Tetesi: Elimu bure: Ilemela watembeza bakuli, DEO atumbuliwa

johnmashilatu

JF-Expert Member
Sep 16, 2010
819
867
Wakati utawala huu ukisisitiza kuwa elimu hadi ya kidato cha nne inatolewa bure, Hali Ni mbaya ktk wilaya ya ilemela Na kupelekea kusimamishwa kazi Kwa afisa elimu wa manispaa hiyo.

DC Na DED wa ilemela ambao wanaiendesha kibabe halmashauri wamewaagiza ma WEO na waratibu elimu kata kumaliza upungufu wa vitu, meza Na madawati Kwa kusaka fedha mitaani.

Watendaji hao ambao hutakiwa kila wiki kwenda ofisi ya halmashauri kutoa taarifa ya matokeo ya msanyo wao, wanatembea mitaani kuomba fedha Kwa kila wanayekutana naye, ikiwa ni pamoja Na vibanda vya mama ntilie, salon, bar Na maduka kusaka fedha.

Halmashauri haijatoa fedha lakini watendaji hao wanapaswa kukamilisha kazi hiyo mwisho ni mwa mwezi huu baada ya kushindwa target ya awali iliyowataka kukamilisha kabla ya shule kufunguliwa.

Wananchi wengi wanagoma kwani viongozi mkuu anasisitiza kuwa jukumu la mzazi Na sare Na madawati.

Hata hivyo vigogo hao wa halmashauri wangekuwa wakiwatisha watumishi hao kupata demotion ikiwa watashinddwa kukamilisha.

Afisa elimu wa manispaa amesimamishwa kazi baada ya DED kumkuta ofisini badala ya kwenda field kata ya sangabuye Kwa kile alichoeleza ni kukosa usafiri.
 
Hahaaa

DED ndio mdudu gani huyo?

Ajiandae kutumbuliwa mara ya pili,ya kwanza alifanya mazingaombwe akarudi
 
Uwajibikaji uwe Wa kiwango cha juu halafu wanakusanyaje fedha kiholela wakati watu wanalipa kodi ?
 
Elimu bure hiyo michango ya nini, au bure ya hewa tukifika kwa vitendo tunatakiwa kulipa, aliyetumbuliwa tena hapo mbona sioni kosa? Jamani wahurumieni watumishi ukienda huku mshahara makato mengi haujakaa sawa 15% tena umefukuzwa kazi ukirudi huku haukopesheki
 
Kuna utofauti gani kati ya WEO NA WARATIBU WA ELIMU KATA AU UMECHANGANYA?? MM NAJUA WEO= WARD EDUCATIONAL OFFICER ndo mratibu elimu kata!!
 
Hakuna kutoa mchango wowote. Tunajua kuwa Serikali ina mihela mingi ndiyo maana hela haionekani mitaani.
 
Kuna utofauti gani kati ya WEO NA WARATIBU WA ELIMU KATA AU UMECHANGANYA?? MM NAJUA WEO= WARD EDUCATIONAL OFFICER ndo mratibu elimu kata!!
Mhhhh umejichanganya mwenyewe,WEO ni Ward Executive Officer yaani Afisa Mtendaji wa Kata na huyo mratibu wa elimu kata yuko chini ya WEO
 
Hamuwezi kula pesa ya rambi rambi na mkasalia sawia, laana hii itausambaratisha huu ...
 
Back
Top Bottom