Elimu bure inawezekana km tuliweza kumlipa richmond 156milioni kwa siku. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Elimu bure inawezekana km tuliweza kumlipa richmond 156milioni kwa siku.

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by rugumye, Nov 5, 2010.

 1. rugumye

  rugumye JF-Expert Member

  #1
  Nov 5, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Watanzania ni wepesi wa kusahau, tukirudi nyuma miaka miwili tu iliyopita, Tanzania ilikuwa inayalipa makampuni ya kufua umeme ya Dowans (T) Ltd shilingi za kitanzania 152 milioni kwa siku. Sawa na shilingi bilioni 58 kwa mwaka. Pia serikali ilikuwa inalipa kampuni ya IPTL shilingi 3.6bilioni kwa mwezi, sawa na bilioni 43.2 kwa mwaka. Kwa malipo ya makampuni haya mawili tu serikali ilikuwa inalipa 98bilioni kwa mwaka. Haya ni baadhi tu ya mabilioni yaliyopotea ukiacha posho na mishahara minono ya mawaziri, wabunge na baadhi ya watumishi wa serikali, TRL, ATC, Melemeta, EPA, deep green, kagoda,rada, Ndege ya Rais,migodi ya madini, Misamaha ya kodi kama ule wa Alex stewart, ticts, safari za nje ya nchi, manunuzi ya magari ya kifahari na n.k.
  kwa nini kusoma bure haiwezekani? Ni kwa sababu Watanzania ni wasahaurifu, Kwa hesabu za haraka tukichukua takwimu za wanafunzi wa elimu ya juu elfu 60. Bajeti ya mwanafunzi mmoja iwe shilingi elfu 10 kwa siku, ni sawa na milioni 600 kwa siku kwa wanafunzi hao. Na muda wa masomo iwe siku 240 kwa mwaka, kwani siku 120 wanafunzi huwa nyumbani likizo. Hivyo gharama kwa wanafunzi wa elimu ya juu ni bilioni 144 kwa mwaka. Malipo yaliyofanywa kwa makampuni haya mawili yangeweza kusomesha Watanzania elfu 60 kwa asilimia 68 elimu ya juu.
  Haya ndiyo majibu ya kwa nini Tanzania ni Maskini swali aliloshindwa kujibu Kiongozi mmoja huko nje ya Nchi. Kusoma bure inawezekana kama rasilimali zikitumika ipasavyo.
   
Loading...