Elimu bure iangaliwe upya.

Nyagalu blood

Member
Feb 3, 2019
5
13
Heshima kwenu wanajamvi...

Nimewaza na kuwazua juu ya hili tatizo /janga lililowakumba baadhi ya wahitimu wa darasa la saba .
Kwani kama tunavyojuwa kunabaadhi ya wanafunzi mpaka muda huu hawajaripoti mashuleni kwa ajili ya kuendelea na masomo ya kidato cha kwanza.
Hii ni kwa sababu ya uhaba wa madarasa,kinachonimiza kichwa nin kiini cha tatizo ni Sera ya serikali ya elimu bure?au idadi ya wanafunzi sambamba na ufaulu imeongezeka kuliko miaka iliyopita?

Nakumbuka kabla ya hii Sera ya Elimu bure kuanzishwa hakujawahi kutokea tatizo kama hili la wanafunzi kushindwa kuripoti shuleni mapema kwa sababu ya uhaba wa madarasa.
Kiukweli na kiuhalisia ile michango tuliyokuwa tukiitoa shuleni ilikuwa na msaada mkubwa hasa katika kuisaidia shule kujiendesha yenyewe,hususani ukarabati wa madarasa,madawati,ulipaji wa waalimu ambao hawajaajiliwa ili kutatua tatizo la uhaba wa walimu,nk.

Kwa ujumla,kama serikali imeona imeshindwa kuendana na hii Sera isione aibu kuifuta na kurudisha utaratibu wa hapo awali,natumai itasaidia kuepukana na changamoto kama hizi.

Nahitimisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali yangu ya awamu ya tano haina kipaombele cha elimu wa ajira, mim ninajenga flyover, stegliers gorge, ndege

Nishasema hakuna pesa za bure pigeni kazi, nchi yetu n tajir sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom