Elimu bure isiwe sababu ya kushindwa kutatua kero za uhaba wa madarasa

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Oct 2, 2020
1,552
2,000
Tatizo la uhaba wa madarasa limekuwepo kwa muda mrefu na lilianza kushamiri hasa miaka ya tisini.

Ukweli ni kuwa sababu kubwa ni ongezeko la idadi ya watoto wanaotakiwa kujiunga na elimu ya msingi na sekondari kwa ujumla.

Kuleta visingizio kuwa eti awamu ya tano kuanza kutoa elimu bure ndio sababu ya ya idadi ya wanafunzi imeongezeka na hivyo kusababisha ongezeko la idadi ya wanafunzi wanaotakiwa kujiunga na elimu ya sekondari na msingi ni hoja hafifu na duni kabisa.

Mwaka 2019-2020 serikali ilibainisha wazi kuwa wanafunzi wapatao 58,666 walishindwa kuendelea na masomo baada ya kukosa madarasa. Na kwa aibu kubwa ilitenga bil 29 tu ili kukabili hili tatizo. Lakini hakuna kilichotatuliwa.

Ifahamike tangu miaka ya tisini mpaka leo ni shule chache sana ambazo zina uwezo wa kusomesha wanafuzi 45 ndani ya darasa moja. Na tatizo hili lipo kwa zaidi ya miaka 40 hapa Tanzania.

Kama serikali ina nia thabiti ya kusomesha watoto wetu kwa standard zinazotakiwa kwa nini isitatue hili tatizo wakati inazo pesa?

Kwa nini isiunde kikosi kazi maalumu na kujenga madarasa yanayotosha ndani ya miezi miwili,maana darasa halihitaji gharama kubwa na ufundi mkubwa? Maana tunaambiwa kila siku pesa zipo,sasa kwa nini msitenge pesa za kutosha kumaliza kero ndogo kama hii?
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
4,377
2,000
Tatizo ni kudandia hoja kwenye ilani za upinzani bila kujua ni kwa namna gani jambo hilo litafanyiwa kazi ili lilete tija kwa wale waliokusudiwa, matokeo yake ndio hayo, wakifanya hapa wanaharibu pale.
 

onjwayo

JF-Expert Member
Apr 8, 2020
965
1,000
Wewe mwananchi mwenzangu subiri tuwabambikize vyesi vya hujumu uchumi tupate hela za kujenga madarasa kwa mpigo.

Huko TRA wanafanya vizuri tusubiri tena mwezi huu.
 

Abdul Mganyizi

JF-Expert Member
Oct 28, 2019
547
1,000
Mkuu elimu imeisha jifia tena hasa kipindi cha Magu,serikali inatumia nguvu nyingi kuonekana inafanya vyema kwenye elimu lakini ni uongo. Leo shule hazina waalim wakutosha hasa shule za msingi but serikali inasema hakikisha wanafunzi wanafaulu wote, kuanzia kwa afisa elimu, mratibu elimu kata, mkuu wa shule wanahakikisha 90% watoto wanafaulu na ndani ya hao wanye uwezo ni 50% sasa unajiuliza serikali inafanya hivyo kumkomoa nani? Tunakoelekea ni kubaya sana make itafika hatua tunavijana wengi waliomaliza kidato cha nne sawa na waliomliza darasa la saba.
 

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Oct 2, 2020
1,552
2,000
Mkuu elimu imeisha jifia tena hasa kipindi cha Magu,serikali inatumia nguvu nyingi kuonekana inafanya vyema kwenye elimu lakini ni uongo.Leo shule hazina waalim wakutosha hasa shule za msingi but serikali inasema hakikisha wanafunzi wanafaulu wote,kuanzia kwa afisa elimu ,mratibu elimu kata,mkuu wa shule wanahakikisha 90% watoto wanafaulu na ndani ya hao wanye uwezo ni 50% sasa unajiuliza serikali inafanya hivyo kumkomoa nani? Tunakoelekea ni kubaya sana make itafika hatua tunavijana wengi waliomaliza kidato cha nne sawa na waliomliza darasa la saba.
Good point.
 

Fumadilu Kalimanzila

JF-Expert Member
Dec 10, 2016
652
1,000
Elimu ya Tanzania inahitaji mjadala mpana sana! Na mimi naamini siku zote elimu haiwezi kutolewa bure kwa zama hizi tulizo nazo!

Ngoja watu waendelee kuchekelea hii elimu bure for the expense of very poor education!

Ni umaskini tu ndo unasababisha watu wanatulia ila kwa mzazi mwenye " akili" huwezi kutulia eti mwanao ameenda shule hizi zetu za serikali hasa za msingi!
Hakuna wanachojifunza watoto ni ujinga mtupu.

Watoto wamejazana madarasani, hakuna vifaa vya maana vya kujifunzia na walimu hawana morali ya kufundisha kabisa!

Kama mtu anabisha ajaribu kuangalia ni viongozi gani watoto wao wanasoma katika shule hizo!

Elimu hii bure tunayoichekelea bado kidogo sana itaanza kutoa wahitimu ambao tofauti yao na misukule ni ndogo sana!

Huwezi kupika chakula ambacho wewe hukiamini na huwezi kukila.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom