide fake degrees for any university or college in the UK and worldwide.

  “With the additional use of authentic crests and logos, you’re the only one who will know that you have a fake certificate.

  “It’s as easy as 1,2, 3.”

  Each certificate costs £39.95. For an extra £49.95, buyers can also have a transcript – a breakdown of the marks they supposedly achieved to earn their degree.

  The website, which has sister sites around the world, claims its products are intended for novelty use.

  But a statement from Universities UK, which represents higher education across the country, said: “You would have to be quite naive to believe that such certificates are being purchased for ‘novelty’ purposes.

  “Despite disclaimers on such websites, it is quite clear that this activity is dishonest and could result in serious consequences for someone trying to pass it off as a genuine UK degree certificate.”

  And Diane Warwick, Universities UK chief executive, said such certificates devalued “the efforts of genuine students who work hard to achieve their degrees”.

  “We have taken a strong line on this issue in the past, including legal action against one individual, and we will continue to work to counteract those who attempt to falsify qualifications,” she said.

  “We will be alerting the Government department to any such activity.”

  She said a change in the law was needed before the issue could be properly tackled.

  Bill Rammell, Minister for Higher Education, agreed. He said: “For those behind the sale of fake degrees to be successfully prosecuted in court, hard evidence is required to prove that they were deliberately complicit with their customers who, in turn, also have to be proven to have purchased fake degrees for financial advantage.”

  Students are also angered by the scam. Jamie McDonnell, president of Newcastle Union Society, said he was deeply concerned.

  “This website makes a mockery of the time and effort that dedicated hard working students put into achieving their qualifications,” he said.

  “I am offended by the nature of the website and by any organisation that condones its use for personal gain.”

  And the higher education watchdog, the Quality Assurance Association, described the website as unacceptable.

  Their spokesman said: “Anyone looking to buy such a certificate with the intention of using it to gain employment or admission into education could find themselves accused of deception.”

  The Journal gave The Certificate Factory operators the chance to answer criticisms of their site, but they failed to take that opportunity.

  Last night, the website appeared to have been taken down.

  A spokeswoman for Northumbria Police said the force would look into the matter if a complaint was received.


  Swali langu ni kwamba kama kweli watu wenye madaraka nchini wanapofanya upuuzi wa namna hii, je tunategemea watoto wafanye nini tofauti? Kwa nini tusiridhike na elimu zetu halali? Tabia hii ya kununua digrii feki kwa pauni 40 na kuzipeleka kwa wananchi ni namna nyingine ya rushwa.
   
 2. m

  mwanamasala JF-Expert Member

  #2
  Nov 18, 2009
  Joined: Jun 20, 2009
  Messages: 248
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Huyo ni mheshimiwa nani?Diallo?hiyo doctorate ya chuo cha newcastle Uingereza/Australia?
  Kwa nini TUC isicheck na hiyo University?
   
 3. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #3
  Nov 18, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Huyo Diallo au nani? We dare speak open is the motto here sir, name names.

  Kama Diallo mbona anajulikana kama darasa la nne? hata hiyo Private Candidate ya Form Four ni suspect.

  Na michongo yote ya shule pamoja na mitihani alikuwa anafanyiwa na mkewe (UDSM graduate) pamoja na wapambe, no wonder midigrii kibao katika kipindi kifupi.
   
 4. m

  mwanamasala JF-Expert Member

  #4
  Nov 18, 2009
  Joined: Jun 20, 2009
  Messages: 248
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  It is a joke!Dr Diallo....oh my God.
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  Nov 18, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,412
  Trophy Points: 280
  Kichuguu, heshima yako mzee.
  Hebu tuwekee hiyo link inayotupeleka moja kwa moja ili kuondoa hofu ama wasiwasi wa hii scanned (?) au print screen (?) document kuwa altered.

  Jambo jingine ambalo watu wengi humu wamekuwa hawaonyeshi kuchukizwa nalo na ambalo mimi tokea zamani nimekuwa nikilipigia kelele sana ni mtu anayewapa madaraka hawa jamaa.

