Elimu hii ya siri ndiyo kitovu cha hekima na upotoshaji katika sayari yetu

Undava King

JF-Expert Member
Aug 11, 2017
3,121
5,215
Ufahamu tokea mwanzo ulijengwa katika misingi ya udadisi na kutenda, baadae likaja suala la kuamini na ikatokea au isitokee lakini kukawako na tumaini wenda itakuwa.

Kitu cha kwanza kuanza nacho binadamu hapo kabla nshaelezea ni UDADISI na udadisi huu ulilenga zaidi kujua namna mazingira yake yalivyo na namna ya kuweza kugundua kile ambacho bado fahamu hazijaweza ng'amua ni nini hasa, au chanzo chake ni nini au mwisho wake ni wapi mf. tabaka la anga hewa, mvua au radi yatokeaje, jua huwa linatoka wapi na kwenda kujificha wapi n.k

Kupitia udadisi huu wakutaka kujua zaidi nje ya mazingira yanayofikika kimwili na kwa kuwa vyote vile vilivyokwisha wezekana kwa njia ya mwili vilitendwa kwa VITENDO napo elimu hii ya kudadisi na kutenda ikapelekea elimu iliyodumu baadae kama sayansi ikijengwa katika misingi ya vinavyoshikika au kuthibitika ndivyo hasa vyenye mwitikio chanya kwa maendeleo ya mwanadamu.

Ombwe kubwa likawa katika vile ambavyo udadisi haukuweza kutoa majibu ya moja kwa moja iwapo kuna njia itayomwezesha binadamu kufanikiwa kwa vitendo kuthibitisha au kuvigusa hili kujiridhisha kuwa ndivyo vilivyo ama la, hapa ndipo elimu yenye siri kuu yaani elimu ya udadisi wa anga inapoanzia.

Udadisi wa mwanadamu ulipoongezeka katika ubashiri na kubuni mambo mbalimbali na kuchunguza kila kinachoendelea juu ya anga lake aliweza kung'amua juu ya vitu vingi sana ambavyo leo hii twavifahamu isipokuwa tu vile vichache tulivyokuja kuvigundua katika siku za usoni.

Lakini katika kudadisi huku ndipo binadamu alipokuja kugundua kuwa siyo vyote anavyoviona kwa macho tu ndiyo vilivyopo isipokuwa vipo vingi ambavyo ni zaidi ya anavyoviona kwa macho ila vimefichika asipate kuviona.

Wapo binadamu wasiokata tamaa katika kutafuta ukweli, hawa walikuja kugundua njia za kupenya nje ya ukuta wa fahamu zao nakuona yafanyikayo katika anga la siri maarufu kama elimu ya astrolojia(forbidden truth).

Elimu hii ntaifafanua kwa ufupi tu kuwa ndiyo elimu pekee ya hatari zaidi duniani, uruhusiwi hata nusu kujulikana kuwa unayo, wenye elimu hii robo tatu ni vichaa(ila wanakuzidi maarifa na hekima kiasi cha kutojilinganisha nao hata robo endapo dishi likitulia wanauwezo wa kukupa shule ambayo utoikuta kwingine maishani, kukubashiria maisha yako kama vile ni miungu n.k) au pengine utoweka kimaajabu katika uso wa dunia hii mapema kabla hawakamilisha mission yao,

Elimu hii ya siri ilipogundulika wengi walihitaji kujifunza na kuijua kama ambavyo walifanya katika elimu zingine zakudadisi na kutenda, ila kutokana na hazina kubwa ya utajiri wa maarifa na hatari iliyopo, binadamu wachache wenye ufahamu huu waliamua kuficha ukweli makusudi ili walio wengi wapate kuambiwa yaliyopo na yatakayojiri kwa njia hii kupitia wawakilishi wachache.

Hili likawa ndilo chimbuko la IMANI juu ya miungu na kukua kwa maendeleo ya sayansi na teknolojia kupitia kwa wawakilishi hawa wachache ambao baadae waliwaibia siri hii baadhi ya wanavitendo(sayansi) ambao walitumia fursa hii kujeuza yale yapatikanayo ndani ya elimu hii kuwa vitendo na hivyo kuchochea gunduzi mbalimbali duniani na katika anga huku wakificha chanzo cha ufahamu wao walipouchagizia.

Imani juu ya visivyoonekana ilipozidi kukoza huku kila mwenye access na elimu hii akizidi kuja na yake kutokana na upana wa elimu hii iliyojificha kuwa kubwa mno kuliko uwezo na fahamu za wanafunzi ikaonekana kuna miungu au nguvu kubwa ambazo zapaswa kuinamiwa au

kusujudiwa na hapo ndipo ukawa mwanzo wa mwanadamu kuibainisha au kuhidhihirisha kwetu hiyo miungu kwa maumbo na taswira zao zilivyo (kwa njia ya masimulizi na michoro mfano ni zodiaki) na pia kuiundia hadhithi kulingana na wasifu wa miungu hiyo hasahasa kitabia,mapambano na kimahusiano na viumbe wengine(mfano ni hadithi tunazoita za wagiriki, misri n.k)

Ukisema astrolojia leo hii mbele za watu ambao tiyari washakuwa brainwashed na sehemu ya elimu waliyopewa udhani kuwa unazungumzia masuala ya kufikirika na kuwa unaongelea elimu moja ya kichawi au ya utabiri au iliyopitwa na wakati kwa sababu ya kuegemea ushahidi toka katika tawi dogo la waliojifunza siri ya astrolojia nakuiwasilisha kwa njia ya vitendo yaani unajimu(wanasayansi)

Kila ukionacho katika astrolojia ya mtandaoni jua umepigwa na kamwe si ukweli na ukweli nikidogo sana mfano zodiaki si 12 au 13 tu ulivyokaririshwa na wala hakuna utabiri wowote wa mtandaoni wenye theluthi ya ukweli na astrolojia ya ukweli si sayansi iliyochapwa kitabuni hivyo usijilishe theory za uongo kuwa umebobea elimu ya astrolojia bali hizo ni principle za wajanja wachache tu kutawala akili za wengine na kupiga pesa,

Jua kuwa elimu ya astrolojia ni karama na ina njia zake zakupita hili ufike huko (sacrifice) na hii ndiyo elimu adimu zaidi kuwa nayo hapa duniani, tofauti na hapo nakuomba tembea kote mtandaoni na kwenye vyanzo vya maarifa kutafuta ukweli juu ya elimu hii utakachoambulia nikupumbazwa tu kuwa ni elimu ya kubuni na kamwe si kweli, mara uambiwe ni majini, mara udanganywe na usomaji nyota, utabiri n.k Lengo ni hili uendelee kukaa humo gizani.

Itaendelea.....
 
Ebu jitaidi kwenda kwenye point usizunguke sana
Uandishi unakanuni zake na hiyo subira kwa msomaji ni sehemu ya kufanikiwa kwa sanaa yangu ukiona nakawia ebu bandika andiko lako la moja kwa moja lisilo na mtiririko wa simulizi
 
Niliwai kuonana na mzee mmoja ivi kimuonekano ni kama kichaa kabisa ila mambo aliyokuwa anaongea nikawa mpaka na shangaa anaweza kutaja mpaka calendar ya mwaka elfu30 na kuzielezea hii tarehe itakuwa juma frani.

Kuna watu wanajua mambo mengi sana yani.
Ni kweli mkuu hawa watu wapo katika jamii zetu na mara zote huwa atuwazingatii kwa lolote tukichukulia ni wehu
 
Hizi mambo aisee. Sasa mnajuaje kua hii nj kweli na hii si kweli??

Kwanini unaamini wewe hujawa brainwashed na hizo taarifa zako??
Ndiyo maana kuna tofauti kati ya karama/kipawa na kujifunza kutoka kwingine iwe kwa mtu, kusoma au kusikia n.k
 
Back
Top Bottom