Elimu Bure: Walimu Mwanza kulipwa tsh. 2,000 kusahihisha mitihani ya Mock

BINARY NO

JF-Expert Member
Dec 29, 2011
2,053
2,000
Jana kilitokea kituko maaneo ya Shule ya sekondari ya wavulana Bwiru ampabo zoezi la usahihishaji wa Mitihani ya Mock kidato cha pili na Nne ulikuwa ufanyike kwa Wilaya ya Ilemela.

Walimu waliteuliwa na wakuu wao kama ada na ikumbukwe hii huwa ni kazi maalumu na miaka yote imekuwa ikifanyika, tatizo mwaka huu mitihani hii imesuasua Tanzania nzima kwani Fedha za uendashaji hakuna kwani wanafunzi walikuwa wakichangia 15000/= na 50000/=NECTA.

Sasa kituko cha jana baada ya walimu kufika Bwiru walikaribishwa na mwenyeji wao mkuu wa kituo hicho na akaanza kwa kusema ndg walimu kuna tofauti kidogo mwaka huu si mnajua ELIMU BURE hivyo kama shule hatukupewa hata SENTI hivyo HAKUNA MALIPO YOYOTE mtakayolipwa zaidi MKURUGENZI amejitahidi angalau awalipe 2000/= za NAULI tu na huku miaka ya nyuma shughuli maalumu za MOCK wasahihishaji walikuwa wakilipwa mpaka 400,000/= Kutegemeana na idadi ya scripts au wanafunzi wote wa MKOA.

Basi walimu kusikia kuwa hakuna malipo na watapewa 2000 tu za nauli ambazo hazitoshi maana wapo walimu waliotokea SHIBULA au IBINZA nauli tu wanatumia mpaka 4700/= achilia ugumu wa kazi yenyewe, walimu waligoma akaja Afisa Elimu wa Wilaya Ndg J KASANDIKO nae alitoa maelezo marefu kuwa DC na MKURUGENZI walikuwa waje ili kuzindua lakini wamekataa hivyo naomba tujitolee Tu. Kwakweli alizomewa ikabidi aondoke huku akitoa lugha ya vitisho.

Zoezi lilikuwa lianze saa 2 asubuhi lakini halikuanza hadi wakuu wa shule kwa busara zao za kuwasihi walimu wao ndio zoezi likaanza saa 7 mchana huku walimu wakiwa na vinyongo vya uzalilishaji huu wa KARNE.

Imagine mtu umeaga kwa Mkeo au Mmeo ukitegemea kulipwa angalau laki 3 lakini unaishia kulipwa Elfu 2 tu za nauli. Walimu wenye Master,degree na diploma zao wanadhalilishwa kiasi hiki maana hata kibarua huwezi mlipa elfu 2 tu.

Kweli KIKWETE watu walimkosea sana ila sasa atakumbukwa sana. Imagine hao walimu watamark kweli hiyo mitihani au watafanya yao tu?

Je, kiwango cha elimu kwa awamu hii ya tano itakuwaje kama mitihani ya Mock ndio imeshushwa thamani kiasi hiki achilia mbali NECTA Form Two Kufanywa km BIG RESULT NOW ambapo hakuna mchujo?
 

BINARY NO

JF-Expert Member
Dec 29, 2011
2,053
2,000
Taarifa nilizonazo kuna walimu wengi tu waligoma na kuondoka Uku wengi wao wakitarajia kutorudi tena baada ya hiyo jana maana zoezi linaendelea taktibani wiki moja.ambapo kazi inaanza saa moja hadi saa 11 jioni..
 

Yohana Kilimba

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
8,115
2,000
Taarifa nilizonazo kuna walimu wengi tu waligoma na kuondoka Uku wengi wao wakitarajia kutorudi tena baada ya hiyo jana maana zoezi linaendelea taktibani wiki moja.ambapo kazi inaanza saa moja hadi saa 11 jioni..
Wajiandae Kutishwa na Kulazwa Ndani!
 

Raynavero

JF-Expert Member
Apr 29, 2014
37,957
2,000
Huku kwetu walisema hawana pesa
Mock wamefanya may Mitihani wamesahihisa this September
Ila washasahihisha sijui wamepewa shilingi ngapi?
 

NJALI

JF-Expert Member
Jan 9, 2014
1,536
2,000
TARIME hawakulipwa HATA buku, Waandaaji WA Practicals, Wasimamizi, Wasahihishaji, Wapangaji wa Matokeo WOTE wamedhulumiwa . Kweli KIKWETE tutakukumbuka daima, pumzika kwa amani MZEE wetu.
 

Mchumi90

JF-Expert Member
Mar 16, 2015
1,021
2,000
Taarifa nilizonazo kuna walimu wengi tu waligoma na kuondoka Uku wengi wao wakitarajia kutorudi tena baada ya hiyo jana maana zoezi linaendelea taktibani wiki moja.ambapo kazi inaanza saa moja hadi saa 11 jioni..
Chakula je? Au ndio wanapikiwa makande
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom