Elimu bure Finland!! Vijana changamkeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Elimu bure Finland!! Vijana changamkeni

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Katoma, Jan 20, 2010.

 1. Katoma

  Katoma Senior Member

  #1
  Jan 20, 2010
  Joined: Mar 11, 2008
  Messages: 135
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dili kwa vijana wa Tanzania, hasa hasa kwa wale waliomaliza Form 6 au wapo Form 6 sasa hivi. Ningependa kuwajulisha kuwa maombi ya kujiunga na vyuo vya Finland yameanza na deadline ni February 12.
  Vyuo vingi vinafundisha kozi kwa kiingereza.

  Procedure ni simple sana:

  1. Tafuta vyuo na kozi unazotaka kusoma kwa ajili ya BA au BSc.
  list ya vyuo na website zao waweza kupata kupitia anuani:

  http://www.minedu.fi/OPM/Koulutus/ammattikorkeakoulutus/ammattikorkeakoulut/?lang=en


  2. Jaza fomu online kupitia anuani:

  https://www.admissions.fi/

  (kujaza fomu na kuituma online inachukua kama dakika 10 hivi)

  3. Tuma makabrasha yote kabla ya tarehe 19 February 2010 4.15 pm Finnish time.

  vyeti vya kutuma ni:
  (a) A copy of the original form 4 and/or form 6 certificate
  (b) Majibu ya mtihani wa kiingereza wa TOEFL (soma chini kuhusu TOEFL)

  kama haujafanya mtihani wa TOEFL (Test of English as a Foreign Language), fanya hima uende pale British Council mitaa ya Posta ili kujiandikisha. Waambie watume majibu directly kwenda chuo ulichochagua as your first choice, (utajua anuani ya chuo baada ya kufanya application online).

  Why spend millions kusoma UK, US au Asia wakati unaweza kusoma bure Ulaya kwa kiingereza?

  Kila la heri
   
 2. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Good news for we as we use to call ourselves poor country for this aid of highlearning is a big help. Thanx for info.
   
 3. D

  Donrich Senior Member

  #3
  Jan 20, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Mkuu samahani labda kama nimelewa vibaya nimejaribu kwenda kwenye hiyo website wanasisitiza kwamba financial aid to foreigners will be limited to people who are working there,staying with families or immigrating otherwise kama unaomba nafasi ukiwa na nia moja tu ya kusoma bila sababu nyingine yeyote,wewe huruhusiwi..Kwa hivyo kusoma kuendane na wewe kuwa raia wa Finland kwa kuhamia,kufanya kazi au kufuata familia,unaweza kunisaidia kama nimeelewa vibaya boss...
   
 4. Katoma

  Katoma Senior Member

  #4
  Jan 21, 2010
  Joined: Mar 11, 2008
  Messages: 135
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa uelewa wangu ni kwamba living expenses unajitegemea mwenyewe. Wanafunzi wengi wanapata part-time job wakati wakiwa huko. Kwahiyo mshahara wako utakuwa ni kujikimu huko na sio kuhangaika kulipia ada kama ilivyo kwa wengi wetu tuliosoma US ama UK.
   
 5. D

  Donrich Senior Member

  #5
  Jan 21, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Pamoja na yote mimi nikushukuru tu ndugu yangu Katoma kwa kufanya jitihada za kutaka watu wengine wafanikiwe,umeonyesha uzalendo ..lets hope for the best...
   
 6. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #6
  Jan 21, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  vya bure wakati mwingine vina gharama kubwa kuliko za vyuo vya UK, Asia, USA etc....
   
 7. Katoma

  Katoma Senior Member

  #7
  Jan 21, 2010
  Joined: Mar 11, 2008
  Messages: 135
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mhh,. fafanua
   
 8. Vitendo

  Vitendo JF-Expert Member

  #8
  Jan 22, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 597
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kaka mimi TOEFL siijafanya na pesa sina kabisa yani ni mtoto wa masikini kabisa,hapo inakuwaje hawa jamaa hawezi kunipa tu admission afu baadae nikapiga hiyo Toefl,maana matokeo yangu yako poa sana tu na nataka kusoma Finland.
  Afu mambo ya pesa ya Nauli na pesa ya kuishi huko inakuwaje?
  sijaelewa elimu bure yani hakuna ada kabisa ua inakuwaje hapo ebu weka wazi kidogo!!!!!!!!!
   
 9. Katoma

  Katoma Senior Member

  #9
  Jan 22, 2010
  Joined: Mar 11, 2008
  Messages: 135
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kwamba haulipi ada. Nauli na gharama zako za kuishi huko unajitegemea.
   
 10. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #10
  Jan 22, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,485
  Likes Received: 19,881
  Trophy Points: 280
  sio ukrain kweli hii?
   
 11. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #11
  Jan 22, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Wacha kuchafua bandiko....
   
 12. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #12
  Jan 22, 2010
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Hiyo TOEFL ni kwa ajili ya kujua uwezo wako wa Kiinglishi ambayo ndo lugha ya kufundishia, sasa watakupa vipi admission kama hawajui uwezo wako wa lugha? Fanya makaratee upate hela ya hiyo TOEFL.