  Kiongozi makini atafanya kila linalohitajika kuhakikisha kuwa mtu au watu anaowateua kuunda serikali yake wana sifa zinazothibitika. Mijitu ina fib resumes zao na inapewa madaraka. Kwa upande wangu siilaumu sana mjitu kama hiyo. Ninayembebesha lawama kwa asilimia 100 ni yule anayeipa madaraka hii mijitu.
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Nov 18, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,577
  Likes Received: 18,557
  Trophy Points: 280
  Macheti yawe feki au real, doesn't matter much, kinachomata ni jee anadeliver?. Wako viongozi wenye vipaji vya uongozi na uwezo wa uongozi ni darasa la saba/nane huku wanadeliver, na wapo wasomi wa vyuo vikuu, na Ph.D za ukweli lakini hamna kitu.

  Pamoja na jamaa kumtosa, ameibeba sana CCM Kanda ya Ziwa, yaani kura za uamuzi (deciding votes) za nani anakuwa rais wa nchi hii ni za kanda ya ziwa pekee, akihamishia majeshi yake popote, CCM kanda ya Ziwa itatoka patupu, ashukuriwe japo kwa hilo.

  Uchaguzi wa Busanda timu yake pia ilifanya kazi nzuri, siku ya mwisho ya kampeni, zilifungwa rasmi saa12:30 jioni, Saa 1:00 usiku Star Tv ikavurumisha kipindi maalum cha kampeni za Busanda ikionyesha violence na kuibambikia Chadema huku CCM kikifagilia funika bovu.

  Kipindi kilirudiwa kesho yake asubuhi saa 1:00-1:30 siku yenyewe ya uchaguzi!.
  Huu ni uzalendo mkubwa kabisa kulko hata sheria ya uchaguzi ya mwisho wa kampeni.
  Jamaa alitakiwa akumbatiwe kwa nyimbo na mapambio. Nakuomba usimchafue na hayo macheti, he is succesifully anyway.
   
 7. K

  Keil JF-Expert Member

  #7
  Nov 18, 2009
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Huu ni mkorogo mtupu, nchi hii tutajaza vihiyo mpaka basi. Ofisi ya Bunge nayo ina matatizo makubwa sana. Hivi kwanini huwa hawa-verify info wanazopewa na wahusika? Ningekuwa ni mimi ninaangalia hiyo fomu ningeweza kujiuliza maswali mengi sana.

  1. Hivi mtu anaweza kupata admission ya kufanya MBA/PhD kabla hajamaliza undergraduate? Undergraduate: 2002 - 2006; MBA: 2003 - 2005; then PhD: 2004 - 2008. Jamaa alipata MBA kabla hajamaliza first degree.

  2. Kwa muda huo mfupi na akiwa Mbunge, Naibu Waziri na baadaye Waziri kamili, aliwezaje kupata degree zote hizo? Maana hiyo inahitaji mtu awe full time shule na siyo part time. Hapo kuna mawili, ama alikuwa hafanyi kazi na muda wote walikuwa anasoma shule, ama shule walikuwa wanamsomea wengine, au kanunua vyeti ili kutuzuga wadanganyika kwamba Mheshimiwa Mbunge/Waziri ni msomi.

  3. Hivi Rais anapoteua mawaziri huwa haangalii CV zao? Usalama wa Taifa huwa hawafanyi vetting ya credentials za waheshimiwa mawaziri?

  Sasa ninaelewa kwanini tunazidi kuwa masikini, ukiongozwa na kiongozi kihiyo, usitarajie awe na priorities, na inawezekana priorities zake zikawa ni utapeli ama akawa anawaelewa zaidi matapeli wenzake kuliko wachapa kazi genuine. Viongozi wa jinsi ya huyo Mheshimiwa hawawezi kuona umuhimu wa elimu, so hata mtu akija na cheti cha mchongo atampa kazi na tena madaraka makubwa sana na matokeo ni uozo kila siku!
   
 8. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #8
  Nov 18, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  (1) Ni kweli huyo ni mheshimiwa Dialo. Ukeinda kwenye tovuti ya Bunge tafuta profile yake utampata.


  (2) Ishu iliyopko mbele yangu siyo kuhusu uwezo wake kibishara au kisiasa. Jambo linalonikera hapa ni huo utaratibu wa watu wenye madaraka katika jamii yetu kununua vyeti vya elimu. Wanakuwa wanaonyesha mfano mbaya kwa watoto kuwa hakuna haja ya kwenda shule ili kupata digrii bali kinachotakiwa ni kuwa na pesa za kununua cheti bila kukisomea. Elimu ni jambo la muhimu sana katioka jamii, na endapo tutajenga jamii ya watu wananoununua vyeti basi hatutafika popote.
   
 9. K

  Keil JF-Expert Member

  #9
  Nov 18, 2009
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu Pasco,

  Hili swala halina uhusiano wowote na ku-deliver, bali ni image ya serikali na hasa ukizingatia kwamba mtu huyo anakuwa ni public figure. Je, anatoa picha gani kwa wananchi na hasa vijana, kwamba kumbe unaweza kuchonga vyeti na wala kusiwe na noma.

  Hii haina tofauti na ufisadi ama mission town. Kama mtu anakaa kijiweni na mambo yanamnyookea unategemea kuna watu watataka kufanya kazi halali? Kila mmoja atakuwa anakaa kijiweni na kusubiri mission ili apige mizinga. Hatuwezi kufika mbali kwa mwendo huu.

  Kama ni successful kwenye politics basi aridhike na mafanikio aliyo nayo na asidanganye kiasi kwamba mpaka watu wamshitukie, na kuanza ku-question vitu ambavyo havina maana. Hivi asipoweka huo uongo wa vyeti inampunguzia nini? He is already a business tycoon, also a politician ambaye ni lulu, JK atake asikate lazima atamhitaji tu na siyo JK hata mgombea mwingine yoyote wa kiti cha urais.

  Hii ni aibu kwa ujumla, na inasikitisha sana. Nitamheshimu sana kama atakubaliana na hali ya elimu aliyo nayo.

  Hivi Msemakweli hakuona hii CV? Maana sikuona jina la huyu Mheshimiwa kwenye orodha ya nshomile Msemakweli aliyoipeleka kwa Spika wa Bunge.
   
 10. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #10
  Nov 19, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180

  Mkuu mbona uchoki kuboronga. His humble beginning is a very good thing, and he doesn't need to spice it up with fake diplomas. Infact, he would have proved to many that there are rooms for people with limited formal education.
   
 11. m

  mzanganyika JF-Expert Member

  #11
  Nov 19, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 257
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wadau.

  Ninaelewa concern zenu lakini naomba niwawekee jambo moja sawa.

  Nataka nisema kwamba University of Phoenix sio degree mill kama maana yake ni degree kibao na nyepesi.yaani za bure bure mradi uwe na hela.

  Hawa jamaa kwanza kupata admission wanasumbua sana, wao wanatambulika na acceditation boards zenye heshima amabazo hazitambua other universities na hata masomo yao si ya mchezo mchezo, inabidi ujipinde sana kuweza kupata distinction.

  Tuangalie mengine lakini fikra kwamba Uni of Phoenix ni degree mill ni misconception kubwa, pengine ni kwa sababu wanajitangaza sana.

  Zungumza na wanafunzi wa hapo na mutasikia kifumbi.
   
 12. Monsignor

  Monsignor JF-Expert Member

  #12
  Nov 19, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 523
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kawaida ya Captain Haddock ni kutukana una bahati nachelea rungu la mods kunishukua vinginevyo ningekuporomoshe mijitusi maana siyo matusi hadi ujione uko uchi wa nyama. acha uongo ni watu wangapi Busanda wana TV?

  Kinacho matter ni kudeliver? Ku deliver my black a**. Ashakuliwe kwako wewe na familia yako. Huyu jamaa ni kansa katika jamii. Huwezi kuishukuru kansa kwenye family line yenu eti tu kwa sababu watu wana kufa katika umri mdogo hivyo mnapungua watu wa kugombea urithi.

  Dawa ya kansa ni kuondoa sehemu iliyoanza kabla haijasambaa mwili mzima. Mwambie anko wako aanze kujiandaa kuna siku atakuja kujibu. Scandarel, mongrel,seven hundred suffering samurais, seven years of bad luck on top of that billions of blisstering banarcles.
   
 13. Kibunago

  Kibunago JF-Expert Member

  #13
  Nov 19, 2009
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 288
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Pasco kasema ,
  Pasco kasema (paraphrased)


  Pasco nakuunga mkono na hivyo ebu shuka na mimi katika propositions zifuatazo tuone tutafika wapi:

  Kwa vile wapo baadhi ya watoto (chini ya miaka 18) wenye kuweza kufanya maamuzi ya busara kuliko baadhi ya wazazi wao, it doesn't matter much, hata watoto hao wakijiandikisha kupiga kura kwa kuwasilisha vyeti feki vya kuzaliwa kuwa wana umri wa miaka 18 au zaidi.


  Kwa vile ndani ya JF kuna baadhi ya waandishi ambao ni bora kuliko baadhi ya wahabarishaji wa Ikulu, it doesn't matter much kuanzia sasa tukijitambulisha duniani kuwa sisi ndio the Tanzanian Presidential Press.


  Kwa vile kuna baadhi ya Makondakta na Ma-day-Worker ambao wanaweza kuendesha vizuri zaidi ya baadhi ya madreva, it doesn't matter much, hao makonda wakiamua kuendesha Magari kwa kuwasilisha leseni badia za udereva.

  Kwa vile kuna baadhi ya Wagombea ambao hawakuchaguliwa ambao wana ushawishi na sifa za uongozi kuliko baadhi ya waliochaguliwa, it doesn't matter much hao jamaa wakitinga Mjengoni na kupokea posho kwa kutumia utambulisho feki wa waliochaguliwa.

  Kwa vile kuna baadhi ya vijana wengi makapela ambao wanajua ‘malavi-davi' kuliko baadhi ya wanandoa, it doesn't much vijana hao wakipokea haki mbalimbali za wanandoa kwa kuwasilisha vyeti feki vya ndoa.

  Kwa vile kuna baadhi ya Wageni nchini kwetu wanaonekana kuonyesha uzalendo zaidi kuliko baadhi ya raia wenzetu wa Tanzania, it doesn't matter much hao wageni wakiingia na kuishi hapa nchini kwa kuonyesha passport za Kitanzania za kughushi.


  Kwa vile…………….., it doesn't matter much…………….
   
 14. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #14
  Nov 19, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,577
  Likes Received: 18,557
  Trophy Points: 280
  baada ya kukusoma, nakiri makosa, nilikosea, nakubali macheti nayo yanamatter.
   
 15. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #15
  Nov 19, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Kwa kweli inasikitisha na kwa kuwa ndivyo tulivyo, haya tunayoyaona ni mavuno ya ujinga wetu.

  Ndio sababu hata rate ya wasiojua kusoma na kuandika tena katika karne hii wamekuwa wengi sana.

  Imekuwa proved wakati wa kura za serikali za mitaa. Inasikitisha sana.
  Kwa kumnukuu rafiki yangu julius "Miafrika/Watanzania ndivyo tulivyo"
   
 16. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #16
  Nov 19, 2009
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  I

  IS HE SUCCESSFULLY OR SUCCESSFUL? mafusadi wote ni successful kwa vigezo vyako. So we have to be very grateful them, eh?
   
 17. O

  Ogah JF-Expert Member

  #17
  Nov 19, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145

  wengine tulikuwa twaona ni chongo mwenzetu ulikuwa waona ni makengeza...........anyhow......Safi sana Pasco kwa kutambua hili jambo kuwa ni chongo.............
   
Loading...