Elia Michael: Kupona kwa Tundu Lissu kumetibua mipango iliyokuwa imepangwa

Mar 3, 2018
75
799
Mipango iliyo kuwepo ni kwamba;

Tundu Lissu auawe,Viongozi wa juu wa Chama wafungwe,wengine wahamie CCM kwa gharama yoyote,wengine waache siasa na wakimbie mapambano, wanachama waogope na wasione taarifa kabisa za upinzani wa CHADEMA, ACT chini ya Zitto ife kifo cha Kawaida kupitia sheria ya vyama vya siasa na ikiwezekana na yeye auawe wakati huo akose nguvu maana chama chake ni kichanga na kina uhaba wa raslimali watu.

TBC itumike kueneza propaganda za CCM na serikali ya Magufuli,Baadhi ya viongozi wa dini watumike kuuhadaa UMMA na waumini wao juu ya utawala huu Mbovu, wanasiasa wenye umri Mkubwa kama Lowassa wachoke kwenye mapambano kutokana na Umri na mikiki mikiki, Mauaji ya watu wasio na hatia yatumike kutishia wakosoaji walioko nje ya mfumo wa vyama vya siasa,Taasisi za vyuo vikuu viongozwe na madali wa CCM, Takwimu zinazoivua nguo serikali zisikike kwenye masikio ya wananchi maana taasisi za utafiti zimepigwa pini kupitia sheria ya Takwimu.

Tengeneza Taifa la wajinga na masikini ambao wakilala na kuamuka wanawaza kodi na tozo dhidi yao ili wawe watumwa kwa wa chakula na serikali ya watu wa chache,mtawala aabudiwe kuliko Mungu wa Mbinguni na kisha watawale wanavyotaka.

Sasa hali ipo hivi;

Tundu Lissu hajafa kwahiyo hawakuweka mikakati ya kufanya endapo asipokufa na sasa wanaongea lugha tofauti kama kipindi kile cha ujenzi wa mnara wa Babeli Waziri wa mambo ya Ndani analopoka,Bashiru analopoka,Bashite na Mabalozi nao hawajaachwa salama maana nao wanalopoka huku wengine wakiomba Dunia isimame washuke maana joto ni kali yaani kila mteule wa Magufuli anatafuta namna ya kumzungumzia Tundu ambae yupo kwenye hatua ya kunyoosha miguu kama sehemu ya matibabu kwa mjibu wa madaktari, Viongozi wapo mahabusu na Chama kinachanja mbuga mtaani mbali na vikwazo vinavyotukabili,matatizo yametuleta pamoja upinzani na sasa wanahangaika na propaganda ya Zitto na Lissu kunyukana kwenye Urais ( sijui wamepata wapi ujasiri wakati malengo ilikuwa ni Lissu afe).

Ugumu wa maisha umekuwa ndio upinzani pekee ambao sasa na Mwananchi wa kawaida anaepatikana Murusagamba Ngara ama Kagezi Kibondo ama Songea Ndani ndani ama Tandahimba anauona,hata Mwananchi anayepatikana kila pembe ya Nchi hii hali sio nzuri. Zamani ilikuwa mpaka uwepo mkutano wa Chama cha upinzani ndipo wananchi wanapata fursa ya kujua hali jinsi ilivyo.

Asante Mungu kwa kutia upofu serikali hii ambayo inafanya biashara ya kuwauzia vitambulisho wajasiliamali wanaopatikana kwenye mipaka ya Nchi hii bila kufuta ushuru wa halmashauri.

Asante Mungu kwa kuwatia upofu Watawala hawa ambao kwao vifo vya watu na kuokotwa kwa miili huku baadhi ya maeneo yakigeuka machinjio ya Vichanga kwao hili ni jambo la kawaida sana. Sisi watu wa Imani tunajua kila jambo unalofanya una makusudi Bwana.

Asante Mungu kwa kuendelea kuwaweka wazi baadhi ya Viongozi wa Dini ambao wanaona hali hii ni kawaida yafaa kushangiliwa kuliko kukemewa. Hawa nao wametajwa kuwa ni manabii wa Uongo kwenye Biblia.

Asante Mungu kwa kuwatia upofu watawala hawa ambao wanataka ndege,daraja la Mfugale na reli viabudiwe na vipewe heshima kuliko uhai wa wanadamu,najua kila kitu kina makusudi ya kutokea.

Neno kwa upinzani Tanzania.

Ni kweli kwamba baadhi ya wanachama wetu tayari wameaga Dunia kwa nyakati tofauti na kwa matukio yaliyoratibiwa na wanadamu lakini niwaambieni kwamba hakuna umwagaji damu unaofanyika duniani halafu damu ile ikapotea hivi hivi,ni vema matukio hayo yakaandikwa na kutunzwa kwakuwa hii itasaidia vizazi vijavyo kwamba kuna watu walipambana hata mara baada ya Uhuru ili kutafuta hali nzuri ya maisha kwa Taifa lao.

Kuwaweka Rumande viongozi wetu kwa Muda mrefu pia viandikwe na vitunzwe,sheria kandamizi zinazotungwa dhidi yetu na matamko haramu ya Watawala yanayotulenga nayo yatunzwe,picha na video za kikatili shidi yetu,dhuluma inayofanywa dhidi yetu na mambo yoote maovu yanayofanywa Dhidi yetu yatunzwe kwenye kumbu kumbu maana kumbukumbu ya mambo haya maovu ndio yatasaidia kuamusha hisia kali kwa kizazi hiki kilichopo na kijacho na kuchukua hatua sitahiki ili kubadili hali ya mambo yalivyo sasa.

Mtawala anapokuwa madarakani,anaweza akafanya chochote dhidi yetu kwa wakati huo,ila hatuwezi kuendelea kuwa wahanga wa wakati wote.
Mazingira yatatufanya tuchague lugha ya kutumia wakati ukifika.
Na wakati ukifika hakuna jeshi wala Mkuu wa mkoa atakayesimama kudhibiti lugha tutakayotumia kwani wakati utatulazimisha zaidi kuitumia lugha husika.

Mpumzike salama Ndugu zetu Mawazo Alphonce,Diwani luena na wengine wote mliouliwa kwa mipango ya Watawala,siku zinakaribia ambapo uozo na na uvundo wa damu yenu iliyomwagwa itawageukia wauaji wenu.

Nikutakie jumapili njema Mwenyekiti wangu FREEMAN MBOWE na ESTHER MATIKO ambao mumetunzwa kwenye kuta za Gereza la SEGEREA kwa mipango ya Watawala ambao wanatafuta njia ya kudhuru hata afya zenu hata muwapo Rumande.

Najua kesho Tar 18/02 mtakuwa mahakama ya rufaa,kwakuwa watawala wameamua mahakama uwe uwanja sahihi wa kuonana na Wewe mwenyekiti basi tutakuwepo japo tukutie machoni mwetu huku Watawala wakiwa wanakunywa mnvinyo na wake zao wakiwa wamekalia kiti walichopata kwa njia haramu.

Kwakuwa sisi ni waumini wa utawala Bora basi siku zaja ambapo ubaya utalipwa kwa wema.

Jumapili njema Watanzania wenzangu!

Elia F Michael.
Diwani Gwarama.
Mwenyekiti wa madiwani Kanda ya Magharibi.
Mbunge nje ya Bunge.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa watu wanamshukuru rais kwa kunusurika ajali, kwa kuamka salama n.k
Taifa sijui linaenda wapi!
Nafasi ya Mungu inachunguliwa na ndugu yetu wenyewe!!!

Naamini Mungu atawajibu wanaomdunisha na wanajikweza.

Lissu for presidency come 2020.
Akishinda lissu urais ni pm!!!! Hata chadema hawezi akapita na mnyooo wake Huo ...hatuwezi tukawa Na rais wa namna hiyo mtu asiyejiheshim mwenye kuumwa deko.. M. Anayetukuza mabeberu haitatokea

Very touching. Aptly put. Bless you Sir!
 
Back
Top Bottom