Elia F Michael achaguliwa kura za Maoni CHADEMA kugombea jimbo la Buyungu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Elia F Michael achaguliwa kura za Maoni CHADEMA kugombea jimbo la Buyungu

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Elia F Michael, Jul 9, 2018.

 1. Elia F Michael

  Elia F Michael Verified User

  #1
  Jul 9, 2018
  Joined: Mar 3, 2018
  Messages: 10
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 15
  Idadi ya wajumbe waliopiga kura;.....140

  Kura zilizopigwa...140

  Kura zilizoharibika....01

  Mchanganuo wa kura walizopata wagombea;

  1. Ashura Masoud Mashaka ..............11

  2. Elia F Michael.....121

  3.Gaston Shundo Garubindi................07

  Leo tar 08/07/2018 chama changu kupitia Kikao cha kamati kuu kwa pamoja wamenipitisha kugombea nafasi ya Ubunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia jimbo la Buyungu. Nipende kushukuru kwa heshima hii kubwa ambayo wanachama kupitia viongozi wameona niwakilishe chama.

  Lakini pia nitoe shukrani kwa chama cha ACT-WAZALENDO kupitia Kaka yangu Zitto Kabwe ambaye yeye pamoja na chama chake wameamua kuniunga mkono. Naomba niwahakikishie Wana Buyungu na wapenda Demokrasia wote kwamba nia ninayo,uwezo ninao na sababu ninazo za kusimama kwenye nafasi hii muhimu katika uwakilishi wa wananchi.

  Aidha naamini wananchi wakijua wajibu wao juu ya kulinda maamuzi yao na serikali ikajua wajibu wake kwa wananchi,Buyungu haiwezi kugeuka uwanja wa damu kama ilivyokuwa Kinondoni kwasababu ya kupinga maamuzi ya wananchi ... Naimani Marehemu Kasuku Bilago anaangalia yanayoendelea Buyungu kupitia Ulimwengu wa Roho. Naendelea kumuombea kwa Mungu aendelee kumpa pumziko jema mahala pema peponi,mbegu ulioipanda Buyungu iliota haikukauka,hauko nasi kimwili ila kiroho upo na sisi.


  Elia F Michael
  Diwani Gwarama,
  Mwenyekiti wa madiwani Kanda ya Magharibi. Mgombea wa Ubunge jimbo la Buyungu kupitia CHADEMA
  08/07/2018 FB_IMG_1523170187406.jpg
   
 2. gemmanuel265

  gemmanuel265 JF-Expert Member

  #2
  Jul 9, 2018
  Joined: Feb 16, 2016
  Messages: 5,466
  Likes Received: 10,048
  Trophy Points: 280
  Nakukubali sana mh diwani kwa misimamo yako isiyoyumba linapokuja suala la maslahi ya nchi
   
 3. Ngushi

  Ngushi JF-Expert Member

  #3
  Jul 9, 2018
  Joined: Jul 8, 2016
  Messages: 7,143
  Likes Received: 13,519
  Trophy Points: 280
  Kwani Si Zitto aliomba waungane?
  au wamegoma?
   
 4. xav bero

  xav bero JF-Expert Member

  #4
  Jul 9, 2018
  Joined: Nov 24, 2016
  Messages: 4,885
  Likes Received: 6,316
  Trophy Points: 280
  Ha ha ha walisusa sasa wamerud,ccm inakwenda kuwachakaza kama kinondoni
   
 5. wa stendi

  wa stendi JF-Expert Member

  #5
  Jul 9, 2018
  Joined: Jul 7, 2016
  Messages: 5,436
  Likes Received: 3,611
  Trophy Points: 280
  Huyo mzee hapo pembeni hayo macho ndo yale wahenga walisema macho kumchuzi ..
   
 6. Thad

  Thad JF-Expert Member

  #6
  Jul 9, 2018
  Joined: Mar 14, 2017
  Messages: 6,404
  Likes Received: 13,360
  Trophy Points: 280
  Kila la heri kamanda
   
 7. monopoly inc

  monopoly inc JF-Expert Member

  #7
  Jul 9, 2018
  Joined: Dec 20, 2016
  Messages: 380
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 80
  jipigie promo tu hamna namna, vijana wa Udsm wanaimani na zao lenu
   
 8. C

  COPPER JF-Expert Member

  #8
  Jul 9, 2018
  Joined: Dec 28, 2012
  Messages: 1,935
  Likes Received: 538
  Trophy Points: 280
  Kila la heri
   
 9. Ujinga wa boko

  Ujinga wa boko New Member

  #9
  Jul 9, 2018
  Joined: Jun 8, 2018
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Pambana kijana njia ipo nyeupe
   
 10. Echililo

  Echililo JF-Expert Member

  #10
  Jul 9, 2018
  Joined: Apr 19, 2016
  Messages: 357
  Likes Received: 256
  Trophy Points: 80
  Kila la kheri mkuu!! Imani yangu inaniambia utashinda
   
 11. P

  Pohamba JF-Expert Member

  #11
  Jul 9, 2018
  Joined: Jun 2, 2015
  Messages: 16,581
  Likes Received: 25,729
  Trophy Points: 280
  Kweli Siasa Sio mchezo

  Leo front page ya Tanzania Daima wameandika Muungano wa Chadema Na ACT Ni mwiba Mkali
  Kwa CCM

  CUF kishapigwa Talaka tatu rejea

  ACT hii iliyokuwa inaitwa CCM B Sasa ndio mshirika muhimu wa Chadema Kuliko CUF

  Mbowe Ni Muasisi wa Gia Za Angani Kuwahi kutokea Africa Mashariki Na kati
   
 12. Ghiti Milimo

  Ghiti Milimo JF-Expert Member

  #12
  Jul 9, 2018
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 739
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 80
  Huwa nakereka kweli, watu wanatumia nguvu nyingi kuhakikisha wanapata nafasi, lakini mwishoe. ....TUNAMUUNGA MKONO. ...!
   
 13. B

  Brother Kaka Member

  #13
  Jul 9, 2018
  Joined: Jun 11, 2013
  Messages: 42
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  CCM anachukua jimbo hilo mapemaaaaaah. Maskini
   
 14. P

  Pagan Amum JF-Expert Member

  #14
  Jul 9, 2018
  Joined: Aug 28, 2015
  Messages: 1,671
  Likes Received: 3,016
  Trophy Points: 280
  Kila la heri. Ingawa sidhani kama Mkurugenzi atakutangaza mshindi. Ana familia, na bado anaipenda hiyo kazi, hivyo hawezi kurisk kazi yake kwa kukutangaza.

  Ingawa kwa haki kabisa unaweza kumshinda Eng. Chiza ambaye tayari kaongoza kura za maoni. Wewe kuwa diwani ni mtaji tosha
   
 15. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #15
  Jul 9, 2018
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 21,666
  Likes Received: 9,209
  Trophy Points: 280
  Cc mkafrend
   
 16. R

  Retired JF-Expert Member

  #16
  Jul 10, 2018
  Joined: Jul 22, 2016
  Messages: 12,703
  Likes Received: 15,596
  Trophy Points: 280
  Uongozi wa CDM umehakikishaje yale ya Kinondoni na Siha hayajirudii? Kama hakuna measures kuyakabili hayo, it is a wastage of time and resources!
  Atakuja askari atabeba sanduku mnaona baada ya muda analirudisha, unafanyaje katika hali kama hiyo? Unashinda lakini anatangazwa wa CCM, unafanyaje? Salary Slip Mwanahabari Huru
   
 17. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #17
  Jul 10, 2018
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 28,314
  Likes Received: 48,983
  Trophy Points: 280
  Sijui kama kutakuwa na uchaguzi zaidi ya vioja vya uchaguzi!!

  Tuongeze juhudi za kudai Tume Huru vinginevyo 2020 itakuwa ni majanga.
   
 18. R

  Retired JF-Expert Member

  #18
  Jul 10, 2018
  Joined: Jul 22, 2016
  Messages: 12,703
  Likes Received: 15,596
  Trophy Points: 280
  Upinzania unatoa tamko gani? Haya siyo ya kunyamazia.
   
 19. MOTOCHINI

  MOTOCHINI JF-Expert Member

  #19
  Jul 10, 2018
  Joined: Jan 20, 2014
  Messages: 24,211
  Likes Received: 12,741
  Trophy Points: 280
  Hongera kwa kuwa mwakilishi
  Ila jiandae kushindikiza
   
 20. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #20
  Jul 10, 2018
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 25,495
  Likes Received: 26,403
  Trophy Points: 280
  Mwigulu aliyekuwa jembe la ccm na kila uchaguzi ndiye anayetumwa kuongoza timu ya kushinda akimridhi Tingatinga ndiye leo anaitwa Mzururaji. Au Nape aliyekuwa anaenda kulala mitaroni na Kinana kuhakikisha goli la mkono hadi akavunjika mkono ili tuu Sizonje ashinde leo ndio anatolewa bastola na vijana wa Bashite kwa vile tuu ana mburudisha Daddy!
  Kweli siasa ni vituko, hata aliyekuachia ofisi kwa kulazimisha Lubuva atende ya kutenda eti leo akisema kitu unamwambia anawashwa! anawashwa nini ili umkune?
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...