ELIMU: Elewa hatua zote za jinsi Radi inavyotokea na njia zake mpaka mwisho

reyzzap

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
6,660
20,989
Kukiwa na Joto maji yanavukizwa na hatimaye kua mvuke ambao taratibu hupanda kuelekea mawinguni, huu mvuke ukishafka juu ukakutana na hali ya hewa/mawingu yaliyopoa/yenye ubaridi basi nao hupoa na kua mzito au kua katika hali ya unyevu unyevu (condensation) ambayo ndio mawingu sasa,

Kwa hiyo basi kule juu kutakua na mawingu ya aina mbili : yaliyopo juu tayari (ambayo hua mazito zaidi) na yanayopanda (ambayo yana uvugu vugu ambayo hupoa na kua mazito kadri yanavyopanda kufikia haya yaliyopoa zaidi)

UKARIBIANO kati ya haya mawingu yaliyopo kule juu (wingu zito ambalo lina hali ya matone tone ya maji) na mawingu yanayopanda (wingu jepesi ambalo bado lipo kwenye hali ya mvuke mvuke) hii itafanya sehemu ya JUU ya wingu linalopanda kua positive au negatively charged, na sehemu ya CHINI ya wingu la juu (wingu zito lenye matone matone ya maji) kua negatively au positively charged (RESPECTIVELY) kutokana na kasi ya mvutano, yaani lazima mawingu mawili yanayoshabihiana yatofautiane charge kwanza, hii hutokea through induction (charging something without direct contact, hahaaa hapa kama hujasoma static electricity lazima ukunje ndita)

Kukitokea upepo unaopita kati ya haya mawingu mawili, negative charge (lets say zipo upande wa juu wa wingu la chini/linalopanda) zitavibrate na hatimaye kufuata zile positive zilizopo upande wa chini wa wingu la juu, haraka zile negative charge zitakapogusana na positive itatokea shoti kali huku zote zikisuguana na kuvutana, za chini zikilazimishwa kuja juu na zikishakutana zitaleta shot (zitaunguzana), mvutano huu kwa kua una ukinzani mkubwa basi hutokea kwa njia ya zigzag, ambao huitwa radar kwenye physics (Ndio ule mwanga mkali unaouonaga unaokaa katika mstari ulio pinda pinda), ukiona umetokea juu haukufika chini basi ujue ni shot kati ya mawingu na mawingu (Japo muda mwingne ukinzani ukiwa mkubwa hufika mpaka ardhini), na kwa maana hiyo kitu chochote kilichopo/kinachopita kati ya yale mawingu mawili basi kitaunguzwa(ule mwanga unakua na jotoridi la nyuzi zaidi ya 30,000'C), hapa ndege haitadhurika au idhurike kidogo sana tena ni maeneo ya pale zile charge zitakapo ingilia au kutokea tu, au kwa sababu ya material mengne yaliyopo ndani ya ndege au yaliyotengenezea ndege kwa nje ambayo sio metal (lightning conductor) kusipokua na hizi kasoro basi ndege haitadhurika maana imetengenezwa kwa metal na metal ni lightning conductor

Ukiona radi imetokea ardhini(hizi ndio zile ambazo huleta maafa) ujue ni muingiliano wa positive charge za wingu la chini na negative charge za ardhi, (Hapa napo nyumba yenye lightning conductor wengi huita earth wire au vitu kama gari havitadhurika maana vina lightning conductor, au gari lidhurike kidogo kwa sababu kama zile za kwenye ndege. Ule mwanga unaouona, unashuka kufuata sehemu yoyote iliyoenda juu kuzidi wenzake mf gorofa, mti mrefu au mnara au kama ni ardhini basi hayo maeneo kuna asili ya madini yenye charge nying tofaut na zile zinazoshuka hivyo kupelekea kuvutana (Ref to the raw of eletric charge, hope form one au form two mwanzo ),
Hii process yote inaitwa LIGHTNING,

Kinachototea baada ya kuunguzana kwa hizo (+)ve & (-)ve ni kutanuka na kusinyaa haraka sana kwa chembe chembe za hewa (air molecules) hivyo kusuguana na kupasuka na matokeo yake ni ile sauti kubwa unayoisikia(Radi) thunder.

UNAWEZA UKAONGEZEA NYAMA.
 
in short , electric spark due to the discharge of stmodpheric electricity . How ! The molecules become charged by cosmic rays which ionize the gas molecules. When the clouds are propelled by the wind , the electron moves from one group to another in a zigzag path known as radar . The path will be seen as a flash of light called lighting . The air around the radar undergo rapid expansion and contraction leading to sound known as thernderstom
 
Asante Sana kwa elimu hii mkuu swali langu kwanini mikoa ya Kanda za ziwa inaonakena kushambuliwa Sana na radio.na mikoa ya kigoma na rukwa kwa hapa Tanzania
swali zuri sana ndugu, hakuna cha uchawi hapo n fact tu,
Ukiangalia mikoa yote hio ina maziwa makubwa kuliko mingne yote, Rukwa ziwa rukwa, kigoma ziwa tanganyika, Kanda ya ziwa, ziwa victoria, Njombe ziwa nyasa/malawi.
Mwanzo kbsa nimeandka chanzo cha radi n maji mengi yaliyovukizwa(hakuna kingne) ambayo yatatengeneza mawingu makubwa juu ya eneo lenye yale maji, Radi nyingne kubwa hutokea baharini

Umepata picha sasa?
 
swali zuri sana ndugu, hakuna cha uchawi hapo n fact tu,
Ukiangalia mikoa yote hio ina maziwa makubwa kuliko mingne yote, Rukwa ziwa rukwa, kigoma ziwa tanganyika, Kanda ya ziwa, ziwa victoria, Mwanzo kbsa nimeandka chanzo cha radi n maji mengi yaliyovukizwa(hakuna kingne) ambayo yatatengeneza mawingu makubwa juu ya eneo lenye yale maji, Radi nyingne kubwa hutokea baharini

Umepata picha sasa?
Vipi kuhusu pwani??dar,,lindi na mtwara
 
kuna kitabu kama sio cha physics basi ni chemistry na sikumbuki kama ilikuwa advance au o-level ila kuna stori fupi ya mwanasayansi ambaye alikuwa anapigwa sana na radi karibu mara 8 mpaka akaamua kuwa anatembea na madumu ya maji kwenye gari ili isimdhuru lakini bado haikusaidia.
Hili unalizungumziaje mtaalamu wa radi?
 
Vipi kuhusu pwani??dar,,lindi na mtwara
Mikoa yote hii imepakana na bahari ila si kwamba ina mrundikano mkubwa wa maji, kwa watu wa maeneo haya n rahsi sana kuona ule mwanga wa radi maeneo ya baharin hasa mda wingu likiwa limepoa, unapoona radi imetokea sehem ambayo chini n pakav, basi jua ya kua wingu lililotengeneza radi limesafrisiwa kwa upepo kutoka kutoka either baharin, ziwan au bwawan, kwa maana hio, mikoa hii radi n nadra kutokea au ikitokea kwa wing bas n kwa ajili ya upepo mkubwa unaotoka baharini unaokuja na wingu
 
Muelimishaji uko vizuri sana.ifaahamike radi haina uhusiano na uchawia radi haikuwahi kutumwa na mtu kama wengi wanavyo dhani hakuna.hakuna binadamu ambae anaweza kutuma radi najua kuna wajinga wapo humu humu ndani wanaamini radi kutumwa na mtu ili likudhuru haipo haipo narududia tena haipo na haikuwahi kutokea.ok ni kweli kuna maeneo radi hupiga sana mfano sumbawanga na huko kanda ya ziwa kwa uzoefu mdogo nilio nao maeneo mengi ambapo bonde la ufa lilipita radi hupenda sana kupiga hapo.na maeneo mengine ambapo radi hupiga ni sehemu hii mfano tuchukilie kunasehemu kuna tambarale kubwa yaani haina miti ktk tambarale hiyo labda kuna kichaka au mti hata mmja tu rad hapo litapiga tu.lakini amini radi halina uhusiano na uchawi kabisa.
 
in short , electric spark due to the discharge of stmodpheric electricity . How ! The molecules become charged by cosmic rays which ionize the gas molecules. When the clouds are propelled by the wind , the electron moves from one group to another in a zigzag path known as radar . The path will be seen as a flash of light called lighting . The air around the radar undergo rapid expansion and contraction leading to sound known as thernderstom
Andika kiswahili
 
swali zuri sana ndugu, hakuna cha uchawi hapo n fact tu,
Ukiangalia mikoa yote hio ina maziwa makubwa kuliko mingne yote, Rukwa ziwa rukwa, kigoma ziwa tanganyika, Kanda ya ziwa, ziwa victoria, Mwanzo kbsa nimeandka chanzo cha radi n maji mengi yaliyovukizwa(hakuna kingne) ambayo yatatengeneza mawingu makubwa juu ya eneo lenye yale maji, Radi nyingne kubwa hutokea baharini

Umepata picha sasa?
Nimekupenda ndugu natamani hii niikopi kwa ajili ya elimu kwa wengine kama hutajali naomba nikupe no.yangu unitumie paragraf hizi nisambaza kama elimu kwa wengine unitumie whatsapu nashindwa kukopi hii
 
Kipindi niko Mtwara ilitokea radi ikapiga mti mmoja mkubwa ukakatika baadae mvua ilivyokata watu tukawa tunapita pale kuangalia vizuri kukawa kama na kucha za mnyama kama chui zimekwaruza kwaruza pale watu wakawa wanasema radi ni mnyama ndo alipita hapo,mi muda wote nilikuwz nikijua radi kisayansi kama alivyosema mtoa mada lakini tukio lile lilinistajabisha sana mpaka leo sijui ilikuwaje pale aisee
 
Usiombe radi ikupige we angalia ilivyo uwa watoto 6 na kujeruhi Kwa sekunde tu

Mungu awalaze pema peponi marehemu na awape kupona Kwa haraka majeruhi
 
kuna kitabu kama sio cha physics basi ni chemistry na sikumbuki kama ilikuwa advance au o-level ila kuna stori fupi ya mwanasayansi ambaye alikuwa anapigwa sana na radi karibu mara 8 mpaka akaamua kuwa anatembea na madumu ya maji kwenye gari ili isimdhuru lakini bado haikusaidia.
Hili unalizungumziaje mtaalamu wa radi?
kwanza kumbuka gari n lightning conductor, unashauriwa unapoona dalili za radi basi kama kuna gari karbu lilimbilie na ukaingie ndan( USISIJE UKASIMAMA NJE) itaanza na wewe,
Halaf kumbuka maji n Bipolar/neutral molecule, inakua na unequal sharing of electrons, hii inamaanisha negative(anions) charge inajishkiza kwenye oxygen na positive(cations) itajishkiza kwenye hydrogen means (-ve) na (+ve) na kwa maana hii maji pure yanatakiwa yawe neutral(HAYA HAYAPITISH RADI), huyu jamaa sijui kama radi alikua anaipata ndan ya gari au laa, kama n ndan ya gar basi kwa vyovyote vile either maji aliyokua anatembea nayo hayakua pure(neutral) hvyo kutengeneza free ions ambazo zitalazmila kuvuta free ions nyingne za kwenye radi ili zibalance na hapo ndo shot(radi) hutokea au material meng yaliyokua yametengenezea gari yake au yaliyokua ndan ya gar yalikua hayana sifa ya lightning conductor(metal) au rangi aliyokua amepaka kwenye gar ilikua inazuia ile conductivity,
Kwaio unatakiwa uelewa ya kua maji hayakuzuii kupatwa na radi kamwe, ila tu yanaweza yakaongeza uwezekano wa wewe kupigwa na radi kama sio neutral, na yakiwa neutral radi ikishuka inaanza na wewe na si maji, Kwa maana hio huyu jamaa hapa ndo alikua anaharbu zaid,
 
Leo ngoja niweke u comedy pemben tuelimishane kdg,

Uzi uliopita nilizungumzia n kwa nini watu weng hupata stroke/kiharusi au hatimae kufa kbsa wawapo bafuni au chooni na mbna ya freebasics kwa undani.

Kukiwa na Joto maji yanavukizwa na hatimaye kua mvuke ambao taratibu hupanda kuelekea mawinguni, huu mvuke ukishafka juu ukakutana na hali ya hewa/mawingu yaliyopoa/yenye ubarid basi nao hupoa na kua mzito au kua katka hali ya unyevu unyevu (condensation) ambayo ndio mawingu sasa,

Kwa hio basi kule juu kutakua na mawingu ya aina mbili : yaliyopo juu tayar (ambayo hua mazito zaid) na yanayopanda (ambayo yana uvugu vugu ambayo hupoa na kua mazito kadri yanavyopanda kufkia haya yaliyopoa zaid)

UKARIBIANO kati ya haya mawingu yaliyopo kule juu(wingu zito ambalo lina hali ya matone tone ya maji) na mawingu yanayopanda (wingu jepesi ambalo bd lipo kwenye hali ya mvuke mvuke) hii itafanya sehemu ya JUU ya wingu linalopanda kua positive au negatively charged, na sehemu ya CHINI ya wingu la juu(wingu zito lenye matone matone ya maji) kua negatively au positively charged(RESPECTIVELY) kutokana na kasi ya mvutano, yan lazima mawingu mawili yanayoshabihiana yatofautiane charge kwanza, hii hutokea through induction(charging something without direct contact, hahaaa hapa kama hujasoma static electricity lazma ukunje ndita)

Kukitokea upepo unaopita kati ya haya mawingu mawili, negative charge (lets say zipo upande wa juu wa wingu la chini/linalopanda) zitavibrate na hatimaye kufuata zile positive zilizopo upande wa chin wa wingu la juu, haraka zile negative charge zitakapogusana na positive itatokea shoti kali huku zote zikisuguana na kuvutana, za chini zikilazmishwa kuja juu na zikisha kutana zitaleta shot(zitaunguzana), mvutano huu kwa kua una ukinzan mkubwa basi hutokea kwa njia ya zigzag, ambao huitwa radar kwenye phyz(Ndio ule mwanga mkali unaouonaga unaokaa katika mstar ulio pinda pinda), ukiona umetokea juu haukufka chin basi ujue n shot kati ya mawingu na mawingu(Japo mda mwingne ukinzan ukiwa mkubwa hufka mpk ardhin), na kwa maana hio kitu chochote kilichopo/kinachopita kati ya wale mawingu mawili basi kitaunguzwa(ule mwanga unakua na jotoridi la nyuz zaid ya 30,000'C), hapa ndege haitadhurika au idhurike kdg sana tena n maeneo ya pale zile charge zitakapo ingilia au kutokea tu, au kwa sbb ya material mengne yaliyopo ndan ya ndege au yaliyotengenezea ndege kwa nje ambayo sio metal(lightning conductor) kusipokua na hz kasoro bas ndege haitadhurika mana imetengenezwa kwa metal na metal n lightning conductor

Ukiona radi imetokea ardhin(hizi ndio zile ambazo huleta maafa) ujue n muingiliano wa positive charge za wingu la chin na negative charge za ardhi, (Hapa napo nyumba yenye lightning conductor weng huita earth wire au vitu kama gari havitadhurika mana vina lightning conductor, au gari lidhurike kdg kwa sbb kama zile za kwenye ndege. Ule mwanga unaouona, unashuka kufuata sehem yoyote iliyoenda juu kuzd wenzake mf gorofa, mti mrefu au mnara au kama n ardhn basi hayo maeneo kuna asili ya madini yenye
charge nying tofaut na zile zinazoshuka hvyo kupelekea kuvutana (Ref to the raw of eletric charge, hope 4m1 au 4m2 mwanzo ),
Hii process yote inaitwa LIGHTNING,

Kinachototea baada ya hapo n kutanuka na kusinyaa haraka sana kwa chembe chembe za hewa(air molecules) hvyo kusuguana na kupasuka na matokeo yake n ile saut kubwa unayoisikia(Radi) thunder.

UNAWEZA UKAONGEZEA NYAMA.
kuna mpuuzi mmoja akawa anajikuta mjuaji
akisema radi ni Mnyama

Nadhani alikuwa anafananisha radi ya sumbawanga na radi Ya juu
 
Back
Top Bottom