Elimu bure na michango ya lazima wilayani Misungwi

viva666

Senior Member
Oct 11, 2016
111
116
Habari wapendwa,

Ndugu zangu hapo siku chache nyuma nilikuja na uzi wa maji machafu yanayotoka kwenye mabomba ya maji wilayani Misungwi.

Hakika JF ni suluhisho la kero zetu tusio hata namba ya mtendaji kijiji.hali hio limerekebishwa na sasa maji yanatoka masafi japo kiasi si salama.

Leo tena katika pitapita zangu nimekumbana na jambo limeniacha hoi kidogo. Basi sote tunajua kuwa elimu ni bure kama Mheshimiwa alivyosema na kusisitiza.

Kuna kipindi hata wakurugenzi hawakutaka kusikia hata mchango wa uji shuleni japo ni kwa manufaa ya watoto wetu.

Leo hii namshuhudia afisa mtendaji na watu kadhaa wameambatana wakipita kuchukua mchango wa sekondari. Basi mtendaji kaenda mbali kufikia hatua ya kukwaruzana na watu kisa huo mchango.

Wana utaratibu wao ukiwa huna huo mchango kiasi cha elfu tatu (3000) watabeba either kiti, mfano kuna kijina ni machinga wamebeba kandambili, kama una duka watabeba chochote tu kile wakijiskia.

Hata hivo kinyume na sheria ilivotaka kutumuka kwa EFD machine ni tofauti wao wana stakabadhi za kuandika kwa mkono tu kitu ambacho hakikinai kuwa mapato yanaenda mfuko salama wa serikali.

NOTE: Shule inayotafutiwa mchango ni ya wilaya na ni ya zamani bado hata shule za kata hazijaanzishwa.

Swali: Je ni nani yupo nyuma ya michango hii dharimu?

Nchi ya asali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom