Elimu bure Vyuo Vikuu inawezekana tukibuni sera ya Higher Education Cost Sharing

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
40,900
2,000
Nimekaa na kutafakari sana tatizo la wanafunzi wa vyuo vikuu kukosa mikopo na athari zake kwa wanafunzi wenyewe,famili zao,jamii na Taifa kwa ujumla na ninaona hili tatizo lina madhara makubwa kuliko tunavyofiki au tunavyodhania kama Taifa.

Binafsi hili tatizo huwa linaniumiza sana kuona mtu anakosa elimu kwasababu tu ya umasikini wa mzazi wake au mlezi wake na hivyo kujikuta akaharibu future yake kwa namna moja au nyingine.

Nimekaa na kujiuliza hivi tukibuni sera ya kuchangia elimu ya juu kupitia vipato vyetu kama watu binafsi,taasisi binafsi,n.k hatuwezi kupata fedha za kuchangia budget ya bodi ya mikopo?

Tukianza na wafanyakazi.Kila mfanyakazi wa umma na sekta binafsi awe anakatwa kwa mfano 0.5% ya mshahara wake ghafi(basic salary yake) na makato hayo yakaelekezwa moja kwa moja Bodi ya Mikopo.

Tuchukue mfano wa watumishi wa umma tu ambao idadi yao ni kama 500,000 na wastani kila mfanyakazi basic salary yake ni iwe ni shilingi 500,000 kwa mwezi.

Angalia hii hesabau kuona watakavyochangia.

Mtumishi mmoja kwa mwezi:
0.5% x 500,000=2500

Watumishi 500,000 kwa mwezi itakuwa:

2500x500,000=1,250,000,000

Mchango wa watumishi 500,000 kwa mwaka(miezi 12) utakuwa:

1,250,000,000 x 12 = 15,000,000,000

Najua kuna wanaopata chini ya 500,000 kwa mwezi ila nimechukua wastani na hapo sijagusa kabisa wafanyakazi wa sekta binafsi ambao wanaweza kufidia mahesabu yao hapo juu.

Mauzo ya viwanja:
Kila kiwanja kitakochouzwa na serikali kupitia Halmashauri za Wilaya,hela itakayopatikana ikatwe asilimia 5 na fedha hiyo ielekezwe Bodi ya Mikopo.

Kwa mfano kiwanja kimoja cha shilingi 3000,000 kitachangia:

5/100 X 3000,000 = 150,000.

Viwanja 100,000 kama hivyo nchi nzima kwa mwaka mmoja vitachangia:

150,000 x 100,000 = 15,000,000,0000

Mashirika/Taasisi
Mtumishi yoyote anakabiliwa na makato ya lazima kisheria kuchangia Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, Bima ya Afya na vyama vya wafanyakazi ingawa kisheria si lazima kujiunga na vyama vya wafanyakazi.

Kwakuwa mifuko hii inatoza asilimia kadhaa ya mahahara wa mtumishi ili kuchangia mifuko hii,napendekeza kila mfuko upunguziwe tozo ya asilimia 0.5 na mchango utakaopatikana uelekezwa Bodi ya Mikopo.

Kwa mfano,

PSPF wanatoza asilimia 5

TUGHE asilimia 2

Bima ya Aya asilimia 3

Sasa badala ya makato hayo,kila mfuko upunguziwe asilimia 0.5 na iwe kama ifuatavyo:

PSPF itoze asilimia 4.5 na 0.5 ielekezwa Bodi ya Mikopo

TUGHE itoze aailimia 1.5 na 0.5 ielekezwe Bodi ya Mikopo(kama itakuwa kubwa basi hata 0.3)

Bima ya Afya itoze asilimia 2.5 na 0.5 ielekezwe Bodi ya Mikopo.

CWT,PPF na mifuko mingine ifanyike hivyo hivyo.

Hii mifuko mingi imewekeza hela nyingi katika ujenzi wa majengo,n.k na hivyo itakuwa haitegemei sana makato ya wafanyakazi tu hivyo inaweza kuchangia pato lake katika kutunisha Bajeti ya Bodi ya Mikopo na kuwezesha watanzania wengi zaidu kupata elimu ya juu.

Tuchukie mfano wa mtumishi mmoja tu wa umma anaekatwa PSPF,TUGHE na Bima ya Afya na mwenywe mshahara wa sh.500,000 kwa mwezi.