  Hakuna ada, hiyo ndege na kuishi ni kivyako. Although kunaweza kukawa na scholarships vilevile za kukusaidia na hizo gharama, maana maisha ni gharama sana hizi nchi za Scandinavia.
   
 13. epigenetics

  epigenetics JF-Expert Member

  #13
  Jan 29, 2010
  Joined: May 25, 2008
  Messages: 260
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
 14. Simple

  Simple JF-Expert Member

  #14
  Jan 29, 2010
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 249
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Ni kweli elimu ni bure kwa sasa hapa Finland, Na jamaa wanakaribisha maombi kutoka kokote duniani, tatizo applicants ni wengi mno kiasi kwa kupata nafasi inakuwa ni ngumu sana,mwaka jana walipokea maombi 3500 kutoka kwa Nigeria and Ghana tu,Jumla ya foreigners walioapply ni 7,200(yle.fi\news) wakati waFinnish wenyewe walia-apply 2000, na katika kila darasa wanataka ratio ya citizen 3,foreigner 1, so chances ni ndogo kwa mtanzania aliyemaliza High School kwa mfumo wetu huo wa elimu duni. ( Sikatishi tamaa,bali andaa documents zilizoshiba,)

  pili ni kwamba wanategemea uwe na 6,000 euros kwenye account yako..yaani 500euros per month. Iko kiwango inabidi kiwepo kwenye personal account yako ili uwe qualified kupata student visa.

  Tatu ni kwamba si rahisi kupata ajira kama mkuu alivyoainisha hapo, ajira nyingi zinatolewa pale utakapoweza kuongea ki-Fin(lugha yao) kwani kila kitu kipo in Finnish or Swedish( English haitambuliki wala haipendwi hapa,,,jamaa they are very proud of their culture)...Ingawa shuleni wanafundisha course za kiingereza ili watu wao waweze ku-internationalize.

  Nne ni kwamba gharama za maisha ni kubwa mno, a room in a shared apartment is around 300euros for students,

  Ubaguzi wa rangi pia ni tatizo, mabaani,,kwenye bus,,train na sehemu nyinginezo,,hawakupigi ila wanakushangaa kama vile ni sanamu ya kinyago..

  Kwa mtanzania wa kawaida,,,culture shock itakuwa kubwa mno mwanzoni,,kwani jamaa wana tamaduni tofauti mno na kwetu.

  Hali ya hewa pia ni tofauti mno na nyumbani,,huku baridi na giza ni miezi nane( august-march)

  Nimeona bora nianishe mambo hayo,,kwani uzuri wa kuishi nchi kama Uk au Us ni kwamba hamna language barrier,,so adoption yako inakuwa mara nyingi smooth if u work hard..

  Vile vile nimeona ni bora nianishe baadhi ya matatizo kwa wanaotaka kuja,,kwani watanzania wengi wanakuja bila maandalizi ya kutosha, then wanataabika sana mwanzoni na kuzani watu wana watosa wakati ndio hali halisi.
   
 15. Katoma

  Katoma Senior Member

  #15
  Jan 30, 2010
  Joined: Mar 11, 2008
  Messages: 135
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Asante kwa kuainisha "the negatives".
  1. UK na USA nako wanataka uwe na kiasi cha kujitosheleza katika account kabla ya kwenda masomoni. Wanafunzi lukuki wameenda ingawa hawana uwezo kama walivyoainisha katika Bank statement zao? 2. Ubaguzi upo kila sehemu, hata TZ.

  Mi naona kama mtu unania ya kwenda nchi za watu, ishu kama ubaguzi haziwezi kukustua, kwani it is the fact of life.

  Waache vijana wajitume, kwani katika kila opportunity kuna vipingamizi kadhaa. Cha muhimu ni namna utakavyojiinua kupambana na hivyo vipingamizi.
   
 16. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #16
  Feb 1, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Baadhi ya vijana wa Kitanzania wanaosoma Finland. Huu ni wakati wa Summer wakijifurahisha.
  [​IMG]
   
 17. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #17
  Feb 1, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  haya 'ilimu' ya bure finland...

  [​IMG]
   
 18. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #18
  Feb 1, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Aisee mbona wamejibanza huko machakani?? Halafu hamna hata kampani ya wenyeji kidogo. Hiyo nchi itakuwa ya wabaguzi na haifai kuishi.
   
 19. k

  komred Member

  #19
  Feb 1, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kijana tunashukuru kwa taarifa lakini mbona umetuma taarifa wakati muda umebaki kidogo sana? Mbona hukutujulisha mara walipotangaza 11 JAN? Wengine walio sehemu za mbali kama Kanyigo, Liwale, Mbinga, Mpanda nk c mambo hayo yatawapaitia mbali sana. Wakati mwingine ukipata taarifa nzuri itume/tujulishe kwa wakati (Information is power)
   
 20. Katoma

  Katoma Senior Member

  #20
  Feb 2, 2010
  Joined: Mar 11, 2008
  Messages: 135
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Komred, hili tangazo limewekwa hapa 20th January 2010, na hii si mara ya kwanza kwa ishu kama hii kusambazwa mtandaoni. Kama wewe ni mchakarikaji utawahi deadline. Ila kama ni mtafuta "excuses" litakupita. You have to act.
   
Loading...