0.5/100 x500,000 = 2500

Kwa mifuko 3 atachangia shilingi 7,500.

Kwa watumishi 500,000 wa umma nchi nzima waliiko katika mifuko tofauti tofauti na wakiwa na wastani wa mshahara wa shilingi 500,000 kila mmoja wao kwa mwezi atachangia:

7500 x500,000 = 3,750,000,000

Kwa mwaka watachangia jumla ya shilingi.

3,750,000,000 x 13 = 45,000,000,000

Sitting allowance za wabunge:

Hii posho inaweza kufutwa kabisa na badala yake hela hizi zikaelekezwa Bodi ya Mikopo.

Kama sikose,posho hii kwa siku kwa mbunge mmoja ni shilingi 220,000 na tuna wabunge wapatao 397 kama sikosei.

Kwahiyo kwa wabunge 397 kwa siku moja tutaokoa jumla ya shilingi:

220,000 x 397 = 87,340,000

Kwa Bunge la Bajeti la karibu siku 90:
87,340,000 x 90 = 7,860,600,000

Bunge la wiki 2 la mwezi Jan/Febr.

87,340,000 x 14 = 122,760,000

Bunge la wiki 2 la mwezi Sept/Nov.
87,340,000 x 14 = 122,760,000

Kama kuifuta hiyo posho itakuwa ni taabu,basi wakatwe asilimia 10 ya hiyo posho kwa kila kikao cha siku moja na hiyo hela ielekezwe Bodi ya Mikopo.

Hesabu ya makato hayo kwa siku kwa mbunge mmoja:
10/100 X 220,000 = 22,000

Kwa Bunge la Bajeti la siku 90 kwa mbunge mmoja:

22,000 x 90 = 1,980,000

Kwa wabunge 397 kwa siku 90:

1,980,000 x 397 = 786,060,000

Kwa Bunge la wiki 2 kwa mbunge mmoja:

22,000 x 14 = 308,000

Kwa wabunge 397 kwa wiki 2 za Bunge la Jan/Feb:

308,000 x 14 = 4,312,000

Kwa Bunge lingine la wiki 2 la Sept/Nov.

308,000 x 14 = 4,312,000

Na hapo sijahusisha posho ya per-diem ambayo nayo kama tutamua kila mtumishi akatwe hiyo asilimia basi kwa wabunge tutakuwa tunapiga mahesabu ya asilimia 10 ya posho ya zaidi ya shilingi 300,000 kwa siku.

Mpaka hapa hii hela yote kwa ujumla itatasaidia watoto wangapi ambao wangeshindwa kusoma kwa kukosa mkopo?

Na mchango wa asilimia 0.5 kama pia utakatwa katika faida ya makampuni makubwa, wafanyabiasha na mabenki kama mchango maalumu ya kuchangia elimi ya juu sambamba na Bajeti ya serikali, tutashindwa kweli kusomesha wanafunzi wa vyuo vikuu bure kwa maana ya mzazi/mlezi kutolazimika kulipa ada yoyote?

Je,tukibuni sera kama hii na tukaitungui sheria maalumu, hatutaweza kutunisha Bajeti ya Bodi na kuwezesha wanafunzi wengi zaidi kusoma?

Kama tunachangia harusi na shughuli nyingine za kijamii,kwanini tusiwe na sheria ya kuchangia elimu ya juu kupitia vipato vyetu?

Mtu ukichangia shilingi 2500 kila mwezi kutoka kwenye mshahara wako na ukaondokana na jukumu zito la kulipa ada ya mamilioni kwa mwanao au makato ya Bodi ya asilimia 15 ya mshara wako, utakuwa hujapata nafuu ya maisha?
 
Kimweri

JF-Expert Member
Apr 16, 2008
4,001
2,000
Nimetaja mifano michache lakini huu uliotaja nakiri kuwa nao kichwani ila nilipitiwa.

Nimeongeza na mauzo ya viwanja ambayo nayo niliyasahau.
Umezunguka sana kuelezea very simple theory.
Elimu ni HUDUMA haitakiwi kukopeshwa kwa taifa la kesho(vijana na watoto).
Nchi zinazotaka kuua taifa TU ndio zinakopesha watoto na vijana wake kitu basic kama ELIMU.

Mikopo ya elimu ni kosa kubwa sana kwa taifa. Hakuna taifa lenye sense of morality linakopesha majukumu yake ya msingi.
 
ramafosa

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
287
250
Nimekaa na kutafakari sana tatizo la wanafunzi wa vyuo vikuu kukosa mikopo na athari zake kwa wanafunzi wenyewe,famili zao,jamii na Taifa kwa ujumla na ninaona hili tatizo lina madhara makubwa kuliko tunavyofiki au tunavyodhania kama Taifa.

Binafsi hili tatizo huwa linaniumiza sana kuona mtu anakosa elimu kwasababu tu ya umasikini wa mzazi wake au mlezi wake na hivyo kujikuta akaharibu future yake kwa namna moja au nyingine.

Nimekaa na kujiuliza hivi tukibuni sera ya kuchangia elimu ya juu kupitia vipato vyetu kama watu binafsi,taasisi binafsi,n.k hatuwezi kupata fedha za kuchangia budget ya bodi ya mikopo?

Tukianza na wafanyakazi.Kila mfanyakazi wa umma na sekta binafsi awe anakatwa kwa mfano 0.5% ya mshahara wake ghafi(basic salary yake) na makato hayo yakaelekezwa moja kwa moja Bodi ya Mikopo.

Tuchukulie mfano wa watumishi wa umma tu ambao idadi yao ni kama 500,000 na wastani kila mfanyakazi basic salary yake ni iwe ni shilingi 500,000 kwa mwezi.

Angalia hii hesabau kuona watakavyochangia.

Mtumishi mmoja kwa mwezi:
0.5% x 500,000=2500

Watumishi 500,000 kwa mwezi itakuwa:

2500x500,000=1,250,000,000

Mchango wa watumishi 500,000 kwa mwaka(miezi 12) utakuwa:

1,250,000,000 x 12 = 15,000,000,000

Najua kuna wanaopata chini ya 500,000 kwa mwezi ila nimechukua wastani na hapo sijagusa kabisa wafanyakazi wa sekta binafsi ambao wanaweza kufidia mahesabu yao hapo juu.

Mauzo ya viwanja:
Kila kiwanja kitakochouzwa na serikali kupitia Halmashauri za Wilaya,hela itakayopatikana ikatwe asilimia 5 na fedha hiyo ielekezwe Bodi ya Mikopo.

Kwa mfano kiwanja kimoja cha shilingi 3000,000 kitachangia:

5/100 X 3000,000 = 150,000.

Viwanja 100,000 kama hivyo nchi nzima kwa mwaka mmoja vitachangia:

150,000 x 100,000 = 15,000,000,0000

Mashirika/Taasisi
Mtumishi yoyote anakabiliwa na makato ya lazima kisheria kuchangia Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, Bima ya Afya na vyama vya wafanyakazi ingawa kisheria si lazima kujiunga na vyama vya wafanyakazi.

Kwakuwa mifuko hii inatoza asilimia kadhaa ya mahahara wa mtumishi ili kuchangia mifuko hii,napendekeza kila mfuko upunguziwe tozo ya asilimia 0.5 na mchango utakaopatikana uelekezwa Bodi ya Mikopo.

Kwa mfano,

PSPF wanatoza asilimia 5

TUGHE asilimia 2

Bima ya Aya asilimia 3

Sasa badala ya makato hayo,kila mfuko upunguziwe asilimia 0.5 na iwe kama ifuatavyo:

PSPF itoze asilimia 4.5 na 0.5 ielekezwa Bodi ya Mikopo

TUGHE itoze aailimia 1.5 na 0.5 ielekezwe Bodi ya Mikopo(kama itakuwa kubwa basi hata 0.3)

Bima ya Afya itoze asilimia 2.5 na 0.5 ielekezwe Bodi ya Mikopo.

CWT,PPF na mifuko mingine ifanyike hivyo hivyo.

Hii mifuko mingi imewekeza hela nyingi katika ujenzi wa majengo,n.k na hivyo itakuwa haitegemei sana makato ya wafanyakazi tu hivyo inaweza kuchangia pato lake katika kutunisha Bajeti ya Bodi ya Mikopo na kuwezesha watanzania wengi zaidu kupata elimu ya juu.

Tuchukie mfano wa mtumishi mmoja tu wa umma anaekatwa PSPF,TUGHE na Bima ya Afya na mwenywe mshahara wa sh.500,000 kwa mwezi.

0.5/100 x500,000 = 2500

Kwa mifuko 3 atachangia shilingi 7,500.

Kwa watumishi 500,000 wa umma nchi nzima waliiko katika mifuko tofauti tofauti na wakiwa na wastani wa mshahara wa shilingi 500,000 kila mmoja wao kwa mwezi atachangia:

7500 x500,000 = 3,750,000,000

Kwa mwaka watachangia jumla ya shilingi.

3,750,000,000 x 13 = 45,000,000,000

Sitting allowance za wabunge:

Hii posho inaweza kufutwa kabisa na badala yake hela hizi zikaelekezwa Bodi ya Mikopo.

Kama sikose,posho hii kwa siku kwa mbunge mmoja ni shilingi 220,000 na tuna wabunge wapatao 397 kama sikosei.

Kwahiyo kwa wabunge 397 kwa siku moja tutaokoa jumla ya shilingi:

220,000 x 397 = 87,340,000

Kwa Bunge la Bajeti la karibu siku 90:
87,340,000 x 90 = 7,860,600,000

Bunge la wiki 2 la mwezi Jan/Febr.

87,340,000 x 14 = 122,760,000

Bunge la wiki 2 la mwezi Sept/Nov.
87,340,000 x 14 = 122,760,000

Kama kuifuta hiyo posho itakuwa ni taabu,basi wakatwe asilimia 10 ya hiyo posho kwa kila kikao cha siku moja na hiyo hela ielekezwe Bodi ya Mikopo.

Hesabu ya makato hayo kwa siku kwa mbunge mmoja:
10/100 X 220,000 = 22,000

Kwa Bunge la Bajeti la siku 90 kwa mbunge mmoja:

22,000 x 90 = 1,980,000

Kwa wabunge 397 kwa siku 90:

1,980,000 x 397 = 786,060,000

Kwa Bunge la wiki 2 kwa mbunge mmoja:

22,000 x 14 = 308,000

Kwa wabunge 397 kwa wiki 2 za Bunge la Jan/Feb:

308,000 x 14 = 4,312,000

Kwa Bunge lingine la wiki 2 la Sept/Nov.

308,000 x 14 = 4,312,000

Mpaka hapa hii hela yote kwa ujumla itatasaidia watoto wangapi ambao wangeshindwa kusoma kwa kukosa mkopo?

Na mchango wa asilimia 0.5 kama pia utakatwa katika faida ya makampuni makubwa, wafanyabiasha na mabenki kama mchango maalumu ya kuchangia elimi ya juu sambamba na Bajeti ya serikali, tutashindwa kweli kusomesha wanafunzi wa vyuo vikuu bure kwa maana ya mzazi/mlezi kutolazimika kulipa ada yoyote?

Je,tukibuni sera kama hii na tukaitungui sheria maalumu, hatutaweza kutunisha Bajeti ya Bodi na kuwezesha wanafunzi wengi zaidi kusoma?

Kama tunachangia harusi na shughuli nyingine za kijamii,kwanini tusiwe na sheria ya kuchangia elimu ya juu kupitia vipato vyetu?

Mtu ukichangia shilingi 2500 kila mwezi kutoka kwenye mshahara wako na ukaondokana na jukumu zito la kulipa ada ya mamilioni kwa mwanao, utakuwa hujapata nafuu ya maisha?
"Tuchukie mfano wa mtumishi mmoja" Na kweli tuchukie
 
Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
40,900
2,000
Umezunguka sana kuelezea very simple theory.
Elimu ni HUDUMA haitakiwi kukopeshwa kwa taifa la kesho(vijana na watoto).
Nchi zinazotaka kuua taifa TU ndio zinakopesha watoto na vijana wake kitu basic kama ELIMU.

Mikopo ya elimu ni kosa kubwa sana kwa taifa. Hakuna taifa lenye sense of morality linakopesha majukumu yake ya msingi.
Ndio hao walioko madarakani sasa tufanyaje?
 
Dumelang

JF-Expert Member
Aug 11, 2011
3,027
2,000
Serikali ya CCM ambayo tulikopesha mil 3 wanakata mil 10 sidhani kama wanaweza kuona haya na muhimu, tena kwa Rais kama Magifuli ambaye akili zake zinamtuma kila kitu kutumia nguvu bila akili, sidhani

Tutahtaji akili kubwa kuliko makada wa CCM kufuta hili
 
Wao wako busy kurubuni watoto wa masikini kwa kuwatumia UVCCM na kina Polepole eti CCM inatoa mikopo/itawasaidia kuomba mikopo Loans Body.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom